Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

#Pmoses95# mm nilijenga msingi wangu kwa kuzingatia vigezo vyote ulivyoeleza.
Kabla kumwaga zege la mwanzo nilitanguliza mchanga laini chini kiasi cha nchi 5 na kushindilia na kumwagilia maji. Ila juu ya msingi sikuweka ring beam, je nitegeme changamoto gani siku za usoni?
Site Location Dodoma.
 
#Pmoses95# mm nilijenga msingi wangu kwa kuzingatia vigezo vyote ulivyoeleza.
Kabla kumwaga zege la mwanzo nilitanguliza mchanga laini chini kiasi cha nchi 5 na kushindilia na kumwagilia maji. Ila juu ya msingi sikuweka ring beam, je nitegeme changamoto gani siku za usoni?
Site Location Dodoma.
Ulifanya Jambo jema, pia ungeboresha zaidi Kama tofali za msingi zilizo chini ya ardhi ungezi backfill kwa mchanga. Hapo usingeona athari yoyote.
 
Hapa nitaelezea Sababu za msingi zinazosababisha majengo yanayofanana kujengwa kwa gharama tofauti.

Tuzungumzie mchoro wa nyumba ya vyumba vitatu vya Kulala kimoja kati ya hivyo ni master bedroom, sitting room, dining, kitchen ,public toilet na store.
Mchoro aliununua ndugu anaitwa Juma, baada ya Juma kununua Alitoa copy akawapa majirani zake wawili Hasani na John.

Hawa wote walijengewa na fundi mmoja ambae ni mimi. Lkn Kila mtu kutumia gharama tofauti kusimamisha boma.

SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA GHARAMA ZA UJENZI ZITOFAUTIANE :

1. location
2. Uimara
3.land type. (slop au tambalale)
4.soil type
5.nyakati.

HAPA NITAZUNGUMZIA UIMARA
Msingi wa nyumba imara utajengwa Kama ifuatavyo.
. Utachimbwa kwenda chini urefu WA mita moja au zaidi.
. Utaanza na zege yenye ratio nzuri kabla ya kujenga tofali
.Utajengwa kwa tofali imara
.Utawekewa Beam yenye kusukwa nondo na ratio nzuri
.Utamwagiliwa maji ya kutosha.
ILI HAYA YOTE YAFANYIKE LAZIMA UMPATE FUNDI MZURI.

Juma aliomba nyumba yake nimjengee kwa viwango hivyo, ndio maana nilitumia tofali nyingi,cement nyingi, nondo nyingi, mchanga mwingi, kokoto nyingi, ring za kutosha, maji mengi nk. Ktk kujenga msingi.

John alisema uwezo wake mdogo , yeye alihitaji tuchimbe futi moja kwenda chini baada ya hapo tujenge tofali, hakuishia hapo pia alisema tusiweke Beam.

Kilichotekea ni utofauti wa Tshs zaidi ya million nne kati ya hiyo misingi miwili.

Kiufupi Juma alitumia 6mil
John Tshs 2.8mil
Hasani Tshs 4mil.

Kilichotofautisha ni uimara WA kujenga msingi. Hawa wote ni majirani.

Mpaka tunamaliza boma Juma alitumia 18m
John 7m
Hasani 12m.
Nyumba zote hizi zikipigwa rangi vizuri hutoweza kujua madhaifu ya awali mpaka pale utakapoanza kuona nyufa (expansion joint)

Hoja yangu hapa ni kwamba unapotokea mjadala wa gharama za ujenzi LAZIMA tuzingatie vitu mhimu vinavyosababisha gharama kuwa kubwa au ndogo.

Ushauri.
1.Tusipende kukimbilia kununua nyumba wakati hujui ilijengwa kwa viwango vipi.
2.Jenga nyumba imara ogopa vya Bei cheee
3.Nyumba kuijenga si lelemama, ili kumudu anza mdogomdogo. Ukiwa na 5m anza hata msingi.

Ukihitaji fundi, usisite kunitafuta, nafanya kazi mikoa yote tanzania
0655173113


UPDATES
tuendelee na mjadala wetu. Hapo awali tulijadili jinsi namna gani uimara wa nyumba unavyoathiri gharama za ujenzi. Leo tujadili namna location inavyoathiri gharama za ujenzi.

NAMNA LOCATION INAVYOSABABISHA GHARAMA ZA UJENZI KUWA TOFAUTI.

Mungu aliumba ardhi ktk mionekano tofauti. Kuna tambalale, milima na mabonde.
Ujenzi ktk Eneo tambalale unagharama nafuu kulinganisha na Eneo lenye slope . Lakini pia ujenzi wa Eneo tambalale lililoko Chanika mkoni DSM Unaweza kuwa na gharama tofauti na ujenzi wa Eneo tambalale lililoko msasani mkoani DSM. Hivyo hivyo ujenzi wa DSM unagharama kubwa kuliko ujenzi wa Mbeya.

SABABU ZA KUTOFAUTISHA GHARAMA KATI YA ENEO TAMBALALE NA LENYE SLOP.

sanasana hapa kimbembe huwa ktk kujenga msingi wa nyumba.

Msingi uliotumia tofali 1500 katika eneo tambalale, msingi huohuo ukitaka kuujenga ktk eneo lenye slope unaweza kutumia tofali 2300 au zaidi kulingana na ukali wa slope.
Tukumbuke kwamba Kwa kadri tofali zinavyoongezeka ndivyo na material mengine yanavyozidi kuongezeka kitu ambacho hupelekea kuongezeka kwa gharama za fundi. Si ajabu kumalizia 10mil ktk msingi wa nyumba ya Vyumba vitatu ktk Eneo LA slope.

Hivyo basi kama hutaki kutumia gharama kubwa kwenye ujenzi epuka kununua viwanja vilivyo na slope.

Jambo lingine linaloathiri ktk location ni upatikanaji wa material.
Mfano mtu anaejenga mbezi beach atanunua tani 18 Za mchanga zaidi ya 450.000 Tshs wakati mtu wa Chanika atanunua Kwa 220,000tshs.

Pia boma utakalojenga kwa 8mil Mbeya, DSM utalijenga Kwa zaidi ya 15mil. Sababu Mbeya tofali ni cheap, labour ni cheap nk.

JE, WAJUA KWAMBA KUNA MFUMO MPYA WA MAJI TAKA AMBAO HAUJAZI MASHIMO YA VYOO! USIHANGAIKE NA MFUMO WA ZAMANI. PATA MFUMO MPYA UACHANE NA GHARAMA ZA KUITA GARI ZA KUNYONYA UCHAFU.

Kwa ujenzi imara na wakisasa tutafutane 0655173113

Nashukuru kwa mada nzuri. Naomba uongee pia ujenzi unanyika eneo moja (viwanja vinafuatana) , ramani ni sawa kabisa, ukubwa wa jengo ni sawa e.g G + 5 lakini gharama zinakuwa tofauti.

Ahsante
 
Nashukuru kwa mada nzuri. Naomba uongee pia ujenzi unanyika eneo moja (viwanja vinafuatana) , ramani ni sawa kabisa, ukubwa wa jengo ni sawa e.g G + 5 lakini gharama zinakuwa tofauti.

Ahsante
Kabla ya kuliongelea hilo , naomba unifahamishe kuhusu umiliki wa hivyo viwànja. Je vinamilikiwa na mtu mmoja? Je , hizo nyumba zimejengwa na fundi mmoja?
 
Kabla ya kuliongelea hilo , naomba unifahamishe kuhusu umiliki wa hivyo viwànja. Je vinamilikiwa na mtu mmoja? Je , hizo nyumba zimejengwa na fundi mmoja?

Vyote ni vinamilikiwa na MAMLAKA (Natumaini umeelewa) Eneo LA nyumba (vyumba+ nje) ni sawa ILA ujenzi umefanywa na Kampuni mbili tofauti.

Ahsante
 
Back
Top Bottom