Familia ya Nyerere mnaaibisha taifa

Status
Not open for further replies.
Pili tushukuru kwa sasa mama maria yuupo hai na baadhi ya gharama za ndogo ndogo anazitoa yeye...
Ulitaka mpaka gharama ndogo ndogo zilipiwe na Serikali?...hivi jamani mipaka ya "ubwaba wa Taifa" inaishia wapi?!
Umefika wakati sasa familia ya Nyerere ijifunze kuwa Serikali (mimi si mshabiki wa serikali za Kisekula)ikikupa unatarajiwa kurudisha/kuchangia japo kidogo!
Ili kuukata huu mzizi wa fitina inabidi cheo cha Ubaba wa Taifa kifutwe! kuabudu kaburi nako kukomeshwe.
Edson said:
jamaa yenu anakula bata Canada...subiri nae afe.....
Unafiki sio kitu kizuri! Joan Wickens aliripoti (nina hakika kuwa hili linajulikana wazi hapa jamvini) kuwa waliwahi yeye na Nyerere kuzuri nchi zaidi ya 30 katika muda usiozidi miezi sita! huku tukidanganywa kuwa Nyerere hatoki sana nje ya nchi!
 

jamani si baba yao? Waacheni? Sasa wanakuabisha nini? Kwani nyerere baba yako?
 

Mamajack,

Asante sana kwa post hii.Inawezekana kuna watu wameona dili hapo.Nyerere aliamini katika utu.Sasa ni jambo la ajabu kabisa kuona kuna watu wanatumia kaburi lake kama kitega uchumi.We're morally bancrupt!
 
Hakika pamoja na kwamba Kaburi ni sehemu ya familia, kutokana na nafasi aliyokuwa nayo Mwl. Nyerere nchini Tanzania, Kaburi hilo lilichukuliwa kama sehemu ya Makumbusho ya Mwl. J. K. Nyerere.

Hivyo malipo ya kuingia museum yamwezeshe mgeni kwa hiyari yake kama pia anataka kutembelea hilo kaburi maana si wote hupenda kutembelea makaburi. Hakuna haja ya kuwa na tozo lingine lolote. Na kazi hii iendeshwe na taasisi ya Mwl. Nyerere Foundation au chini ya makumbusho ya Taifa na si familia.
 
mbona kulipia makumbusho ya Taifa hampigi kelele? Mnataka kwenda bure bure tu. Hamna kitu kama hicho
 

He! museni anamtunza mama Maria, isije tu ikawa kama ya Mzee Mandela na Graca Machel!
 
Nani ana uhakika kwamba hiyi familia haitunzwi tena?

Sidhani kama ni rahisi kiasi hicho kuiacha hiyo familia wanaweza kuwa wameweka hiyo fee kwa tamaa zao wenyewe.

Unahitaji kuwa kiongozi mwendawazimu kuitelekeza familia ya mwalimu
mkuu kwa aina ya viongozi tulionao sasa tz si ajabu kusikia familia ya hayati nyerere imetelekezwa.... kama hakuna wanachokivuna kutoka kwa familia hiyo unategemea nini?
 
Kama kuna uongo basi ni huu wa huyu jamaa yetu, kaburi la Mwalimu Nyerere ni sehemu ya makumbusho yake na hakuna mahali popote duniani ambako makumbusho haitozi fedha walau kidogo kwa ajili ya kuona 'mikusanyo' iliyoko ndani yake au iliyo katika eneo la makumbusho-kwa suala la kaburi la Baba wa Taifa, lile ni sehemu ya makumbusho na ulipaji haukutokana na familia yake, bali ni kwa mujibu wa sheria inayoongoza makumbusho nchini, hivyo ni serikali iliyoweka kiingilio. Faida za kuweka viingilio katika makumbusho ni nyingi, mosi ni kuhakikisha kuwa mikusanyo iliyopo inaweza kukarabatiwa kwa sehemu ya fedha inayopatikana, pili ni kuyaweka mazingira yenye mikusanyo kuwa mazuri muda wote kwa maana nyingine ikiwa kila mtu ataingia pale kwa Mwalimu kama anaenda chooni pataharibika na kuchoka ajabu, lakini mwisho ni utaratibu tu wa kawaida wa uendeshaji wa makumbusho na hii ni dunia nzima. Labda nenda pale Taj Mahal India, ambapo kila mhindi anataka sana kwenda kuona kaburi lile lakini ni wengi wanazeeka na hatimaye kufa bila kufika hapo kutokana na kutokuwa na uwezo huo. Hivyo usikimbilie kulaumu tu, ila unapaswa kusoma na kuelewa taratibu za makumbusho na ikiwezekana duniani kote, makumbusho si choo ambacho kila mtu anaweza kuingia kujisaidia na zingatia kwamba siku hizi pia vyoo wanalipia
 

Chuki binafsi itakuua. Nimemquote mswahili mwenzako humu.
 
ila wanapata pesa sana wale wazee wa nec wakienda wote kule kutambika lile kundi lote si ni mipesa kibao. Tra nao waende basi wachukue chao manake si ni biashara
 
mi nitaendelea kuwa namsoma kwenye magaze na kusubiri kipindi cha kumbukumbu yake ili niweze kujifunza yale amabay sijajifunza lakini hili la kwenda kulipia hela yangu kuangalia kaburi lake ni kama ufujaji wa fedha na rasilimali za familia yangu wakati nazipata kwa shiada,nitamsoma kama navyosoma waasisi wengine na nitamheshimi sana kama baba wa taifa hili lakini sintolipia hata mia yangu kwenda kuangalia kaburi lake
 


ACHA ILE JAMANI... MARAIS WOTE HATA WALE walio Ua wananchi wao kama KAMUZU BADA yeye yuko kwenye

MAUSOLEUM na ni NCHI IMEMZIKA na WANAILIPA FAMILIA YAKE... ambayo ni LIUKOO LOOOTE... AMEZIKWA KARIBIA

NA KAMUZU BANDA ACADEMY... Very Expensive One... Nyerere hakujilimbikizia MASHULE KWA JINA LAKE


KAMUZU MAUSOLEUM




MTI WAKE NA SHULE ILIANZISHWA NA ALIZIKWA HAPO KAMUZU ACADEMY








HII NDIO MBELE YA KAMUZU ACADEMY




GETINI KUINGIA KAMUZU ACADEMY NA PIA KWENYE MAUSOLEUM


JOMO KENYATTA - DOWNTOWN NAIROBI MAUSOLEUM


SERIKALI YA KENYA INAILIPA KENYATTA FAMILY na Unajua FAMILIA HIYO ILIVYO TAJIRI kwa kubeba ARDHI za WAKIKUYU WAKAMBA na Makampuni kuchukua 10% au 20% NYERERE na FAMILIA YAKE wanazo hizo???

PICHA ZA KENYATTA ONLINE HADI LEO BADO ZINAUZWA HAUPATI BURE, LAZIMA UNUNUE...



Umeona GATE; Hauingii BILA KULIPA... Sasa kwanini wengine MATAJIRI WAMEKUFA wanatoza, Nyerere Masikini Asitoze?




Shule yake
Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology -

Mpeni Basi Account moja ya USWISI kwa FAMILIA yake? kama kweli Mna Uchungu wa kutozwa ?
Yaani Watanzania Mmekuwa wa BURE kiasi hicho kama vile hamtoki Nje ya NCHI...
Mnajua kabisa hakuna cha bure duniani... NYERERE ndie aliyewadekeza... ANGALIA MKAPA; KIKWETE kawatoa MACHO

Sasa MNAJUA UFISADI, MNAJUA WIZI, MNAJUA KUISHI na MISHUMAA, MNAJUA KUPIGANA... lakini cha NYERERE bado
Mnataka vyake vya BURE TUUUU
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…