Nyerere ni mfano wa kiongozi bora kabisa wa taifa lisilo na dini "secular"

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,260
Kwa hakika Baba wa taifa hili Mwl. Julius Nyerere alijua kutenganisha dini na siasa. Pamoja na kuwa alikuwa Mkatoliki madhubuti sana lakini hakujaribu kuingiza dini yake kwa namna yoyote ile katika siasa za nchi.

Sioni kumbukumbu zozote Nyerere akiwa anahutubia kanisani, akiwa anachangisha pesa za kujenga makanisa au misikiti, akiwa anaomba kuombewa ombewa kila mara, akiwa anawapa nafasi za mbele katika mambo ya kisiasa viongozi wa dini.

Huenda hata wale wanaolalamika kwamba alihusika kuvunjwa kwa EAMWS ni kwasababu aliona mambo ya kidini ya chama hicho yanataka kuletwa barazani kwa serikali.

Katika kutenga dini na siasa hakika hakuna kama Nyerere katika taifa hili na Africa kwa ujumla, ni kiongozi wa mfano wa kuigwa.
 
Back
Top Bottom