Fanya yafuatayo ukitaka usivamiwe sana na vibaka au hata wakuokoe kwenye hatari

1. Penda Kujichanganya nao kupiga stori ukiwa na muda

2. Ukibakiza vichenji chenji wape

3. Ukijua wanavuta Bangi au Pombe siku ukiwa nazo mfukoni wanunulie

4. Ukisikia Mmoja wao kakamatwa onyesha hata kinafiki tu kuwa unampambania Kumtoa

5. Wakosoe kwa kuwajenga na siyo kwa Kuwadhalilisha na kama ukisikia kuna Kazi yoyote (hasa za Kawaida tu) waunganishe / watafutie

6. Usiwe na Kiherehere Kingi cha Kuwachomesha kwa Polisi mpaka labda itokee sana na imebidi

7. Ukiwa nao Maskani unapiga Story Mbili Tatu penda mara kwa mara kuingizia Mambo ya Kiimani ( hasa ya Mwenyezi Mungu ) na jinsi ya kuwa Mwema hapa duniani na kutubu ili kuyaanza Maisha mapya na mema

Ukiyafanya haya mambo Makuu Saba (7) Tajwa hapa nakuhakikishia kuwa hata ukiwa unaishi nao Mtaani unaweza hata Kukaa miaka 20 wasikufanye lolote lile na ukashangaa.

Kwa KEROZENE kuandika haya (hivi) sisemi kuwa nawapenda au nawaunga mkono hawa Wahalifu bali nimejaribu tu kuwapeni Mbinu ya Kisaikolojia ya kuweza Kuishi nao na Kuwakabili pia bila ya wao Kukudhuru kwa lolote / chochote.

Nina Mtu hapa Majuzi kati Usiku mida ya Saa 7 Gari yake ilimsumbua na alikuwa Safarini hivyo akabidi aje Kulala Ghettoni Kwangu na akiwa njiani na Kukutana nao akiwa na Simu zake Mbili za thamani na Hela mfukoni walipomuweka Mtu kati ili Kumdhuru huku wakimhoji akasema anakuja kwangu KEROZENE na kilichofuatia wakaachana na Mpango wao huo na kumsindikiza hadi Ghettoni Kwangu na Kunigongea kisha nikaamka na wakanikabidhi Mgeni wangu huku Wawili wakisema watalilinda Gari lake mpaka Asubuhi hivyo asiwe na Wasiwasi.

Tulipoamka Asubuhi na kuanza harakati za Kushughulikia Gari lake Jamaa yangu alipowaona akatoa Tsh 10,000/= kama Asante yake Kwao na kwa Mshangao Jamaa waliikataa na kumwambia wakiipokea hiyo Hela itakuwa ni kama vile wananilipisha Mimi Kaka yao wa Mtaa kwani huwa nawasaidia mno wakiwa na Shida.

Baada ya Jamaa yangu kuona Tukio lile na nikamuelezea Mishe zao zote za Kimatukio Mtaani (Mitaani) ameshawatafutia Watatu kati yao Kazi katika DalaDala zake na sasa wamebaki kama Wanne baada ya wengine pia Kuwaunganisha katika Mishe za Ujenzi, Uvuvi na Ulinzi.

Tuwasaidie na kamwe tusiwadidimize!
Kw hiyo unashiriki uovu siyo ?
 
Gharama za pombe ulizowanunulia miaka yote ungetafuta chumba ushuani
😂 😂 Pombe zenyewe viroba, vilikuwa vinauzwa kwa mafungu, buku tu watu watatu wanalewa na nilikuwa siwapi kila siku, hivyo atakama ningetunza chumba ushuani nisingepata, Kipindi kile tu hapo Sinza Mugambe chumba cha kujitengemea ( self contained) nilikuwa nalipa laki na ishirini na hakikuwa kizuri kivile, sasa ushuani ingekuwaje?​
 
Mtaani juzi hapa wameiba kwa jamaa fulani hivi.
Wamepuliza dawa ndani usiku wakavunja wakaiba kila kitu isipokuwa kitanda tuu jamaa alicholalia na familia yake.
Hatari sana asee unapuliza dawa hivyo ya nusu kaputi unaweza kuwalaza watu mazima.
Wamemaliza kuiba wakajisaidia haja zote hapo wakaondoka kwa imani kwamba jamaa asiwaloge
Ili dawa zao zisifanye kazi wewe jaza ndoo ya maji na uiweke wazi wakipulizia dawa inafyonzwa na maji. Hivyo inamaliza nguvu
 
1. Penda Kujichanganya nao kupiga stori ukiwa na muda

2. Ukibakiza vichenji chenji wape

3. Ukijua wanavuta Bangi au Pombe siku ukiwa nazo mfukoni wanunulie

4. Ukisikia Mmoja wao kakamatwa onyesha hata kinafiki tu kuwa unampambania Kumtoa

5. Wakosoe kwa kuwajenga na siyo kwa Kuwadhalilisha na kama ukisikia kuna Kazi yoyote (hasa za Kawaida tu) waunganishe / watafutie

6. Usiwe na Kiherehere Kingi cha Kuwachomesha kwa Polisi mpaka labda itokee sana na imebidi

7. Ukiwa nao Maskani unapiga Story Mbili Tatu penda mara kwa mara kuingizia Mambo ya Kiimani ( hasa ya Mwenyezi Mungu ) na jinsi ya kuwa Mwema hapa duniani na kutubu ili kuyaanza Maisha mapya na mema

Ukiyafanya haya mambo Makuu Saba (7) Tajwa hapa nakuhakikishia kuwa hata ukiwa unaishi nao Mtaani unaweza hata Kukaa miaka 20 wasikufanye lolote lile na ukashangaa.

Kwa KEROZENE kuandika haya (hivi) sisemi kuwa nawapenda au nawaunga mkono hawa Wahalifu bali nimejaribu tu kuwapeni Mbinu ya Kisaikolojia ya kuweza Kuishi nao na Kuwakabili pia bila ya wao Kukudhuru kwa lolote / chochote.

Nina Mtu hapa Majuzi kati Usiku mida ya Saa 7 Gari yake ilimsumbua na alikuwa Safarini hivyo akabidi aje Kulala Ghettoni Kwangu na akiwa njiani na Kukutana nao akiwa na Simu zake Mbili za thamani na Hela mfukoni walipomuweka Mtu kati ili Kumdhuru huku wakimhoji akasema anakuja kwangu KEROZENE na kilichofuatia wakaachana na Mpango wao huo na kumsindikiza hadi Ghettoni Kwangu na Kunigongea kisha nikaamka na wakanikabidhi Mgeni wangu huku Wawili wakisema watalilinda Gari lake mpaka Asubuhi hivyo asiwe na Wasiwasi.

Tulipoamka Asubuhi na kuanza harakati za Kushughulikia Gari lake Jamaa yangu alipowaona akatoa Tsh 10,000/= kama Asante yake Kwao na kwa Mshangao Jamaa waliikataa na kumwambia wakiipokea hiyo Hela itakuwa ni kama vile wananilipisha Mimi Kaka yao wa Mtaa kwani huwa nawasaidia mno wakiwa na Shida.

Baada ya Jamaa yangu kuona Tukio lile na nikamuelezea Mishe zao zote za Kimatukio Mtaani (Mitaani) ameshawatafutia Watatu kati yao Kazi katika DalaDala zake na sasa wamebaki kama Wanne baada ya wengine pia Kuwaunganisha katika Mishe za Ujenzi, Uvuvi na Ulinzi.

Tuwasaidie na kamwe tusiwadidimize!
8. Wape 0713 kabisa Kila unapokutana nao
 
Nah, I'll never do this kind of shit.

Mwizi ni Mwizi tu sababu tayari yeye alishaamua kuona kudhuru wengine ni jambo la kawaida hivyo kumuogopa na kumsaidia sio kitu sahihi.
Njia pekee ya kumsaidia ni kumfanya aache wizi na sio kujipendekeza kwake ili akuache huku akiendelea kufanya uovu kwa wengine.
Kumsaidia ni kumreport polisi akitoka awe raia mwema au kumpa kipigo mpaka ajute kwanini aliamua kuwa mwizi.

Au kama kila mtu akiwa hivi kama wewe basi wizi hautoisha na wataona fahari kuendeleza hizo tabia mbovu sababu wanajua watu watajipendekeza kwao kwa uoga hivyo wao kuwa na power kwenu.

Kuishi namna hii ni uoga wa maisha yaani unaishi jinsi jamii inavyotaka na sio unavyotaka wewe now huo ni utumwa wa kisaikolojia wa kujitakia.

Maisha ni mafupi mno kuishi jinsi kima fulani anataka sababu ya uoga na kuogopa vitu ambavyo huna uhakika navyo kama vitatokea.
Na wanasema asilimia 99 ya vitu unavyoviogopa vitatokea havitatokea so hapa ni kujipa tabu, stress zisizo na msingi na kujichosha bure na kupoteza muda tu kufanya maisha yako na mambo yako ya maana ya maendeleo.
Unless na wewe unaendana na hao wezi walivyo na ndio maana unaweza kukaa kijiweni kuongea pumba na wezi. ndege wafananao huruka pamoja.

Iko hivi, mimi naishi ninavyotaka kama siku utaibiwa basi utaibiwa au kama hautaibiwa basi hautoibiwa na hakuna cha kufanya kuzuia hicho hicho kitu especially kama hujui kitatokea au lah.

Mimi katika maisha yangu nina kanuni moja yanapokuja mambo ya fujo, ukilianzisha ni eidha nikupige au tupigane au wewe unipige mimi na kama ukishindwa kunipiga basi mimi nitakupiga wewe.
Ukiondoa majambazi wenye silaha za moto siku mwizi au kibaka atakapo jaribu kuvunja ndani kwangu basi nondo lazima ihusike na ni lazima mmoja aende chini hakuna kulialia na bila shaka hatorudia tena.
 
3. Ukijua wanavuta Bangi au Pombe siku ukiwa nazo mfukoni wanunulia
Nakuunga mkono kwenye hoja zako zote isipokuwa hiyo namba 3.
Kwangu mimi naona kuwanunulia bangi na Pombe ni kama kuendelea kuwapoteza zaidi. Ila kwa mengine naona yako vizuri sana. Hasa la kuwatafutia njia halali za kuwaingizia kipato na kuwaambia habari njema za kiimani za kumrudia Mungu.

Hakika mkuu Alosto mbaya sana kuna mteja mmoja kitaa alishawahi kumwibia mkewe chupa ya uji wa mtoto wake yaan ilikuwa hv mkewe yupo geto anamnyeshwa mtoto uji jamaa akamwita mkewe kwa nje basi yule dada kutoka jamaa akazunguka mlango wa nyuma akachukua chupa ya uji akasepa mkewe kurudi chupa ya uji hakuna ikabidi aulize wapangaj wenzie wakamwambia mbona mumeo Kapuya hapa na chupa Bi Dada alichokaa sana
Tatizo asilimia kubwa ya vibaka ni waraibu wa madawa ya kulevya. Unapokuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya hata uwe na busara kiasi gani, ukipigwa na alosto tu unaweza mkaba hata mama yako mzazi.
Kama ukichunguza wengi wao huwa na maono makubwa sana na uwezo mkubwa mno wa kujenga hoja pale wanapokuwa hawana alosto. Unamuona kabisa ana majuto ya dhati juu ya tabia yake. Ila akipigwa na alosto utu wake wote hupotea.
Kibaka ana mithilika na mnyama pori, unaweza mfuga, ukamlisha na kumtunza lakini siku moja tu ile instinct yake ya unyamapori ikiingia anakumaliza.
 
kuna ka ukweli ila elewa tu kwamba binadamu hatabirikiii anyway heshimu kila mtu na ishi kimachaleeee yaaani kuna watu mtaani/maofisini ni ma snitch kuliko hata vibaka ulowaongelea
 
Back
Top Bottom