Mkuu wangu sana Mwanakijiji,yaani ni kama ndoto......
Regia ameondoka mapema mnoo wakati Taifa likimhitaji....Kwa kweli alikuwa ni binti jasiri,mwenye uthubutu wa kufanya jambo na alikuwa tayari kujishusha na kujifunza kila uchao......Hakika hili ni pigo kwa Tanzania, CHADEMA na vijana wapenda maendeleo na mabadiliko nchini Tanzania...
Kwangu mimi Regia alikuwa ni zaidi ya Mbunge/Mwanasiasa ndani ya JF.......Alikuwa ni mtu maalum hasa......Hakika nimeumizwa sana na taarifa hizi na hata nilipopigiwa simu kuelezwa kwamba mpendwa wangu Regia amefariki sikuamini,nilikataa katakata.....Ameondoka mapema sana Regia wetu....
Regia pamoja na kupata ubunge hakuitenga/kuiacha JF......Daima alikuwa nasi katika shida na raha na alijitahidi kuutumia muda mchache anaoupata kuja humu kutujuza mambo mbalimbali yanayojiri bungeni na katika medani za siasa kwa ujumla......She was born for JF na JF tutamlilia daima....
Yeye ni tofauti sana na wanasiasa wengine ambao waliitumia JF kama daraja la mafanikio yao kisiasa na mara baada ya kufanikiwa kisiasa wanaacha kabisa kuingia JF,Regiia/GS hakuwa hivyo........Yeye daima tulikuwa nae JF,hakuchagua jukwaa....Jukwaa la siasa utamkuta,MMU kama kawa, kule kwetu kwenye Michezo na Burudani kulikuwa kwake pia.....Chit Chat ndo usiseme, yaani alikuwa anaingia kila jukwaa tofauti na wanasiasa wengine ambao wao kila siku ni SIASA tuuuu.....
Kwangu mimi Regia alikuwa zaidi ya ndugu,sikujuana na Regia tangu utotoni wala sehemu yoyote nyingine, nimekutana nae JF na tangu tumefahamiana nae tumekuwa zaidi ya ndugu.......Kwa hakika hili ni pigo,sisi tumempenda lakini Mungu amempenda zaidi....
Kwa hakika nilikosa la kusema mara baada ya kupata taarifa kwamba mpendwa wetu/kamanda wetu na mpiganaji wetu Gender Sensitive amefariki........
Upumzike kwa amani rafiki yangu,dada yangu na kiongozi wetu mpendwa...
Umeondoka katika kipindi ambacho Tanzania inakuhitaji hasa....
Kwa heri rafiki.......Umetangulia nasi tuko njiani...
Pole kwa familia, Pole kwa CHADEMA, Pole kwa vijana wote wa Tanzania, Pole kwa wana Kilombero, Pole kwa watanzania kwa jumla...
Hakika hili ni PIGO kwa watanzania........Bala na JF Tutakukumbuka daima dada yetu Gender Sensitive/Regia Mtema
Raha ya milele umpe mpendwa wetu Regia ee bwana, na Mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani......Amina.