Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Agreed Mkuu FMES

Ndio maana tunasema it takes someone/all of us to say NO to ubinafsi na miujiza yote inayoambatana nayo hivi sasa................lakini inaelekea watu bado tumefungwa katika box la ubinafsi ambao unadai ulipandikizwa na Mwl JKN........very suprising bado tunaendeleza ubinafsi!!.....na ndio maana nakubaliana na usemi wako kuwa yote yatokeayo sasa ni reflection yetu wenyewe

Mwl JKN alikiri kuwa yalikuwepo mazuri aliyoyaanzisha na basi tuyadumishe na ikiwezekana yawe bora zaidi........yale yaliyo mabaya tuyarekebishe/kuyaacha na kuchukua mfumo mpya.............Now look at what we are doing to our economy (doomed hell)........yaani kundi fulani limeamua kuliibia taifa.......we can not just sit aside........saying.........Yes one of the things Mwl JKN alivyotuachia ni Ubinafsi.........si atleast alituambia tuache yale mabaya.......whats is wrong with us then.

Nakubaliana nawe pia kuwa Viongozi wabovu CCM watoke....na wa kuwaondoa i believe wewe ni mmoja wao unayesema NO to Ubinafsi

sorry mwanakijiji......kwa kutoka nje ya mjadala

Ogah..

kwa yale yanayotokea Tanzania miaka yote hii baada ya kufa kwa NYerere, inaonekana kuwa tatizo sio nyerere bali ni ccm na wana ccm na viongozi wa ccm mafisadi.

Kama ukiona mtu anatetea CCM na wakati huo akisema kuwa yote haya ni kwa sababu ya Nyerere, basi kuna swali kubwa sana la kuulizwa hapa....
 
Hivi hii thread si inazungumzia "FIKRA" za Nyerere au? Maana naona sasa imeanza kuchukua detour isiyoeleweka...
 
1.

Pole pole mkuu, hatujui mbele ya safari itakuwaje, lakini mimi ninajaribu tu kutoa maoni yangu kuhusiana na utawala wa Mwalimu, na impact ya mazuri na mapungufu yake kwa taifa langu, na ninajifunza m,engi toka kwa wale wanaodhani kuwa alikuwa malaika.

Anayedhani kuwa Nyerere alikuwa malaika na alaaniwe! Lakini abarikiwe anayedhani alikuwa shetani!

2.

Hapana CCM siku zote imekuwa safi kwa maandishi na maneno tu, na hiyo imetokana na kuongozwa na kiongozi aliyekuwa na maneno mazuri lakini matendo hakuna.

Sasa itakuwaje CCM iwe safi kwa maandishi wakati maandishi yenyewe yametokana na mtu mwenye mawazo mabaya. Yaani CCM iwe safi kutokana na maneno ya mtu? CCM ni chafu kwa sababu hawakuyafanyia kazi maneno ya Nyerere jinsi ilivyopaswa, na wewe mwenyewe umeelezea kwa sababu waligeuka kuwa wanafiki, waoga, wavivu wa kufikiri n.k CCM siyo safi kwa sababu waliziacha fikra za Nyerere na sasa hawana cha kushikilia wanaenda mzoba mzoba tu.

Mimi na CCM na ndio maana nipo hapa JF kwa sasa, nikikemea maovu na ninajua kuwa I am on the right track kwa sababu ya yaliyoikuta JF hivi karibuni, that is all I can do for now as far as kukemea uovu ndani ya chama changu.

mzee chama chenye kukumbatia fikra za Nyerere ni chama hatari kabisa! Kwa sababu Nyerere alikuwa kiongozi hatari na mawazo yake mabaya, kama ni yeye aliandika Katiba ya CCM (kama ulivyodai mwanzoni) na kama ni yeye aliyeandika mambo mengi ya CCM inashangaza kwanini uendelee kukikumbatia chama hicho.

Umefika wakati wa wewe kuwa kama mimi toka CCM na usijiunga na upinzani ili uwe huru kukemea maovu bila kuangalia sura au jina la Chama! Na wakikuta mpinzani huhitaji kuomba radhi. Mzee, wakati umefika wa kuachana na CCM hasa baada ya chama hicho kurudi Butiama na kutaka kuyakusanya maandishi ya Mwalimu na "kumuenzi Baba wa Taifa". Hiyo ingekuwa sababu tosha ya kuagana na CCM.

Karibu kwenye uwanja wa mawazo huru! tuweze kulikomboa Taifa letu toka utumwa wa CCM.
 
1.

Pole pole mkuu, hatujui mbele ya safari itakuwaje, lakini mimi ninajaribu tu kutoa maoni yangu kuhusiana na utawala wa Mwalimu, na impact ya mazuri na mapungufu yake kwa taifa langu, na ninajifunza m,engi toka kwa wale wanaodhani kuwa alikuwa malaika.

Bado hakuna aliyesema hapa kuwa Nyerere alikuwa Malaika. Lakini ni vyema pia na wewe usidanganye kuwa Nyerere alikuwa shetani

2.

Hapana CCM siku zote imekuwa safi kwa maandishi na maneno tu, na hiyo imetokana na kuongozwa na kiongozi aliyekuwa na maneno mazuri lakini matendo hakuna.

Wewe ndio ulisema hapa kuwa ccm ni safi. Ukweli ni kuwa ccm sio safi kabisa hata miaka kumi baada ya kifo cha Nyerere. Inaonekana tatizo liko kwa wanaccm na viongozi wake na wala sio Nyerere.

Mambo yaliyofanyika Tanzania kuanzia mwaka 1999 ni makubwa kabisa ya kuonyesha uovu wa ccm na viongozi wake wa sasa ambao wamedumaza nchi kwa kiwango cha kutisha

3.

Hadithi ya Wana-Israeli, ndio unapaswa kuwa mfani mzito kwa wananchi wa Tanzania, kuwa Freedom ni very expensive, maana hata Farao hakuutoa kwa hiari, na Mungu kwa kuwatumia wao chanzo cha kuzaliwa kwa neno Freedom, wananchi wetu bado hawajaelewa maana wangekuwa, basi CCM isngeshinda Tunduru na Kiteto, wa kulaumiwa ni sisi ambao we know better kwa kutowaamsha mapema,

Mimi na CCM na ndio maana nipo hapa JF kwa sasa, nikikemea maovu na ninajua kuwa I am on the right track kwa sababu ya yaliyoikuta JF hivi karibuni, that is all I can do for now as far as kukemea uovu ndani ya chama changu.

Swala la "ushindi" wa ccm sidhani kama ni issue hapa hasa ukichukulia kuwa huko Afrika mtu yeyote anaweza kusema kuwa ameshinda - Kenya na kinachotaka kutokea Zimbabwe
 
Wakuu haya kesho, naona mjadala umeanza kuwa personal badala ya mawazo ya Mwalimu, anyway:-

mzee chama chenye kukumbatia fikra za Nyerere ni chama hatari kabisa! Kwa sababu Nyerere alikuwa kiongozi hatari na mawazo yake mabaya, kama ni yeye aliandika Katiba ya CCM (kama ulivyodai mwanzoni) na kama ni yeye aliyeandika mambo mengi ya CCM inashangaza kwanini uendelee kukikumbatia chama hicho.

Hapana, ninaaamini kuwa kuna mabadiliko mengi sana yamefanywa since Mwalimu aondoke, ndani ya maandishi ya CCM ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa Azimio la Arusha, na kukumbatia ubepari, sasa CCM tunahitaji kasi zaidi kuondokana kabisa na mawazo ya kijamaa ya Mwalimu, then taifa letu litakuwa sawa, na kuna ambao tuko serious kuhakikisha hilo linafanyika na kuwezekana.
 
Hivi hii thread si inazungumzia "FIKRA" za Nyerere au? Maana naona sasa imeanza kuchukua detour isiyoeleweka...

Nyani Ngabu,

ukisoma post nyingi mno hapa hasa zile ambazo ziko negative kwa Nyerere, nyingi zinaongelea "mabaya" aliyowafanyia Nyerere watu fulani fulani na wala sio fikra au sera za alichofanya.

Nadhani hii mada kwa muda mrefu imekuwa ikienda all over the map na kwa muda kila kitu hapa kimekuwa fair game.
 
ukisoma post nyingi mno hapa hasa zile ambazo ziko negative kwa Nyerere, nyingi zinaongelea "mabaya" aliyowafanyia Nyerere watu fulani fulani na wala sio fikra au sera za alichofanya.

Hapana so far nimekubali mazuri aliyoyafanya Mwalimu, ila the most important ninajaribu kuchambua matatizo ya fikra za Mwalimu na impact yake kwa taifa letu, na kuyaoanisha na kwa nini taifa letu limedumaa, kisheria, kisiasa, na kiuchumi, kwangu mimi chanzo chake ni Mwalimu, wa sasa waneendeleza tu matendo, na sio mafundisho ya Mwalimu, ambayo yalikuwa tofauti kabisa na mahubiri yake,

Ndio maana leo Tanzania tunatafuta ukombozi wa Kenya na Comoro, badala ya kujikomboa hapa Tnazania kwanza na ufisadi, hiyo ilikuwa ni tabia ya Mwalimu ya kusaidia nchi zingine zote badala ya kuwasaidia wananchi wa hapa bongo kwanza, sisi sasa tunaiga tu.

Otherwise, Mwalimu was the greatest ever!

Haya kesho wakuu!
 
FMES,

Taifa limedumaa kwa vile wanaccm na viongozi wa serikali wamefanya ufisadi na kuiba mali ya nchi kwa manufaa yao wenyewe na wala sio kwa sababu ya maneno ya Nyerere. Kama sera na mambo ya Nyerere ni maovu kama unavyosema, basi taifa limeoza kwa vile miaka kumi tangu kifo cha Nyerere bado kuna watu wanaamini kuwa ushetani wa Nyerere ndio unadunisha nchi.

Ndio maana leo Tanzania tunatafuta ukombozi wa Kenya na Comoro, badala ya kujikomboa hapa Tnazania kwanza na ufisadi, hiyo ilikuwa ni tabia ya Mwalimu ya kusaidia nchi zingine zote badala ya kuwasaidia wananchi wa hapa bongo kwanza, sisi sasa tunaiga tu.

Otherwise, Mwalimu was the greatest ever!

Haya kesho wakuu!

Sidhani kama mwalimu alikuwa the greatest ever na wala sio kweli alikuwa the worst ever. Kuna mema mengi mazuri aliyofanya Nyerere na kusema Nyerere na pia kuna mabaya aliyofanya au yaliyofanywa kwa jina lake.

Kinachotafutwa hapa ni yale mazuri yafuatwe na mabaya yaachwe. Hata hivyo inashangaza kuona kuwa nchi nyingi duniani leo hii zinaongozwa kwa sera za kijamaa zaidi kuliko za kibepari. Hii sidhani kama ni ajali. Ubepari typically ulishindwa na ujima pia ulishindwa. Mchanganyiko wa sera mbili ndio umefanikiwa. Ni heshima kujua kuwa Nyerere aliruhusu vyote - ubepari kidogo na ujamaa sana na kuchanganya na ujima kidogo.
 
....hivi buraza, unadhani shimo alochimba Nyerere kwa miongo miwili unusu(akiwa kama rais) na mwongo mwingine na nusu akitawala kwa remote toka Butiama...unadhani ni rahisi kulifukia ktk miaka kumi hii toka alegee mbele ya haki!!??

Kwa logic yako,

Unategemea shimo lilochimbwa na wakoloni kwa miaka zaidi ya mia moja lingezibwa na Nyerere kwa miaka mingapi?

itachukua miaka mia(tena kama tupo committed hasa) kuweza kurekebisha makosa na misingi mibovu iloachwa na Mchonga!!........hii sio kazi rahisi, na hatua ya kwanza hapa ni kukubali kwamba mchonga overall alichemka! kwa bahati mbaya watu tunaofikiria hivyo ni minority, ushahidi ni hapa JF hasa kwenye hii thread......sasa basi kwa mwendo huu itachukua generations tatu kurekebisha uovu wa Nyerere!!!

I hope nimeeleweka...........

Wewe ukiamua kuhamisha lawama kwa Nyerere, basi kila kizazi kina kila sababu ya kulaumu uongozi uliopita kwa makosa yake. Itafikia wakati, kila baada ya miaka kumi, uongozi mpya unafanya uovu na kulaumu uongozi uliopita. Kwa mchezo huu basi itachukua zaidi ya generation tatu kusafisha uovu wote kuanzia kwa wakoloni hadi kwa huu wa sasa hivi unaofanywa na Kikwete.
 
....hivi buraza, unadhani shimo alochimba Nyerere kwa miongo miwili unusu(akiwa kama rais) na mwongo mwingine na nusu akitawala kwa remote toka Butiama...unadhani ni rahisi kulifukia ktk miaka kumi hii toka alegee mbele ya haki!!??
itachukua miaka mia(tena kama tupo committed hasa) kuweza kurekebisha makosa na misingi mibovu iloachwa na Mchonga!!........hii sio kazi rahisi, na hatua ya kwanza hapa ni kukubali kwamba mchonga overall alichemka! kwa bahati mbaya watu tunaofikiria hivyo ni minority, ushahidi ni hapa JF hasa kwenye hii thread......sasa basi kwa mwendo huu itachukua generations tatu kurekebisha uovu wa Nyerere!!!

I hope nimeeleweka...........

Katika mawazo yako historia ya Tanzania imeanza mwaka 1961! na kabla yake hakukuwa na mashimo yoyote!
 
Mwafrika,
Shukran sana kwani hizi ndizo sababu alokuwa akitumia Lowassa kumlaumu Mkapa wakati alichokuwa akifanya yeye hakina tofauti kabisa, fisadi ni yeye mwenyewe...

wakuu wa baraza,
Mwalimu kama kiongozi alikuwa na makosa yake kama kiongozi na sidhani kama kuna mtu hapa anaweza simama na kumtaja kiongozi hata mmoja asiyekuwa na doa ktk utawala wake..
Fikra za watu kama Costro, Che, MLK, Ghandi, Nkurumah pamoja na kwamba wao hawakuleta maendeleo ya haraka kiuchumi kutokana na sababu nje ya uwezo wao haina maana fikra zao tangulizi hazina maana. Hata kama tutasema zilikuwa hazina maana then kwa nini sisi tusionyehse zile zenye maana na kuonyesha changes za haraka kutokana na kusahihisha makosa yake ikwa bado hatujasahihisha makosa hayo na inakuwaje tunayaona mabaya ya wakati ule hali bado yanaendelea hadi leo hata kama yuko kaburini ama bado anaongoza akiwa kaburini! Oooh nimesahau ni fikra za mwalimu bado zinadumishwa au sio....which one?

Hukumu yenu yote kwa Nyerere ni sawa na kumlaumu mwanamke anayeitaka taraka kutoka ktk ndoa ilijaa abuse, kisha tuna hukumu maamuzi yake kuwa hayana busara kwa kutazama maisha ya huyo mwanamke kiuchumi baada ya kuachika...Na kweli ndivyo waswahili huwa tunatazama.. kama mwanamke ka punch baada ya ndoa tutasema alifikiria la maana sana, hali yake ikiwa mbaya tunamcheka na kusema kwani abuse nini ikiwa mtu ulikuwa unakula kuku kwa mrija utumwani - mjinga tu..

Miaka 23 Ya Nyerere tuliyaona mabaya na mazuri yake miaka 24 baada yake tunachokiona zaidi ni gap kubwa kati ya matajiri na maskini...na hakuna kiongozi hata mmoja aliyezungumzia tahadhali ya viongozi wetu kujitajirisha ktk hali hii isipokuwa Nyerere mwenyewe hakuna kati yao aliyeona mbali, tena naweza diriki kusema hao kina Mtei, Kambona na wengineo wenyewe walifikiria hali kama hii haiwezi tokea chini ya mfumo wa Kibepari... wao waliona ni win win situation kama anavyosema JK.. Kisha cha ajabu basi huyo Mtei mwenyewe kayaona makosa ya CCM ndani ya mfumo huu mpya na ndio maana kawa mpinzani wa sera za CCM sio Ujamaa wala fikra za mwalimu bali kwa sababu ya wizi wao...Haya hata Freeman mbowe mwenyewe anazitukuza fikra za mwalimu, kitendo ambacho kiliwachukiza CCM kina Kingunge!..
Hivyo basi sio fikra pekee inayotuangusha sisi isipokuwa ni mazingira yetu (ardhi), viongozi na siasa mbaya vyote vinachangia ktk kudumaza uchumi wa nchi yetu..Less of any of that hakuna mafanikio..
At least Nyerere aliweza kutuasa kuhusu mazingira kama haya ya kiuchumi tukafunga mikanda kwa miaka 17, kwa sababu ya kuhofia hali kama hii ambayo leo inajitokeza kwa kasi ya ajabu miaka 40 baada.
 
.....sie tunaanza kuhesabu baada ya uhuru na sio wakati wa mkoloni!! kwani kabla ya mkoloni maisha ya waTZ yalikuwaje?? je kulikuwa na Tanzania?? acha mambo yako bwana......ala!!!

Ukishaanza kutumia neno sisi na wao, basi unaweka vipimo tofauti kati yako na wengine. Kinatumika hapa kipimo kimoja na ambacho ni kwamba, kila kiongozi anatuhumiwa au kusifiwa kwa kipimo sawa na nothing short of that

kulaumiana ni sehemu ya maisha, ilimradi tu lawama hizo ziwe halali!! sisi tutalaumiwa na vizazi vijavyo kwa ubwege wetu wa kukumbatia 'fikra' mbovu, zilizoitwa sahihi ambazo time and again zime-prove kuwa ni failures!!!...........hatua ya kwanza, ni kuanza kukubali kwamba yes nyerere was somewhat ok, lakini alikuwa na fatal flaws ktk nchi, hasa kiuchumi na kiutawala kwa ujumla!! kabla ya kufanya hivyo, tutaendelea kucheza mduara......na kuimba zidumu fikra sahihi kama ma-bwege yaliolishwa limbwata!!.

Inaonekana unadhani kuwa kutumia matusi na maneno ya kashifa inachangia chochote kujenga point. Huwezi kujenga taifa lolote kama unakuwa na taifa la watu wa kulaumu wengine tu bila wao kufanya chochote au kumiliki makosa yao.

Matatizo ya Tanzania kulingana na wanaompinga Nyerere hapa hasa FM ES, yanaonekana yanaletwa zaidi na ccm ambayo inafanya mambo ya aibu na ajabu miaka yote hii baada ya kifo na utawala wa Nyerere. Kinachofanyika sasa hivi ni kuondoa hii kansa ya sasa hivi (ambayo ni CCM) na sio kutafuta mtu aliyekufa miaka mingi iliyopita ili umtwishe mizigo yako.
 
tatizo tunashindana, ndio maana mnatafuta makosa ya kiufundi ktk sentensi ili ku-score points!!!! mie naanza kuongea baada ya uhuru........kwani wakati wa mkoloni ni issue nyingine na kabla yao kulikuwa hamna Tanzania!!!

ama sivyo(kama unaelewa.....) basi title ya "ubaba wa taifa" haimfai Nyerere!!! yeye si ndio founder na baba.........halloooow!!

Unachosema hapa hakisaidii point yako yoyote unayojenga ya kumlaumu Nyerere kwa matatizo yako leo miaka 10 baada ya kifo ya kifo chake. Hili la baba wa taifa unalileta wewe na halina uhusiano wowote na sera au fikra za Mwalimu.
 
nadhani unajua huwa sipendagi dizaini hizo!!! debate kwa amani na upendo.........ass/u/me(assume) upo kwenye therapy session, kuna mistari hutakiwi kuivuka!!!!! please.

Naona ulichoandika hapa chini kina spirit zote za amani na upendo au sio?

......na kuimba zidumu fikra sahihi kama ma-bwege yaliolishwa limbwata!!.
 
Mwafrika,
Shukran sana kwani hizi ndizo sababu alokuwa akitumia Lowassa kumlaumu Mkapa wakati alichokuwa akifanya yeye hakina tofauti kabisa, fisadi ni yeye mwenyewe...

wakuu wa baraza,
Mwalimu kama kiongozi alikuwa na makosa yake kama kiongozi na sidhani kama kuna mtu hapa anaweza simama na kumtaja kiongozi hata mmoja asiyekuwa na doa ktk utawala wake..
Fikra za watu kama Costro, Che, MLK, Ghandi, Nkurumah pamoja na kwamba wao hawakuleta maendeleo ya haraka kiuchumi kutokana na sababu nje ya uwezo wao haina maana fikra zao tangulizi hazina maana. Hata kama tutasema zilikuwa hazina maana then kwa nini sisi tusionyehse zile zenye maana na kuonyesha changes za haraka kutokana na kusahihisha makosa yake ikwa bado hatujasahihisha makosa hayo na inakuwaje tunayaona mabaya ya wakati ule hali bado yanaendelea hadi leo hata kama yuko kaburini ama bado anaongoza akiwa kaburini! Oooh nimesahau ni fikra za mwalimu bado zinadumishwa au sio....which one?

Hukumu yenu yote kwa Nyerere ni sawa na kumlaumu mwanamke anayeitaka taraka kutoka ktk ndoa ilijaa abuse, kisha tuna hukumu maamuzi yake kuwa hayana busara kwa kutazama maisha ya huyo mwanamke kiuchumi baada ya kuachika...Na kweli ndivyo waswahili huwa tunatazama.. kama mwanamke ka punch baada ya ndoa tutasema alifikiria la maana sana, hali yake ikiwa mbaya tunamcheka na kusema kwani abuse nini ikiwa mtu ulikuwa unakula kuku kwa mrija utumwani - mjinga tu..

Miaka 23 Ya Nyerere tuliyaona mabaya na mazuri yake miaka 24 baada yake tunachokiona zaidi ni gap kubwa kati ya matajiri na maskini...na hakuna kiongozi hata mmoja aliyezungumzia tahadhali ya viongozi wetu kujitajirisha ktk hali hii isipokuwa Nyerere. Tena naweza diriki hata Kusema hao kijna Mtei wenyewe walifikiria hali kama hii haiwezi tokea chini ya mfumo wa Kibepari... wao waliona ni win win situation kama anavyosema JK.. Kisha cha ajabu basi huyo Mtei mwenyewe kisha yaona makosa ya CCM ndani ya mfumo huu mpya na ndio maana kawa mpinbzani wa CCM sio kwa sababu ya Ujamaa bali kwa sababu ya wizi wao...Hivyo basi sio policy pekee inayotuangusha sisi isipokuwa ni mazingira yetu (ardhi), viongozi na siasa mbaya vyote vinachangia ktk kudumaza uchumi wa nchi yetu..Less of any of that hakuna mafanikio...

At least Nyerere aliweza kutuasa kuhusu mazingira kama haya ya kiuchumi tukafunga mikanda kwa miaka 17, kwa sababu ya kuhofia hali kama hii ambayo leo inajitokeza kwa kasi ya ajabu miaka 40 baada.

Mkandara,

asante sana kwa hayo kweny bold. Watu wametamka sana kuhusu ujamaa na ubepari. Kuna swali hapa limeulizwa kuwa ni nchi ngapi leo duniani zinatawaliwa kibepari? Hakuna hata mmoja aliyetoa jibu.

Unajua kuna logic sana kwenye hii thread ya Mwanakijiji. Ingawa watu wengi wanadhani kuwa ujamaa ulikuwa mbovu na wanamlaumu Nyerere kwa hilo. Dunia ya leo inaongozwa na sera za kijamaa zaidi kuliko za kibepari.

Kumbuka hapa naongelea socialism na sio communism. Nyerere alitaka sera za ujamaa (socialims) na hili ndilo swali la Mwanakijiji kama hizi fikra za Nyerere zilizovutiwa zaidi kwenye utaifa na ujamaa zilikuwa na mafanikio na mapungufu gani?
 
itabidi niachane na huu mjadala kwa sasa maana naona mwenzangu umepania!!! tusi gani ambalo nimetukana??? upo busy na technicalities badala ya substance, wewe lawyer nini??

Sidhani kama unataka nicopy post yako uliyoniita mimi bwege na mbwiga sijui mbwinga?

nimetumia sisi kwa makusudi kabisa, kwani hapa ninapo pinga nyerere nipo serious......its personal to say the least!!!! hata usemaje, kwa upande wangu hakuna kitakachobadilika kuhusu nyerere.

kama issue hapa ni ushindi, basi mmeshinda, lakini miaka mia ijayo kizazi hicho kitatuhukumu......i hope mawazo yangu yata prevail!!

Sidhani kama mimi nataka ushindi hapa zaidi ya kuzuia sumu zako unazotaka kumwaga dhidi ya mtu aliyekufa miaka zaidi ya 10 iliyopita na unayetaka kumlaumu kwa kila baya linaloendelea leo.

Wewe baki na msimamo wako ila pia nakukumbusha kuwa kama wote tukianza mchezo wa kulaumu viongozi waliopita, Nyerere atalaumu wakoloni, Mwinyi atamlaumu Nyerere, Mkapa atamlaumu Mwinyi na Nyerere, Kikwete atalaumu viongozi wote waliopita (kama vile anafanya sasa hivi) na mchezo utaendelea mpaka mwisho wa kiama
 
sasa naelewa kwanini, mapema ulikwaruzana na mwafrika wa kike!!! una issues......nitajaribu kuku avoid!! mgumu sana wa kuelewa na ni trouble maker. goodluck!!

Watu wengi wanajua hapa kuwa mwafrika wa kike ana mambo yakitoto na yeye na mwenzake Kada Mpinzani wanachafua mada za watu hapa. Sidhani kama unataka kuchukua upande wake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom