FBI kuhusika katika kuchuja viongozi watakaompokea Obama

FBI kuhusika katika kuchuja viongozi watakaompokea Obama

Wewe watu wenye akili Zao Hawawezi kuamini Polisi wa Tanzania na Serikali yake.
 
Ingekuwa enzi ya MUSSA upuuzi huu wala usingetokea; lakini kwa vile watawala wetu ni vifuu ndio maana nchi haina hadhi tena!!!
 
Kwa hiyo Obama akisema ccm muondoke madarakani mnaondoka sio? Halafu hujaelewa logic.....,sio kwmba Obama asije,leo hii mtu wa kumpa mkona Obama anateuliwa kama sio aibu nini nini? Kweli akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa.

rais ni wa marekani acha wamarekani wachague rais wao nani wa kumpa mkono nani sio wa kumpa... do you have any problem with that..

i mean come on... utalazimishaje mtu flani nimsalimie hata kama itikadi zetu za kisiasa / au mambo flani hatuelewani..?

ni sawa sawa unambie me nimpe mkono msigwa .. that will never happen "over dead body".. but within CDM wapo ninao weza kuwapa mkono
 
Hii ni kutokana ziara ya siku mbili ya Rais Obama nchini.
Hii ni aibu ya Tz kwani haiwezekani kila kitu kiendeshwe na mgeni wako wakati mwenyeji yupo.Shughuli zote za uwanja wa ndege kupokea wageni,kukagua mizigo ni kazi ya usalama waTaifa la Marekani.Hivi tuko huru au? Hata mambo yetu ya ndani tunaingiliwa? Hii ni aibu kubwa sana!
Tunaona wafanyakazi wa uwanja wa ndege wamepewa likizo ya siku mbili kwa ajilia ya ujio wa Obama.Hii ni aibu! Huku tukijadili nani/mawaziri gani watshikana mikona na Obama,hii ni aibu!. Wenzetu wanajadili masharti gani magumu ya kuyaweka kwenye misaada yao,sisi tunajadili upuuzi.
Jiji la Dar limekuwa safi na halina msongamano tena,najiuliza kumbe tunaweza kuondoa tatizo la msongamano wa magari na uchafu wa jiji ila kumbe ni uzembe,uvivu na udhaifu wa kusimamia/kutatua matatizo haya.
Najiuliza kwa nini kwa ujio wa Obama imewezekana? Kweli serikali ya Jk ni dhaifu,kwa hili la ziara ya Obama ni ushahidi tosha.
Kwa mantiki hii,Tanzania si lolote si chochote.Kumbe hata Obama akisema rais Kikwete akamate wala rushwa,mafisadi na wauza madawa ya kulevya anaweza.kama haya yanawezekana bila kushinikizwa akishinikizwa je itakuaje?
Leo hii,ofisi za uwanja wa ndege wamepewa wageni,unafikiri watatoka na nini? Au watajua mabaya na siri ngapi za kwetu? Kama sio aibu ni nini? Magamba najua watapinga hili
This is unbeliavable. Why would they treat us like this? Actually they have reduced us to nothing. Lakini inawezekana huyu bwana mkubwa ana maadui wengi.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 


rais ni wa marekani acha wamarekani wachague rais wao nani wa kumpa mkono nani sio wa kumpa... do you have any problem with that..

i mean come on... utalazimishaje mtu flani nimsalimie hata kama itikadi zetu za kisiasa / au mambo flani hatuelewani..?

ni sawa sawa unambie me nimpe mkono msigwa .. that will never happen "over dead body".. but within CDM wapo ninao weza kuwapa mkono
Mbona wale maustadhi wa uarabuni hawapati mapokezi mazito Kama haya?
 


rais ni wa marekani acha wamarekani wachague rais wao nani wa kumpa mkono nani sio wa kumpa... do you have any problem with that..

i mean come on... utalazimishaje mtu flani nimsalimie hata kama itikadi zetu za kisiasa / au mambo flani hatuelewani..?

ni sawa sawa unambie me nimpe mkono msigwa .. that will never happen "over dead body".. but within CDM wapo ninao weza kuwapa mkono

Hata wewe Msigwa sidhani kama anaweza kukupa mkono wake kwani unajulikana kama jangili unaemaliza tembo wetu huko mbugani!!
 
Hakuna ugeni mkubwa zaidi ya wakwe, lakini wakija huwaachi wajifanyie kila kitu
 
Kama sio GT utapinga tu...wewe mgeni unamkaribisha kwako halafu anakuwa ndio mwenye maamuzi ya familia yako,kama sio aibu ni nini?
Hii ni tofauti na ugeni wa familia. Kwa sheria za kimataifa, rais wa nchi yoyote akihujumiwa akiwa nchi ya ugeni, basi nchi hiyo (mwenyeji) atalazimika kugharimia uchaguzi wa kumpata mrithi wake. Wamerekani wanaamini ni gharama sana kumpata rais wao. Hiyo wanamlinda kwa gharama kubwa. Kwa mantiki hiyo rais wa marekani akiuwawa hapa nchini, tanzania italazimika kugarimia uchaguzi wa marekani, je tanzania itaweza?
 
Obama yupo live cnn...wakenya uganda wanamuuliza maswali kupitia video moja ya jibu anasema ataashuhulika na serikali zibazo kandamiza vyama vipya
 
Dar es Salaam - Juni 29, 2013

Wakati magari 150 ya msafara wa ziara ya Rais Barack Obama yamewasili nchini, majina ya mawaziri wa Tanzania yatakayoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo kuchujwa na makachero wa FBI.

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Moses Malaki aliliambia gazeti hili jana kuwa matayarisho ya ujio wa Rais huyo ni kabambe na hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Pia alisema shughuli za kumpokea Rais Obama, anayetarajiwa kutua Jumatatu saa 8:40 mchana, zitaanza asubuhi kwa maofisa wa Marekani kushika majukumu yote katika uwanja huo, ikiwemo kuongoza ndege, ukaguzi wa abiria na mizigo, kwa maana wafanyakazi wa uwanja huo kuwa likizo kwa siku mbili.

“Wamesema kuwa wao watasimamia kila kitu kuanzia wageni watakaoingia na kutoka na wataamua nani aingie na kutoka,” alisema Malaki. Imebainika kuwa hata idadi ya maofisa wa Tanzania wakiwemo viongozi watakaompokea pia itapangwa na Wamarekani wenyewe.

“Wenyewe wana orodha yao na wanajua nani atakuwepo au hatakiwi kuwepo katika kundi la wageni watakaompokea Rais Obama,” alisema na kuongeza:

“Nilimuuliza Ofisa Usalama wa Marekani iwapo nitaweza kumwona Rais Obama, akaniambia: Utamwona ukibahatika kuwepo kwenye orodha.”

Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe naye alikiri kuwa mawaziri wanaotakiwa kuwepo katika msafara wa kumpokea Rais Obama ni wachache watakaochaguliwa tu na Wamarekani, baada ya kuyapitia na kuyachunguza majina hayo kwanza kabla ya kuyakubali.

“Hii sijawahi kuiona, hata sisi wenyewe tunateuliwa na wakishayapitia wataamua, nani aende au asiende,” alisema Chikawe.

Hi ni hatari, lakini ni kawaida kwa nchi changa kama yetu kwa Wamerikani kufanya hivyo, lakini Rais wao akifanya ziara China kila kitu atapangiwa na serikali ya China kwani ili ni Taifa kubwa.
 
Katika hili Jakaya umeniabisha sana. Inamaana tunawaamini sana Wamarekani kiasi cha kuwakabithi kila kitu.

Lazima tuonyeshe kuwa tupo ndani ya nchi yetu, yenye uhuru kamili. Nchi inaweza kutekwa kizembe namna hii.

Punguzeni "ushikaji" ktk maswala "sensitive" kama usalama wa taifa.
 
Back
Top Bottom