FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread

rome_9_-_A_Manchest_813016a.jpg


teh teh teh teh mupo wana Man U?
 
I honestly thougt it was going to be United's nite, nilikua na uhakika baada ya kuangalia tu ile defence ya Barca kwa kuwa hawa jamaa hata wakiwa na defenders wao wa first eleven bado wengi tunaona kuwa pale ndo weakness point yao ilipo. Na niliamini kwa kuwa Barca na Gunners wana similar playing styles, nikajua Fergie atatumia tactics zilezile zilizomnyoa Arsenal, and would have put all my saving for them to score a goal tonight! Im so glad thou cause the better team won and its so good to see the best team in europe being crowned as the european champions. Man U winning this title would have been so unfair to other teams in Europe. Poleni wana Manure, you are not alone,we are all missing out, at least we managed a goal with one man down!
 
I honestly thougt it was going to be United's nite, nilikua na uhakika baada ya kuangalia tu ile defence ya Barca kwa kuwa hawa jamaa hata wakiwa na defenders wao wa first eleven bado wengi tunaona kuwa pale ndo weakness point yao ilipo. Na niliamini kwa kuwa Barca na Gunners wana similar playing styles, nikajua Fergie atatumia tactics zilezile zilizomnyoa Arsenal, and would have put all my saving for them to score a goal tonight! Im so glad thou cause the better team won and its so good to see the best team in europe being crowned as the european champions. Man U winning this title would have been so unfair to other teams in Europe. Poleni wana Manure, you are not alone,we are all missing out, at least we managed a goal with one man down!

yeah, not alone indeed; we will walk alongside liverpool.
kwa nini ulidhani man united wangechukua wakati barca ni the best team?
 
....grrrrrrrrrrr, nyinyi vipi bana... hizi threads hazina mwisho?! matokeo yameshajulikana, si mzifunge sasa.
 
I really know how it feels kama wewe wakati ule..Man Utd bado wapo juu na nimekubali tumefungwa maana Barca wamecheza bwana na wanastahili kombe..
Congrats Barca

BJ na Watani wetu wote wa jadi poleni sana kwa kipigo cha leo. Mbabe wa soka Europe amejulikana rasmi leo lakini msikate tamaa maana kuvunjika mpini siyo mwisho wa uhunzi. Sasa hivi muelekeze nguvu zenu kuhakikisha Ronaldo hatingishi tena kiberiti kama mwaka jana na pia kuhakikisha mnambakisha Tevez au kutafuta replacement yake ya nguvu. Poleni sana siku ya leo haikuwa yenu.
 
mie nilisema toka mwanzo kwamba barca anashinda 2-1 .ni goli moja ru man united wameninyima.vijana wangu walishndwa kupiga mashuti tu kama kawaida ndio maana nimemleta arshavin mwakani.fainali utasema mechi ya kirafiki.
 
Wana Ki-ManuManu wamepiga kelele sana.. ngoja niwapooze kwa songi la Fredi Mekyuri...

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=7oH5SNmUZkc]YouTube - Freddie mercury and Montserrat Caballé - Barcelona[/ame]
 
Jamani ndugu zanguni nimejitahidi kutafuta thread ya ndugu zetu ......,
MAN U siipati jamani....wame edelete nini...polen mama belly;n compny
dont worry kuna nexty. year....
tujitahidi tunaweza kufanikiwa kuchukua kombe
big up cuddy boys
 
ha ha haa...

nakweli! ...Belo, Nziku, Manda, Saikosisi, Mtaalamu wapo wapi na wana hali gani jamani? ...hatari, game kama hizi kuna watu roho zishaacha mwili!

Ab-Tichaz sasa tuletee mapicha mazee, wiki nzima kusherehekea ubingwa wa Barca mpaka Icadon azoee!

Messi-Manchester-United-Barcelona-Champions-L_2311583.jpg



Supporters-Manchester-United-Barcelona-Champi_2311546.jpg




Fan-Zone-Outside-Stadium-Manchester-United-Ba_2311564.jpg



Supporters-Manchester-United-Barcelona-Champi_2311548.jpg
 
VIDEO - Barcelona Mabingwa wa Ulaya, Yaibanjua Manchester 2-0
2099594.jpg

Thierry Henry akiwa emebeba kombe la mabingwa wa ulaya walilolitwaa usiku huu kwa kuifunga ManchesterThursday, May 28, 2009 1:50 AM
Mabingwa wa Hispania Barcelona, wameliteka jiji la Roma usiku wa leo na kuwa mabingwa wapya wa ulaya kwa kuigaragaza Manchester United kwa kuifunga mabao 2-0. VIDEO za magoli yote mawili ya Barcelona na sherehe nzima ya kukabidhiwa kombe mwisho wa habari hii.Barcelona ikicheza kwa kujiamini sana na ikitandaza pasi fupi fupi za uhakika imefanikiwa kutwaa taji la ubingwa wa Ulaya kwa mara ya tatu katika historia yake baada ya kuwabanjua mabingwa watetezi Manchester United ya Uingereza kwa mabao 2-0.

Kocha wa Barcelona Josep Guardiola ameweka historia kwa kuwa kocha kijana kuliko wote kutwaa kombe la mabimgwa wa ulaya.

Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson akiongea baada ya mechi alikiri kwamba Barcelona ilistahili kutwaa kombe hilo kutokana na uwezo mkubwa sana iliouonyesha leo.

"Kusema kweli tumefungwa na timu iliyokuwa bora sana zaidi yetu", alisema Ferguson.

Manchester United ilianza kipindi cha kwanza kwa kasi sana na kuitia ngome ya Barcelona katika mashaka makubwa kwa kosa kosa nyingi za Cristiano Ronaldo.

Manchester United ilinyamazishwa na kupoteza muelekeo kabisa katika mechi ya leo pale Samuel Eto'o alipoifungia Barcelona goli la kuongoza katika dakika ya 10 baada ya kuipangua ngome ya Manchester na kumuacha kipa wao akigaragara huku mpira ukitinga nyavuni.

Goli hilo liliifanya Manchester ianze kucheza bila mpangilio maalumu na kuanza kupoteza mpira mara kwa mara na kuipa nafasi Barcelona kuitawala mechi hiyo.

Goli hilo lilidumu hadi mapumziko na kuifanya Barca iende mapumziko ikiwa kifua mbele.

Katika kipindi cha pili, pamoja na Alex Ferguson kuingiza vifaa vyake vyote uwanjani ili kuokoa jahazi lakini Barcelona ilikuwa bora zaidi ikicheza kwa kujiamini zaidi kwa pasi zake fupi fupi huku ikilisakama lango la Manchester.

Alikuwa ni Lionel Messi aliyehitimisha mazishi ya Manchester pale alipoifungia Barcelona goli la pili kwa kichwa safi katika dakika ya 70.

Baada ya goli hilo Manchester iliendelea kucheza hovyo huku baadhi ya wachezaji wake kama Cristiano Ronaldo, Vidic na Scholes wakianza kuwacheza rafu hovyo zilizopelekea wapewe kadi nyekundu.

Nyota wa mechi ya leo alikuwa ni Andres Iniesta ambaye alicheza kwa ustadi mkubwa sana akiwaunganisha vyema washambuliaji wa Barcelona. Alikuwa ni Iniesta aliyemtengenezea Eto'o goli la kwanza.

Uwanja wa Stadio Olimpico uligubikwa na sherehe za washabiki wa Barcelona baada ya refa wa mechi hiyo kupuliza kipyenga cha mwisho kilichoitangaza Barcelona mabingwa wapya wa ulaya.

Chini ni video za magoli yote mawili ya Barcelona na sherehe nzima ya kukabidhiwa kombe.
 
Mkuu huu sasa utani. Hii nayo ni thread ya kisiasa? Si kuna jukwaa la michezo? Au sasa kuna maana gani kuwa na forums mbali mbali?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom