D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,633
- 121,022
Messi anacheza upande wa kulia, Dembele anacheza upande wa kulia, Willian nae anacheza upande wa kulia.
Hatuna mapungufu kwenye upande huo!
Tunahitaji striker mbadala wa Suarez, tunahitaji winga wa kushoto, na world class midfielder (namtamani Alcantara).
Huyo Willian hatuna uhitaji wa kumsajili.
- muheshimiwa -KANA- upo sahihi kwenye maelezo yako ya kwamba barcelona tayari yupo messi na dembele upande wa kulia lakini natofautiana na wewe kimtazamo unaposema ya kwamba barcelona haimhitaji mchezaji aina ya willian kwa kutumia kigezo cha kuwa upande wa kulia tayari nafasi zimejaa. naamini unafahamu ya kwamba unaweza ukawa na wachezaji 4 kwenye nafasi moja lakini wote uwezo wao ukawa ni wa kawaida sana. kwa pumzi tulioionyesha barcelona msimu na iliopita naamini ya kwamba tunamhitaji zaidi willian kuliko willian anavyohitaji kuja barcelona licha ya kuwa ana miaka 29.
- tuna miaka 3 hatujafika hata nusu final kwenye champions league na cha kushangaza tunatolewa na timu dhaifu sana ukilinganisha na brand yetu, barcelona si timu ya kunyanyaswa na juventus, roma na athletico madrid lakini yote yanatokezea kwa sababu tumejaza average player kwenye timu yetu ukilinganisha na wapinzani wetu wakuu ambao ni real madrid japokuwa tunaonekana kwenye ligi kuu tuna mafanikio mazuri ukilinganisha na wao.
- niwe mkweli kiupande wangu inaniwia vigumu kuamini ya kwamba msimu huu tutavuna matunda kupitia osmane dembele, ni kijana mwenye kipaji cha hali ya juu lakini siamini ya kwamba kama atatupa faida kubwa msimu huu, dembele hawezi kuufurahia mpira wake akiwa barcelona hivyo basi naona njia pekee ni kwa klabu kumuuza na mapema kabla hajawa flop, barcelona haimhitaji mchezaji mwenye maamuzi ya mwisho yasiotabirika, anaweza akapiga assist nzuri ukafurahi, anaweza akapiga chenga mpira akauacha njiani, anaweza akakaa na mpira sehemu ambayo alipaswa ampe mwenzake. barcelona hawachezi mpira wa kuoteana hivyo basi dembele anapaswa aende uingereza akakuze zaidi jina lake na sababu timu zote za uingereza zinacheza mpira wa kutegeana, hivyo basi kama biashara ya willian itafanikiwa basi haitokuwa biashara kichaa.
- ni kweli suarez anaonekana kupoteza makali yake lakini suali la kujiuliza kwenye dunia hii ya sasa hivi ni wapi utampata mshambuliaji mwenye tabia za suarez, namaanisha mshambuliaji mwenye uhakika wa kuwapiga chenga washambuliaji watatu, uhakika wa kukimbia na mpira, na pia najua washambuliaji wapo wengi lakini je wanaendana na soka la barcelona, nahofia tusije tukaishia kwa diego costa na roberto lewandowski yakaja kutukuta ya zlatan ibrahimovic, munaingia uwanjani mupo 11 lakini wanaocheza mpira ni 10.ikiwa tunahitaji mbadala wa suarez nadhani dyabala anatufaa zaidi kuliko griezmann.
- tujaribu kuwaangalia wapinzani wetu jinsi wanavyozitesa timu pinzani kwa utatu wao mtakatifu (casemiro + modric + kroos), miaka 5 iliopita ilikuwa ni sisi ndio tunaozitesa timu kwa utatu mtakatifu (sergio + xavi + iniesta) lakini leo hii imekuwa kinyume chake. xavi aliondoka na mafanikio ya ligi ya ulaya na leo hii anaondoka iniesta kiukweli inaumiza sana na sioni dalili ya kutibu ugonjwa huu unaotukabili, kama klabu inasajili wachezaji kama arda turan, alex vidal, andre gomez na paco alcarez. hivi tunashindwa kitu gani kuwapa pesa athletico ili watuuzie koke na saul?
- tumelipa euro million 40 msimu uliopita kwa average player paulinho halafu ndani ya msimu mmoja anaondoka na kurudi kule kule alikotoka, kuna taarifa nimekutana nayo imenishangaza sana kwa sababu inasemekana dili la paulinho kuja barca ilikuwa ni la kibiashara zaidi kwa rais Josep Maria Bartomeu, huyu bwege alikaa madarakani kwa ajili ya maslahi yake zaidi na ndio maana sishangai kukuta anashitakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi na mahakama kuu ya spain muda huu.
- eneo jengine ambalo hatupendi kuambiana ukweli wapenzi wa barcelona japokuwa lina udhaifu ni kiungo mkabaji, sergio bosquet amechoka mnooo na klabu wala haijali kutafuta mchezaji mwengine atakayempa ushindani sergio. kabla ya kombe la dunia kwenye thread ya dondoo za kombe la dunia niliwahi kuandika ya kwamba spain wanakwenda kudhalilika kwenye michuano hii kama hawajapata dawa ya kupambana na timu zinazocheza soka la kisasa, kudhalilika kwa spain ni sawa sawa na kudhalilika kwa barcelona na sababu kifalsafa tunafanana.ilifika wakati msimu huu bila ya aibu tunamsifu umtiti eti amecheza vizuri sana jambo ambalo si kawaida yetu wapenzi wa barcelona kusifia mabeki. tunahitaji kiungo mwenye uwezo wa kucheza soka la aina yoyote lile linalochezwa na timu pinzani, jaribu kuwaangalia wapinzani wetu jinsi wanavyofaidika na uwepo wa casemiro, manchester city wana fernandinho, ufaransa na chelsea wanaringia ngolo kante. kwenye timu inayojengwa na wachezaji nyota unahitaji mwanadamu asiyewaza muda wa kukoga kama hawa lakini kwetu sisi tokea aondoke seidou keita tumekuwa kimya sana.wakati ambao PSG wanapeleka ofa ya 35 million kwa ngolo kante sisi tunapeleka ofa ya 35 million kwa mchezaji kutoka ligi ya brazil. tusipokuwa makini hata liverpool watatudhalilisha msimu huu na baadae mashabiki pinzani wapate kumtukana mungu wa mpira lionel messi. viva barcelona
ngoja niisome hii habari inayosema ndege ya mpya inagharimu 67 million ikiwa kwenye lami na 30 million ikiwa angani, kiukweli imenivutia sana