Inna liLlahi wa Inna iLlahi Rajiun.
Moja katika siku ambayo sitoisahau katika maisha yangu ni leo. Baada ya kufunguwa JF kama kawaida yangu na kukutana na habari za kututoka Regia haikuwa kama kawaida yangu tena. Nna uhakika haitokuwa kawaida kwangu tena.
Regia na mimi binafsi tumeshakuwa na "heated debates" za kutosha humu jamvini za kutufanya tuwe na "invisible bond" somehow, lakini nna uhakika yote si katika kubomoa, yote ni katika kujenga kwa kila mmoja wetu kwa muono wake.
Kweli kifo ni kwa kila mmoja wetu na hakuna atakae kiepuka, ukweli ni kwamba kifo hiki kimenistuwa sana kupita kiasi. Nilipofiwa na mama yangu mzazi ilinichukuwa wiki nzima, baada ya kumaliza msiba na kusafirisha wageni waliokuja msibani, kuanza kuona upweke na "gap" aliyoiacha maishani mwangu, cha kusikitisha ni kuwa, kifo cha Regia kimenitia upweke na "gap" kubwa nnaiona immediately. Kila ntapofunguwa kurasa za JF ntamkumbuka Regia.
Nashindwa kuandika zaidi jamani, ni msiba mzito sana, si kwa wana CHADEMA pekee bali kwa Taifa zima. Kuondokewa na kijana mdogo ambae alikuwa ana uhakika wa kuleta mabadiliko ni pigo kubwa sana, nnatumai ataemrithi wadhifa wake atapigania, kuheshimu na kuyaendeleza yote mema aliyoyadhamiria Regia.
Poleni sana ndugu, jamaa na marafiki wa Regia, Poleni sana Taifa, Poleni sana CHADEMA, Poleni sana wana JF wote.