Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,063
- 744
DHAMBI NYINGINE YA NYERERE NI KUTOSEMA UKWELI
Siasa ya kutofungamana na upande wowote haikuwa kweli. Aliingilia siasa za ndani za Uganda, Zaire, Msumbiji na nyingine nyingi. Nje ya Afrika alikuwa anafungamana na siasa za ki Komunisti za Cuba na Uchina.
Wakati anasema tunafuata siasa ya kujitegemea, nchi ina njaa ile mbaya. Tunategemea misaada kulia na kushoto. Juzi waziri mstaafu Kiula ametoa dhihirisho moja kubwa sana kuhusu mambo yalivyo kuwa wakati wa utawala wa Nyerere. Alipokuwa mkuu wa mkoa Singida alimwambia Sokoine watu wanakufa njaa Singida. Makachero wa Nyerere wakamburura kwenda kuhojiwa Oysterbay eti kwa kumdanganya Sokoine. Duh! Yani noma ile mbaya.
Sijasema lolote kuhusu ubora au uozo wa siasa zake za kufungamana na upande wowote. Nimesema alichosema jukwaani hakukifanya uani!
Hii ni kweli kabisa.
Miaka ya 70 na 80 niliwahi kushuhudia watu wakifa kwa njaa, katika maana ya mwili kukosa chakula kwa muda mrefu hadi roho inaacha mwili, kula matunda,mizizi au mimea yenye sumu na kufa, baada ya kukosa chakula kwa muda mrefu.
Hili la viongozi wa kitaifa kuzuia viongozi wa kada za wilaya au mikoa kutoa taarifa kamili za hali ya chakula lipo hadi leo hii.
Viongozi wetu wa kitaifa wanaongoza as if Malkia Elizabeth bado ni bosi wao, isije ikatoka siri kwamba nchi aliyowaachia watu wanakufa kwa njaa akwanyang'anya.
Viongozi wetu wengi ni viongozi wa kulinda Uhuru wa Bendera na si kuutafuta na kuuimarisha Uhuru wa Kiuchumi.
Watu wengi baada ya Operesheni Sogeza walikufa kwa njaa na serikali ilikaa kimya bila kutoa tamko lolote.
Watu tulihamishwa toka kwenye mashamba yetu mazuri tukawekwa mahali fulani karibu na barabara kwa kisingizio cha kufuata huduma ambazo hazijaja mpaka leo karne ya 21.
Tunaambiwa eti tujitafutie maendeleo yetu wenyewe, swali langu ni moja kwa nini mlikuja kutuhamisha kule tuliko kua tukiishi tukilma kula na kushiba???
Tungeachwa kule tuliko kua na kuambiwa tujitafutie maendeleo yetu wenyewe somo hilo lingetuiingia vyema.
Operesheni sogeza haikua Hiari ilikuwa ni Amri toka Mezani kwa Julius Ikulu, katika juhudi zake kuiga comunal village zilizo anzishwa na Mao kule China.
Nyerere hakumwiga mzungu alimwiga mchina bila kuzingatia utamaduni wa Tanzania.
Adhari za watu kufa kwa njaa vijijini kutokana na kuwa misplaced zinaendelea hadi leo na lawama za kushindwa kuendelea wanajaziwa wananchi.
Kibaya zaidi na kinacho nipa hasira kiasi cha kutaka kumtoboa mtu shimo kwenye bichwa lake ni;maeneo mazuri yaliyoachwa miaka ya 70 yalichukuliwa na serikali sasa yanauzwa kwa wageni ambao wanayatumia kuzarisha bidhaa za kuuza nje na ambazo siyo chakula.
Siasa za Nyerere za ujumla majukwaani na kueleza maoni yake juu ya Afrika kana kwamba Afrika ni nchi moja kweli zilifanikiwa.
Siasa za kuelezea maendeleo ya Tanzania kwa kuchambua jambo moja hadi jingine kwa kufuata kanuni za asili na za kiutafiti hazikuwahi kufanyika kabisa.
Kulikuwa na siasa za kiimla za kuingilia kila fani kwa gia ya siasa, huku wazungu wa ulaya wakirushiwa lawama kibao hata pale tukishindwa kusafisha vyoo tunavyo tumia wenyewe.
Tafsiri ya siasa za Mwalimu Nyerere haikuwahi kuandikwa wala kuongelewa wazi, sababu moja wapo kubwa ni kwamba siasa zake Nyerere zilikuwa hazitekelezeki kwa namna yeyote. Zililenga kuwadumaza zaidi Watanzania ili kuendeleza utawala wa kiimla kuliko kujenga taifa la watu wanao taka kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Ujamaa ni kushirikiana.
Vipi Nyerere aliua vyama vyote vya ushirika Tanzania kwa kisingizio cha Siasa ya ujamaa na kujitegemea?
Ujamaa upi na kujitegemea kupi?