FBI kuhusika katika kuchuja viongozi watakaompokea Obama

FBI kuhusika katika kuchuja viongozi watakaompokea Obama

Tatizo letu Waafrica wasasa sio wazalendo ka walio tutangulia, achilia mbali kuji tambua na kuji thamini, tena wengi wetu hatuji amini yani utafikiri tumekuja duniani kuja kuwa wanyonge kwa hawa wenye rangi nyeupe. Hii ndio nafasi waitumiayo wenzetu kutu dharirisha na kutu buruza kila leo. Utakuta mpaka kiongozi wa ngazi yajuu katika taifa (Rais) nae ni walewale (kama raia wake tu) unaweza ukasikia kati ya mambo yatakayo jadiliwa siku hiyo baina ya viongozi hao ni Rais wetu kumshitakia Rais mwenzie (Obama) kua Kagame kamtukana na mambo ya kijinga kama hayo. Sasa je unategemea nini kama sio kudharauliwa? Kwani Obama ninani ktk dunia hii? Kama ni kiongozi basi hana tofauti na Ermando Imirio Gebuza, sasa kwanini tumtukuze kama mungu mtu? Nachukia sana tabia hiyo
Pole leo umekasirika kwa sababu bwana yako mwigulu sio mmoja wa kumpokea, mwenye tatizo ni Kikwete mwenyewe amemkubalia kuja nchini na kukanyaga ikulu yake juu ya kichwa uwanja wa ndege kwa siku mbili unakuwa mikononi mwa wamerekani pwani yote ya Tanzania chini ya wamerekani,jiji lote chini ya wamerekani watanzania wamekataliwa kuingia na kutoka hapo mjinga ni nanai si kikwete
 
Mtu kama Mwingulu Chemba, Kinana, Nchimbi, Pinda kwa nini wasichujwe? Hebu ongezea hii list ya watu waliopoteza sifa ya kumlaki Baraka Husseni Obama
 
Ulinzi wetu si dhaifu kwa viwango vyetu vya kibongo, lakini ulinzi wetu ni dhaifu mno kwa viwango vyao, yaani wanaona tuko nyuma miaka 60 kwenye ulinzi! Kuna mzungu mmoja anaandika makala kwenye gazeti moja la kila wiki anasema hata ndege zetu za ulinzi ni zile za miaka ya sitini au early 70's. Na kwa jinsi hii tunathibitisha hatuwezi kuwapa ulinzi wanaoutaka.
Mkuu hizo ni fikra zako wewe kama wewe, ila hawa jamaa wamelenga kutudhalilisha waafrika. Jiulize, kama issue ni ulinzi kwani ni matukio mangapi ya nayo itwa ya kigaidi yanayo tokea kila uchao nchini kwao? Tuache kujishusha waafricw wenzangu tupinge jambo hili (maswala ya ulinzi kwenye ujio wao kua chini yao). Waziri waulinzi unafanya nini watu wanatuchezea makalio nchini kwetu?
 
Chonde chonde Pinda na Wasira msiende uwanjani watoto Sasha na Malia watastuka
 
zenj sii nchi kamil????

sasa kwa nini Obama anakuja Tanganyika na haendi Zenj??

Bkb na Kigoma ni Mikoa ya Bara

kuna nini zenj mti wenye matunda ndiyo hufuatwa. Labda sema kwa nini haendi Kenya ili hali ni kwao kiasili
 
Kama Waziri anachukua Rushwa kuangamiza wananchi wake, atashindwa kuchukua Rushwa kumdhulu Obama? Integrity ndio key ya mchujo huu, wote watakaotolewa katika list, mh JK wateme
 
Ndugu zangu ziara yote ya raisi obama imepangwa na makachero wa marekani wenyewe na sio mashushushu wa kitanganyika....!!! Hivyo wamarekani wenyewe wameamua kutofika zanzibar na sio akina membe wala mamba....!!! Sasa iweje iwe gumzo eti mbona bwana obama hajafika zanzibar....??
Pia wamarekani wanajua fika kuwa wazanzibar hawana haja ya kumuona wala kumpokea raisi obama ndio maana hawajampeleka zanzibar.
Lakini ndugu zangu mnalijua lililomleta obama au mnashangiria tu ujio wake.....??? Na kama hamlijui basi
sisi tunawasubirini watanganyika tuje kukuoweni......!!!!
 
Pole leo umekasirika kwa sababu bwana yako mwigulu sio mmoja wa kumpokea, mwenye tatizo ni Kikwete mwenyewe amemkubalia kuja nchini na kukanyaga ikulu yake juu ya kichwa uwanja wa ndege kwa siku mbili unakuwa mikononi mwa wamerekani pwani yote ya Tanzania chini ya wamerekani,jiji lote chini ya wamerekani watanzania wamekataliwa kuingia na kutoka hapo mjinga ni nanai si kikwete
Mjinga namba moja ni wewe unae sapoti udhalilishaji huu. Zingekua enzi zaakina Erduard Mondelane tunge kuita kibaraka lakini ktk dunia ya leo wewe ni kishuruwala, huna uzalendo hujui thamani yako kama MuAfrica. Mimi Mwafrica, najivunia kua/kuitwa mwafrica nitapigana vita baridi kuutetea uafrica wangu. Napinga kwanguvu zote (mpaka povu linanitoka) udhalilishaji watufanyiao wazungu.
 
sasa kama mtanzania anaweza kupakaziwa madawa ya kulevya uwanja wa ndege na watu wa usalama, je juna nchi makini inayoweza kuwa na imani na ulinzi wa rais wao hapo uwanjani.
 
Ndugu wana jf nimejiuliza sijapata majibu naomba ufafanuzi kwa suala hili la ujo wa obama. Kwa kawaida huwa najua mgeni anapomtembelea mwenyeji anakuta ameshaandaliwa kila kitu hapo ugenini lakini kwa mgeni wetu huyu obama naona mambo ni tofauti!
Mkuu labda jibu unalo lakini unasita kuliweka, nitakusaidia kidogo kulitema jibu kamili
Je kauli zitolewazo na wengi wa viongozi wetu, wananchi tunaziamini? Matendo mengi yafanywayo/maamuzi mengi yatolewayo na viongozi watu, wananchi tunayakubali? Kama kiongozi anachukua Rushwa kuangamiza wananchi wake, Je huyu kiongozi ni wa kuaminiwa?
 
Ivi uhuru tulio upata wa Africa ni upi? Ivi mpaka lini tatacha kuji dhalilisha na kudharauliwa na hawa tunao waita wahisani? Yani mgeni ajiamulie ni viongozi gani watakao mpokea! Sijaona na sikutegemea kuona. Hivi kweli viongozi wetu wakiendaga huko ktk nchi zao hufanyaga hivi? Jamani sisi wa Afrika bado ni watumwa bado hatujawa huru mwafrika bado si chochote kwa wazungu, roho ina niuma sijui chakufanya. Laiti ninge kua na nguvu ya ushawishi ningeitisha maandamano nchi nzima kupinga ujio wa huyu shetani (Obama). Sisi huku ktk nchi zao tuna dharaulika nakuonekana kama vibweka, hata wanapo kuja viongozi wetu wa kitaifa huwezi jua labda uwe ni mtu mfuatilia habari. Mfaransa hawezi kushulika na ujio wa mtu kama Kikwete, Zuma wala sal ni sisi tu Africa. Leo mpaka mtu aliopo chamwino mtamba swala kiteto mpaka rwaluke anajua kua kuna ujio wa Obama nchini kwetu. Nachukia sana.

Nakubaliana na wewe mkuu sisi bado ni watumwa na hasa viongozi wetu ndo watumwa zaidi nina uhakika mwalimu asingekubali huu usengerema na hata marekani yenyewe isingedhubutu kufanya hivyo sasa hivi na huyu mzururaji wetu tunadharauriwa sana
 
Hawa fbi wasengerema sana yani wanafukuza wafanyakazi wa airport kwa siku 2 na jeikei karuhusu? This is the ish the country is totally serukamba up.
 
Back
Top Bottom