Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,272
- 144,437
Ingekuwa hili swali la Fikra za Mwalimu ni swali katika mtihani, wengi wangefeli kutokana na majibu yaliyotolewa humu ndani.
Swali lililenga Fikra na si Sera (Vision not Policy)! Majibu ya knee jerk reaction yamekuwa kuhusiana na policy na si Vision.
Hata bandiko la awali la kumnukuu Mwalimu lilikuwa ni kuhusiana na theme ya maneno yale na uwiano wake katika mazingira tuliyomo.
Kama kawaida, ndivyo tulivyo que sera sera, tumekimbilia kuwa subjective kutokana na hisia zetu hasi kuhusiana na Mwalimu Nyerere na kushindwa kuwa objective na kujibu swali kuhusu Fikra zilizobandikwa.
Naungana na Bob Mkandara kuwa hii ni aibu sana kwa sisi ambao tunajiita "Wasomi" na "Elite" kama tunashindwa kujibu masali na hoja kama zilivyoulizwa na kukimbilia kutoa majibu ya hisia zetu na chuki juu ya Nyerere.
Hivyo basi, wengi wetu tumeshindwa jibu ama kuzikubali Fikra zilizoletwa au kuzipinga kwa kuonyesha ni vipi zinaweza tumika au haziwezekani kabisa. Kama tulifikiri tumepata Msonge, tujiangalie tena tumezungusha Sifuri hivyo pepa ni F (FAIL)!
Mimi nilisema toka mapema hizo zinazoitwa "fikra" (wewe unaziita vision mwenzako anaziita ideas, sijui tofauti yake ni nini...labda hayo maneno yako interchangeable..sijui) za Mwalimu sidhani kama kuna binadamu hapa duniani anayeweza kuzipinga kwa sababu wengi kama sio wote tunazitamani ziwe katika maisha yetu hapa ulimwenguni. Hivi ni nani atabisha kuwa kila binadamu anastahili kutendewa vyema, kwa haki, na usawa? Ukibisha hilo basi wewe utakuwa unaishi sayari nyingine kabisa. Hivi ni mtu gani hapa anayetaka mabadiliko katika maisha yake au mazingira anayetegemea mtu mwingine kuja kumbadilisha au kumbadilishia kitu bila ya yeye mwenyewe kuanzisha hayo mabadiliko?
Nikasema hizo fikra ni za wote, mahali pote, kwa wakati wote! Nikaonekana kama mjinga fulani niliyefikia kikomo cha upeo wa kung'amua. Mnaona sasa thread ilipofikia? Mmmmhhh....labda mwenzenu hapa nimeshindwa kuelewa kitu. Ngoja ninyamaze nifiche ujinga wangu.