Yanga walicheza jana kama wanacheza na Pamba fc Kirumba Stadium

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Ukiangalia gemu ya jana Yanga anakula vyuma vitatu dhidi ya waAlgeria ni kama Jana Yanga walijisahau wakahisi wanacheza na Pamba ya Mwanza au Lipuli ya Iringa na kusahau wale ni professional players wamekamilika kila idara.

Ukifanya kosa moja tu lazima watakuadhibu na Yanga walifanya makosa matatu ya kizembe na jamaa wakayatumia kweli, Yanga ilijisahau kwamba haya ni mashindano ya kimataifa, hatukatai walicheza mchezo mzuri ila sio lengo la hii michuano hapa piga hata OBJECTIVE FOOTBALL as longer unaibuka na pointi tatu hii ndio advantage walitumia simba kipindi cha nyuma na wakatoboa.

Ni kweli fitness ya wachezaji wa Yanga jana ilikua chini labda kwa sababu walitumika kwenye mechi za kimataifa kwa timu zao za Taifa sijui, ila pia ukiangalia wachezaji wengine walienda kwa mafungu tena kwa kuchelewa na pia safari ndefu.

Yanga inawapasa kujifunza kucheza gemu za ugenini hata ukiangalia mwaka jana shirikisho Prof Nabi alianza vibaya na yeye alikuja na soka la kutaka kuburudisha ila aligundua mapema na kuanza kucheza direct football sio ajabu kuona alikua akianza na mabeki wengi na viungo wa kutosha na akaanza kupata matokeo

Mfano ukiangalia gemu ya jana Yanga walikua wanawapa nafasi sana wachezaji wa timu pinzani pia walikua wakiacha space kubwa sana kiwanjani sababu ni ndogo tu Yanga walianza na viungo wakabaji kwa asili wawili lakini bado Mudathir hakua kwenye kiwango bora jana na kumfanya Aucho kuwa bize muda wote, tukumbuke Mudathir ni kati ya wachezaji waliochelewa kujiunga na Yanga.

Pia beki za timu pinzani walikua huru kusogea sana kutokana na yanga kuanza na mshambuliaji mmoja Musonda ambaye naye percee sio mzuri wa kukaa kwenye D ya wapinzani muda mwingi anatokea pembeni na kuwafanya beki 4 na 5 kuwa huru zaidi kucheza mipira.

At least jana nlitegemea kumwona kocha akimtumia mkude au Sure boy ili kusaidiana na Aucho na pia kusaidia timu kupress kuanzia lango la wapinzani na pia kucover space za Yao na Lomalisa wakienda kuattack hata ukiangalia magoli yote yametoka pembeni kutokana na mabeki wa pembeni kushindwa kureact kwa haraka.

Kuna pira linapigwa hapa Medeama Vs Al ahly Medeama ukiwaangalia wamewaheshimu Al ahly na mpango wao wa kwanza ni kukaba japo washapigwa kamoja.

Hata Simba leo wamekuja na plan ya kujilinda zaidi ila bahati haikua yao, nategemea mabadiliko zaidi next gemu kwa Yanga.
 
Yanga ni wazuri wakiwa na Mpira tu
 
Uzi za wanayanga utaziona, Uzi zenye akili, Yanga ikishinda tunasifia, ikifungwa tunakosoa sio kule umbumbumbuni kolokoloni kila kitu kusifia , wakikandwa badala ya kukubali wanasema tumekufa kiume!

Gamondi aambiwe ukweli sasa ni wakati kocha atuwekee mezani plan ya Champions league iliyo tofauti na NBC premier league!!
 
Mkuu ya juzi yale ni matokeo tu, ni ajali kazini ila Yanga alikuwa vizuri saana, Liverpool aliwahi kuiburuza saana kimpira Barca pale Camp Nou ila akafungwa yeye goli 3, Barca hakuwahi kuburuzaa namna, Barca ya akina Messi, Iniesta n.k
 
Kuna watu nawaambia wakati mwingine unaachwa ucheze wewe mpira siyo kwamba unaogopwa bali ni mtego huo kuwa na tahadhari otherwise uwe na wachezaji wa daraja la juu kabisa kama wa ulaya Ili kushinda Kwa style ya uchezaji ule wa yanga na waarabu.
 
Uzi za wanayanga utaziona, Uzi zenye akili, Yanga ikishinda tunasifia, ikifungwa tunakosoa sio kule umbumbumbuni kolokoloni kila kitu kusifia , wakikandwa badala ya kukubali wanasema tumekufa kiume!

Gamondi aambiwe ukweli sasa ni wakati kocha atuwekee mezani plan ya Champions league iliyo tofauti na NBC premier league!!
Elezea Yanga.Simba hawapo hapo.Au una wenge bado?
 
Back
Top Bottom