MUSEVEN WA UGANDA!!!!KWA LIPI M7 amtunze!mamajack,
Haya uliyoandika hapa sio kweli.
Mjane wa Mwalimu analipwa 40% ya mshahara wa Rais wa sasa kama pensheni kila mwezi hadi atakapofariki. Wanae Mwalimu ni watu wazima na walianza kujitegemea siku nyingi kabla ya Mwalimu kufariki.
Kama wanatoza kiingilio pale ni masuala mengine kabisa. Mama Maria Nyerere anatunzwa vizuri tu sio na serikali hii bali hata Museveni wa Uganda.
Hivi karibuni nilitembelea Butiama kuzuru makazi, kaburi na Makumbusho ya Mwl. Nyerere.
Kitu kilichonisikitisha na kunishangaza ni kwamba mtu haruhusiwi kuona kaburi la Baba wa Taifa hadi alipie huduma hiyo! Nilipouliza utaratibu huu upo tangu zamani, muhudumu wa pale getini alinijibu kwamba FAMILIA YA MWL NYERERE IMEAMUA KUANZISHA UTARATIBU HUU ILI KUPATA FEDHA ZA KUTUNZA FAMILIA!
Baadaye nilitembelea Makumbusho nikauliza suala hili nikajibiwa na maofisa wa Makumbusho kwamba hapo awali Makumbusho ilikuwa na dhamana ya kuwatembeza wageni wote kwenye makazi, kaburi isipo kuwa baadhi ya maeneo. Hali hiyo ilibadilika baada ya baadhi ya wanafamiilia kuanzisha utaratibu huo ambao kwa kweli wageni wengi, na watanzania kwa ujumla wanaushangaa na ni aibu kwa taifa.
Maoni yangu ni kwamba serikali inapaswa kuchukua dhamana ya kutunza eneo hilo hii ikiwa ni pamoja na usalama wake.
Kadhalika familia ama kikundi cha watu kamwe kisipewe ruhusa ya kufanya biashara ya aina yoyote katika eneo hilo.
Tena wangetangaza kwenye vyombo vya habari ili wapate wateja wengi.
Wewe unamtisha mtoa mada iLi pindi aatakapoona uoza mwengine asiongee, hayo si mageni nchi hii unashanga nini, kila mahala nchi hii ImeozaMkuu,
Hili jambo ulilotumwa kuandika hapa ni zito na nafikiri wewe unatambua. Itakuwa ni jambo la busara kutuwekea ushahidi wa haya yote uliyoyasema kwani utakuwa na stakabadhi ya malipo ya hiyo tour yako kwenye kaburi.
Pia hao watu wa kwenye geti ambao walikuzuia kuingia hadi ulipe itabidi uwatambue endapo utahitajika kufanya hivyo.
Si wewe pekee ambae umefika hapo kiasi cha kutoona ulinzi wa askari kwani makumbusho hayo ni kwa raia wa Tanzania na kigeni pia ambao hupenda kufika mahali hapo.
Vinginevyo naona ulichoandika hapa ni nje kabisa ya mstari na pia uangalie maana naona unatoa kashfa kwa familia ya Mwalimu.
mamajack,
Haya uliyoandika hapa sio kweli.
Mjane wa Mwalimu analipwa 40% ya mshahara wa Rais wa sasa kama pensheni kila mwezi hadi atakapofariki. Wanae Mwalimu ni watu wazima na walianza kujitegemea siku nyingi kabla ya Mwalimu kufariki.
Kama wanatoza kiingilio pale ni masuala mengine kabisa. Mama Maria Nyerere anatunzwa vizuri tu sio na serikali hii bali hata Museveni wa Uganda.
Baba wa Taifa amezikwa kwenye shamba lake. Tatizo ni nini? Tusishangae kwa hayo yanayotokea labda angezikwa pale Makumbusho!!!! Uongozi wa CCM haukuwa na ujasiri wa kuzungumzia juu ya watu mashuhuri kisiasa nchini watakapoitwa na Mungu watahifadhiwa wapi. Hili lina ugumu wake lakini pia ni ukweli kila mtu atakufa. Kifo cha ghafla cha Edward Sokoine ilikuwa fundisho tosha kuwa watu kama hawa ambao wana nafasi ya kipekee katika taifa wapumzishwe wapi siku wakiondoka duniani.
Ukweli ni kuwa serikali imewapa vingi sana familia ya Nyerere kiasi cha kuwa familia ya Nyerere yenyewe haina cha kurudisha serikalini! hapo ndipo gogoro la kichinichini kati ya familia ya Nyerere na serikali linapoanzia!
Kuna aliyeshangazwa na Makongoro kukosa hata nauli ya kwenda Dodoma!hivi huyu mtu anataka hata usafiri wa Makongoro mwenyewe uhudumiwe na Serikali?! mwisho atakuja kutaka serikali imlipie mfanyakazi wa kukata nyasi za nyumbani kwake (kama hawajafikia hatua hii)?!...na wale mama zetu wanaouza vitumbua barabarani nao mbona hakuna wa kuyakimu maisha yao au hata kuwasemea? au si Watanzania wale?
Hili kaburi lifukuliwe na akazikwe kwao kule ambako wazazi wake wametokea labda huko familia yake inaweza kupatiwa hizo huduma wanazozitaka, lakini isiwe katika ardhi ya Tanzania.
kwanza ukaangalie kaburi la nyerere ili upate nini?mimi siamini kwenye hayo mambo..the man is dead and long buried,let him rest in peace
Nani ana uhakika kwamba hiyi familia haitunzwi tena?
Sidhani kama ni rahisi kiasi hicho kuiacha hiyo familia wanaweza kuwa wameweka hiyo fee kwa tamaa zao wenyewe.
Unahitaji kuwa kiongozi mwendawazimu kuitelekeza familia ya mwalimu
Majita,Mie hii taarifa imeongeza hasira zangu ZA MAKAO MAKUU YA WILAYA YA MUSOMA VIJIJINI eti kupelekwa Butiama.Hivi kweeeeelii kweli kweli mura wane kweli.Inamaana hawakupaona Mugango,Murangi,Bukima au sehemu yoyote ya Majita kuwa makao makuu hadi "Buti-hama" tuuu?? lol eti kusogeza huduma kwa wananchi,fyuuuuu
Hivi karibuni nilitembelea Butiama kuzuru makazi, kaburi na Makumbusho ya Mwl. Nyerere.
Kitu kilichonisikitisha na kunishangaza ni kwamba mtu haruhusiwi kuona kaburi la Baba wa Taifa hadi alipie huduma hiyo! Nilipouliza utaratibu huu upo tangu zamani, muhudumu wa pale getini alinijibu kwamba FAMILIA YA MWL NYERERE IMEAMUA KUANZISHA UTARATIBU HUU ILI KUPATA FEDHA ZA KUTUNZA FAMILIA!
Baadaye nilitembelea Makumbusho nikauliza suala hili nikajibiwa na maofisa wa Makumbusho kwamba hapo awali Makumbusho ilikuwa na dhamana ya kuwatembeza wageni wote kwenye makazi, kaburi isipo kuwa baadhi ya maeneo. Hali hiyo ilibadilika baada ya baadhi ya wanafamiilia kuanzisha utaratibu huo ambao kwa kweli wageni wengi, na watanzania kwa ujumla wanaushangaa na ni aibu kwa taifa.
Maoni yangu ni kwamba serikali inapaswa kuchukua dhamana ya kutunza eneo hilo hii ikiwa ni pamoja na usalama wake.
Kadhalika familia ama kikundi cha watu kamwe kisipewe ruhusa ya kufanya biashara ya aina yoyote katika eneo hilo.
Mkuu hapa hoja umeilewa au imekupita kidogo?
Makumbusho ya Nyerere inalipiwa hivi sasa ila ukitaka kuona kaburi unatakiwa ulipie kwa huduma hiyo ya kuona kaburi
Duniani kote makumbusho mengi ni ya kulipia ila hii ya kulipia kuona kaburi ndio naipta sasa.
Nenda kwa waasisi wa usoshalisti kama kina Ho Chi Min na V.I. Lenin, makaburi yao yapo kwenye public squares kuona bure.
Nenda Uturuki, makaburi ya waasisi wao yamejengewa na kuona ni bure, nenda Iraq na Iran hali ni vile vile. Nenda Uingereza na watu wao maarufu, makaburi ni sehemu ya makumbusho au bure
Heck, nenda Tumbuktu na makaburi ya maulamaa maarufu katika mji huo wa kihistoria ni bure.
Hata hapo Zanzibar kuona kaburi la Karume ni bure.