FASTJET: My first and last experience

FASTJET: My first and last experience

mhm mbona kosa ni lako na si wao tatizo hili mimi mwenyewe lisha nikuta na nikajifanya najua kufatilia sana niakumbuka kwani kwenye ticket inasema cheking close 40 min b4 dpt na main gate closes 10 min b 4 dpt kwenye kwenye ticket ina sema ukichelewa mwenyewe they dnt refund na uki change route kuna kahela pia unless wao ndo wame sababisha ukachelewa au usisafiri wanatoa 8000 kwa masaa mawili if not 6 au rfund TATIZO HATUSOMI TERMS AND CONDITION
nilipata tatizo kama lako ila sasa nimejifunza hata niki nunua kitu dukani nasoma ph ingridients na exp date na manufacture date....kwa hiyo mkuu pole kwa gharam nyingi ila kosa ni lako wala si fast jet ungelisoma ticket yote yasinge tupata hayo

Mkuu, mbona hayo masharti niliyazingatia vizuri tu?

Tiba
 
After night the in purgatory A1 a mode detailed experience, including the single player mode and cooperation mode, encountering a variety of elite strange and rare and strange, and whether killing off according to the specific team situation; can not kill resolutely notice teammate pass out next through direct SKIP. Goldwto sell many game gold,such as : diablo 3 gold d3 gold runescape gold rs gold diablo 3 gold d3 gold diablo3 gold blade and soul gold wow gold tibia gold aion gold rom gold runes of magic gold age of wushu gold aion kinah dofus kamas cabal gold cabal alz eve isk atlantica gold dfo gold guild wars 2 gold gw2 gold tera gold c9 gold rappelz gold rappelz rupees second life linden mabinogi gold maple story mesos rift gold dragon nest gold itunes gift card App Store Gift Card Rare and strange: with a rare name (usually blue, but at the same time may also be gold elite), it is difficult to find, but to get rid of, there is often a special surprise, because fixed and affixes equipment, regardless of the blue-loaded or yellow equipment, are to the edge, in fact, is the best SP produced strange fortune depends on it. Open the list of your accomplishments, an achievement which lists the most rare and strange, but not all! In addition, rare and strange fall the best equipment is not 100% drop, but if you want, you could do nothing but find them, rs gold because they can. If you encounter, but you can not beat , please hurry to invite your friends list into your game together to engage it, and to drop more than a goodly portion of luck, but also a way of getting money to the Friends of the base! Daobao Wizard: Drop equipped with everything falling energy saving in this chapter, in addition to rare and strange part of falling! Drop the game settings, through research nethack (known as the originator of the Diablo setting items randomly drop) settings, blade and soul gold in fact, a setting is as follows: Rare and strange list of rare and strange list: this figure may be possible, each unique drop list of rare and strange, usually the main producing strange Need rings and necklaces; Blue strange list: this picture ordinary strange, it may appear strange blue, just blue strange installed it must be out of the blue, drop list is the list of the world fall in each of the sections that, that does not beyond the the chapter drop the other chapters will be out equipment. (FARM A1 friend Note, A4 was a good blue-loaded, drag a drag the corpse into the A4.) 3 golden elite list: mainly wow gold used to increase this figure a bit of a challenge and entertainment, to be honest, not farm their significance, and this strange basically impossible to be done FARM their fall list and blue The strange world drop, as limited by chapter, but the yellow loading a relatively high probability it wants. So, I'll give you advice: Careful and meticulous to a certain figure, the difficulty is not great, you can complete single FARM again, all the blame, all the stones, all the local touch it again, and then reset it again, and so forth NNNN times and times, you can put this figure there might be rare and strange touch, we also know this "specialty". Another supplement on suits and legendary equipment drop set: part of the world falling, broken jar and trash mobs and the like can be a goodly portion of luck, but the mobs die so much, the opportunity is always there; portion of the fixed BOSS out drop, multi-brush it, the opportunity is always there, after all, is fixed drop FARM when a lot of bad street but in the end is inevitable; part fall by rare and strange, the same can not be met seeking to encourage you and diligent traveled to every corner of the map; also part of falling exists only in the advanced chest, face. About rare and strange location: each figure with surface and underground (cave) in two parts, this strange wandering the entire surface of each figure, that might be buried in the ground, but mainly present in the underground; each figure has a fixed number of underground cave spawn points, and each picture to refresh the total number of points is fixed, but each time the refresh only a few points, to refresh a few point and which point to refresh are random; Members diligent little more effort, run a race map, summarize the law, there will always be the outcome! ! ! ! ! Random number paradox: while the computer is set between 1-100 random samples of any single chance, from long statistical point of view, are the same, but in a short period of time during the actual operation, you extracted to a 1 and 100 chance is very small; the improved random numbers, often using double-random number divided by the ratio rounded, for example, taken from 1-100 where two duplicate number, and then divided by 2 rounded . Refer to the above extract random set model of random numbers, each picture looks much spawn points, but a subset of locations and 1 or 100 is actually more difficult to be able to get from another point of view, mean that other spawn points easily be able to get refreshed, this rule can be found by summing. My last most important conclusion: Some rare and strange appears only in the rare spawn points, this setting is also normal, everyone can sum up, there is always the law to be investigated!

Inawezekana ni matatizo ya uvivu wangu wa kusoma, but surely what is this all about?

Tiba
 
We umetumwa na mmiliki wa Precision? uchelewe "menyewe" afu ualamike, yaani story yako ni mikasa tu we unachuki na walinzi? Kule mlinzi wa uwanjani huku mlinzi wa Hoteli.
 
Pole ndugu yangu hizi ndio low cost airline au budget airline kule ulaya ryan air ukiwa ndani ya ndege choo unalipia kupunguza gharama kojoa kabisa airport ukipanda ndani unalipia, tupende kusoma TERMS AND CONDITIONS.ila pia ni kweli abiria hua wanafanya makosa kuchelewa nishawahi kuona hili lakin wafanyakazi wa fastjet na precision nao they are too arrogant mteja kachelewa si unamuelewesha taratibu badala ya kuanza kumfokea na majibu ya kejeli "eti tiket yenyewe ya bei rahisi halafu unataka usubiriwe"hahahahaha mdogo wangu alijibiwa hivyo
 
Kiswahili hiki, khaaa!! You made my day hahahahaaaaa

Sikonge hebu nisaidie kidogo hapo, hiyo sio hali halisi? kuna nilichoongezea au kupunguza?unashangaa mtu yuko boxini ila habari zote za Dar za leo anazijua A-Z
 
Last edited by a moderator:
Ni vyema kuuliza kwa undani kabla hujapanga safari ya ndege kama huna uzoefu wa kusafiri kwa ngede kwasababu hakuna airport duniani abiria wanacheki dakika arobaini kabla ya kuondoka, ila unatakiwa kuingia kwenye ndege dakika arobaini kabla ila check in inafanyika masaa mawili kabla ya kuondoka. Inaweza isikuingie akilini lakini kuna vitu vingi na muhimu vinavyofanyika baada ya kucheck in ambavyo kama sio lahisi kuvijua, pamoja na hilo Fastjet inabeba abiria 154 ikijaa full ukisema abiria wachek dakika 40 kabla ya kuondoka ni kitu kisichowezekana hata kidogo. Fastjet wanamapungufu yao lakini kwa hili sidhani kama wanapaswa kulaumiwa na kama abiria atakua anaenda kucheck 40 before na anajiapiliza kutopanda hiyo ndege akiachwa basi hakuna ndege inayomfaa hapa duniani.
 
Akili nyingine bana! Hivi wote mkifika 2 hours before mtaingia kwa wakati mmoja? 40 minutes before departure ndo wanafunga. Ina maana ukifika bado dakika 50 upo ndani ya muda
Sio kweli hata kidogo chek-in ni masaa mawili then counter ikifungwa kuna nusu saa ya kufanya loading baada ya hapo ndio kuanza kuingia kwenye ndege kuna utofauti wa kufunga check in na kuingia kwenye ndege unapofika kabla ya dakika 50 utakua umechelewa pia itategemea hisani ya utakayemkuta
 
Kiongozi kama counter inafungwa dk 30 kabla ya kuruka, huo muda kabla ya hizo dk 30 ni kwa ajili ya nini??

Kuna muda wa kuanza kupokea abiria wa ndege husika (check-in say 2hrs before dept) na muda wa kufunga kupokea abiria (say 40min before dept). Sasa hayo maelezo mengine mnayatoa wapi jamani??

Mtu akifika counter dk 41 kabla ya ndege kuruka bado yupo ndani ya muda...sasa kwa sababu saa wakati mwingine hazisomi sawa ndio maana naweza kujipa dk kama 10 kwamba angalau 50dk kabla ya kuruka niwe kaunta.

Mie kuchelewa ama kuwahi huwa inategemea kama nina mizigo au la!
 
Pole sana, hii ndio bongo, usanii kuanzia juu mpaka chini
 
Hata makampuni makubwa sana duniani hufa kwa ajili ya kutemper na wateja.
 
Hahahaaa, hiki Kiswahili chako yani sina mbavu. Unanikumbusha Dogo mmoja huwa anasema "....chukua Juice Frijini" au dogo fulani anaishi Mwanza anasema "Bus lilipofika, tukadumbukiamo......"

What about "mtu yupo kwenye Box" badala ya hii yako inayonivunja mbavu ya "yupo Boxini"?

Box ndiyo lenyewe Dada yangu Mrembo. Wewe chumia tu juani na siku ikifika uje uliye kivulini.
Sikonge hebu nisaidie kidogo hapo, hiyo sio hali halisi? kuna nilichoongezea au kupunguza?unashangaa mtu yuko boxini ila habari zote za Dar za leo anazijua A-Z
 
Hahahaha!!!
Unasema ukweli wa upande mmoja tu.
Wewe unaamini usafiri wa ndege wa hapa Tanzania kuwa ni salama?
Chunguza kwanza kabla ya kusema.
Kuanzia Air Tanzania, Precision Air mpaka Fastjet, wote hao ndege zao ni Second handed, zimechoka mbaya na Spanner mkononi.
Yale pia ni majeneza ya Angani.

Japokuwa usafiri wa bus hapa Tanzania sio salama sana lakini route ya Dar-Arusha ya bus ndio ina huduma nzuri zaidi kwa hapa Tanzania.

Tunaangalia rate ya kupata ajali! Sawa kuna factors nyingi kuwa one may argue kuwa number ya ndege ni ndogo kuliko mabasi which implies that chances za kupata ajali kwenye mabasi ni kubwa kuliko ndege. Lakini tufanye basi kilomita travelled> Nadhani ndege zinaweza kuwa na km nyingi kuliko mabasi! Pamoja na yote, bado ndege ni salama kulinganisha na mabasi. Tena rafiki kumbuka hata mabasi ni second hand FUSOs modified to serve as buses!!
 
Wana Jamvi,

Siku ya tarehe 26 April 2013, nilikutana na mkasa wa hawa jamaa zetu wa Fastjet na tangia siku hiyo nilinuia, kutokufikiria kutumia usafiri wa hii ndege tena. Kisa chenyewe kilikuwa hivi;

Nilisafiri kwa gari binafsi kutoka Dar kwenda Arusha tarehe 21 April 2013 na nilitarajia kurudi Dar Ijumaa ya tarehe 26 April 2013 kwa kutumia ndege ya Fastjet iliyokuwa iondoke Arusha (KIA) saa 3:30 usiku. Nilikuwa na tiketi mkononi. Taratibu za Fastjet ni kuripoti dakika 40 kabla ya muda wa ndege kuondoka. Nilikodisha taxi kutoka Arusha na nilifika KIA saa 2:40 usiku. Nilipofika, taxi iliyonipeleka pale iliondoka. Kufika mlangoni, walinzi wakanimbia kwamba nimechelewa na kwamba counter tayari imefungwa na hakuna mtu wa kunicheck in. Nilimkuta na Bwana mwingine aliyekuwa amenitangulia kufika na yeye akibembeleza kuruhusiwa kuingia. Wale walinzi walikataa katakata na ukweli ni kwamba pale counter hakukuwa na mtu hata mmoja. Kwa kushirkiana na msafiri mwenzangu niliyemkuta pale, tulianza jitihada za kutaka kuonana na mwakilishi wa Fastjet pale uwanjani. Jitihada zetu za kumwona mwakilishi wa Fastjet hatimae zilifanikiwa lakini to our suprise, yule Bwana alikuwa too arrogant kupita kiasi. Alitwambia hakuna msaada wowote anaoweza kutupatia. Ndege ilikuwa bado iko pale uwanjani. Wakati tukiendelea kumbembeleza, aliitwa kwenye radio call na hivyo akatutaka tutoke ofisini kwake na kwamba angekuja kutusikiliza baadae lakini akasema msaada pekee anaoweza kutupa ni kutukatia ticket nyingine kwa ajili ya ndege ya Jumamosi asubuhi tarehe 27 April 2013.

Baadae tulipata taarifa kwamba ndege haiwezi kuondoka kwa kuwa imepata hitilafu na kwamba abiria ambao tayari walikuwa wamepanda wameshushwa na kurudi waiting room. Yule mwakilishi wa Fastjet hakurudi tena ofisini pale ingawaje tuliendelea kumsubiri. Kwa kuwa nilikuwa na mkutano muhimu wa kuhudhuria Dar Jumamosi tarehe 27 April 2013, nilianza kufanya mpango wa kuangalia uwezekano wa kupata seat kwenye ndege ya Precision Air iliyokuwa iondoke Arusha (KIA) saa 1:55 asubuhi kuelekea Dar. Bahati nzuri nilimpata mwakilishi wa Precision Air pale uwanjani ambaye baada ya mawasiliano alinihakikishia kunipatia seat kwenye hiyo ndege. Tatizo sikuwa na cash ya kulipia hiyo ticket ambayo gharama yake ilikuwa Tshs. 195,000 one way. Baada ya kuhakikishiwa seat, nililazimika kukodisha taxi ya kunirudisha mjini ili kupata hela za kulipia ticket ya Precision kutoka kwenye ATM. Nilifanikiwa kupata hela na baada ya hapo kazi ya kutafuta hotel ikaanza. Nilipata Hotel na nililala karibu saa 6 usiku.

Saa 11:30 alfajiri tayari nilikuwa kwenye ofisi za Precision Air pale Arusha ili kupanda shuttle kwenda KIA. Kufika tu, nikaambiwa tayari shuttle ilikuwa imeondoka hivyo nalazimika kutumia usafiri wangu kwenda KIA (Ukweli ni kwamba shuttle ilikuwa haijaondoka na wala ilikuwa haijafika ila mlinzi anashirikiana na taxi drivers kudanganya abiria ili wakodishe taxi zao). Nilifanya hivyo na kufanikwa kufika Dar kwenye saa 3:45 asubuhi Jumamosi. Wakati turuka pale KIA, ile ndege ya Fastjet tuliiacha pale na sijui iliondoka saa ngapi. Abiria walilala pale uwanjani bila huduma yoyote hata maji ya kunywa hawakupewa.

Nia ya kuleta uzi huu ni kuwaambia wana Jamvi kwamba wakati mwingine rahisi ni ghali. Safari hii ilinigharimu pesa nyingi sana kwa kuwa tu nilitaka ticket rahisi ya Fastjet (Tshs. 107,000) one way lakini matokeo yake niliingia gharama zifuatazo;

1. Ticket ya Fastjet Tshs. 107,000
2. Taxi Arusha KIA x 3 Tshs. 150,000
3. Hotel tarehe 26/4 Tshs. 50,000
4. Ticket ya Precision Tshs. 195,000
Jumla Tshs. 502,000

Nilinuia hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kujaribu kusafiri na Fastjet na ilikuwa mara ya mwisho pia. Sitakaa nithubutu kufanya makosa tena hata kama Fastjet wata improve huduma kwa wateja na kuajiri watu wanaoweza kuwasiliana kwa heshima na wateja.

Tiba

Pole sana dada mi mwenyewe yalishanikuta, hawa jamaa wa fastjet hawako serious kabisa
 
Pole sana dada mi mwenyewe yalishanikuta, hawa jamaa wa fastjet hawako serious kabisa

Asante mkuu wangu, customer care hapa kwetu ni janga kwa kweli!!!!!

Tiba
 
Ni vyema kuuliza kwa undani kabla hujapanga safari ya ndege kama huna uzoefu wa kusafiri kwa ngede kwasababu hakuna airport duniani abiria wanacheki dakika arobaini kabla ya kuondoka, ila unatakiwa kuingia kwenye ndege dakika arobaini kabla ila check in inafanyika masaa mawili kabla ya kuondoka. Inaweza isikuingie akilini lakini kuna vitu vingi na muhimu vinavyofanyika baada ya kucheck in ambavyo kama sio lahisi kuvijua, pamoja na hilo Fastjet inabeba abiria 154 ikijaa full ukisema abiria wachek dakika 40 kabla ya kuondoka ni kitu kisichowezekana hata kidogo. Fastjet wanamapungufu yao lakini kwa hili sidhani kama wanapaswa kulaumiwa na kama abiria atakua anaenda kucheck 40 before na anajiapiliza kutopanda hiyo ndege akiachwa basi hakuna ndege inayomfaa hapa duniani.

Nashukuru Mzee kwa bandiko lako. Sasa mimi na hao fastjet sijui nani alikosea. Wao wenyewe, wanasema abiria akifika 40 minutes kabla ya ndege kuondoka, wanam check in. Mimi nilifika zaidi ya muda huo lakini kwa uhuni wao, waliishaondoka counter!!!!

Tiba
 
Ofisi nyingi bongo ongea nao kwa kiingereza na hata mawasiliano fanya kwa kizungu lazima upate huduma wanababaika sana. Kuna siku niliwapigia CRDB kuulizia sim banking.....nikatema yai, walihangaika sana kupata walau wa kuelewa na kunielewesha.....jaribu sikumoja kuwapigia CCM makao makuu ongea kiingereza uone watakavyohangaika hata kukata simu yako.
Ukitaka huduma za haraka luka na Rugha ya Malkia UK ila sasa kuwa makini na jina lako lifanane na iyo Lugha sio unaanza kusema My name is Sikujua Mwigulu watajua mbongo unajilipua Gordon John

Ila jamani mimi several times huwa nachek in izi local flights nusu saa kabla.
Kuna siku walitaka komaa nami nikapiga bit kuwa nitaruka na MD unajua mimi ni nani?Faster nikaruhusiwa
Ila pole kwa yaliyoukuta usikute ndege ilisha jaa ndo zao hawa jamaa apo ata kama ungekuja lisaa kabla.
Cheap things are expensive sometimes
 
Back
Top Bottom