hivi messi ni binadamu wa kawaida kweli?
Ni binadamu lakini siyo wa kawaida. Ni kutoka sayari nyingine huyo.
Kama ningekuwa na uwezo, ningeruhusu wazee wa Genetic Engineering watutengezee kopi ya Messi10 kwenye Maabara.
Na hili linawezekana, kwa maarifa yangu kidogo niliyonayo, sayansi hiyo inaitwa "Cloning". "Cloning" ni mchakato wa kutengeneza kopi sawa (identical copy) ya kiumbe hai (organism), seli au dutu (gene) kutokana na kiumbe, seli au dutu (gene) halisi (original).
Kiumbe hai, seli au dutu (gene) sawa (identical) inayopatikana kutokana na kiumbe hai, seli au dutu (gene) halisi (original) huitwa "clone".
"Cloning" hufanyikaje?, seli ya kawaida (somati cell) yenye "chromosomes 46" huchukuliwa toka sehemu ya mwili, isiwe "sex cell" kutoka kwenye kiumbe, cell au dutu (gene) halisi (original) (hapa, somatic cell lazima itolewe kwenye mwili wa Messi10) ili kupata kopi ya Messi10) ili kutengeneza kopi yake (clone).
Baada ya hapo, inachukuliwa "female sex cell" yenye "chromosomes 23" kutoka kwa kiumbe hai chochote (kwa kesi hii hapa lazima awe binadamu).
Kisha, zile chromosomes 23 ktk "female sex cell" zote zinatolewa linabaki kasha tu. zoezi linalofuata, huwa ni kuchukua zile "chromosomes 46" kutoka kwenye "somatic cell" na kuzi-fix (kuziweka) ndani ya lile kasha la "female sex cell".
Mwisho, upandikizaji (implantation) wa hiyo "female sex cell" (ikiwa na zile "chromosomes 46" zilizowekwa baada ya kutolewa kwenye "somatic cell") hufanyika katika mji wa mimba kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke.
Mwanamke huyo atakuwa ana ujauzito kama ule unaopatikana kwa njia ya kawaida. Na baada ya miezi 9 atajifungua kopi ya Messi10 kwa 100% kwa sababu "chromosomes 46" zote zimetokana na yeye mwenyewe.
NB: International conventions kuhusu haki za binadamu haziruhusu hii kitu. So, its an illegal and strictly prohibited.