Philippe Coutinho amethibitisha kwamba amepokea maneno ya pongezi kutoka kwa nyota mwenzake wa Brazil Neymar kufuatia kujiunga na Barcelona
Nyota huyo mwenye miaka 25 siku ya Jumatatu amekamilisha dili lake la kujiunga Nou Camp kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 142
Coutinho kwa sasa yupo nyuma ya Neymar kwenye orodha ya wachezaji ghali duniani, baada ya mshambuliaji huyo kuwa ghalimu PSG paundi milioni 198 kuinasa saini yake
"Nina cheza na Neymar timu ya Taifa na tumekuwa marafiki tangu tuko wadogo" Coutinho aliwaambia ripota. "Alinipongeza na aliniambia mimi kwamba kuna vyumba vya kubadilishia vizuri.
"Luis Suarez and Paulinho pia wameaniambia mimi kuwa wanazani nitakuwa na maisha mazuri hapa
Coutinho hatoweza kucheza Barcelona kwa sasa hadi mwezi wa pili baada ya kusumbuliwa ma maumivu madogo