miss strong
JF-Expert Member
- Jul 4, 2012
- 7,012
- 3,694
Pigeni business nchi ishauzwa hii,hakuna cha bure.....magamba wameitelekeza family ss kabur lao ndo mnallitaka?
hivi karibuni nilitembelea butiama kuzuru makazi, kaburi na makumbusho ya mwl. Nyerere.
Kitu kilichonisikitisha na kunishangaza ni kwamba mtu haruhusiwi kuona kaburi la baba wa taifa hadi alipie huduma hiyo! Nilipouliza utaratibu huu upo tangu zamani, muhudumu wa pale getini alinijibu kwamba familia ya mwl nyerere imeamua kuanzisha utaratibu huu ili kupata fedha za kutunza familia!
Baadaye nilitembelea makumbusho nikauliza suala hili nikajibiwa na maofisa wa makumbusho kwamba hapo awali makumbusho ilikuwa na dhamana ya kuwatembeza wageni wote kwenye makazi, kaburi isipo kuwa baadhi ya maeneo. Hali hiyo ilibadilika baada ya baadhi ya wanafamiilia kuanzisha utaratibu huo ambao kwa kweli wageni wengi, na watanzania kwa ujumla wanaushangaa na ni aibu kwa taifa.
Maoni yangu ni kwamba serikali inapaswa kuchukua dhamana ya kutunza eneo hilo hii ikiwa ni pamoja na usalama wake.
Kadhalika familia ama kikundi cha watu kamwe kisipewe ruhusa ya kufanya biashara ya aina yoyote katika eneo hilo.
Magamba wamemtelekeza mjane wa mwasisi wao wewe unategemea itakuwaje, watoto wote waliwatema kwenye system mpaka juzi makongoro kaponea mikononi mwa wapinzani akapata africa mashariki,sasa unategemea mama nyerere afanyeje?
Auze vitumbua, banaogopa kukamwatwa na mgambo wa jiji, kila mtu anafaidi na kile anachoweza kutumia.
Kama huamini fatilia familia za wastaaf waliowahi kuwa na mchango wa kizalendo kwenye nchi hii uone walivyotelekezwa,na kwasababu makaburi ya waume zao hayatembelewi,hawana mbadala wa kupata pesa.
Safi sana familia ya Mwl. Aibu ni kwa serikali ya magamba.
mimi nijizalilishe au wewe unazalilisha kupingana na ukweli?hivi unadhanu watanzania wanaishi kwa nadhali ?hizo huduma feki uamtangazia nani?tunajua kila kitu na ndiyo maanatunasema laana ya mwl itawamaliza mAGAMBA!mamajack,
Kukaa kimya ni bora kuliko kuropoka, hujui unachosema naona umeamua kujidhalilisha, familia ya Nyerere wanapewa huduma zote na serikali.
Nani ana uhakika kwamba hiyi familia haitunzwi tena?
Sidhani kama ni rahisi kiasi hicho kuiacha hiyo familia wanaweza kuwa wameweka hiyo fee kwa tamaa zao wenyewe.
Unahitaji kuwa kiongozi mwendawazimu kuitelekeza familia ya mwalimu
Inawezekana. Hata mtoa hoja hana risiti aliopewa kwa malipo hayo. Mbaya zaidi aliongea na mlinzi getini. Moja kati ya mambo mema aliofanya Mkapa na Sumaye ni kuhakikisha pensheni ipo kwa wastaafu wa ngazi kubwa za kitaifa na wajane wa viongozi wakuu wa kitaifa. Walikosea tu kutowaondoa wanaotuibia wakiwa madarakani kama akina Mkapa, Lowasa na Sumaye.
Zitakuwa njaa tu za hao watu wa Butiama waliopewa dhamana ya kutunza.
Hivi karibuni nilitembelea Butiama kuzuru makazi, kaburi na Makumbusho ya Mwl. Nyerere.
Kitu kilichonisikitisha na kunishangaza ni kwamba mtu haruhusiwi kuona kaburi la Baba wa Taifa hadi alipie huduma hiyo! Nilipouliza utaratibu huu upo tangu zamani, muhudumu wa pale getini alinijibu kwamba FAMILIA YA MWL NYERERE IMEAMUA KUANZISHA UTARATIBU HUU ILI KUPATA FEDHA ZA KUTUNZA FAMILIA!
Baadaye nilitembelea Makumbusho nikauliza suala hili nikajibiwa na maofisa wa Makumbusho kwamba hapo awali Makumbusho ilikuwa na dhamana ya kuwatembeza wageni wote kwenye makazi, kaburi isipo kuwa baadhi ya maeneo. Hali hiyo ilibadilika baada ya baadhi ya wanafamiilia kuanzisha utaratibu huo ambao kwa kweli wageni wengi, na watanzania kwa ujumla wanaushangaa na ni aibu kwa taifa.
Maoni yangu ni kwamba serikali inapaswa kuchukua dhamana ya kutunza eneo hilo hii ikiwa ni pamoja na usalama wake.
Kadhalika familia ama kikundi cha watu kamwe kisipewe ruhusa ya kufanya biashara ya aina yoyote katika eneo hilo.
Hivi karibuni nilitembelea Butiama kuzuru makazi, kaburi na Makumbusho ya Mwl. Nyerere.
Kitu kilichonisikitisha na kunishangaza ni kwamba mtu haruhusiwi kuona kaburi la Baba wa Taifa hadi alipie huduma hiyo! Nilipouliza utaratibu huu upo tangu zamani, muhudumu wa pale getini alinijibu kwamba FAMILIA YA MWL NYERERE IMEAMUA KUANZISHA UTARATIBU HUU ILI KUPATA FEDHA ZA KUTUNZA FAMILIA!
Baadaye nilitembelea Makumbusho nikauliza suala hili nikajibiwa na maofisa wa Makumbusho kwamba hapo awali Makumbusho ilikuwa na dhamana ya kuwatembeza wageni wote kwenye makazi, kaburi isipo kuwa baadhi ya maeneo. Hali hiyo ilibadilika baada ya baadhi ya wanafamiilia kuanzisha utaratibu huo ambao kwa kweli wageni wengi, na watanzania kwa ujumla wanaushangaa na ni aibu kwa taifa.
Maoni yangu ni kwamba serikali inapaswa kuchukua dhamana ya kutunza eneo hilo hii ikiwa ni pamoja na usalama wake.
Kadhalika familia ama kikundi cha watu kamwe kisipewe ruhusa ya kufanya biashara ya aina yoyote katika eneo hilo.
Ukweli ni kuwa serikali imewapa vingi sana familia ya Nyerere kiasi cha kuwa familia ya Nyerere yenyewe haina cha kurudisha serikalini! hapo ndipo gogoro la kichinichini kati ya familia ya Nyerere na serikali linapoanzia!Serikali na mamlaka zake wako usingizini, unategemea familia ifanyeje? Hakuna haki bila wajibu. Tafakari, chukua hatua.