Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Mwafrika;

Nimeeleza sheria ilivyo tumika kabla na baada ya Nyerere. Umeweka sahihisho langu hapo lakini sioni unachotaka kusema. Umeshtuka kuona mtu anarekebisha makosa? Hivyo ndivyo viwango nilivyo jiwekea ninapokuwa najadili hoja. Najiwajibisha nikikosea hata neno moja. Sibishi bishi bure tu!

Hata ulivyojisahihisha, uliendelea kutumia mwaka 1982 na bado ukasema tofauti na kilicho kwenye real act yenyewe. Nilikushauri mwanzoni upate fact kabla ya kuongea hapa JF maana hapa ni facts tu na sio ubishi usio na data!

Je uko tayari kujisahihisha kwa mwaka na content ya act?
 
Mwanakijiji;
Kabla ya kuanza kubisha bila kufikiri, jua unatetea sheria zinazotumiwa na Mafisadi.
Kasome kurasa chache hapo nyuma kuhusu haja ya watu kuheshimi sheria hata kama hawazipendi; na kama hawazipendi na ni sheria halali basi wanafanya jitihada ya kuzibadilisha. Patriot Act ya Marekani ni mojawapo ya sheria ambazo kwa wengine ni very draconian kuliko hiyo ya kwetu na zimefanyika juhudi nyingi za kuibadilisha siyo kutoitii.

Sheria ya Prevention and Detention ni sheria halali ya nchi yetu na kama tunaamini (rightly so) kwamba kuna vitu ambavyo vimepitwa na wakati basi ni jukumu letu kuihakikisha inabadilishwa.

Ni mzuka wa hii sheria ndio ulifanya watu wa Jambo Forums wawekwe kizuizini kwa kushukiwa kutishia amani za Mafisadi.

Kama kuna kitu kilichofanywa nje ya sheria basi tunakiangalia, kama walifanya kitu ndani ya sheria halali hata kama hatuipendi ni sheria halali na ni jukumu letu kuonesha kuwa sheria hiyo licha ya kuwa ni halali lakini ni mbaya. Bado haijaoneshwa kuwa Nyerere alifanya kitu nje ya sheria!

Weka ushindani na jazba pembeni kidogo. Hii sheria imetumika kufunga watu bila hatia kama ukidhaniwa.

Nipe mfano wa watu kufungwa kwa kutumia sheria hii "kama ukidhaniwa". Nitajie mtu aliyewekwa kizuizini kinyume cha sheria iliyopo.

Kwa maneno mengine kushukiwa ni makosa, ni hatia. Ni tafsiri yangu mimi. Wanaosoma juu juu wanadhani nimenukuu uongo, na wewe unajua watu waliopanda mkokoteni wako wote watupu kwa hiyo wataenda na vile ulivyo watafsiria nilichosema. Lakini kuna wenye akili humu wananielewa vizuri.

mwanzoni ulisema sheria "inasema" kisha ukasema "ina maana" sasa unasema "kwa maneno mengine". Sheria inatumia lugha za kisheria na maana yake hujulikana mahakamani. Hakuna cha "maneno mengine" zaidi ya yale yaliyomo ndani ya sheria hiyo.

NYALALI COMMISION
The Act has constantly been abused by Regional and District Commissioners and the Police. Further that it has become a weapon to silence political opposition as well as common means used by the police to combat ordinary crimes in the country.

Mbona Hakusema imekuwa abused na Rais.?

The Commission concludes that the Act violates the provisions of Article 17(1) of the Constitution which guarantees freedom of movement and recommended that the Act as amended by Act No.2/1985 be repealed.

good point na wengi tumeililia sheria hii kufutwa pamoja na ile ya Usalama wa Taifa na ile ya Magazeti ya 1976. Hicho ndicho watu hufanya kwa sheria yoyote mbaya au iliyopitwa na wakati. Kwa sasa hivi sheria hii ya kikoloni bado ipo na Rais Kikwete kama vile Mkapa na Mwinyi kabla yake wana uwezo huo huo wa sheria.

Mbona mimi ulivyo kataa vidhibiti vyangu vya hii sheria, nilikwambia haya sina zaidi, nipe vyako, hukuja navyo? Ukataka nikuombe, lakini bado tu. Unafagiliwa fagiliwa humu ndani huku una tabia za kitoto, halafu mtupu tu. Watu wanakuheshimu kwa sababu wanadhani una umaarufu wa ki Podocast kwa hiyo unajua unachokisema, kumbe mtupu tu. Na kama ndio wewe kweli, ki Podocast chako ni mdosho ile mbaya. Sikiliza NPR Radio wanavyo uliza maswali. Na uache kusema sema ‘ndio, ndio’ katikati ya jibu la mhojiwa! Haya waambie wakadiri wa Jambo Forums wafute tundiko hili na wanifukuze!

ukishindwa hoja ulete vihoja! inaitwa ad hominem.. karibu kwenye klabu cha walioshindwa hoja!

Vidhibiti unavyo vitaka vya kuporomoka kwa uchumi wa Nyerere vinakuja. Dili kwanza na hii ishu. Na naomba fikiri kwanza!

Kwa maneno yako mwenyewe umethibitisha kuwa Nyerere hakufanya kitu chochote kinyume cha sheria ambayo yeye mwenyewe hakuitunga!
 
Mwanangu hizi draconic acts walizirithi kutoka kwa "Governor General" enzi ya ukoloni, wakabadilisha kutoa wakoloni weupe kuleta wakoloni weusi.

Civil Societies the world over wanazipigia kelele sheria hizi.Mungu ambariki yule babu Nyalali kwa maana katika watu waliokuwa wanaweza kusimamia "checks and balance" Tanzania Nyalali alinifurahisha sana, mpaka wanasiasa walimuogopa.Sio siku hizi.

Yaani sheria hizi hizi ndizo zilitumika ku oppress TANU na baba kabwela, halafu watu wanataka kutetea nini?

Wewe wa kuitwa Pundit, aksante mwanangu!

Nilijua - na nilisema - kuna watu wananielewa humu. Kumbe mmeuchuna, mi nasulubishwa utafikiri nimedai mimi Mfalme wa Wayahudi. Mlidhani nimetoa mi data ya uongo! La Hasha. Ni Mwanakijiji anawatafsiria watu nilichosema.

Duh, kazi ipo!
 
Hii ni JF, ukileta data za uongo na kudai kuwa ni za kweli unapewa ukweli ili next time uwe makini kidogo. Usilaumu yeyote kwa kinachokutokea hapa.

Leta data kama wenzako na utakuwa very safe
 
Mwanangu hizi draconic acts walizirithi kutoka kwa "Governor General" enzi ya ukoloni, wakabadilisha kutoa wakoloni weupe kuleta wakoloni weusi.

Civil Societies the world over wanazipigia kelele sheria hizi.Mungu ambariki yule babu Nyalali kwa maana katika watu waliokuwa wanaweza kusimamia "checks and balance" Tanzania Nyalali alinifurahisha sana, mpaka wanasiasa walimuogopa.Sio siku hizi.

Yaani sheria hizi hizi ndizo zilitumika ku oppress TANU na baba kabwela, halafu watu wanataka kutetea nini?

Pundit, nadhani unaelewa vibaya kinachotetewa hapa; mimi ni mtu wa kwanza kabisa kupinga sheria tatu ambazo ni za hatari kabisa TAnzania, hiyo ya Prevention and Detention, ya National Security na ya Magazeti. Sizitetei kwa sababu najua athari zake zinapopata kiongozi au mtu anayetaka kuzitumia vibaya.

Baada ya Uhuru Taifa lilihitaji sheria kali na zenye kuhakikisha TAifa linajengwa na linakuwa salama. Hakuna nchi ambayo inasheria ambazo zitaangamiza Taifa hilo au serikali iliyoko madarakani. Jambo la msingi wakati wote ni kuhakikisha kama ulivyosema kuna civil society ambazo inalilia balance ili watawale wasijibebeshe nguvu zaidi na kugeuka madikteta.

Lakini sheria za namna hiyo zinabadilishwa kwa kutumia utaratibu wa kisheria aidha kwa njia ya kawaida au hata kwa kutumia political pressure na kuna wakati ambapo watu wanaweza kutumia nguvu kupinga sheria za kiukandamizaji.

Sasa, kama mtu ataonesha kuwa Nyerere alifanya kitu kinyume cha sheria zilizokuwepo hiyo ndiyo argument ya kuiangalia; lakini hata hivi sasa kuna watu wanapinga vipengele kadhaa vya Patriot Act lakini hata wale wanaopinga kwa wakati huu they have to obey it wakati wakifanya kazi kuibadilisha.

Sheria ya Detention kama ulivyosema tuliirithi kwa Wakoloni (mojawapo ya sheria tulizozirithi) na ukiangalia tunakotoka yawezekana ilikuwa muhimu tuwe nayo wakati wa kuanza kwa jamhuri yetu; Wakati anakaribia kuondoka yeye mwenyewe Nyerere alihakikisha inabadilishwa kwa sababu alijua kuwa nguvu iliyomo ndani yake inaweza kumgeuza mtu yeyote kuwa Dikteta (hata yeye). Ndio maana alihakikisha inabadilishwa kabla hajaondoka ili isije kutoa mwanya kwa viongozi wa baadaye. Huyo anaitwa kiongozi.

Hawa waliopo sasa kwanini wasiamua kuifuta? Jaji Warioba yupo leo hii mbona hajakampeni kuona inabadilishwa? Wabunge wa CCM ambao ndio wanaweza kuhakikisha sheria hii inafutwa mbona hadi leo miaka zaidi ya ishirini toka Nyerere afanyie mabadiliko ya mwisho kwanini haijafanyiwa mabadiliko? Si wao wamepitisha sheria ya Anti-Terrorism?
 
Naamini kuna uwoga wa aina fulani wa kukubali kuwa fikra za Nyerere kwenye maeneo mengi zilikuwa bora kuliko fikra ambazo ziko sasa ambazo kiini na msingi wake ni ubinafsi uliobobea. Fikra bora ni bora regardless nani alikuwa nazo.

Uoga mkuu unatokana na wananchi wengi kama mimi ambao tunajua kuwa mbegu za ubinafsi zilipandwa na Mwalimu mwenyewe, hasa mwishoni mwa urais wake na hata alipokuwa akituongoza akiwa nje ya madaraka, kwanza kwa kutuchagulia Mwinyi, Mkapa, na kumpa okay muungwana kumsubiri Mkapa kwanza ndio zamu yake ije, haya yote alikuwa akiyafanya against our will, yaaani wananchi karibu millioni 35 wa Tanzania,

Again, ubinafsi wake unaonyeshwa pia kwenye kitendo chake cha kumpa okay Salmini kubadili matokeo ya uchaguzi Visiwani, ambako ilishatangazwa rasmi kuwa upinzani umeshinda, na hata naibu katibu mkuu wa CCM kule then Ameir kutangaza kuwa CCM iakwenda mahakamani kupinga matokeo ya ucgauiz ule, lakini baada ya masaaa kadhaaa kamati ya uchaguzi ikatangaza kuwa ni CCM walioshinda na sio upinzani, kama vile Mugabe ambavyo amekuwa akifanya Zimbabwe,

Now hizi ni mbegu za ubinafsi ambazo Mwalimu mwenyewe alizipanda, ambazo hazihusiani kabisa na sera za itikadi na intellectual zake, lakini viongozi wote waliofuatia wamekuwa wazuri sana kwenye kuziiiga, ubinafsi aliuanzisha Mwalimu hawa wa sasa wanauendeleza tu mkuu, na ni moja ya tatizo kubwa la Mwalimu, kuacha mazuri yake ambayo ni mengi pia, lakini ubinafsi lilikuwa ni tatizo lake pia, ingawa ubinafsi wake haukuwa kwenye ufisadi, lakini ukishapanda mbegu sio lazima zibaki kwenye box la kuiba kura tu na pia huwezi kuzi- control tena.

Ahsante!
 
Inaonekana CCM kuna watu waoga sana ambao hawakuweza, hawawezi na hawataweza kamwe kupingana na sera za Mwalimu. Kama yote ya leo hii yaliletwa na Mwalimu, basi kuna sababu ya kufuta CCM toka kwenye katiba, registration, vitabu vya siasa, na kila kitu nchini ambacho kinataja CCM ili kuondoa kabisa sumu ya Nyerere na labda taifa la watanzania milioni karibu arobaini litapata uhuru finally.
 
Ahsante mkuu, kwani sasa unakubaliana kabisa na mimi kuwa kiongozi wa kulisaidia taifa letu kusonga mbele, ni yule atakaye achana kabisaa na mawazo ya Mwalimu, in any way or form,

na taifa hili tunapaswa kuwa macho sana na kiongozi yoyote mwenye mawazo ya Mwalimu, ya ujamaa ujamaa na fikra za itikadi zake maana ni hatari sana kwa taifa, na huishia ku-create ubinafsi wa hali ya juu, kuliko hata ule unaokubaliwa kwenye mfumo wa ubepari, matokeo yake ni kulifikisha taifa kama letu kuwa lilipo sasa.
 
Sijakubaliana nawe katika angle hii zaidi ya kukupa ushauri utoke ccm maana imeshindwa kabisa kuachana na mambo ya nyerere miaka yote hii baada ya kifo chake hata pamoja na wewe kusema kuwa unajua mabaya yote ya mwalimu. Unataka kupata both sides?
 
Hapana siwezi kutoka CCM, maana siwezi kuingia upinzani wa Tanzania ambao sielewi kabisa unasimamia nini zaidi tu ya uchaguzi.

CCM ni safi isipokuwa tu ina baadhi ya viongozi wabovu na waliooza, wanatakiwa kuondoka wenyewe au kuondolewa mara moja, otherwise ni chama makini sana, lakini pia tunahitaji kuwapa moyo wanachama wote wa CCM ili waachane na tabia ya uoga uoga ambayo walikuwa wamefundishwa na kuwa nayo kwa muda mrefu sana, tunahitaji kuwaambia kuwa kwanza Tanzania ni a freee country, na kwamba Mwalimu baba wa taifa, sio rais tena na hatakuja kurudi tena kwa hiyo wasihofu kwenye kutoa au kuyapitisha maamuzi mema kwa taifa letu.

Ahsante mkuu.
 
Hili ndilo swali linalosumbua... kama CCM na viongozi wake ni waoga, wavivu wa kufikiri na wanagwaya mbele ya mzimu wa mtu aliyekufa miaka hiyo yote kwanini bado wanaendelea kuwa madarakani na kushikilia kadi?

Waliotuletea matatizo ni viongozi wote wa CCM ambao walishindwa kumsimamia Nyerere na kumpinga kwa sababu ya woga wao! Leo hii MDC chini ya Morgan wameweza kusimama na kukubali kibano na leo tuna ZANUPF inatetemeka, viongozi wetu sisi walikuwa wapi?

Yaani mtu mmoja dhidi ya watu milioni 35? aidha he was a genious or an incredible mind maana ukijumlisha viongozi wote ambao wamepitia chini ya mkono wa Mwalimu na wakaona mabaya yake mbona hakuna aliyeweza kudinda.. hata Fundikira na Kasanga Tumbo wote wakajikuta wamerudi CCM!!!
 
Hapana siwezi kutoka CCM, maana siwezi kuingia upinzani wa Tanzania ambao sielewi kabisa unasimamia nini zaidi tu ya uchaguzi.

Kutoka ccm sio lazima uingie upinzani. Unaweza kuprotest uovu na sera za ccm. Kukaa ndani ya ccm na bado hujafanya chochote kile kubadilisha ccm basi hii inakutafsiri vizuri kuliko maandishi yako.

CCM ni safi isipokuwa tu ina baadhi ya viongozi wabovu na waliooza, wanatakiwa kuondoka wenyewe au kuondolewa mara moja, otherwise ni chama makini sana, lakini pia tunahitaji kuwapa moyo wanachama wote wa CCM ili waachane na tabia ya uoga uoga ambayo walikuwa wamefundishwa na kuwa nayo kwa muda mrefu sana, tunahitaji kuwaambia kuwa kwanza Tanzania ni a freee country, na kwamba Mwalimu baba wa taifa, sio rais tena na hatakuja kurudi tena kwa hiyo wasihofu kwenye kutoa au kuyapitisha maamuzi mema kwa taifa letu.

Ahsante mkuu.

Kama CCM nzima inaweza kukaa kikao muhimu kama cha juzi cha Butiama na kisitoe hata tamko moja la kukemea ufisadi nchi au kutoa hatua kali kwa walioshukiwa na ufisadi, basi huo usafi wa ccm ni wa maneno zaidi kuliko matendo.

Inaonekana kuwa ingawa unampinga Nyerere lakini ccm unayoitetea bado inatoa maneno tu bila vitendo. Na wewe kutofanya chochote kuhusu ufisadi basi inaonekana nawewe bado unafuata kile ambacho unadai Nyerere alifanya!
 
Hili ndilo swali linalosumbua... kama CCM na viongozi wake ni waoga, wavivu wa kufikiri na wanagwaya mbele ya mzimu wa mtu aliyekufa miaka hiyo yote kwanini bado wanaendelea kuwa madarakani na kushikilia kadi?

Waliotuletea matatizo ni viongozi wote wa CCM ambao walishindwa kumsimamia Nyerere na kumpinga kwa sababu ya woga wao! Leo hii MDC chini ya Morgan wameweza kusimama na kukubali kibano na leo tuna ZANUPF inatetemeka, viongozi wetu sisi walikuwa wapi?

Thanks very much,

Wote ndani ya ccm wanagwaya na kuogopa mzimu wa mtu aliyekufa. Hii inathibitisha kuwa ubovu ni wanaccm wenyewe na wala sio Nyerere. Ingekuwa ni Nyerere basi kungekuwa na mabadiliko miaka kumi baada ya kifo chake.

Yaani mtu mmoja dhidi ya watu milioni 35? aidha he was a genious or an incredible mind maana ukijumlisha viongozi wote ambao wamepitia chini ya mkono wa Mwalimu na wakaona mabaya yake mbona hakuna aliyeweza kudinda.. hata Fundikira na Kasanga Tumbo wote wakajikuta wamerudi CCM!!!

Na bado wanadai kuwa ccm ni safi! Ajabu kubwa sana
 
Hapana siwezi kutoka CCM, maana siwezi kuingia upinzani wa Tanzania ambao sielewi kabisa unasimamia nini zaidi tu ya uchaguzi.

Kwanini usianzishe upinzani wako wewe mwenyewe au kuongoza mawazo ya kinyume na CCM nje ya CCM siyo lazima uwe upinzani.
CCM ni safi isipokuwa tu ina baadhi ya viongozi wabovu na waliooza, wanatakiwa kuondoka wenyewe au kuondolewa mara moja, otherwise ni chama makini sana,

mzee CCM iliwahi kuwa safi lakini si safi tena na viongozi wabovu na waliooza wamejaa tele na wenyewe tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia leo hii. Nadhani viongozi wa safi wa CCM wako kwenye ngazi ya kata au mashina..

l
akini pia tunahitaji kuwapa moyo wanachama wote wa CCM ili waachane na tabia ya uoga uoga ambayo walikuwa wamefundishwa na kuwa nayo kwa muda mrefu sana, tunahitaji kuwaambia kuwa kwanza Tanzania ni a freee country, na kwamba Mwalimu baba wa taifa, sio rais tena na hatakuja kurudi tena kwa hiyo wasihofu kwenye kutoa au kuyapitisha maamuzi mema kwa taifa letu.

Mzee kama wanachama hawa hadi sasa hawajaelwa kuwa TAnzania ni nchi huru hakuna elimu au chuo kitakachoweza kuwasaidia kutambua hilo. NI wakati wao wao kuachana na Misri ya TAnzania. Hata wana Israel hawakuhuburiwa uzuri wa Kanaani wakiwa Misri na kufundishwa ubaya wa Farao, waliuona na wakati wa kutoka waliondoka hata bila kuaga.

Wana CCM ambao wanaona maovu ya CCM na wanayakubali ni wao wanatoa baraka ya uovu huo!
 
1.
Hili ndilo swali linalosumbua... kama CCM na viongozi wake ni waoga, wavivu wa kufikiri na wanagwaya mbele ya mzimu wa mtu aliyekufa miaka hiyo yote kwanini bado wanaendelea kuwa madarakani na kushikilia kadi?

Ni kwa sababu waligundua siku nyingi kuwa ukitaka kuwadanganya wananchi ni rahisi kutumia maneno ya Mwalimu, na kumleta Kawawa ili athibitishe hayo, lakini pole pole tunaanza ku-make a progress ili kubadili hiyo tabia iliyopandwa kwa karibu miaka 23.

2.
Waliotuletea matatizo ni viongozi wote wa CCM ambao walishindwa kumsimamia Nyerere na kumpinga kwa sababu ya woga wao! Leo hii MDC chini ya Morgan wameweza kusimama na kukubali kibano na leo tuna ZANUPF inatetemeka, viongozi wetu sisi walikuwa wapi?

Mkuu wangu umesahau kuwa viongozi wetu ni sisi wenyewe wananchi?

3.
Yaani mtu mmoja dhidi ya watu milioni 35? aidha he was a genious or an incredible mind maana ukijumlisha viongozi wote ambao wamepitia chini ya mkono wa Mwalimu na wakaona mabaya yake mbona hakuna aliyeweza kudinda.. hata Fundikira na Kasanga Tumbo wote wakajikuta wamerudi CCM!!!

Unajua kuna viongozi wasiokuwa na ubinafsi waliompa nafasi Mwalimu, bila kinyongo kuwa mwenyekiti wa TANU, ambayo waliianzisha bila yeye, lakini alipopewa tu akaanza kuonyesha wazi ubinafsi wake, kwa kuwaondoa wale wote waliompa nafasi in the first place, na kuanza kuwaweka wale tu wanyonge wa kufikiri, tabia aliyoiendeleza kwenye maisha yake yote ya utawala wake ya kuwafanya viongozi kutojiamini, wale walioonyesha kujiamini akawaundia majungu na uzandiki kila kona kwa kuwatumia wale wanyonge wa kufikiri, akaa-create taifa la wananchi waoga, wanafiki, wavivu wa kufikiri, wavivu wa kazi wakisubiri serikali, akaufanya uongozi kuwa ni kina fulani tu wenye uwezo mdogo wa kufikiri, akaweka kila kitu cha serikali mikononi mwake, mlo ukawa unategemea yeye tu, taifa lisilokuwa na sheria, maana sheria ikaishia kuwa yeye, waliobisha angalau kidogo kina Jumbe, Seif, Seif Bakari, Masha, Kambona, na wengineo tunajua yaliyowakuta,

Tizama sasa taifa alilotuachia, Mungu Ibariki Tanzania yetu!
 
1.

Ni kwa sababu waligundua siku nyingi kuwa ukitaka kuwadanganya wananchi ni rahisi kutumia maneno ya Mwalimu, na kumleta Kawawa ili athibitishe hayo, lakini pole pole tunaanza ku-make a progress ili kubadili hiyo tabia iliyopandwa kwa karibu miaka 23.

Ni miaka kumi imepita tangu kifo cha Nyerere na hii inathibitisha kuwa tatizo ni la ccm na wanachama wa ccm na wala sio Nyerere.

2.

Mkuu wangu umesahau kuwa viongozi wetu ni sisi wenyewe wananchi?

3.

Juzi nimekumbushwa kuwa halimashauri ya Tarime (kilomita chache tokea Butiama) inaongozwa na Chadema. Nimekumbushwa kuwa mwaka 1995 mkoa wa Mara walichagua upinzani kwa wingi sana (kuna stori kuwa wapinzani walishinda mkoa wote ila wakaibiwa kura).

Hii inaonyesha kuwa watu wa karibu na Nyerere wamegundua kuwa tatizo ni ccm na sio wananchi wenyewe. CCM ndio tatizo la Tz na wala sio watanzania wenyewe.

Unajua kuna viongozi wasiokuwa na ubinafsi waliompa nafasi Mwalimu, bila kinyongo kuwa mwenyekiti wa TANU, ambayo waliianzisha bila yeye, lakini alipopewa tu akaanza kuonyesha wazi ubinafsi wake, kwa kuwaondoa wale wote waliompa nafasi in the first place, na kuanza kuwaweka wale tu wanyonge wa kufikiri, tabia aliyoiendeleza kwenye maisha yake yote ya utawala wake ya kuwafanya viongozi kutojiamini, wale walioonyesha kujiamini akawaundia majungu na uzandiki kila kona kwa kuwatumia wale wanyonge wa kufikiri, akaa-create taifa la wananchi waoga, wanafiki, wavivu wa kufikiri, wavivu wa kazi wakisubiri serikali, akaufanya uongozi kuwa ni kina fulani tu wenye uwezo mdogo wa kufikiri, akaweka kila kitu cha serikali mikononi mwake, mlo ukawa unategemea yeye tu, taifa lisilokuwa na sheria, maana sheria ikaishia kuwa yeye, waliobisha angalau kidogo kina Jumbe, Seif, Seif Bakari, Masha, Kambona, na wengineo tunajua yaliyowakuta,

Tizama sasa taifa alilotuachia, Mungu Ibariki Tanzania yetu!

Haya yote yameongelewa hapa na ikaonekana kuwa hawa watu wengi wao walikuwa na matatizo yao wenyewe na wala sio Nyerere. Na hata kama hii ilikuwa ni kweli, je miaka yote tokea kifo cha Nyerere, ni nani ambaye anawafanyia fitina hawa kina Kambona? au ni yaleyale ya Lowasa na mwenzake kusema kuwa watu wa meru wanaonewa ccm wakati wanajua kabisa uovu waliofanya?
 
1.

Ni kwa sababu waligundua siku nyingi kuwa ukitaka kuwadanganya wananchi ni rahisi kutumia maneno ya Mwalimu, na kumleta Kawawa ili athibitishe hayo, lakini pole pole tunaanza ku-make a progress ili kubadili hiyo tabia iliyopandwa kwa karibu miaka 23.

sasa kama hili ni kweli basi angalau tunajua tatizo letu liko wapi.

Mkuu wangu umesahau kuwa viongozi wetu ni sisi wenyewe wananchi?

Mbona mnamlaumu Nyerere kama uongozi ni sisi wenyewe au una apply kwa viongozi wengine lakini ikifika kwa nyerere "kiongozi" ni yeye. Badala ya kumlaumu Nyerere kama chanzo cha matatizo yetu tukubaliani ni wananchi wenyewe na viongozi wengine wote ndio chanzo cha matatizo yao!

Unajua kuna viongozi wasiokuwa na ubinafsi waliompa nafasi Mwalimu, bila kinyongo kuwa mwenyekiti wa TANU, ambayo waliianzisha bila yeye, lakini alipopewa tu akaanza kuonyesha wazi ubinafsi wake, kwa kuwaondoa wale wote waliompa nafasi in the first place, na kuanza kuwaweka wale tu wanyonge wa kufikiri, tabia aliyoiendeleza kwenye maisha yake yote ya utawala wake ya kuwafanya viongozi kutojiamini, wale walioonyesha kujiamini akawaundia majungu na uzandiki kila kona kwa kuwatumia wale wanyonge wa kufikiri, akaa-create taifa la wananchi waoga, wanafiki, wavivu wa kufikiri, wavivu wa kazi wakisubiri serikali, akaufanya uongozi kuwa ni kina fulani tu wenye uwezo mdogo wa kufikiri, akaweka kila kitu cha serikali mikononi mwake, mlo ukawa unategemea yeye tu, taifa lisilokuwa na sheria, maana sheria ikaishia kuwa yeye, waliobisha angalau kidogo kina Jumbe, Seif, Seif Bakari, Masha, Kambona, na wengineo tunajua yaliyowakuta,

angalia watoto wa kina Masha wako wapi sasa, watoto wa Kambona wanafanya nini kuendeleza legacy ya baba yao; mtoto wa Tumbo yuko wapi leo hii, hata Seif mwenyewe amefanya nini zaidi ya kutumia karata za vitisho!

Haiwezekan mtu mmoja afanye hayo yote mbele ya watu wenye akili. Aidha Nyerere alikuwa ni genius au wote waliomzunguka walikuwa ni waoga na watu ambao siyo tu hawakustahili uongozi inabidi wabebeshwe mzigo wa matatizo yetu. Walikuwa wapi kina Morgan wetu. Mbona Morgan hajakimbia Zimbabwe au kufyata mkia... Hao unaowasema ndio watu walitarajiwa kuliongoza Taifa na kwa maneno yako unasema wazi kuwa Nyerere hakuwa na watu wa kuweza kutekeleza na kuliinua Taifa na nakubaliana nawewe labda ni kizazi chetu ndicho kitaleta mabadiliko hayo, wakati wa wazee wa CCM kuendelea kutoa mawazo yao ya kivivu umekwisha.

Turudi kwenye kulijenga TAifa letu!!!
 
Agreed Mkuu FMES

Ndio maana tunasema it takes someone/all of us to say NO to ubinafsi na miujiza yote inayoambatana nayo hivi sasa................lakini inaelekea watu bado tumefungwa katika box la ubinafsi ambao unadai ulipandikizwa na Mwl JKN........very suprising bado tunaendeleza ubinafsi!!.....na ndio maana nakubaliana na usemi wako kuwa yote yatokeayo sasa ni reflection yetu wenyewe

Mwl JKN alikiri kuwa yalikuwepo mazuri aliyoyaanzisha na basi tuyadumishe na ikiwezekana yawe bora zaidi........yale yaliyo mabaya tuyarekebishe/kuyaacha na kuchukua mfumo mpya.............Now look at what we are doing to our economy (doomed hell)........yaani kundi fulani limeamua kuliibia taifa.......we can not just sit aside........saying.........Yes one of the things Mwl JKN alivyotuachia ni Ubinafsi.........si atleast alituambia tuache yale mabaya.......whats is wrong with us then.

Nakubaliana nawe pia kuwa Viongozi wabovu CCM watoke....na wa kuwaondoa i believe wewe ni mmoja wao unayesema NO to Ubinafsi

sorry mwanakijiji......kwa kutoka nje ya mjadala
 
....

Mbona mnamlaumu Nyerere kama uongozi ni sisi wenyewe au una apply kwa viongozi wengine lakini ikifika kwa nyerere "kiongozi" ni yeye. Badala ya kumlaumu Nyerere kama chanzo cha matatizo yetu tukubaliani ni wananchi wenyewe na viongozi wengine wote ndio chanzo cha matatizo yao!

......

Hili ni swali ambalo nimejiuliza pia. Ikifikia viongozi wa sasa wakifanya "makosa" basi inasemwa kuwa viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe.

Ikifikia watu baadhi kusema kuwa Nyerere alikosea basi inasemwa kuwa ni makosa ya Nyerere na wala sio yetu wenyewe. Hii ni kazi kubwa sanaa.
 
1.
Kwanini usianzishe upinzani wako wewe mwenyewe au kuongoza mawazo ya kinyume na CCM nje ya CCM siyo lazima uwe upinzani.

Pole pole mkuu, hatujui mbele ya safari itakuwaje, lakini mimi ninajaribu tu kutoa maoni yangu kuhusiana na utawala wa Mwalimu, na impact ya mazuri na mapungufu yake kwa taifa langu, na ninajifunza m,engi toka kwa wale wanaodhani kuwa alikuwa malaika.

2.
mzee CCM iliwahi kuwa safi lakini si safi tena na viongozi wabovu na waliooza wamejaa tele na wenyewe tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia leo hii. Nadhani viongozi wa safi wa CCM wako kwenye ngazi ya kata au mashina..

Hapana CCM siku zote imekuwa safi kwa maandishi na maneno tu, na hiyo imetokana na kuongozwa na kiongozi aliyekuwa na maneno mazuri lakini matendo hakuna.

3.
Mzee kama wanachama hawa hadi sasa hawajaelwa kuwa TAnzania ni nchi huru hakuna elimu au chuo kitakachoweza kuwasaidia kutambua hilo. NI wakati wao wao kuachana na Misri ya TAnzania. Hata wana Israel hawakuhuburiwa uzuri wa Kanaani wakiwa Misri na kufundishwa ubaya wa Farao, waliuona na wakati wa kutoka waliondoka hata bila kuaga. Wana CCM ambao wanaona maovu ya CCM na wanayakubali ni wao wanatoa baraka ya uovu huo!

Hadithi ya Wana-Israeli, ndio unapaswa kuwa mfani mzito kwa wananchi wa Tanzania, kuwa Freedom ni very expensive, maana hata Farao hakuutoa kwa hiari, na Mungu kwa kuwatumia wao chanzo cha kuzaliwa kwa neno Freedom, wananchi wetu bado hawajaelewa maana wangekuwa, basi CCM isngeshinda Tunduru na Kiteto, wa kulaumiwa ni sisi ambao we know better kwa kutowaamsha mapema,

Mimi na CCM na ndio maana nipo hapa JF kwa sasa, nikikemea maovu na ninajua kuwa I am on the right track kwa sababu ya yaliyoikuta JF hivi karibuni, that is all I can do for now as far as kukemea uovu ndani ya chama changu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom