Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!

Fikra za Mwalimu: Hizi hapa.. mzikubali au mzipinge!


Masahihisho

Nyerere alikuwa anahubiri Uhuru wakati anaomba ulinzi Uingereza. Katika tundiko langu la mwisho niliandika kimakosa kwamba alikuwa anahubiri Kujitegemea.

Pia, Nyerere aliibua Sheria ya ‘Preventive Detention Act’ ya 1962 kufunga watu mwaka 1982. Niliandika kimakosa kwamba alikuja nayo mwaka 1982.

Sheria hii ya Kikangaruu inasema Rais anaweza kuamuru mtu afungwe bila mashitaka kama akidhani anahatarisha usalama. Ukishukiwa unafungwa. Nimekosea nini nikisema chini ya Sheria hii kushukiwa ni hatia?[/SIZE][/FONT]

Kusahihisha uongo kwa uongo hakuufanyi uongo kuwa ukweli.

a. Sheria hiyo ya Detention haimtaji Rais na hivyo inaonesha hata kuisoma hujaisoma.

b. Pili hakuna sheria inayosema Rais anaweza kuamuru "mtu afungwe bila mashtaka akidhani anahatarisha usalama". Hakuna sheria hiyo. Hakuna ukweli kuwa ilikuwa "ukishukiwa unafungwa"! na tatizo hukusema "chini ya sheria hii kushukiwa ni hatia" ulisema hiyo sheria inasema kushukiwa ni hatia!

Nakushauri utafute hiyo sheria uisome na mabadiliko yake ya 1985 siyo sheria ya 1982. Siyo sheria ndefu hiyo ya detention yenyewe haizidi kurasa tano na mabadiliko yake hayazidi kurasa mbili.
 

Kabla hatujanza kujadili, au kuumiza mishipa ya kichwa kubishana, kama Nyerere ni Fisadi ama sio, naomba unipe aini ya neno Fisadi ili tujue tunaongelea nini hasa.

Wewe umwite Nyerere fisadi, halafu mimi ndio nikupe maana ya neno fisadi!..huh! 😕
 
Wewe umwite Nyerere fisadi, halafu mimi ndio nikupe maana ya neno fisadi!..huh! 😕


Bubu Ataka Kusema
;
Kuthibitisha Madai ya ulichosema nimesema, kwamba Nyerere Fisadi, tuanze na Aini ya neno:
Nadondoa kutoka Kamusi ya Chuo Kikuu cha Yale, Marekani (Nisingeweza kutuma Kamusi ya Kitanzania kwa sababu haiko Mtandaoni)

fisadi , pl mafisadi { English: destroyer , pl destroyers } [derived: Arabic]
noun 5/6an, - [ edit entry ] [ photos: upload ]

fisadi , pl mafisadi { English: evil person } [derived: Arabic]
noun 5/6an, - [ edit entry ] [ photos: upload ]


Kama ulikubali mwanzoni kwamba Nyerere aliharibu Uchumi, halafu hukukataa kwamba alitumia Sheria za Kikangaruu kufunga wasio na hatia, basi ni Mwovu, Mharibifu.

Kiinikizo kimehamia kwako kusema kwa nini sio Mharibifu au Mwovu. Halafu ukimaliza kubishia uharibifu, elezea kwa nini mwanzoni ulisema kwamba hamkatai makosa.

Mwanakijiji;

Umebisha kwamba kwa mujibu wa Sheria, ni Nyerere ndiye alikuwa anaamua mtu afungwe bila hatia. Ripoti ya Idara ya Haki za Binadamu, Chuo Kikuu Cha California, San Diego kinasema kuhusu Sheria ya Nyerere:
Under the Preventive Detention Act, the President may order the arrest and indefinite detention without bail of any person considered dangerous to the public order or national security.

http://www-rohan.sdsu.edu/faculty/rwinslow/africa/tanzania.html

ambao wamedondoa kutoka ripoti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani:

http://www.state.gov/g/drl/rls/hrrpt/2004/41630.htm

(Siwezi kutuma vidhibiti kutoka hapa nyumbani kwa sababu haviko mtandaoni)

Sasa nawewe naomba uthibitishe ubishi wako kwamba sio Nyerere anae amuru mtu afungwe bila hatia. Ukishindwa kunithibitishia ngoma yako itakuwa ngumu ile mbaya. Nakuahidi!
 


Mwanakijiji;

Umebisha kwamba kwa mujibu wa Sheria,


Ni sheria ipi hiyo? Umesema prevention and detention..

ni Nyerere ndiye alikuwa anaamua mtu afungwe bila hatia. Ripoti ya Idara ya Haki za Binadamu, Chuo Kikuu Cha California, San Diego kinasema kuhusu Sheria ya Nyerere:
Under the Preventive Detention Act, the President may order the arrest and indefinite detention without bail of any person considered dangerous to the public order or national security.

huu ni uongo mkubwa. Hivi majuzi nilizungumza na mtu mmoja wa CPJ (Committee for the Protection of Journalist) na akasema hicho ulichonukuu. Nikamuuliza umeiona hiyo Prevention and Detention Act akasema hapana. Wewe umechukua maneno hayo ya Chuo Kikuu cha California na kuyaamini neno kwa neno badala ya kuitafuta sheria ya Prevention and Detention na wewe mwenyewe usome (pamoja na mabadiliko yake ya 1985) kama kuna kitu kama hicho.

tuma vidhibiti kutoka hapa nyumbani kwa sababu haviko mtandaoni)

Haviko mtandaoni au hujatafuta au kuuliza wapi vilipo uelekezwe?

Sasa nawewe naomba uthibitishe ubishi wako kwamba sio Nyerere anae amuru mtu afungwe bila hatia. Ukishindwa kunithibitishia ngoma yako itakuwa ngumu ile mbaya. Nakuahidi!

kwanini mimi nithibitishe lolote, siyo mimi niliyeleta madai hayo. Nimekukatalia kuwa hakukuwa na sheria inayompa nguvu hizo za kumuamuru mtu "afungwe bila hatia" ni jukumu lako wewe kunionesha sheria hiyo. The burden of proof is not on me to prove anything, it is on you to prove that he did have that legal power.
 
kwanza kabisa, sija jitwika ujinga!!! kama ni huo uelevu, I think mie nipo juu yako....evidence mojawapo ni hiyo signature yako(something wrong with it)...kukusaidia tu ni kwamba ina mawazo matatu tofauti, ni kichaa hicho.(mpaka hapo usha fail)

kina!?? kina gani? kuna kina inapokuja issue ya bwege nyerere?? ......kwahiyo nikiandika maneno miiiiingi ndio kina hicho?? nikikubali kwamba nyerere was the greatest ndio nakuwa mjuvi!! halafu unashangaa kwanini mie na wewe hatuoni jicho kwa jicho.........sijui nani kati yetu mwenye tongo machoni!!!

Na nani kati yenu mlevi wa gongo.....kwikwikwiiiiii
 
Usibishe hili mkuu,

Elimu ya msingi na upili huko marekani ni bure. Wasiopenda public schools ndio wanakwenda hizo za private. Elimu ya juu pia inapewa ruzuku na serikali kwa asilimia zaidi ya 50%


Kumbe ndio unayoita elimu ok kama ndio hivyo mimi nimepata elemu ya msingi almost bure kipindi cha mwinyi
Na elimu ya upili 1995 nikilipa elfu nane(8,000) kwa mwaka(Azania S.S tena nilikuta wanafunzi wengine kutoka mikoani wanakula na kulala bure pale)
Nimefanya B.eng hapo hapo Dar tech(now DIT) kipindi utelekezaji wa third phase of cost sharing(ambayo ni 40% unachangia) unaanza ila niliuwahi basi serikali iliendelea kulipa 90% (this was second phase of cost sharing) ya gharama zote hiyo(2004-2007).

Sasa wewe ubure wa elimu USA unaosema ni ule wa grade school maana High school kuna registration fee na mengineyo.Na hiyo ya chuo ujue kutofautisha Federal gov.grants and loan maana loan unapewa kiasi utakacho tena hata hawakawii ili mradi uwe na vigezo kupata hiyo ni kama kupata credit card si mkopo unarudisha tehe tehe wanabana mbaya kurudisha.Grants kupata unafanyiwa wanachoita needs analysis na unaweza kupata mpaka hiyo 50% unayosema kutokana na kipata cha family yenu na hujifichi hata ukishinda kamari data zipo.
Mimi nilochumuuliza aliyesema elimu marekani bure ni Marekani ipi, USA? maana nilikuwa navijua visivyo bure na vilivyo bure ndani ya USA ambayo nikujifunza kuandika na kusoma bure kama ulivyosema wewe elimu ya msingi tehe tehe.
 
Ni sheria ipi hiyo? Umesema prevention and detention..

huu ni uongo mkubwa. Hivi majuzi nilizungumza na mtu mmoja wa CPJ (Committee for the Protection of Journalist) na akasema hicho ulichonukuu. Nikamuuliza umeiona hiyo Prevention and Detention Act akasema hapana... na wewe mwenyewe usome (pamoja na mabadiliko yake ya 1985).

Haviko mtandaoni au hujatafuta au kuuliza wapi vilipo uelekezwe?

kwanini mimi nithibitishe lolote, siyo mimi niliyeleta madai hayo. Nimekukatalia kuwa hakukuwa na sheria inayompa nguvu hizo za kumuamuru mtu "afungwe bila hatia" ni jukumu lako wewe kunionesha sheria hiyo. The burden of proof is not on me to prove anything, it is on you to prove that he did have that legal power.

Kwanza, kwani hujui tunaongelea sheria gani, mbona unaleta ubishi wa Juma na Roza? Sio Preventive Detention Act ya 1962?

Pili, mazungumzo yako na huyo mja hayasemi lolote kuhusu mimi na hoja zangu.

Tatu, katika hiyo sheria -bila kuirudia rudia - yale marekebisho ya mwaka 1985 hayahusiki hapa. Tunaongelea ukandamizaji wa haki za binadamu na uovu wakati wa Nyerere.

Ningekuwa mimi wewe, japokuwa nashukuru sio, nisingeibua kabisa marekebisho ya 1985, kwa sababu yaliibadilisha hii sheria ya Nyerere na kuruhusu mtu apinge mahakamani kutiwa ndani baada ya kushukiwa. Hapa ni wakati Nyerere anang'atuka -baada ya kujibandika kwa karne mbili na nusu . Yaani alipotoka, ndio vitanzi vikaanza kulegezwa! Hiki kilembwa kinanisaidia mimi katika hoja yangu ya ukavu wa moyo wa Nyerere. Usingekisema!

Nne, unavyo nukuu kwamba nimesema "kushutumiwa ni hatia" jua kwamba unaninukuu mimi, maneno yangu mimi, sio ya hiyo Sheria. Mimi sikuyanukuu. Na nimeeleza kwa nini hiyo Sheria maana yake kushutumiwa ni hatia. Najua unaelewa, lakini nadhani unataka kupotosha watu utetee hoja yako. Lakini kwa sababu sina uhakika na nia yako sitafikia kukuita mwongo, mbishi mbishi, duwanzi mwovu, fisadi!

Mwisho, mimi niliposema kiinikizo kimehamia kwako maana yake mimi nimemaliza na vidhibiti vyangu. Sasa wewe badala ya kuonyesha hiyo Sheria unataka nikuombe kwanza. Haya, naomba uniambie.
 
yale yale mambo ya kufikirika....oooh "nimekula na kunywa mwili na damu," how? hamna ushahidi, ni maneno tu!! hovyooooo

Acha kunivunja mbavu mshikaji.....boy...you're on fire tonight...
Hebu rudi kule kwa Obama bana...waachie haya ya Nyerere wenyewe....Lol...you crack me up son....
 
Ndugu Bubu;
Ukisema tumwache Mwalimu apumzike, inabidi na wewe upumzike kumtetea, kwa sababu ukianza kumtetea tu na wengine tunaanza kumshitaki, kama Mfisadi na Mtesi wake.

Isitoshe, Nyerere alipo kaburini huko anataka watu wamzungumzie kwa sababu ni mtu wa Kihistoria. Hapana sijaenda makaburini, isipokuwa alisema mwenyewe kabla ya kufa. Aliwahi kuulizwa katika siku zake za mwisho akiwa Marekani - Wabongo wenye kende za kumswalisha Nyerere kama hivi walifungwa - ilikuwaje mawazo yake na Nkurumah kuanzisha Taifa la Afrika yalitoswa na Waafrika. Akajibu hilo jambo wana Historia watajadili, na kwamba yeye alijaribu. Kwa hiyo, hata yeye hataki kufa akasahaulika.

Tukiendelea na mashikata yalioalikwa na utetezi, kama Nyerere alileta vyama vingi ni kwa sababu alikuwa na juto moyoni. Yeye ndiye alivifuta 1965 alipokuja na fikra za Wachina Wekundu. Alikuwa anaogopa yaliyomkuta mwaka 1964 jeshi lilipoona isiwe tabu likaasi. Nyerere alijificha kwenye nyumba ya manyasi Kigamboni, akamtuma Biti Titi akajadiliane na Jeshi na kuongea na Wananchi. (Sikuweka dondoo.) Halafu akaomba msaada wa ulinzi Uingereza. Huku anahubiri kujitegemea.

Soo lilipoisha Bibi Titi akamwambia hizi siasa za Kichina China Mzee hazileti mantiki. Ungedhani atalipa fadhila, basi asivyo kuwa na soni, kamsweka Bibi Titi jela, na nyumba yake kaitaifisha. Ha ha aaaaa! Unasikitika mpaka unacheka.

Mwaka 1982 kidogo yamkute tena. Nyerere akaona isiwe tabu: akaja na Sheria ya Kikangaruu ya 'Preventive Detention Act' inayosema ni hatia kushukiwa!

Unaongelea Vyama Vingi? Nyerere toka lini anajua Demokrasia mjomba?


Kuhani Mkuu
Mbona umeweka hadithi za kwenye vikao vya kahawa hapa ambazo maudhui yake inategemeana nani anahadithia na ni shabiki wa nani maana siku zote hakuna source of info kwenye habari hizo anakwambia kipindi hicho niko middle school .Kama unajua kuhusu jeshi "kuto kutii amri na uasi unastahili adhabu kubwa au hata kifo" wanajeshi walishiliki wakafungwa na wengi wametoka 1994 nchi nyingine wanauwa kimya .Ila hadithi yako inadai bibi Titi ndiye aliye save issue inasimuliwa tofatu sana maana inadaiwa na yeye alikuwa yumu.Na ukweli ni kwamba jiribio hilo lilizimwa na wanajeshi hatiifu kwa rais .Bibi Titi alisave nini mbele mtutu? acha hadithi za Alinacha ww.Basi habari zisizo sibitika ziachwe.
Ila mapinduzi yalikuwa hivi ndugu Nimenukuu kutoka African Security Review Vol 10 No 1, 2001 -Herman Lupongo.

Tanganyika Rifles mutiny - January 1964
Soldiers of the Tanganyika Rifles mutinied in January 1964. It began in Colito barracks in Dar es Salaam, spread to Kalewa barracks in Tabora with Nachingwea, a new barracks, following suit. The mutiny was over pay, promotions, the removal of British officers and Africanisation. Mwalimu Nyerere conceded that the "soldiers had genuine grievances and the demands presented a perfectly reasonable case." However, he could not tolerate a mutiny. It has been convincingly argued that the mutiny was not a coup attempt. Most contemporaries emphasised that it was an industrial strike that focused on the soldier's grievances. At no time did they challenge the legitimacy of the political leadership, nor did they attempt to take over the government. They wanted to be heard. However, the mutiny raised questions about the place of the military in the newly independent Tanganyika - a military under a foreign command and not integrated into the country's system. It was also an eloquent, though crude commentary on a military leadership who was not in touch with a popular civilian government leadership. In a way, it was a blessing in disguise as the government set out to rectify the situation.

In 1968, Mwalimu Nyerere was heard to remark:
"The mutiny was a strike of the army people, and it went out of control. It shocked the country. But every cloud has a silver lining, as the British say. It enabled us to build an army almost from scratch. Many institutions we have inherited, but the army is something we built ourselves."
After the mutiny, the army was disbanded and fresh recruits were sought with the Tanganyika African National Union (TANU) youth wing as a base. Military personnel, as well as other public officials were allowed to join TANU, the ruling party, in a de facto one-party state. Membership of TANU was a prerequisite for enrolment in the army. The first recruits passed out on 1 September 1964 as the Tanzania Peoples' Defence Force (TPDF). Political commissars were introduced into the army. Later, battalion-size units became party branches and every commander was party chairman in his command. The long march had started to integrate the military into Tanzanian society.

Politicisation of the armed forces
 
Mbona hiyo nukuu haijasema lolote kuhusu nini kilizima maasi? Maana hilo ndio pingamizi lako kwa madai yangu?
 
Nakubali kuwa Mwal alikuwa na mengi mazuri, ila kimsingi kuna mambo mengi ambayo aliyafanya yametufikisha hapa tulipo kiuchumi na kadhalika.
 
Kuhani mkuu,

Swala la Wanajeshi wetu kina Sarakikya kugoma hivyo kushukiwa kuwa ni mapinduzi lilitoka ana kwamba serikali yetu baada ya Uhuru iliendelea kuwatumia Army officers wa kiingereza, ambao walipewa mishahara mikubwa mbali na huduma nyingine za kijeshi ambazo hupewa viongozi (ni rahisi kufahamu kama umeshawahi kwenda jeshi)
Viongozi wetu wazalendo hata wale waliokuwa na vyeo vya juu walikuwa wakilala ktk mabweni tofauti na viongozi wa kiingereza, wakila nje ya officers mess bila kujichanganya wa wazungu na kadhalika...
Hivyo mkuu, mgomo wa jeshi letu ulikuwa kutafuta haki zao haukuhusiana kabisa na mapinduzi kama wengi tulivyofikiria hapo awali..baada ya mgomo huo ndipo JWTZ lilipoundwa rasmi..

Kisha mnaposema Nyerere alikuwa FISADI ati aliharibu uchumi wetu, napenda kuuliza ni uchumi gani huo mnao uzungumzia ikiwa Muingereza hakutuachia kitu..
 
Unanipinga kuhusu nia ya Uasi wa jeshi la 1964? Sijasema lolote kuhusu hilo.

Jamaa mmoja alinibishia kwamba Nyerere hakusaidiwa na wasaidizi wake kujadiliana na Jeshi kuzima maasi. Akasema naleta uongo wa kwenye vikao vya kahawa ambako huko hadithi inategemea ni nani kasema. Halafu hapo hapo akajifunga akaja na hadithi ya mtu mwingine, ambae nadhani anamwamini kwa sababu ni mwandishi wa kigeni, na ni kweli tunajua wazungu hawakai kwenye vijiwe vya kahawa Temeke kwa Mama Mele. Akatoa makala fulani ambayo haisemi lolote kuhusu maasi yaliisha isha vipi.

Unasema Nyerere hakuharibu uchumi kwa sababu hakuachiwa uchumi na Waingereza? Kwa hiyo unapinga kwamba 1985 uchumi wa Bongo haukuwa umechoka kuliko miaka ya nyuma? Unajua sababu ya Nyerere kung'atuka (baada ya kujibandika karne mbili na nusu)? Unajua thamani ya shilingi miaka ya 70 na 60? Unajua historia ya Bongo?
 
Kuhani mkuu,

Swala la Wanajeshi wetu kina Sarakikya kugoma hivyo kushukiwa kuwa ni mapinduzi lilitoka ana kwamba serikali yetu baada ya Uhuru iliendelea kuwatumia Army officers wa kiingereza, ambao walipewa mishahara mikubwa mbali na huduma nyingine za kijeshi ambazo hupewa viongozi (ni rahisi kufahamu kama umeshawahi kwenda jeshi)
Viongozi wetu wazalendo hata wale waliokuwa na vyeo vya juu walikuwa wakilala ktk mabweni tofauti na viongozi wa kiingereza, wakila nje ya officers mess bila kujichanganya wa wazungu na kadhalika...
Hivyo mkuu, mgomo wa jeshi letu ulikuwa kutafuta haki zao haukuhusiana kabisa na mapinduzi kama wengi tulivyofikiria hapo awali..baada ya mgomo huo ndipo JWTZ lilipoundwa rasmi..

Kisha mnaposema Nyerere alikuwa FISADI ati aliharibu uchumi wetu, napenda kuuliza ni uchumi gani huo mnao uzungumzia ikiwa Muingereza hakutuachia kitu
..

Mkandara,

Wakati mwingine inabidi watu warudishwe kwenye the underlining argument. Hii issue ya mgomo wa wanajeshi imekuwa inarushwa hapa kila mahala bila kuwekewa sababu ya hakika. Asante sana kwa maelezo mazuri.

Kwenye bold, hilo ni swali ambalo nimekuwa nawauliza watu hapa kuanzia kwenye ile thread ya kwanza kuhusu Nyerere. Watu wanalia tu kuwa Nyerere aliharibu uchumi bila kusema ni uchumi gani huo ambao aliharibu kama wote wanakubali kuwa miaka ya utawala wa muingereza hakuna chochote kilichojengwa kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa Tanzania.

Emotions zaidi ya hoja vinatawala sana mijadala kama hii.

Asante sana Bob!
 
Watu wanalia tu kuwa Nyerere aliharibu uchumi bila kusema ni uchumi gani huo ambao aliharibu kama wote wanakubali kuwa miaka ya utawala wa muingereza hakuna chochote kilichojengwa kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa Tanzania.

Emotions zaidi ya hoja vinatawala sana mijadala kama hii.

Mnasema Nyerere hakuharibu uchumi kwa sababu hakuachiwa uchumi na Waingereza? Kwa hiyo unapinga kwamba 1985 uchumi wa Bongo haukuwa umechoka kuliko miaka ya nyuma? Mnajua sababu ya Nyerere kung'atuka (baada ya kujibandika karne mbili na nusu)? Mnajua thamani ya shilingi miaka ya 70 na 60? Mnajua historia ya Bongo?

Usilete ushabiki unaojifanya kuupinga wewe mwenyewe!
 
Mnasema Nyerere hakuharibu uchumi kwa sababu hakuachiwa uchumi na Waingereza? Kwa hiyo unapinga kwamba 1985 uchumi wa Bongo haukuwa umechoka kuliko miaka ya nyuma? Mnajua sababu ya Nyerere kung'atuka (baada ya kujibandika karne mbili na nusu)? Mnajua thamani ya shilingi miaka ya 70 na 60? Mnajua historia ya Bongo?

Usilete ushabiki unaojifanya kuupinga wewe mwenyewe!

Leta numbers za kuthibitisha madai yako.

Sema kuwa uchumi ulikuwa ..... mwaka 1961 na ulikuwa .... mwaka 1985 wakati Nyerere anastaafu. Ikiwezekana weka chati kuonyesha namna uchumi ulivyokuwa unaharibika kwenye miaka ya Nyerere.

Hapa ni Jamboforums na sio kibaraza cha huko kariakoo...

OK?
 
Unanipinga kuhusu nia ya Uasi wa jeshi la 1964? Sijasema lolote kuhusu hilo.

Jamaa mmoja alinibishia kwamba Nyerere hakusaidiwa na wasaidizi wake kujadiliana na Jeshi kuzima maasi. Akasema naleta uongo wa kwenye vikao vya kahawa ambako huko hadithi inategemea ni nani kasema. Halafu hapo hapo akajifunga akaja na hadithi ya mtu mwingine, ambae nadhani anamwamini kwa sababu ni mwandishi wa kigeni, na ni kweli tunajua wazungu hawakai kwenye vijiwe vya kahawa Temeke kwa Mama Mele. Akatoa makala fulani ambayo haisemi lolote kuhusu maasi yaliisha isha vipi.

Unasema Nyerere hakuharibu uchumi kwa sababu hakuachiwa uchumi na Waingereza? Kwa hiyo unapinga kwamba 1985 uchumi wa Bongo haukuwa umechoka kuliko miaka ya nyuma? Unajua sababu ya Nyerere kung'atuka (baada ya kujibandika karne mbili na nusu)? Unajua thamani ya shilingi miaka ya 70 na 60? Unajua historia ya Bongo?

Kuhani Mkuu
Ndio maana nimeweka source of inf. kiasi kwamba unaweza ukahoji kuhusu reliability yake.Lakini nikakwambia kwenye vikao hivyo hivyo mimi nilipata habari tofauti kuhusu bibi Titi na uasi huo ndio maana nika comment kwamba inategemeana na nani anahadithi kwenye baraza la kahawa na ana umpenda na nani.Basi ni juu yetu habari za kuhadithia kuzichekecha kabla ya kuweka mezani .Pia ni busara to acknowledge aliyekupa habari ndivyo inavyofanyika.

Pili nani kakwambia aliyo andika hiyo makala ni mzungu kwani imeandikwa hapo kwamba ni mzungu that is kind of inferiority complex.

Tatu unasema hukusema chochote kuhusu nia ya uasi umesahau comments zako kutoka vikao vya kahawa kwamba Bibi Titi alimwambia Mwl aache siasa zake kutoka Uchina baada ya uasi !ulinaanisha nini?flow na habari yako kama ni utunzi,uongo usiwe msahaurifu shame on You!
 
Mbona una dharau "huko Kariakoo"?

We kwenu wapi?
 
Kweli kama hujui kitu hujui haka ukikisema kana kwamba unajua:



...Ningekuwa mimi wewe, japokuwa nashukuru sio, nisingeibua kabisa marekebisho ya 1985, kwa sababu yaliibadilisha hii sheria ya Nyerere na kuruhusu mtu apinge mahakamani kutiwa ndani baada ya kushukiwa.


Hivi unajua ni nini alitunga sheria ya Detention ya 1962 na ni nani aliipitisha kuwa Sheria? Siyo Nyerere!! Kaisome!


H
apa ni wakati Nyerere anang'atuka -baada ya kujibandika kwa karne mbili na nusu .

Nne, unavyo nukuu kwamba nimesema "kushutumiwa ni hatia" jua kwamba unaninukuu mimi, maneno yangu mimi, sio ya hiyo Sheria. Mimi sikuyanukuu. Na nimeeleza kwa nini hiyo Sheria maana yake kushutumiwa ni hatia. Najua unaelewa, lakini nadhani unataka kupotosha watu utetee hoja yako. Lakini kwa sababu sina uhakika na nia yako sitafikia kukuita mwongo, mbishi mbishi, duwanzi mwovu, fisadi!

Huwezi kusema maana ya sheria ni kitu fulani wakati sheria haisemi hivyo. Ulivyosema mwanzo hukusema maana ulisema "sheria inasema"! You need to get your story straight kabla hujaanza kuyumba yumba. Kuniita majina, believe me.. it is the last of my worry. Kama ni mwongo niite mwongo, kama ni mbishi niite mbishi! usisite.

Mwisho, mimi niliposema kiinikizo kimehamia kwako maana yake mimi nimemaliza na vidhibiti vyangu. Sasa wewe badala ya kuonyesha hiyo Sheria unataka nikuombe kwanza. Haya, naomba uniambie. [/FONT]

Sikuambii, kwa sababu ulivyozungumza kana kwamba umeiona:

Umedai sheria inasema kuwa kushukiwa ni hatia - haisemi
Umedai ni sheria ya 1982 - si kweli ni ya 1962
Umedai ni shereia ya Nyerere - Si kweli nyerere hakutia sahihi sheria hiyo

sasa kama hujui hicho sheria inasema na ungependa kuona nakala yake omba upewe. Usilazimishe uongo uwe ukweli kwa sababu ya chuki zako za binafsi kwa Nyerere.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom