Feitoto na Mudathir wamecheza mechi za jana, wamefutiwa adhabu ya kufungiwa mechi 3 ?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Siku ya jana Azam imecheza dhidi ya Namungo, Fei alikuwemo kwenye kikosi.

Yanga dhidi ya Singida, Mudathir alikuwemo kwenye kikosi.

Mudathir na Fei walipewq adhabu ya kufungiwa mechi tatu baada ya tukio la wao kuchelewa kuingia uwanjani.

Adhabu ipo ?
 
Wanasubiri Mechi na Simba ipite .

Mudathiri ni mchezaji tegemeo kwa yanga.

SOKA LETU KIVYETU VYETU.
 
Ila tuweke ushabiki pembeni, kitendo walichofanya hawa wachezaji wanatakiwa adhabu kali sana maana wanaharibu brand kubwa inayojengwa ya league yetu kwa vitendo vya kishamba niseme.
 
Mshamba ni wewe
Kila kitu na mazingira yake
We unataka kila kitu kiende kama ulaya

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani wewe hata sijui umefikaje humu Jamii forum, wapi nimesema tuwe kama ulaya? mazingira gani unayotaka kusema hapa, kama nyinyi wataalamu wa haya mazingira tunashindwa nini kuchukua makombe yote. Nadhani Sumbawanga huko na Pemba wangekuwa na team zinachukuwa ubingwa tu maana mazingira yanawaruhusu. Mjinga mkubwa nenda katufute forum za wachawi sio hapa.
 
Siku ya jana Azam imecheza dhidi ya Namungo, Fei alikuwemo kwenye kikosi.

Yanga dhidi ya Singida, Mudathir alikuwemo kwenye kikosi.

Mudathir na Fei walipewq adhabu ya kufungiwa mechi tatu baada ya tukio la wao kuchelewa kuingia uwanjani.

Adhabu ipo ?
Ni sehemu gani umeona kuwa wamepewa adhabu? Embu lete taarifa ya TFF au bodi ya ligi ikitoa adhabu kwa hao wachezaji.
 
Ila tuweke ushabiki pembeni, kitendo walichofanya hawa wachezaji wanatakiwa adhabu kali sana maana wanaharibu brand kubwa inayojengwa ya league yetu kwa vitendo vya kishamba niseme.
Kwani kulikuwa kuna kitendo gani kibaya kwa hao wachezaji? Mimi niliona wote wawili walisimama tu kwenye mstari wa uwanja wakati wachezaji wengine wakiendelea kusalimiana.
 
Ila tuweke ushabiki pembeni, kitendo walichofanya hawa wachezaji wanatakiwa adhabu kali sana maana wanaharibu brand kubwa inayojengwa ya league yetu kwa vitendo vya kishamba niseme.
Kuna ile timu ilitembea na basi kinyumenyume kilometa 50 kwenye mechi na Raja ikaishia kugongwa 3 haikuadhibiwa wao hawaharibu brand ya mpira.
 
Back
Top Bottom