Ni yapi madhumuni ya kijiji cha Makumbusho?

Mfufua Nyuzi

Senior Member
Mar 11, 2024
193
240
Kijiji cha Makumbusho ni sehemu ya makumbusho inayoonesha nyumba na vifaa vilivyojengwa kihalisi kutoka kwa makabila machache ya Tanzania na liko katikati ya jiji la Dar es Salaam. Ni miongoni mwa makumbusho matano nchini, mengine yakiwa ni makumbusho ya Taifa ya Dar es Salaam, makumbusho ya Mwalimu Nyerere, makumbusho ya historia ya asili na makumbusho ya azìmio la Arusha.

Swali langu; Ni muda mrefu umepita, Je Makumbusho haya yamekuwa na tija gani kwa taifa hususan kwenye jiji la kimkakati na biashara kama Dar es Salaam?

Kwa maoni na mtazamo wangu binafsi, Kwa taifa ambalo uchumi wake bado unasua sua yale ni matumizi mabaya ya ardhi hususan kwa eneo la biashara na kimkakati kama Dar es salaam. Kwanza kabisa tayari kuna maeneo ya aina hiyo yaliyoshiba maudhui kama ya hapo Makumbusho, Mfano kuna makumbusho ya Mwalimu Nyerere, Azimio la Arusha, makumbusho ya vita ya majimaji n.k Sasa kulikuwa na haja gani ya kuweka makumbusho eneo lingine?

Kwa nchi masikini ambayo bado uchumi wake unakua lile eneo ilipaswa pajengwe aidha kiwanda kidogo cha kuchakata vifaa vya umeme au technology innovation space centre ili nchi izalishe vijana wenye ujuzi katika technology wachangie katika uchumi wa taifa. Badala yake eneo muhimu kama lile panajengwa vibanda vya vijumba vya udongo ambavyo si vitu vigeni hata kwa wageni kusema kwamba wataenda kushangaa, kwa sababu ukitoka tu nje kidogo ya Dar es salaam bado kuna watu wanaishi maisha hayo! Kwa hiyo kujenga vile vinyumba pale ni kama kuwakebehi! Kwa sababu bado kuna watu wanaishi maisha yale kutokana na umasikini.

Natambua umuhimu wa Museum, hata ukienda Uingereza pale Yorkshire kuna museum inaitwa York Museum, pia Ujerumani huko kuna museum za Nazi regimes, lakini zilijengwa baada ya mataifa hayo kukua na kuinuka kiuchumi na hata location zilipojengwa haikuathiri shughuli za uzalishaji! Pia tayari wameshatoka huko wapo hatua nyingine ndiyo maana yale yanabaki kuwa makumbusho! Ila sisi bado hatujatoka kuishi kwenye nyumba za udongo au kutumia vinu n.k sasa makumbusho ya nini?

USHAURI; Kwa kifupi Makumbusho village ibomolewe au ihamishiwe huko Kigamboni, Eneo lile pajengwe ICT/Technology Innovation hub/Centre.
 
Mimi naona haina shida, Ardhi tunayo kubwa sana wala hiyo sio shida yetu kabisa. Waangalie tu namna gani hii Makumbusho ikae kimkakati kuingiza Pesa.
 
Kwani lazima na nyie mjenge hyo it innovation blahblah hapo
Alafu unafikiri kijiji hiko hapo kimekaa kwa bahati mbaya!
Umeona jirani wako wakina nani hapo ???

Ova
 
Ile ni sehemu sahii. Hakuna haja ya kuhamisha. Tanzania ina eneo kubwa sana wakuze miji sehemu nyingine.

Nyie ndio wale waliouza viwanja vya michezo vyote kwa tamaa za pesa na sasa jiji halina viwanja vya wazi na watu wamejenga kwenye mitaro.....

Kila mji lazima uwe na mipango sio tamaa tamaa tu ya kila kitu.

Useless uzi.
 
Hata nikipita Lugalo nikitazama ile kambi ya jeshi na lile pori katikati ya mji wa kibiashara kama Dsm, naona pia ni matumizi mabaya ya ardhi.

Kwanini hizo kambi wasiwe wanazisogeza mbali na miji pale miji inapokuwa? kwanini inakuwa ni lazima zibaki maeneo hayo hayo miaka yote licha ya ukuaji wa miji yetu?

Matokeo yake watafuga nyoka wataokuja kuwadhuru wapita njia na kuhatarisha afya zao.
 
Back
Top Bottom