FBI kuhusika katika kuchuja viongozi watakaompokea Obama

FBI kuhusika katika kuchuja viongozi watakaompokea Obama

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,483
Dar es Salaam - Juni 29, 2013

Wakati magari 150 ya msafara wa ziara ya Rais Barack Obama yamewasili nchini, majina ya mawaziri wa Tanzania yatakayoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo kuchujwa na makachero wa FBI.

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Moses Malaki aliliambia gazeti hili jana kuwa matayarisho ya ujio wa Rais huyo ni kabambe na hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Pia alisema shughuli za kumpokea Rais Obama, anayetarajiwa kutua Jumatatu saa 8:40 mchana, zitaanza asubuhi kwa maofisa wa Marekani kushika majukumu yote katika uwanja huo, ikiwemo kuongoza ndege, ukaguzi wa abiria na mizigo, kwa maana wafanyakazi wa uwanja huo kuwa likizo kwa siku mbili.

"Wamesema kuwa wao watasimamia kila kitu kuanzia wageni watakaoingia na kutoka na wataamua nani aingie na kutoka," alisema Malaki. Imebainika kuwa hata idadi ya maofisa wa Tanzania wakiwemo viongozi watakaompokea pia itapangwa na Wamarekani wenyewe.

"Wenyewe wana orodha yao na wanajua nani atakuwepo au hatakiwi kuwepo katika kundi la wageni watakaompokea Rais Obama," alisema na kuongeza:

"Nilimuuliza Ofisa Usalama wa Marekani iwapo nitaweza kumwona Rais Obama, akaniambia: Utamwona ukibahatika kuwepo kwenye orodha."

Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe naye alikiri kuwa mawaziri wanaotakiwa kuwepo katika msafara wa kumpokea Rais Obama ni wachache watakaochaguliwa tu na Wamarekani, baada ya kuyapitia na kuyachunguza majina hayo kwanza kabla ya kuyakubali.

"Hii sijawahi kuiona, hata sisi wenyewe tunateuliwa na wakishayapitia wataamua, nani aende au asiende," alisema Chikawe.
 
kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la leo, ni kuwa viongozi wakiwemo mawaziri na wabunge wataokutana na Obama watachaguliwa na wamarekani wenyewe kwa kutumia vigezo vyao , bila shaka watu wenye sifa katika kukuza demokrasia na wasio mafisadi. kwa kuwa kuna ushahidi wa wazi kuwa mwigulu na wenzake hapo juu ni waratibu wa vikundi vya kutesa watu, kubambikizia wengine kesi za uongo, na kulitumia jeshi la polisi vibaya ni vema hawa watu wasiruhusiwe kabisa kushiriki hiyo ziara, hili litakuwa funzo kwa madikteta wengine
 
Ivi uhuru tulio upata wa Africa ni upi? Ivi mpaka lini tatacha kuji dhalilisha na kudharauliwa na hawa tunao waita wahisani? Yani mgeni ajiamulie ni viongozi gani watakao mpokea! Sijaona na sikutegemea kuona. Hivi kweli viongozi wetu wakiendaga huko ktk nchi zao hufanyaga hivi? Jamani sisi wa Afrika bado ni watumwa bado hatujawa huru mwafrika bado si chochote kwa wazungu, roho ina niuma sijui chakufanya. Laiti ninge kua na nguvu ya ushawishi ningeitisha maandamano nchi nzima kupinga ujio wa huyu shetani (Obama). Sisi huku ktk nchi zao tuna dharaulika nakuonekana kama vibweka, hata wanapo kuja viongozi wetu wa kitaifa huwezi jua labda uwe ni mtu mfuatilia habari. Mfaransa hawezi kushulika na ujio wa mtu kama Kikwete, Zuma wala sal ni sisi tu Africa. Leo mpaka mtu aliopo chamwino mtamba swala kiteto mpaka rwaluke anajua kua kuna ujio wa Obama nchini kwetu. Nachukia sana.
 
Kikwete alikuwa UK juzi juzi hata gazeti la Evening Standard linalogawiwa bure hawakuandika chochote kuhusu Kikwete. Mkuu nakukubalia Africa tuna miaka 2000 kufikia walipo wenzetu sasa hivi. Na bado kuna watu wanajidanganya ukiwa na pesa Dar kama huko New York thubutu!
 
Back
Top Bottom