Hatima ya Pacome, Aucho na Yao kuelekea mechi ya Mamelodi Sundowns

Mr Lukwaro

JF-Expert Member
Jun 3, 2023
357
621
Taarifa Rasmi kuhusu Khalid Aucho ni kwamba kuanzia kesho ataanza mazoezi mepesi.

Taarifa hii inaashiria kuwa Mchezaji huyo , Kiungo wa kati wa Dar Young Africans (YANGA) , Atakuwa sehemu ya Kikosi cha Yanga kwenye Mechi yao Ya Robo fainali Club bingwa Africa.

Aidhaa.........

PACÖME NA YAO WAKO CHINI YA UANGALIZI

Meneja wa Yanga Walter Harrison amewatoa hofu wanachama na mashabiki wa timu hiyo juu ya hali za wachezaji Pacome Zouzoua na Yao Kouassi ambao jana walipata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Azam Fc ambao Wananchi walikubali kipigo cha mabao 2-1 uwanja wa Benjamin Mkapa

Walter amesema uchunguzi wa awali unaonyesha wachezaji hao walipata majeraha ya kawaida hivyo anaamini watakuwa tayari kuikabili Mamelodi Sundowns March 30 katika mchezo wa ligi ya mabingwa

"Niwatoe hofu juu ya wachezaji wetu Pacome na Yao, walipata majeraha lakini hali zao zinaendelea vizuri. Wapo katika uangalizi wa madaktari wetu na naamini mpaka kufikia siku ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns, watakuwa tayari kuwapa furaha Wananchi," alisema Walter

Akizungumzia mchezo dhidi ya Azam Fc, Walter aliseema wamekubali matokeo ya kupoteza mchezo huo ingawa malengo yao ilikuwa kushinda.
 
Back
Top Bottom