Familia ya Nyerere mnaaibisha taifa

Status
Not open for further replies.
Apr 5, 2012
58
66
Hivi karibuni nilitembelea Butiama kuzuru makazi, kaburi na Makumbusho ya Mwl. Nyerere.

Kitu kilichonisikitisha na kunishangaza ni kwamba mtu haruhusiwi kuona kaburi la Baba wa Taifa hadi alipie huduma hiyo! Nilipouliza utaratibu huu upo tangu zamani, muhudumu wa pale getini alinijibu kwamba FAMILIA YA MWL NYERERE IMEAMUA KUANZISHA UTARATIBU HUU ILI KUPATA FEDHA ZA KUTUNZA FAMILIA!

Baadaye nilitembelea Makumbusho nikauliza suala hili nikajibiwa na maofisa wa Makumbusho kwamba hapo awali Makumbusho ilikuwa na dhamana ya kuwatembeza wageni wote kwenye makazi, kaburi isipo kuwa baadhi ya maeneo. Hali hiyo ilibadilika baada ya baadhi ya wanafamiilia kuanzisha utaratibu huo ambao kwa kweli wageni wengi, na watanzania kwa ujumla wanaushangaa na ni aibu kwa taifa.

Maoni yangu ni kwamba serikali inapaswa kuchukua dhamana ya kutunza eneo hilo hii ikiwa ni pamoja na usalama wake.

Kadhalika familia ama kikundi cha watu kamwe kisipewe ruhusa ya kufanya biashara ya aina yoyote katika eneo hilo.
 
Magamba wamemtelekeza mjane wa mwasisi wao wewe unategemea itakuwaje, watoto wote waliwatema kwenye system mpaka juzi makongoro kaponea mikononi mwa wapinzani akapata africa mashariki,sasa unategemea mama nyerere afanyeje?

Auze vitumbua, banaogopa kukamwatwa na mgambo wa jiji, kila mtu anafaidi na kile anachoweza kutumia.

Kama huamini fatilia familia za wastaaf waliowahi kuwa na mchango wa kizalendo kwenye nchi hii uone walivyotelekezwa,na kwasababu makaburi ya waume zao hayatembelewi,hawana mbadala wa kupata pesa.

Safi sana familia ya Mwl. Aibu ni kwa serikali ya magamba.
 
Dah, hii kweli ni aibu, lakini sidhani kama kweli kuwa hiyo tozo ni kwa ajili ya kutunza familia, hii sidhani kama ni sahihi!
 
Nyerere believed in socialism; and he left nothing to his family, yote aliyoyasimamia na kuyatunza yameharibiwa Sasa na kuuzwa!

Aibu ya magamba! Magamba hayaoni hii Aibu ila yataona wakati yanaelekea akhera.
 
Bora wanufaike angalau na kaburi la baba yao.

Mungu amuweke peponi baba wa taifa, alikuwa mtanzania asiye na tamaa, kafa BILA KASHFA YA UFISADI na kaacha familia yake ikiganga njaa kama wa TZ wengine.

Hakuwa na ubinafi, kwani alikuwa na uwezo wa kujilimbikizia vyakutosha.

R.I.P Mwalimu
 
Mwl Nyelele alikuwa mfano halisi na mzalendo wa kweli, hakujilimbikizia mali na ni kitu ambacho viongozi waliopo wa CCM wanaona kama ulikuwa udhaifu kwa marehemu baba wa taifa ndo maana wao sasa ni wizi kwa kwenda mbele.

Cha muhimu tuendelee kuichangia familia ya muasisi wa taifa hili kwani hata zile fedha za michango ya rambirambi nchi nzima zaidi ya 50% zimeliwa na wakuu wa wilaya na mikoa wakati huo.
 
Wafanyeje na wenyewe wametelekezwa na Kikwete?

Nakumbuka Makongoro alipokuwa akiomba kura kwa ajili ya ubunge wa Afrika Mashariki alisema, kafika Dodoma kwa nauli ya msaada.

Jamani hii si aibu?
 
Unahitaji kuwa kiongozi mwendawazimu kuitelekeza familia ya mwalimu
uwendawazimu upi zaid ya huu tulionao utakaokufanya uamini kuwa jk na serikali yake wanaweza kwa makusudi kabisaaaa kuitelekeza hiyo familia! Jk na mama mwana-asha ni zaidi ya uwajuavyo! Ni balaa nchini kwetu nakwambia!

RIP Nyerere, pray for me!
 
mamajack,

Haya uliyoandika hapa sio kweli.

Mjane wa Mwalimu analipwa 40% ya mshahara wa Rais wa sasa kama pensheni kila mwezi hadi atakapofariki. Wanae Mwalimu ni watu wazima na walianza kujitegemea siku nyingi kabla ya Mwalimu kufariki.

Kama wanatoza kiingilio pale ni masuala mengine kabisa. Mama Maria Nyerere anatunzwa vizuri tu sio na serikali hii bali hata Museveni wa Uganda.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom