Hii ni kutokana ziara ya siku mbili ya Rais Obama nchini.
Hii ni aibu ya Tz kwani haiwezekani kila kitu kiendeshwe na mgeni wako wakati mwenyeji yupo.Shughuli zote za uwanja wa ndege kupokea wageni,kukagua mizigo ni kazi ya usalama waTaifa la Marekani.Hivi tuko huru au? Hata mambo yetu ya ndani tunaingiliwa? Hii ni aibu kubwa sana!
Tunaona wafanyakazi wa uwanja wa ndege wamepewa likizo ya siku mbili kwa ajilia ya ujio wa Obama.Hii ni aibu! Huku tukijadili nani/mawaziri gani watshikana mikona na Obama,hii ni aibu!. Wenzetu wanajadili masharti gani magumu ya kuyaweka kwenye misaada yao,sisi tunajadili upuuzi.
Jiji la Dar limekuwa safi na halina msongamano tena,najiuliza kumbe tunaweza kuondoa tatizo la msongamano wa magari na uchafu wa jiji ila kumbe ni uzembe,uvivu na udhaifu wa kusimamia/kutatua matatizo haya.
Najiuliza kwa nini kwa ujio wa Obama imewezekana? Kweli serikali ya Jk ni dhaifu,kwa hili la ziara ya Obama ni ushahidi tosha.
Kwa mantiki hii,Tanzania si lolote si chochote.Kumbe hata Obama akisema rais Kikwete akamate wala rushwa,mafisadi na wauza madawa ya kulevya anaweza.kama haya yanawezekana bila kushinikizwa akishinikizwa je itakuaje?
Leo hii,ofisi za uwanja wa ndege wamepewa wageni,unafikiri watatoka na nini? Au watajua mabaya na siri ngapi za kwetu? Kama sio aibu ni nini? Magamba najua watapinga hili