FASTJET: My first and last experience

FASTJET: My first and last experience

Pole sana Tiba, ila ni vyema, hata kama hutatumia usafiri wa FastJet tena, uende kwa top boss wao hapa nchini ueleze mkasa wote huo. Unajua sisi Waafrika mtu akiwa kwenye ofisi ya kutoa huduma anajiona sijui kama kitu au mtu gani! Ule wajibu wake anakuwa haujui; even if huwezi kumsaidia mtu kupata solution ya tatizo lake, hata namna unavyowasiliana na mteja wako inaweza kuwa msaada kwake! Aisee nenda Ofisi za FastJet utoe malalamiko haya labda itakua fundisho kwa wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo, INAUMA SANA! POLE

Rushasha, asante, iliniuma siku ile, bado inaniuma na uenda ikaendelea kuniuma. Ushauri wako ni mzuri nashukuru lakini unajua unaweza kujikuta unapoteza muda wako zaidi na suluhisho usipate. Hapo utaanza kuulizwa ushahidi kama kweli ulifika 40 minutes before departure time na mambo kama hayo ambayo kwa kweli siwezi kuya prove beyond doubt.

Tiba
 
Kwa ARUSHA hiyo ni sawasawa MACHIMACHI RESORT ya Kinondoni Shamba!....:heh::heh::heh::heh::heh:

Safariiiiii🙂 Hii MACHIMACHI umenikumbusha mbali kidogo......Na zile taulo zao kama kokoro kwa jinsi zilivyochoka!!!!
 
Ukiacha ile arrogance Fastjet wako sahihi kabisa. Kawaida check-in inapaswa kumaliza dakika 30 kabla ya ndege kuruka ili kuwapa marubani kupitia loadsheets kujua wana abiria wangapi, mizigo ya uzito kiasi gani na mafuta kiasi. Bila kufanya hivyo ndege haiwezi kuondoka. Kama check-in imeshafungwa sio rahisi kufungua kwa ajili ya abiria wachache labda liwe jambo la kufa na kupona. Hata pale ambapo ndege imepata hitilafu kama Ground handling Agent yaani Swissport wamefunga usiku Manager wa Fastjet hana cha kufanya. Jifunze kuwahi maana ndege haisubiri mtu labda awe Rais
 
kweli kila ntu ina akili yake, hakuna ntu 2 inayoshea akili ,hardly mapacha wa ajabu
 
Zilijulikana kama "msasa"....ubachela bana we acha tu....iko ingine ikiitwa BUIBUI (sijui kama bado ipo)

Hahaahahaaa:heh: Hii hata ulikuwa ukenda saa nne asubuhi inabidi upange foleni kupata chumba!!!!! Kweli ubachela kiboko!!! Hadi mhudumu wa vyumbani anakuwa mshikaji ili kukuwezesha ku-jump foleni!!!
 
Pole sana mkuu.....kumbe tulikuwa wote pale......ila mwenzio nilicheza ushapu nikaondoka na 5H-CCM.......
 
Ukiacha ile arrogance Fastjet wako sahihi kabisa. Kawaida check-in inapaswa kumaliza dakika 30 kabla ya ndege kuruka ili kuwapa marubani kupitia loadsheets kujua wana abiria wangapi, mizigo ya uzito kiasi gani na mafuta kiasi. Bila kufanya hivyo ndege haiwezi kuondoka. Kama check-in imeshafungwa sio rahisi kufungua kwa ajili ya abiria wachache labda liwe jambo la kufa na kupona. Hata pale ambapo ndege imepata hitilafu kama Ground handling Agent yaani Swissport wamefunga usiku Manager wa Fastjet hana cha kufanya. Jifunze kuwahi maana ndege haisubiri mtu labda awe Rais

Mkuu asante kwa mchango wako, lakini ukiangalia muda ambao nilifika pale na muda ambao ndege ilipashwa kuondoka kulikuwa na karibu dakika zaidi ya 50 ingawaje wao Fastjet wanasema ukifika dakika 40 kabla ya ndege kuruka watakusikiliza. Mimi sikusikilizwa ingawaje nilifika ndani ya muda wao!!!! Halafu sio kusikilizwa tu, nilihisi dharau za hali ya juu kutoka kwa mtu wao pale uwanjani. Wakiweka taratibu, wahakikishe wao wenyewe wanaziheshimu kama wanavyotaka sisi tuziheshimu hizo taratibu.

Tiba
 
this is a receipt for your luggage
 

Attachments

  • IMG-20130402-00252.jpg
    IMG-20130402-00252.jpg
    219.1 KB · Views: 147
wana jamvi,

siku ya tarehe 26 april 2013, nilikutana na mkasa wa hawa jamaa zetu wa fastjet na tangia siku hiyo nilinuia, kutokufikiria kutumia usafiri wa hii ndege tena. Kisa chenyewe kilikuwa hivi;

nilisafiri kwa gari binafsi kutoka dar kwenda arusha tarehe 21 april 2013 na nilitarajia kurudi dar ijumaa ya tarehe 26 april 2013 kwa kutumia ndege ya fastjet iliyokuwa iondoke arusha (kia) saa 3:30 usiku. Nilikuwa na tiketi mkononi. Taratibu za fastjet ni kuripoti dakika 40 kabla ya muda wa ndege kuondoka. Nilikodisha taxi kutoka arusha na nilifika kia saa 2:40 usiku. Nilipofika, taxi iliyonipeleka pale iliondoka. Kufika mlangoni, walinzi wakanimbia kwamba nimechelewa na kwamba counter tayari imefungwa na hakuna mtu wa kunicheck in. Nilimkuta na bwana mwingine aliyekuwa amenitangulia kufika na yeye akibembeleza kuruhusiwa kuingia. Wale walinzi walikataa katakata na ukweli ni kwamba pale counter hakukuwa na mtu hata mmoja. Kwa kushirkiana na msafiri mwenzangu niliyemkuta pale, tulianza jitihada za kutaka kuonana na mwakilishi wa fastjet pale uwanjani. Jitihada zetu za kumwona mwakilishi wa fastjet hatimae zilifanikiwa lakini to our suprise, yule bwana alikuwa too arrogant kupita kiasi. Alitwambia hakuna msaada wowote anaoweza kutupatia. Ndege ilikuwa bado iko pale uwanjani. Wakati tukiendelea kumbembeleza, aliitwa kwenye radio call na hivyo akatutaka tutoke ofisini kwake na kwamba angekuja kutusikiliza baadae lakini akasema msaada pekee anaoweza kutupa ni kutukatia ticket nyingine kwa ajili ya ndege ya jumamosi asubuhi tarehe 27 april 2013.

Baadae tulipata taarifa kwamba ndege haiwezi kuondoka kwa kuwa imepata hitilafu na kwamba abiria ambao tayari walikuwa wamepanda wameshushwa na kurudi waiting room. Yule mwakilishi wa fastjet hakurudi tena ofisini pale ingawaje tuliendelea kumsubiri. Kwa kuwa nilikuwa na mkutano muhimu wa kuhudhuria dar jumamosi tarehe 27 april 2013, nilianza kufanya mpango wa kuangalia uwezekano wa kupata seat kwenye ndege ya precision air iliyokuwa iondoke arusha (kia) saa 1:55 asubuhi kuelekea dar. Bahati nzuri nilimpata mwakilishi wa precision air pale uwanjani ambaye baada ya mawasiliano alinihakikishia kunipatia seat kwenye hiyo ndege. Tatizo sikuwa na cash ya kulipia hiyo ticket ambayo gharama yake ilikuwa tshs. 195,000 one way. Baada ya kuhakikishiwa seat, nililazimika kukodisha taxi ya kunirudisha mjini ili kupata hela za kulipia ticket ya precision kutoka kwenye atm. Nilifanikiwa kupata hela na baada ya hapo kazi ya kutafuta hotel ikaanza. Nilipata hotel na nililala karibu saa 6 usiku.

Saa 11:30 alfajiri tayari nilikuwa kwenye ofisi za precision air pale arusha ili kupanda shuttle kwenda kia. Kufika tu, nikaambiwa tayari shuttle ilikuwa imeondoka hivyo nalazimika kutumia usafiri wangu kwenda kia (ukweli ni kwamba shuttle ilikuwa haijaondoka na wala ilikuwa haijafika ila mlinzi anashirikiana na taxi drivers kudanganya abiria ili wakodishe taxi zao). Nilifanya hivyo na kufanikwa kufika dar kwenye saa 3:45 asubuhi jumamosi. Wakati turuka pale kia, ile ndege ya fastjet tuliiacha pale na sijui iliondoka saa ngapi. Abiria walilala pale uwanjani bila huduma yoyote hata maji ya kunywa hawakupewa.

Nia ya kuleta uzi huu ni kuwaambia wana jamvi kwamba wakati mwingine rahisi ni ghali. Safari hii ilinigharimu pesa nyingi sana kwa kuwa tu nilitaka ticket rahisi ya fastjet (tshs. 107,000) one way lakini matokeo yake niliingia gharama zifuatazo;

1. Ticket ya fastjet tshs. 107,000
2. Taxi arusha kia x 3 tshs. 150,000
3. Hotel tarehe 26/4 tshs. 50,000
4. Ticket ya precision tshs. 195,000
jumla tshs. 502,000

nilinuia hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kujaribu kusafiri na fastjet na ilikuwa mara ya mwisho pia. Sitakaa nithubutu kufanya makosa tena hata kama fastjet wata improve huduma kwa wateja na kuajiri watu wanaoweza kuwasiliana kwa heshima na wateja.

Tiba

nadhani hizo gharama ulizoingia ni kujitakia mkuu. Na pengine kudekeza wanakofanya precission ndiko kuna waharibu watu. Mtu unajua unasafari na taratibu za ndege zinajulikana wazi inakuwaje unasubiri hadi dakika ya mwisho?
 
nadhani hizo gharama ulizoingia ni kujitakia mkuu. Na pengine kudekeza wanakofanya precission ndiko kuna waharibu watu. Mtu unajua unasafari na taratibu za ndege zinajulikana wazi inakuwaje unasubiri hadi dakika ya mwisho?

Mkuu Maboso, soma tena bandiko langu kwa makini halafu uniambie hiyo last minute iko wapi? Nilifika uwanjani kabla ya muda wanaoutangaza wao Bwana, naona unataka kunikumbusha tu machungu yaliyonipata siku ile.

Tiba
 
gharama nyingi ni zakujitakia...hapakuwa na sababu ya kukodi tax mara tatu toka arusha kwenda KIA. kuna hoteli za kutosha moshi bado ungepata hifadhi. pia gharama ya hoteli ni ya kujitakia.
 
Mkuu pole, lakini naona hauko makini, check in time closes 40min before departure kwanini unangojeanhadi last minute ifike ile 40 min ndio uingie? Ungewahi kidogo....inawezekana wana sababu za msingi kukwambiamhuwezi,kuingia...pili unajifanya mtasha sana mpaka mlinzi wa shuttle anakwambia shuttle imeshaondoka inaonesha uliongea naye kiingereza....
 
Mkuu pole, lakini naona hauko makini, check in time closes 40min before departure kwanini unangojeanhadi last minute ifike ile 40 min ndio uingie? Ungewahi kidogo....inawezekana wana sababu za msingi kukwambiamhuwezi,kuingia...pili unajifanya mtasha sana mpaka mlinzi wa shuttle anakwambia shuttle imeshaondoka inaonesha uliongea naye kiingereza....

Kumbuka ndege haikuruka pia. Jenga mazoea ya kusoma habari yote kabla hujacomment

Asante kunielewa
 
Back
Top Bottom