Familia ya Nyerere mnaaibisha taifa

Status
Not open for further replies.
Mbona mie nilitembelea na sikulipa chochote!wameanza lini huu utaratibu!?

Lakini hata hivyo ni nani wa kulaumu!? Kwanini JK mdogo haitunzi hiyo familia mpaka inafikia hatua hiyo!

Ukweli ni aibu na ni aibu yetu sote kama taifa kuwa tumeshindwa kumsaidia mjana wa mmoja wa wasisi wa taifa hili ambaye pia ni waziri mkuu wa kwanza wa iliyokuwa tanganyika lakini vile vile rais wa kwanza wa jamuhuri ya muungano wa tanzania.

Mbona wenzetu zanzibar wanamjali mke wa Karume!? Tawala zote kama sikoesi ukiondoa ya komando, zote zimekuwa zikimjali yule mama.... Kwa nini tawala zetu hazifanyi hivyo! Na hasa hii ya mtani wangu JK?
 
kwanza ukaangalie kaburi la nyerere ili upate nini?mimi siamini kwenye hayo mambo..the man is dead and long buried,let him rest in peace
 
mamajack,

Haya uliyoandika hapa sio kweli.

Mjane wa Mwalimu analipwa 40% ya mshahara wa Rais wa sasa kama pensheni kila mwezi hadi atakapofariki. Wanae Mwalimu ni watu wazima na walianza kujitegemea siku nyingi kabla ya Mwalimu kufariki.

Kama wanatoza kiingilio pale ni masuala mengine kabisa. Mama Maria Nyerere anatunzwa vizuri tu sio na serikali hii bali hata Museveni wa Uganda.

Bora umekuja kufafanunu mkuu that's was my point sio tunaishambulia tu serikali eti haimtunzi kuna mtu yeyote mwenye uhakika kuwa hatunzwi? Mama Maria si mtu wa kuhitaji kiingilia cha kaburini kuishi kama wamefanya hivyo ni kwa malengo mengine sio ya kujikimu
 
Mkuu ktk malalamiko yako haya;
Je umezingatia gharama za kuendesha makumbusho yenyewe?
Nani anahusika kulipa gharama hizo?
Je tuingize siasa pale ili pazorote halafu tupate aibu zaidi?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Wafanyeje na wenyewe wametelekezwa na Kikwete?

Nakumbuka Makongoro alipokuwa akiomba kura kwa ajili ya ubunge wa Afrika Mashariki alisema, kafika Dodoma kwa nauli ya msaada.

Jamani hii si aibu?
Tusiongopeane. Makongoro ni mtu mzima sana. Mke wake ni Jaji wa Mahakama Kuu. Yeye mwenyewe ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa. Mwalimu hadi anastaafu hakuwa na mwanae wakuzaa aliyekuwa akimtegemea kwa lolote labda ushauri tu.
 
uwendawazimu upi zaid ya huu tulionao utakaokufanya uamini kuwa jk na serikali yake wanaweza kwa makusudi kabisaaaa kuitelekeza hiyo familia! Jk na mama mwana-asha ni zaidi ya uwajuavyo! Ni balaa nchini kwetu nakwambia!

RIP Nyerere, pray for me!

Na Nyerere Foundation inafanya kazi ipi?
 
Sina shaka serikali inamtunza mjane wa Mwalimu, na naamini kuna watumishi wa serikali pale wenyejukumu la kutunza makazi ya Baba wa Taifa, lakini ninachosema hapa na nilichoshuhudia ni kwamba "WANATOZA VIINGILIO ILI WATU KUONA, KUSALI KWENYE KABURI" la Baba wa Tifa!!!!!! Hii si sawa hata kidogo na ni aibu kwa tamaduni zetu za kiafrika kwamba watu kuja kwenu hadi walipie? Watu kuona kaburi la mzee wako ati hadi walipie??.
 
mamajack,

Haya uliyoandika hapa sio kweli.

Mjane wa Mwalimu analipwa 40% ya mshahara wa Rais wa sasa kama pensheni kila mwezi hadi atakapofariki. Wanae Mwalimu ni watu wazima na walianza kujitegemea siku nyingi kabla ya Mwalimu kufariki.

Kama wanatoza kiingilio pale ni masuala mengine kabisa. Mama Maria Nyerere anatunzwa vizuri tu sio na serikali hii bali hata Museveni wa Uganda.

Mkuu hata mimi nakubaliana na wewe kwmba Mama Maria Nyerere anatunzwa vizuri na serikali. Lakini pia kuna taarifa kwamba serikali hiyo hiyo imeshindwa kuyatunza makumbusho ya mwl Nyerere huko butiama inawezekana familia imefanya hivyo ili kupata fedha kidogo za kuyaweka sawa mazingira ya makumbusho pamoja na kaburi la mwalimu.
 
Serikali na mamlaka zake wako usingizini, unategemea familia ifanyeje? Hakuna haki bila wajibu. Tafakari, chukua hatua.
 
Halafu mnataka vingozi wasiibe, nani atakubali aiache familia yake inateseka wakati ulaji uko mbele ya macho, hata mimi nikipata nafasi hiyo lazima nifungue account uswiss.
 
Hivi karibuni nilitembelea Butiama kuzuru makazi, kaburi na Makumbusho ya Mwl. Nyerere.

Kitu kilichonisikitisha na kunishangaza ni kwamba mtu haruhusiwi kuona kaburi la Baba wa Taifa hadi alipie huduma hiyo! Nilipouliza utaratibu huu upo tangu zamani, muhudumu wa pale getini alinijibu kwamba FAMILIA YA MWL NYERERE IMEAMUA KUANZISHA UTARATIBU HUU ILI KUPATA FEDHA ZA KUTUNZA FAMILIA!

Baadaye nilitembelea Makumbusho nikauliza suala hili nikajibiwa na maofisa wa Makumbusho kwamba hapo awali Makumbusho ilikuwa na dhamana ya kuwatembeza wageni wote kwenye makazi, kaburi isipo kuwa baadhi ya maeneo. Hali hiyo ilibadilika baada ya baadhi ya wanafamiilia kuanzisha utaratibu huo ambao kwa kweli wageni wengi, na watanzania kwa ujumla wanaushangaa na ni aibu kwa taifa.

Maoni yangu ni kwamba serikali inapaswa kuchukua dhamana ya kutunza eneo hilo hii ikiwa ni pamoja na usalama wake.

Kadhalika familia ama kikundi cha watu kamwe kisipewe ruhusa ya kufanya biashara ya aina yoyote katika eneo hilo.
Kuna harufu ya upotoshaji katika habari hii!
 
Sina shaka serikali inamtunza mjane wa Mwalimu, na naamini kuna watumishi wa serikali pale wenyejukumu la kutunza makazi ya Baba wa Taifa, lakini ninachosema hapa na nilichoshuhudia ni kwamba "WANATOZA VIINGILIO ILI WATU KUONA, KUSALI KWENYE KABURI" la Baba wa Tifa!!!!!! Hii si sawa hata kidogo na ni aibu kwa tamaduni zetu za kiafrika kwamba watu kuja kwenu hadi walipie? Watu kuona kaburi la mzee wako ati hadi walipie??.
Ulitozwa shs ngapi omokora nyangi? Post yako ya kwanza ndio imetushtua wengi. Ni vizuri unapotembelea mahala na ukatatizwa na lolote unawatafuta wahusika wenyewe kuliko mlinzi wa getini au house girl! Kaburi la Mwalimu linatembelewa na watu wengi sana. Imekuwa kama ni sehemu ya kuhiji vile. Haihitaji akina Zomba kwenda huko. Utaratibu wa kulipa kama upo labda ni kwa ajili kupunguza idadi hii ya watu wanaotembelea pale.
 
Hivi karibuni nilitembelea Butiama kuzuru makazi, kaburi na Makumbusho ya Mwl. Nyerere.

Kitu kilichonisikitisha na kunishangaza ni kwamba mtu haruhusiwi kuona kaburi la Baba wa Taifa hadi alipie huduma hiyo! Nilipouliza utaratibu huu upo tangu zamani, muhudumu wa pale getini alinijibu kwamba FAMILIA YA MWL NYERERE IMEAMUA KUANZISHA UTARATIBU HUU ILI KUPATA FEDHA ZA KUTUNZA FAMILIA!

Baadaye nilitembelea Makumbusho nikauliza suala hili nikajibiwa na maofisa wa Makumbusho kwamba hapo awali Makumbusho ilikuwa na dhamana ya kuwatembeza wageni wote kwenye makazi, kaburi isipo kuwa baadhi ya maeneo. Hali hiyo ilibadilika baada ya baadhi ya wanafamiilia kuanzisha utaratibu huo ambao kwa kweli wageni wengi, na watanzania kwa ujumla wanaushangaa na ni aibu kwa taifa.

Maoni yangu ni kwamba serikali inapaswa kuchukua dhamana ya kutunza eneo hilo hii ikiwa ni pamoja na usalama wake.

Kadhalika familia ama kikundi cha watu kamwe kisipewe ruhusa ya kufanya biashara ya aina yoyote katika eneo hilo.

Daima duniani kote Makumbusho ni suala la Utalii na ni kitegauchumi. Nenda China makumbusho ya Mao Zedong, Israel alikozaliwa Nabii Issa, nk. nk. kuna utaratibu wa kulipia. Sioni tatizo la kuwepo kwa utaratibu wa kulipia fedha kuingia/kuona Makumbusho ya Mwal. Nyerere. Labda hoja ingekuwa uhusika wa moja kwa moja wa familia ya mwalimu Nyerere katika kupokea fedha hizo ili kujikimu maana ni kama Serikali ya CCM imewatupa.

Muda umefika sasa wa Watanzania kuthamini Makumbusho na kwa kweli kuwa tayari kulipia gharama ili kuyatembelea. Wenzetu wa mataifa yaliyoendelea wamefanikiwa sana katika hili, Makumbusho yamekuwa ni vivutio vikubwa vya utalii. Tuna majina makubwa kwenye historia kama ya akina Mkwawa, Mtemi Mirambo, Kinjekitile Ngware, Mtemi Mangi, Mangungo nk. nk. lakini tumeshindwa kuyaboresha ili yatuingizie fedha za kigeni.

Msiba wa Kanumba (Acha huo wa Bababa wa Taifa letu Mwal. Nyerere) umevuta watu wengi sana lakini familia yake hadi leo haijiulizi ni kwa nini? Je kuna fursa gani hapo? Atakuja Mzungu atakusanya kazi zote za Kanumba, camera na kompyuta zake, nguo alizokuwa anavaa, maandishi yake nk. na ataanzisha Makumbusho makubwa ambayo bila shaka tutalipia fedha nyingi sana kuyatembelea maana wengi walimpenda.
 
mamajack,

Haya uliyoandika hapa sio kweli.

Mjane wa Mwalimu analipwa 40% ya mshahara wa Rais wa sasa kama pensheni kila mwezi hadi atakapofariki. Wanae Mwalimu ni watu wazima na walianza kujitegemea siku nyingi kabla ya Mwalimu kufariki.

Kama wanatoza kiingilio pale ni masuala mengine kabisa. Mama Maria Nyerere anatunzwa vizuri tu sio na serikali hii bali hata Museveni wa Uganda.

Zitakuwa njaa tu za hao watu wa Butiama waliopewa dhamana ya kutunza.
 
Nani ana uhakika kwamba hiyi familia haitunzwi tena?

Sidhani kama ni rahisi kiasi hicho kuiacha hiyo familia wanaweza kuwa wameweka hiyo fee kwa tamaa zao wenyewe.

Unahitaji kuwa kiongozi mwendawazimu kuitelekeza familia ya mwalimu

kuna kinachoshindikana kwa serikali hii? Uwendawazimu imekuwa ndo jadi ya viongozi wetu,mangapi tumeshuhudia wakiyafanya ambayo hadi mtu unajiuliza kama waliokuwa wanafanya walikuwa na akili timamu kweli, sembuse hili la kutelekeza familia ya Nyerere, it is possible, kwanza katika hali ya kawaida yale makumbusho na kaburi la BABA WA TAIFA ilipaswa viwe chini ya Serikali, How come familia ikawa na mkono wake? Serikali mbovu na utaratibu wake mbovu
 
Zitakuwa njaa tu za hao watu wa Butiama waliopewa dhamana ya kutunza.
Inawezekana. Hata mtoa hoja hana risiti aliopewa kwa malipo hayo. Mbaya zaidi aliongea na mlinzi getini. Moja kati ya mambo mema aliofanya Mkapa na Sumaye ni kuhakikisha pensheni ipo kwa wastaafu wa ngazi kubwa za kitaifa na wajane wa viongozi wakuu wa kitaifa. Walikosea tu kutowaondoa wanaotuibia wakiwa madarakani kama akina Mkapa, Lowasa na Sumaye.
 
Daima duniani kote Makumbusho ni suala la Utalii na ni kitegauchumi. Nenda China makumbusho ya Mao Zedong, Israel alikozaliwa Nabii Issa, nk. nk. kuna utaratibu wa kulipia. Sioni tatizo la kuwepo kwa utaratibu wa kulipia fedha kuingia/kuona Makumbusho ya Mwal. Nyerere. Labda hoja ingekuwa uhusika wa moja kwa moja wa familia ya mwalimu Nyerere katika kupokea fedha hizo ili kujikimu maana ni kama Serikali ya CCM imewatupa.

Muda umefika sasa wa Watanzania kuthamini Makumbusho na kwa kweli kuwa tayari kulipia gharama ili kuyatembelea. Wenzetu wa mataifa yaliyoendelea wamefanikiwa sana katika hili, Makumbusho yamekuwa ni vivutio vikubwa vya utalii. Tuna majina makubwa kwenye historia kama ya akina Mkwawa, Mtemi Mirambo, Kinjekitile Ngware, Mtemi Mangi, Mangungo nk. nk. lakini tumeshindwa kuyaboresha ili yatuingizie fedha za kigeni.
.

Mkuu hapa hoja umeilewa au imekupita kidogo?

Makumbusho ya Nyerere inalipiwa hivi sasa ila ukitaka kuona kaburi unatakiwa ulipie kwa huduma hiyo ya kuona kaburi

Duniani kote makumbusho mengi ni ya kulipia ila hii ya kulipia kuona kaburi ndio naipta sasa.

Nenda kwa waasisi wa usoshalisti kama kina Ho Chi Min na V.I. Lenin, makaburi yao yapo kwenye public squares kuona bure.

Nenda Uturuki, makaburi ya waasisi wao yamejengewa na kuona ni bure, nenda Iraq na Iran hali ni vile vile. Nenda Uingereza na watu wao maarufu, makaburi ni sehemu ya makumbusho au bure

Heck, nenda Tumbuktu na makaburi ya maulamaa maarufu katika mji huo wa kihistoria ni bure.

Hata hapo Zanzibar kuona kaburi la Karume ni bure.
 
Nani ana uhakika kwamba hiyi familia haitunzwi tena?

Sidhani kama ni rahisi kiasi hicho kuiacha hiyo familia wanaweza kuwa wameweka hiyo fee kwa tamaa zao wenyewe.

Unahitaji kuwa kiongozi mwendawazimu kuitelekeza familia ya mwalimu

mimi naona anayetakiwa kutuzwa ni yule MAMA tu wengine wakubwa wajitegemee kwa kila kitu in maana Nyerere angekuwepo mpaka leo wangekuwa wanamtegemea kwa kila kitu.
 
Daima duniani kote Makumbusho ni suala la Utalii na ni kitegauchumi. Nenda China makumbusho ya Mao Zedong, Israel alikozaliwa Nabii Issa, nk. nk. kuna utaratibu wa kulipia. Sioni tatizo la kuwepo kwa utaratibu wa kulipia fedha kuingia/kuona Makumbusho ya Mwal. Nyerere. Labda hoja ingekuwa uhusika wa moja kwa moja wa familia ya mwalimu Nyerere katika kupokea fedha hizo ili kujikimu maana ni kama Serikali ya CCM imewatupa.

Muda umefika sasa wa Watanzania kuthamini Makumbusho na kwa kweli kuwa tayari kulipia gharama ili kuyatembelea. Wenzetu wa mataifa yaliyoendelea wamefanikiwa sana katika hili, Makumbusho yamekuwa ni vivutio vikubwa vya utalii. Tuna majina makubwa kwenye historia kama ya akina Mkwawa, Mtemi Mirambo, Kinjekitile Ngware, Mtemi Mangi, Mangungo nk. nk. lakini tumeshindwa kuyaboresha ili yatuingizie fedha za kigeni.

Msiba wa Kanumba (Acha huo wa Bababa wa Taifa letu Mwal. Nyerere) umevuta watu wengi sana lakini familia yake hadi leo haijiulizi ni kwa nini? Je kuna fursa gani hapo? Atakuja Mzungu atakusanya kazi zote za Kanumba, camera na kompyuta zake, nguo alizokuwa anavaa, maandishi yake nk. na ataanzisha Makumbusho makubwa ambayo bila shaka tutalipia fedha nyingi sana kuyatembelea maana wengi walimpenda.
HAPA UMENENA, Watanzania lazima twende na wakati,haya mambo yanafanyika the world over,sisi watanzania yanatushangaza,sisi tunatembea wakati dunia inakimbia. Kuliona kaburi la Karl Marx,Highgate,London ina bidi uache 7£ mlangoni
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom