FASTJET: My first and last experience

FASTJET: My first and last experience

Mkweli umesema kweli; sasa dawa yake ipo na ndogo mkuu;
Nia za wengi wetu !! " Nia na ile Dhana tuliyo nayo " tukitibu hiyo tu....tija nzuri itakuwepo!!
ila kumbuka ujinga ni mwingi bado!
 
Mzee Ndege ya fasjet kutoka JRO kwenda dar inaondoka saa 2135 abiria wote wanashauriwa kuwa uwanjani masaa 2 kabla ya safari hata hivyo Kaunta inafungwa Dk 4o kabla ya ndege kuondoka ikiwa na maana kaunta itafungwa saa 2255 hili halina utata kabisa hata kama utachelewa Dk 2 ni vigumu kuruhusiwa ku board sababu wale jamaa wako on time na muda unaopewa wewe kuripoti ni masaa 2 kabla.
Hata kama ndege ilipata hitilafu kama huku chek in huwezi safiri nayo mjomba unless upate mtu wa kujuana hapo Airport ndo atakusaidia sababu kampuni ya inayotumiwa kukupatia boarding pass ni swissport na wao hawa husiani na mambo ya kuruka au kutokuruka kwa ndege.. Na siku ni kweli FJ ilipata matatizo kwenye Engine yake moja hali iliyolazimu kusubiri matengenezo ya hali ya juu...
Mimi nina DOUBT hapa
-Inawezekana uli mis calculate muda wako wa ku check in that's why ulikataliwa ku board, kwangu mimi sikubaliani na wewe kuwa kaunta ilifungwa Dk 55 kabla ya ndege kuondoka.. hiyo haiwezekani hata kidogo..
 
Wana Jamvi,

Siku ya tarehe 26 April 2013, nilikutana na mkasa wa hawa jamaa zetu wa Fastjet na tangia siku hiyo nilinuia, kutokufikiria kutumia usafiri wa hii ndege tena. Kisa chenyewe kilikuwa hivi;

Nilisafiri kwa gari binafsi kutoka Dar kwenda Arusha tarehe 21 April 2013 na nilitarajia kurudi Dar Ijumaa ya tarehe 26 April 2013 kwa kutumia ndege ya Fastjet iliyokuwa iondoke Arusha (KIA) saa 3:30 usiku. Nilikuwa na tiketi mkononi. Taratibu za Fastjet ni kuripoti dakika 40 kabla ya muda wa ndege kuondoka. Nilikodisha taxi kutoka Arusha na nilifika KIA saa 2:40 usiku. Nilipofika, taxi iliyonipeleka pale iliondoka. Kufika mlangoni, walinzi wakanimbia kwamba nimechelewa na kwamba counter tayari imefungwa na hakuna mtu wa kunicheck in. Nilimkuta na Bwana mwingine aliyekuwa amenitangulia kufika na yeye akibembeleza kuruhusiwa kuingia. Wale walinzi walikataa katakata na ukweli ni kwamba pale counter hakukuwa na mtu hata mmoja. Kwa kushirkiana na msafiri mwenzangu niliyemkuta pale, tulianza jitihada za kutaka kuonana na mwakilishi wa Fastjet pale uwanjani. Jitihada zetu za kumwona mwakilishi wa Fastjet hatimae zilifanikiwa lakini to our suprise, yule Bwana alikuwa too arrogant kupita kiasi. Alitwambia hakuna msaada wowote anaoweza kutupatia. Ndege ilikuwa bado iko pale uwanjani. Wakati tukiendelea kumbembeleza, aliitwa kwenye radio call na hivyo akatutaka tutoke ofisini kwake na kwamba angekuja kutusikiliza baadae lakini akasema msaada pekee anaoweza kutupa ni kutukatia ticket nyingine kwa ajili ya ndege ya Jumamosi asubuhi tarehe 27 April 2013.

Baadae tulipata taarifa kwamba ndege haiwezi kuondoka kwa kuwa imepata hitilafu na kwamba abiria ambao tayari walikuwa wamepanda wameshushwa na kurudi waiting room. Yule mwakilishi wa Fastjet hakurudi tena ofisini pale ingawaje tuliendelea kumsubiri. Kwa kuwa nilikuwa na mkutano muhimu wa kuhudhuria Dar Jumamosi tarehe 27 April 2013, nilianza kufanya mpango wa kuangalia uwezekano wa kupata seat kwenye ndege ya Precision Air iliyokuwa iondoke Arusha (KIA) saa 1:55 asubuhi kuelekea Dar. Bahati nzuri nilimpata mwakilishi wa Precision Air pale uwanjani ambaye baada ya mawasiliano alinihakikishia kunipatia seat kwenye hiyo ndege. Tatizo sikuwa na cash ya kulipia hiyo ticket ambayo gharama yake ilikuwa Tshs. 195,000 one way. Baada ya kuhakikishiwa seat, nililazimika kukodisha taxi ya kunirudisha mjini ili kupata hela za kulipia ticket ya Precision kutoka kwenye ATM. Nilifanikiwa kupata hela na baada ya hapo kazi ya kutafuta hotel ikaanza. Nilipata Hotel na nililala karibu saa 6 usiku.

Saa 11:30 alfajiri tayari nilikuwa kwenye ofisi za Precision Air pale Arusha ili kupanda shuttle kwenda KIA. Kufika tu, nikaambiwa tayari shuttle ilikuwa imeondoka hivyo nalazimika kutumia usafiri wangu kwenda KIA (Ukweli ni kwamba shuttle ilikuwa haijaondoka na wala ilikuwa haijafika ila mlinzi anashirikiana na taxi drivers kudanganya abiria ili wakodishe taxi zao). Nilifanya hivyo na kufanikwa kufika Dar kwenye saa 3:45 asubuhi Jumamosi. Wakati turuka pale KIA, ile ndege ya Fastjet tuliiacha pale na sijui iliondoka saa ngapi. Abiria walilala pale uwanjani bila huduma yoyote hata maji ya kunywa hawakupewa.

Nia ya kuleta uzi huu ni kuwaambia wana Jamvi kwamba wakati mwingine rahisi ni ghali. Safari hii ilinigharimu pesa nyingi sana kwa kuwa tu nilitaka ticket rahisi ya Fastjet (Tshs. 107,000) one way lakini matokeo yake niliingia gharama zifuatazo;

1. Ticket ya Fastjet Tshs. 107,000
2. Taxi Arusha KIA x 3 Tshs. 150,000
3. Hotel tarehe 26/4 Tshs. 50,000
4. Ticket ya Precision Tshs. 195,000
Jumla Tshs. 502,000

Nilinuia hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kujaribu kusafiri na Fastjet na ilikuwa mara ya mwisho pia. Sitakaa nithubutu kufanya makosa tena hata kama Fastjet wata improve huduma kwa wateja na kuajiri watu wanaoweza kuwasiliana kwa heshima na wateja.

Tiba

Ww pesa unayo kama uliweza lala room ya elfu 50 si nimambo ulijitakia mwenyewe
 
Ww pesa unayo kama uliweza lala room ya elfu 50 si nimambo ulijitakia mwenyewe

Mkuu Zamlock, wewe kwa mapendekezo yako, ulitaka nilale kwenye room ya elfu ngapi? Kumbuka to me security is my first priority and I cannot afford to sleep in a Hotel where my security will be at risk.

Tiba
 
Yaani Binti mzuri huyu akalale Guest House we jamaa...
 
ulikuwepo? kuna watu mnapenda kubishana hata na taarifa ya habari
Mzee Ndege ya fasjet kutoka JRO kwenda dar inaondoka saa 2135 abiria wote wanashauriwa kuwa uwanjani masaa 2 kabla ya safari hata hivyo Kaunta inafungwa Dk 4o kabla ya ndege kuondoka ikiwa na maana kaunta itafungwa saa 2255 hili halina utata kabisa hata kama utachelewa Dk 2 ni vigumu kuruhusiwa ku board sababu wale jamaa wako on time na muda unaopewa wewe kuripoti ni masaa 2 kabla.
Hata kama ndege ilipata hitilafu kama huku chek in huwezi safiri nayo mjomba unless upate mtu wa kujuana hapo Airport ndo atakusaidia sababu kampuni ya inayotumiwa kukupatia boarding pass ni swissport na wao hawa husiani na mambo ya kuruka au kutokuruka kwa ndege.. Na siku ni kweli FJ ilipata matatizo kwenye Engine yake moja hali iliyolazimu kusubiri matengenezo ya hali ya juu...
Mimi nina DOUBT hapa
-Inawezekana uli mis calculate muda wako wa ku check in that's why ulikataliwa ku board, kwangu mimi sikubaliani na wewe kuwa kaunta ilifungwa Dk 55 kabla ya ndege kuondoka.. hiyo haiwezekani hata kidogo..
 
Mkuu Fighter, tafadhali tiririka, mbona unafanya kutuonjesha story halafu unaacha?

Tiba

Haka kastori katamu sana lakini naogopa kushambuliwa na kukosa vitamu tena next time.....

Lakini kwa ufupi tu, makamanda tukifika kwenye mkusanyiko macho yetu huwa kwenye flowers!!

Fast jet ya tarehe hiyo Wadosi walikua wengi... hawa nao wanapenda vyabure sana!!

Totos za maana mimi niliziona mbili pale!

Mmoja alikua akienda kumcheki bro wake aliyepata ajali Dar!!

Na mwengine e bana bonge la mdada na hii stori ndio all about............
 
Jamani mbavu zangu, yaani nimecheka mpaka basi. Unajua kufanya hivyo mpaka uwe na guts la sivyo wengine tuliumbwa na nyuso za aibu na woga. Ulichokisema ni kweli customer care ni janga la kitaifa. Unakuta mtu anamhudumia mteja halafu anampandishia sauti, can you imagine?

Tiba

Sorry mkuu, mie na bibi DC tulishaapa kutopandishiwa na mtoa huduma tunayolipia kwa pensheni yetu. Ikibidi hata bukta tunavaa!!

Labda kama tumepewa complementary.

Babu DC!!
 
Haka kastori katamu sana lakini naogopa kushambuliwa na kukosa vitamu tena next time.....

Lakini kwa ufupi tu, makamanda tukifika kwenye mkusanyiko macho yetu huwa kwenye flowers!!

Fast jet ya tarehe hiyo Wadosi walikua wengi... hawa nao wanapenda vyabure sana!!

Totos za maana mimi niliziona mbili pale!

Mmoja alikua akienda kumcheki bro wake aliyepata ajali Dar!!

Na mwengine e bana bonge la mdada na hii stori ndio all about............

Roho mbaya hiyo mkuu....point yangu hapo ni kuonyesha customer care zilivyokuwa mbovu. Kuweka mbwembwe za lugha ni walau upate msaada Dark City yeye hujipa hata vyeo asivyokuwa navyo ili mradi ahudumiwe

Tena kama nimevaa ile suti yangu ya kariakoo na kupiga lile pank la Makutupora ndiyo wananikoma!
 
Remember! FASTJET - SMART TRAVEL
if ur not smart you won't travel by fastjet............!
 
ulikuwepo? kuna watu mnapenda kubishana hata na taarifa ya habari

Acha maneno yasiyo ya kistaarabu bana mi nimejaribu kumwelewesha kutokana na ninachokifamu na nimeandika hayo sababu nafanya kazi kwenye industy hiyo so..
 
Bwana au Bibi Tiba yaliyokukuta ni kama yaliyonikuta mimi. Story ni ndefu ila kwa kifupi nilisafiri na FASTJET DAR/KIA kwa mara ya kwanza lakini yaliyonikuta niliapa sitarudia tena kusafiri na ndege hii.
 
kama wanaofanya kwenye industry hii na haya ndio maelezo yao basi watz bado tuna safari ndeeefu.Check-in cut off time wamesema 40min....ina maana natakiwa kuja muda wowote before cut off time, hata kama ni kasoro dakika moja.Tujifunze kufuata utaratibu...tatizo watu wa airlines wanauza nafasi kwa watu walio kwenye waiting list.......40 min zinamtosha abiria kutoka check in dest kwenda departure lounge. Kwa waendao nje muda unaongezeka kwa sababu ya taratibu za uhamiaji.
 
Back
Top Bottom