FASTJET: My first and last experience

FASTJET: My first and last experience

Pole Tiba hata mimi niliwahi kukutana na dhahama inayofananafanana ya kwako kutoka kwa hao FastJet. Ukweli ni kwamba sales officers wao hawako makini wanapowasiliana na wateja.Mimi nilisafiri nao kwa mara ya kwanza kutoka DAR kwenda KIA lakini yaliyonipata kabla ya ku check in niliapa sijku hiyo kuwa sitarudia tena kutumia usafiri huo.akwa kifupi nililipishwa nauli mara mbili kwa kosa lililotokana na uzembe wasales officer wao
 
Ungewahi kufika ungeruhusiwa. Mimi nimefanya safari na fast jet mara kibao sijapata usumbufu wowote hata precision air sijapata usumbufu ila kuna moja nilichelewa precision na wakanikatalia ku check inn na nikakubali uzembe ulikuwa wangu
 
kama wanaofanya kwenye industry hii na haya ndio maelezo yao basi watz bado tuna safari ndeeefu.Check-in cut off time wamesema 40min....ina maana natakiwa kuja muda wowote before cut off time, hata kama ni kasoro dakika moja.Tujifunze kufuata utaratibu...tatizo watu wa airlines wanauza nafasi kwa watu walio kwenye waiting list.......40 min zinamtosha abiria kutoka check in dest kwenda departure lounge. Kwa waendao nje muda unaongezeka kwa sababu ya taratibu za uhamiaji.

Huo ndo ukweli mkuu mimi naamini hata kama FJ ilipata matatizo na ni kweli FJ ilipata hitilafu kwenye injini moja lakini kama unachelewa kaunta hata kwa dk hata 5 ku board na ndege ya Fastjet ni ngumu sana na hiyo yote inatoka na sababu wanao handle ground operation ni swiss port na wanafanya kwa kukodisha which means wanafunga katika muda ule ule kuepusha extra time cost unless kuwe na que ndefu.. Hapa mdau ameshindwa kuelewa hili..
 
Remember! FASTJET - SMART TRAVEL
if ur not smart you won't travel by fastjet............!


Kweli SMART TRAVEL!!

Mnaboard alafu mnashuswa eti ndege aijakaguliwa ..this is only with FASTJET!!
 
Ni uzoefu wa kutumia ndege za namna hiyo. Nilishashuhudia ndege ikiondoka dakika 15 kabla ya muda ulioandikwa na kisa walikuwa wanatakiwa kuipeleka ndege sehemu nyingine ikabebe abiria. Waliacha hadi watu waliokuwa wamecheck-In.

Ni ushauri tu wa kusema "za kuambiwa, changana na za kwako." Siyo lazima uufuate wangu. Wewe fuata waliouandika wao yaani dakika 40 kabla kama dada yetu hapo juu.
Hizo sheria umezitoa wapi mkuu?

Naomba msaada ili nisije kufumaniwa.....

Hadi leo najua kuwa local flights in saa 1 kabla ya safari na international flights in 2-3hrs.

Hizo za kwako umezitoa wapi kaka?

Babu DC!!
 
Mie nilishashuhudia Local na International ndege ikisimamishwa kusubiri abiria. Juzi tu jamaa yangu kaniambia kuwa walikuwa UK na ndege ikasimamishwa kwa sababu tu abiria mmoja alikuwa ana matatizo kwenye ticket yake na wakawa wanamsumbua. Huyo Mama msumbufu alipata simu moja tu na akashika adabu yake. Ila akafanya juu chini jamaa achelewe. Ubabe wa jamaa wakafanya wale madada wanaoruhusu abiria waingie kwenye ndege wakadai computer yao ina matatizo na jamaa alipofika tu, computer ikapona.

Hiyo hiyo Precision tulishawahi kucheleweshwa Mwanza na hakukuwa na sababu ila mwisho tukamuona Muheshimiwa sana Waziri Masha akiingia kwenye ndege bila haraka yoyote na alipoingia tu, ndege ikaondoka.

Ila kwa muda naona unaleta utata maana Dark City anasema hivi "...Hadi leo najua kuwa local flights in saa 1 kabla ya safari na international flights in 2-3hrs." na wewe unasema masaa tofauti kwa local flight. Sasa sijui nani anasema ukweli kati yenu.

Anyway, wangu ulikuwa ushauri ili usije ukakuta siku Pilot mkorofi au akina mama wakorofi wakakuacha, ni heri ufike mapema.
Kaka acha kulinganisha international flight na local.. Mfundishe huyu Tiba ajue kwamba international wanasaidia wanaochelewa but local airline haiwezekani maana wanakodisha madirisha ya check in

Binafsi ni mteja mzuri sana wa fast jet na nitaendelea kuwa mteja wao kwa sababu nimeyakubali mapungufu yao.. Na ukilinganisha Fast jet na precision fast jet wana mapungufu machache kuliko precision.. Muhimu ni kuelewa terms and condition zao vizuri...

Terms za fast jet reporting time ni 3 hours before departure na ukichelewa sana watakusaidia lakini mwisho wa kufanya check in ni 40 minutes before departure.. So kwa kigezo hicho mtoa mada alichelewa check in..

Na wanafanya hivyo sababu Fast jet hawana dirisha la check in kama qatar au emirates. Wao wanachofanya wanaazima dirisha kwa ajili ya check in na ndio maana wanasema dakika 40 before safari hawawezi kusaidia wacherewaji sababu muda wa kukodisha dirisha unakuwa umeshaisha...

Binafsi nilishachelewa Qatar airways nakumbuka ilikuwa tarehe 24/6/2012 pale JNIA na tulifika saa sita kama na nusu hivi wakati ndege inaondoka saa 7 lakini kwa huruma walikuja wafanyakazi wao wakawasha computer za check in, wakatuprintia sticker za bags.. Tukachekiwa airport fasta na tukaingia kwenye ndege na kuondoka na hii iliwezekana sababu wao wana dirisha lao maalumu pale airport hawakodishi na wana haki ya kuwasha computer muda wowote tofauti na fast jet wanaotegemea Swissport..

Ukichelewa local airline imekula kwako lakini ukichelewa international airline unaweza ukaeleweka na kuwashiwa computer for check in maana wanajua wao wanatembea kwa Connections kwenye hubs zao so wakikuacha wanajua utateseka sana kwenye connection maana kuna miji mingine hazina connection flights za kila siku so lazima upandishwe ndege tu ili wakuokoe ukaiwahi connection yako
 
Last edited by a moderator:
Ni uzoefu wa kutumia ndege za namna hiyo. Nilishashuhudia ndege ikiondoka dakika 15 kabla ya muda ulioandikwa na kisa walikuwa wanatakiwa kuipeleka ndege sehemu nyingine ikabebe abiria. Waliacha hadi watu waliokuwa wamecheck-In.

Ni ushauri tu wa kusema "za kuambiwa, changana na za kwako." Siyo lazima uufuate wangu. Wewe fuata waliouandika wao yaani dakika 40 kabla kama dada yetu hapo juu.


Sawa mkuu,

Kwa sababu tuna level tofauti ya uzoefu, naomba niishie hapa.

Suala la msingi ni mtu kuangalia masharti yaliyoko kwenye ticket kwani mwisho wa siku, huo ndiyo mkataba kati ya mteja na kampuni.

Babu DC!!
 
Tiba, bado una hasira? Simanzi au kisasi? Kila jambo linawezekana mahali popote hakuna mkamilifu. Na usitegemee ukamilifu kwa yeyote, kwa sababu wana mapungufu. Huduma kamilifu asilimia zote hakuna. Vilevile, kila mtu ana haki ya maoni yake binafsi, ila haiingii akilini kuwategemea wengine wakubaliane na msimamo wako, ukiangalia msimamo wako umejengwa na matukio machache na hata yangekuwa mengi mbona kawaida tu, kula ugali wako, maisha yanaendelea. Kuna mtu alisema, wasamehe kabla!!
 
Pole sana kwa matukio na samahani kwa nitakayoyasema.

Nilishaona kwa macho yangu, desk check ya Turkish Air ikiwa imefungwa saa moja kabla. Ila alikuwepo Mbabe mmoja akapiga simu kwa mama mmoja ndani na wakafungua ingawa wafanyakazi wa Turkish Air walishasema kuwa hadi kesho.
Naona nyie mlikosa mtu kama huyo.

Ila nashindwa kuelewa kitu kimoja, ninavyofahamu mie ni kuwa kwa sasa kwa sheria za ulinzi zilivyo uwanja wa ndege, unatakiwa ufike masaa mawili kabla yaani dakika 120 kabla. Sasa wewe nani alikuambia unafika dakika 40 kabla? Dakika 40 kabla ni kuwa ndiyo mnajiandaa kwenda kuingia kwenye ndege tayari na si kwamba ndiyo unafanya Check-In.
Naona ukaja tena kuchelewa hata Bus la kwenda KIA. Yaani hata Bus likakuacha jamani? Nalo sijui utasingizia nini?

Pole sana kwa tukio ila kumbuka kuwa uwanja wa ndege unatakiwa kufika saa MBILI kabla popote pale duniani labda kama umesha Check-In online na huna mzigo, yaani unafika tu na kuingia ndani kusubiri kupanda ndege.

International flight ndio 2 hrs, domestic ni 1 hr....... hiyo dakika 40 ya fast jet ni ya kwao
 
Mhhh kama hali zenyewe ndio hizi bora niendelee na box tu, at least life is predictable kwa maeneo flani huku duniani...... ntarudi huko badae sana kuja kula pensheni ya box
CC. Nyani Ngabu na wabeba box wooote popote walipo.
 
Last edited by a moderator:
Whaaat! Kumbe na wewe unapiga boksi?

Mimi ndio najiandaa kuzamia pande za boxini, ila nishapewa orientation ya kazi yenyewe inavyofanyika(akili kidogo ukitoka hapo unapata hot shower unapata kapuchino au kinginecho, unakaa online unasoma blog zote za bongo weeee, unabishana blogini weeeeeee, unapiga umbea wote then unalaza ubavu kidogo box linaaza tena next day....mzunguko unajirudia hadi muda wa pensheni)...........vipi kuna la ziada uniongezee nondo?
 
mhm mbona kosa ni lako na si wao tatizo hili mimi mwenyewe lisha nikuta na nikajifanya najua kufatilia sana niakumbuka kwani kwenye ticket inasema cheking close 40 min b4 dpt na main gate closes 10 min b 4 dpt kwenye kwenye ticket ina sema ukichelewa mwenyewe they dnt refund na uki change route kuna kahela pia unless wao ndo wame sababisha ukachelewa au usisafiri wanatoa 8000 kwa masaa mawili if not 6 au rfund TATIZO HATUSOMI TERMS AND CONDITION
nilipata tatizo kama lako ila sasa nimejifunza hata niki nunua kitu dukani nasoma ph ingridients na exp date na manufacture date....kwa hiyo mkuu pole kwa gharam nyingi ila kosa ni lako wala si fast jet ungelisoma ticket yote yasinge tupata hayo
 
Kiswahili hiki, khaaa!! You made my day hahahahaaaaa
Mimi ndio najiandaa kuzamia pande za boxini, ila nishapewa orientation ya kazi yenyewe inavyofanyika(akili kidogo ukitoka hapo unapata hot shower unapata kapuchino au kinginecho, unakaa online unasoma blog zote za bongo weeee, unabishana blogini weeeeeee, unapiga umbea wote then unalaza ubavu kidogo box linaaza tena next day....mzunguko unajirudia hadi muda wa pensheni)...........vipi kuna la ziada uniongezee nondo?
 
Pole sana mkuu.....kumbe tulikuwa wote pale......ila mwenzio nilicheza ushapu nikaondoka na 5H-CCM.......

Preta usinikumbushe hii kitu, hii ndio ndege ya kwanza kunitoa ushamba wa kupanda ndege

97863.jpg
 
Wasipo badilika vichwa vyote vitawakimbia.
 
Kuna mfanya kazi wa fast jet?? Ani inbox nina maswali kidogo.
Fast jet swala la time wako serious mie nina mkosi na precision kukaa uwanjani zaidi ya masaa matatu ni kawaida sanaaa.watu tunaendelea na story tukisubiri .
 
Very high Risk traveling by buses! magari ya Arusha ni majeneza yanayotembea. Generally, usafiri wa mabasi ni majeneza yanayotembea! They are very rough!
Hahahaha!!!
Unasema ukweli wa upande mmoja tu.
Wewe unaamini usafiri wa ndege wa hapa Tanzania kuwa ni salama?
Chunguza kwanza kabla ya kusema.
Kuanzia Air Tanzania, Precision Air mpaka Fastjet, wote hao ndege zao ni Second handed, zimechoka mbaya na Spanner mkononi.
Yale pia ni majeneza ya Angani.

Japokuwa usafiri wa bus hapa Tanzania sio salama sana lakini route ya Dar-Arusha ya bus ndio ina huduma nzuri zaidi kwa hapa Tanzania.
 
Pole Tiba hata mimi niliwahi kukutana na dhahama inayofananafanana ya kwako kutoka kwa hao FastJet. Ukweli ni kwamba sales officers wao hawako makini wanapowasiliana na wateja.Mimi nilisafiri nao kwa mara ya kwanza kutoka DAR kwenda KIA lakini yaliyonipata kabla ya ku check in niliapa sijku hiyo kuwa sitarudia tena kutumia usafiri huo.akwa kifupi nililipishwa nauli mara mbili kwa kosa lililotokana na uzembe wasales officer wao

baba koku, pole kwa mkasa uliokupata. Now you can imagine una safari ya muhimu ambayo ukiihairisha unatengeneza matatizo zaidi, na hivyo unajikuta unalazimika kuingia extra costs. It very disgusting lakini nadhani wenzetu hawa they dont care na wala hawaoni kwamba kumuingiza mteja wao extra cost si kitu kizuri. Mtu anakwambia tena kwa urahisi, nitakusaidia lakini msaada pekee ninaoweza kukupa ni kuku uzia ticketi nyingine.

Tiba
 
Back
Top Bottom