Fanya yafuatayo ukitaka usivamiwe sana na vibaka au hata wakuokoe kwenye hatari

Umeandika ukweli mtupu, nakumbuka mara ya kwanza nimehamia Sinza mtaa wa Mugabe au kamanyola kama unavyojulikana kwa wengine, siku dalali ananipeleka kukiona chumba hali ilikuwa shwari kabisa na vijana hawakuepo yaani ni kama vile aliwashtua waondoke,basi nikakiona chumba na kukipenda hivyo nikafanya malipo kwa baba wenye nyumba wangu ambaye ni kijana mdogo msela tu baadae nilikuja kufahamu kuwa nyumba ile aliirithi kutoka kwa babu yake.

Siku ya kuhamia pale nilishangaa kukuta vijana wengi wakiume na wakike wamekaa karibu na chumba changu wakivuta bangi, kunywa pombe na kupiga soga, kimoyomoyo nikamlaani dalali kwa kunileta pale ila nikajipa moyo kuwa nitaweza kukaa tu mbona wengine wamekaa maana kulikuwa na daktari wa Mwananyamala nae alikuwa amepanga hapo pia, basi nikawasabahi na kuingiza vitu vyangu ndani ya chumba changu. Baada ya kukaa kama wiki nakaanza kuwa naongea nao na kuwanunulia pombe kali aina ya viroba na bangi, iliyokuwa inauzwa na mdogo wake na baba wenye nyumba. Baadae sana nikagundua kuwa madada poa wengi uja pale kununua na kuvuta bangi maana kuna usalama kwani eneo lilikuwa na uzio, yaani kuna kipindi madada poa na wauhuni walikuwa wanajaa kupitiliza.

Ila sikuacha utamaduni wangu wa kuwanunulia bangi, sigara na pombe pindi nipatapo nafasi, aisee walinipenda mno na kwa muda nilioishi pale sikuwahi kuibiwa chochote, kuna kipindi kitasa kilikuwa kimeharibika, baba mwenye nyumba akaniambia niwe naegesha tu mlango hakuna wa kuniibia, amini usiamini nilikuwa naacha vitu vya thamani ndani lakini sikuibiwa kamwe hata kuna siku nilisahau hela nyingi kidogo mezani kweupe kabisa, japo kuna muhuni aliingia kuchukua pasi ila hela zangu nilizikuta zote, wale madada poa wengi wao ni video vixens siku hizi nilipokuwa nakutana nao maeneo ya unywaji walikuwa wanang'ang'aniza kuninunulia vinywaji, nilikuwa nawakwepa ila kuna nyakati nilikuwa nagida tu.

katika maisha usije ukamdharau mtu, hata watu tunaowaona ni wa ovyo nao wana umuhimu wao, mara moja moja kuwa karibu nao ila usishiriki mambo yao, hakika watakuheshimu na kukupa msaada siku na eneo ambalo hauwezi kuamini, mimi nilipokuwa Sinza kulikuwa hakuna mhuni wa kunikaba hata usiku wa manane nilikuwa nakatiza tu bila wasiwasi, kwa kuwa wahuni wengine walikuwa wanakuja kutoka maeneo mengine kama Buguruni, Manzese nk kuja kuvuta bangi pale, nilijikuta nafahamia na wahuni wa mitaa mingi, yaani kama umenitangulia halafu tukapita uchochoro mmoja, utakabwa mimi wengeniacha salama.
Maisha......
 
Story yangu kuhusiana na hili; kuna siku nilikosea shortcut.. nikajikuta mtaa mmoja ulioashiria una wahuni kinyama kutokana na harufu harufu za ile kitu.. ilikuwa around saa 4 usiku..
Nikapata akili hapa ili nijiepushe na lolote ambalo pengine lingetokea, ngoja nicheze ngoma yao mapema.. nikashusha vioo vya mbele, nikaforward nyimbo hadi ilipo playlist yangu matata.. nikaanza na "notorious thugs".. beat nzito, nikaweka sauti ya kati, halafu katikati ya washkaji nikaita "oya man", nisaidie fegi hapo shop, nikampa buku 2, wakati nasubiri fegi tayari tukawa kwa "wu shot ya", then "hit em up"-- Nikaletewa fegi, nikamwachia jero na fegi, nikauliza njia huko mbele inatokaje; fegi nikaitupa kama mita 100 mbele..
 
Kwangu Mimi naona ukishafanya hayo uliyosema unakuwa umefadhiri vibaka.

Huo upuuzi wao unapaswa kupingwa na kila aliye na akili timamu haiwezekani mtu atafute kwa jasho wewe ukae uchochoroni uchukue tu kirahisi. Aisee mi labda nisimiliki chuma ntawalaza wengi tu watao jaribu kuleta ujinga kwenye jasho langu
Kama nimemuelewa njia hiyo lengo kuu nikuwabadilisha
 
1. Penda Kujichanganya nao kupiga stori ukiwa na muda

2. Ukibakiza vichenji chenji wape

3. Ukijua wanavuta Bangi au Pombe siku ukiwa nazo mfukoni wanunulie

4. Ukisikia Mmoja wao kakamatwa onyesha hata kinafiki tu kuwa unampambania Kumtoa

5. Wakosoe kwa kuwajenga na siyo kwa Kuwadhalilisha na kama ukisikia kuna Kazi yoyote (hasa za Kawaida tu) waunganishe / watafutie

6. Usiwe na Kiherehere Kingi cha Kuwachomesha kwa Polisi mpaka labda itokee sana na imebidi

7. Ukiwa nao Maskani unapiga Story Mbili Tatu penda mara kwa mara kuingizia Mambo ya Kiimani ( hasa ya Mwenyezi Mungu ) na jinsi ya kuwa Mwema hapa duniani na kutubu ili kuyaanza Maisha mapya na mema

Ukiyafanya haya mambo Makuu Saba (7) Tajwa hapa nakuhakikishia kuwa hata ukiwa unaishi nao Mtaani unaweza hata Kukaa miaka 20 wasikufanye lolote lile na ukashangaa.

Kwa KEROZENE kuandika haya (hivi) sisemi kuwa nawapenda au nawaunga mkono hawa Wahalifu bali nimejaribu tu kuwapeni Mbinu ya Kisaikolojia ya kuweza Kuishi nao na Kuwakabili pia bila ya wao Kukudhuru kwa lolote / chochote.

Nina Mtu hapa Majuzi kati Usiku mida ya Saa 7 Gari yake ilimsumbua na alikuwa Safarini hivyo akabidi aje Kulala Ghettoni Kwangu na akiwa njiani na Kukutana nao akiwa na Simu zake Mbili za thamani na Hela mfukoni walipomuweka Mtu kati ili Kumdhuru huku wakimhoji akasema anakuja kwangu KEROZENE na kilichofuatia wakaachana na Mpango wao huo na kumsindikiza hadi Ghettoni Kwangu na Kunigongea kisha nikaamka na wakanikabidhi Mgeni wangu huku Wawili wakisema watalilinda Gari lake mpaka Asubuhi hivyo asiwe na Wasiwasi.

Tulipoamka Asubuhi na kuanza harakati za Kushughulikia Gari lake Jamaa yangu alipowaona akatoa Tsh 10,000/= kama Asante yake Kwao na kwa Mshangao Jamaa waliikataa na kumwambia wakiipokea hiyo Hela itakuwa ni kama vile wananilipisha Mimi Kaka yao wa Mtaa kwani huwa nawasaidia mno wakiwa na Shida.

Baada ya Jamaa yangu kuona Tukio lile na nikamuelezea Mishe zao zote za Kimatukio Mtaani (Mitaani) ameshawatafutia Watatu kati yao Kazi katika DalaDala zake na sasa wamebaki kama Wanne baada ya wengine pia Kuwaunganisha katika Mishe za Ujenzi, Uvuvi na Ulinzi.

Tuwasaidie na kamwe tusiwadidimize!
Wenzio wanatafuta pesa. Wewe unatafuta kuridhisha wavuta bhange
 
Ni kweli kabisa Ndugu kuna Siku niliibiwa Suruali zangu za Jeans kama Tatu hivi na nilipowaambia tu ndani ya dakika 45 waliniletea na wakasema aliyeziiba alikuwa bado ni Mgeni, hajazoea Mitaa na hakujua Mipaka yake ya Kuiba.
😂😂😂😂
 
1. Penda Kujichanganya nao kupiga stori ukiwa na muda

2. Ukibakiza vichenji chenji wape

3. Ukijua wanavuta Bangi au Pombe siku ukiwa nazo mfukoni wanunulie

4. Ukisikia Mmoja wao kakamatwa onyesha hata kinafiki tu kuwa unampambania Kumtoa

5. Wakosoe kwa kuwajenga na siyo kwa Kuwadhalilisha na kama ukisikia kuna Kazi yoyote (hasa za Kawaida tu) waunganishe / watafutie

6. Usiwe na Kiherehere Kingi cha Kuwachomesha kwa Polisi mpaka labda itokee sana na imebidi

7. Ukiwa nao Maskani unapiga Story Mbili Tatu penda mara kwa mara kuingizia Mambo ya Kiimani ( hasa ya Mwenyezi Mungu ) na jinsi ya kuwa Mwema hapa duniani na kutubu ili kuyaanza Maisha mapya na mema

Ukiyafanya haya mambo Makuu Saba (7) Tajwa hapa nakuhakikishia kuwa hata ukiwa unaishi nao Mtaani unaweza hata Kukaa miaka 20 wasikufanye lolote lile na ukashangaa.

Kwa KEROZENE kuandika haya (hivi) sisemi kuwa nawapenda au nawaunga mkono hawa Wahalifu bali nimejaribu tu kuwapeni Mbinu ya Kisaikolojia ya kuweza Kuishi nao na Kuwakabili pia bila ya wao Kukudhuru kwa lolote / chochote.

Nina Mtu hapa Majuzi kati Usiku mida ya Saa 7 Gari yake ilimsumbua na alikuwa Safarini hivyo akabidi aje Kulala Ghettoni Kwangu na akiwa njiani na Kukutana nao akiwa na Simu zake Mbili za thamani na Hela mfukoni walipomuweka Mtu kati ili Kumdhuru huku wakimhoji akasema anakuja kwangu KEROZENE na kilichofuatia wakaachana na Mpango wao huo na kumsindikiza hadi Ghettoni Kwangu na Kunigongea kisha nikaamka na wakanikabidhi Mgeni wangu huku Wawili wakisema watalilinda Gari lake mpaka Asubuhi hivyo asiwe na Wasiwasi.

Tulipoamka Asubuhi na kuanza harakati za Kushughulikia Gari lake Jamaa yangu alipowaona akatoa Tsh 10,000/= kama Asante yake Kwao na kwa Mshangao Jamaa waliikataa na kumwambia wakiipokea hiyo Hela itakuwa ni kama vile wananilipisha Mimi Kaka yao wa Mtaa kwani huwa nawasaidia mno wakiwa na Shida.

Baada ya Jamaa yangu kuona Tukio lile na nikamuelezea Mishe zao zote za Kimatukio Mtaani (Mitaani) ameshawatafutia Watatu kati yao Kazi katika DalaDala zake na sasa wamebaki kama Wanne baada ya wengine pia Kuwaunganisha katika Mishe za Ujenzi, Uvuvi na Ulinzi.

Tuwasaidie na kamwe tusiwadidimize!
Kuna uwezekano raia wenzako wakakuchukulia nawe ni kibaka, usishangae wakikutia kiberiti.
 
Back
Top Bottom