Busquets ni engine nyingne pale kati hakuna wakuikama dunia hii
Unajua Mkuu pale Barca mfumo ambao ulizoeleka ni tiki taka, kwa sasa tiki taka haina faida tena, ule mpira wa kupooza na kuumiliki kwa muda mrefu hauna maana tena.
Rejea Barca ya Enrique aliyobeba UEFA, Uliona Barca ikimiliki mpira for nothing, kulikuwa na Neymar, Messi, Rakitic na Iniesta, watu walikuwa hawana mambo ya kumiliki mpira pasipo faida.
Hata Iniesta kiuhalisia hanaga mpira wa kuhold, ni mtu wa kugusa na kugawa ama kudrible, wanapooza mpira kwa Barca ni Busquets kwa sasa, na hiki ndicho ambacho hata Coutinho kilimshinda Barca, alizoea akikamata mpira atoe kisha akaombe sehemu nyingine na sio kukaa hapo hapo ili apige vipasi viwili vitatu.
Timu inapaswa kubadilika, WHY tusiweke viungo ambao hawana mambo mengi, pale kati tia De Jong, tia Arthur Melo, tia na Rakitic. Kwa bahati mbaya tumemkosa Neymar, ungeweka pale mbele Neymar, Messi na Suarez. Pale kati pangechangamka saaana, kungekuwa hakuna haja ya viungo pinzani kuwa wanarelax na kupumua, muda wote wangekuwa wanawaza wakabe wapi.
Kwa upande wangu, Bisquets anapoza sana mipira na kwa tunakoenda Barca tikitaka haitufai tena kwa asilimia kubwa, uliona Liver walivyotuendesha pale Nou Camp, sema ndo hivyo tu Messi alikuwepo, unafikiri Barca ingekuwa na mpira ambao haupozi pale Anfield tungekufa kizembe vile? Hata yule Pique mwehu tu, weka pale ukuta akae Umtiti, apate uzoefu zaidi, hii ni mashine haswa ila basi tu ndo hivyo.