Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Fundi mahiri wa ujenzi

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
3,954
2,439
Screenshot_20210417-075736.png

Hapa nitaelezea Sababu za msingi zinazosababisha majengo yanayofanana kujengwa kwa gharama tofauti.

Tuzungumzie mchoro wa nyumba ya vyumba vitatu vya Kulala kimoja kati ya hivyo ni master bedroom, sitting room, dining, kitchen ,public toilet na store.

Mchoro aliununua ndugu anaitwa Juma, baada ya Juma kununua Alitoa copy akawapa majirani zake wawili Hasani na John.

Hawa wote walijengewa na fundi mmoja ambae ni mimi. Lkn Kila mtu kutumia gharama tofauti kusimamisha boma.

SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA GHARAMA ZA UJENZI ZITOFAUTIANE
1. Location
2. Uimara
3. Land type. (slop au tambalale)
4. Soil type
5. Nyakati.

HAPA NITAZUNGUMZIA UIMARA
Msingi wa nyumba imara utajengwa Kama ifuatavyo.
. Utachimbwa kwenda chini urefu WA mita moja au zaidi.
. Utaanza na zege yenye ratio nzuri kabla ya kujenga tofali
.Utajengwa kwa tofali imara
.Utawekewa Beam yenye kusukwa nondo na ratio nzuri
.Utamwagiliwa maji ya kutosha.
ILI HAYA YOTE YAFANYIKE LAZIMA UMPATE FUNDI MZURI.

Juma aliomba nyumba yake nimjengee kwa viwango hivyo, ndio maana nilitumia tofali nyingi,cement nyingi, nondo nyingi, mchanga mwingi, kokoto nyingi, ring za kutosha, maji mengi nk. Ktk kujenga msingi.

John alisema uwezo wake mdogo , yeye alihitaji tuchimbe futi moja kwenda chini baada ya hapo tujenge tofali, hakuishia hapo pia alisema tusiweke Beam.

Kilichotekea ni utofauti wa Tshs zaidi ya million nne kati ya hiyo misingi miwili.

Kiufupi Juma alitumia 6mil
John Tshs 2.8mil
Hasani Tshs 4mil.

Kilichotofautisha ni uimara WA kujenga msingi. Hawa wote ni majirani.

Mpaka tunamaliza boma Juma alitumia 18m
John 7m
Hasani 12m.
Nyumba zote hizi zikipigwa rangi vizuri hutoweza kujua madhaifu ya awali mpaka pale utakapoanza kuona nyufa (expansion joint)

Hoja yangu hapa ni kwamba unapotokea mjadala wa gharama za ujenzi LAZIMA tuzingatie vitu mhimu vinavyosababisha gharama kuwa kubwa au ndogo.

Ushauri
1. Tusipende kukimbilia kununua nyumba wakati hujui ilijengwa kwa viwango vipi.
2. Jenga nyumba imara ogopa vya Bei cheee
3. Nyumba kuijenga si lelemama, ili kumudu anza mdogomdogo. Ukiwa na 5m anza hata msingi.

UPDATES
tuendelee na mjadala wetu. Hapo awali tulijadili jinsi namna gani uimara wa nyumba unavyoathiri gharama za ujenzi. Leo tujadili namna location inavyoathiri gharama za ujenzi.

NAMNA LOCATION INAVYOSABABISHA GHARAMA ZA UJENZI KUWA TOFAUTI
Mungu aliumba ardhi ktk mionekano tofauti. Kuna tambalale, milima na mabonde.
Ujenzi ktk Eneo tambalale unagharama nafuu kulinganisha na Eneo lenye slope . Lakini pia ujenzi wa Eneo tambalale lililoko Chanika mkoni DSM Unaweza kuwa na gharama tofauti na ujenzi wa Eneo tambalale lililoko msasani mkoani DSM. Hivyo hivyo ujenzi wa DSM unagharama kubwa kuliko ujenzi wa Mbeya.

SABABU ZA KUTOFAUTISHA GHARAMA KATI YA ENEO TAMBALALE NA LENYE SLOP
Sanasana hapa kimbembe huwa ktk kujenga msingi wa nyumba.

Msingi uliotumia tofali 1500 katika eneo tambalale, msingi huohuo ukitaka kuujenga ktk eneo lenye slope unaweza kutumia tofali 2300 au zaidi kulingana na ukali wa slope.

Tukumbuke kwamba Kwa kadri tofali zinavyoongezeka ndivyo na material mengine yanavyozidi kuongezeka kitu ambacho hupelekea kuongezeka kwa gharama za fundi. Si ajabu kumalizia 10mil ktk msingi wa nyumba ya Vyumba vitatu ktk eneo la slope.

Hivyo basi kama hutaki kutumia gharama kubwa kwenye ujenzi epuka kununua viwanja vilivyo na slope.

Jambo lingine linaloathiri ktk location ni upatikanaji wa material.

Mfano mtu anaejenga mbezi beach atanunua tani 18 Za mchanga zaidi ya 450.000 Tshs wakati mtu wa Chanika atanunua Kwa 220,000tshs.

Pia boma utakalojenga kwa 8mil Mbeya, DSM utalijenga Kwa zaidi ya 15mil. Sababu Mbeya tofali ni cheap, labour ni cheap nk.

JE, WAJUA KWAMBA KUNA MFUMO MPYA WA MAJI TAKA AMBAO HAUJAZI MASHIMO YA VYOO! USIHANGAIKE NA MFUMO WA ZAMANI. PATA MFUMO MPYA UACHANE NA GHARAMA ZA KUITA GARI ZA KUNYONYA UCHAFU.

Kwa ujenzi imara na wakisasa tutafutane 0655173113

Screenshot_20210416-102139_1.jpg
3-1.jpg
IMG_20210520_142353.jpg
IMG_20210401_122453_030.jpg
IMG_20210520_142336.jpg
IMG_20210524_170016.jpg
IMG_20210930_102446.jpg
IMG_20210715_144345_370.jpg
 
Nashukuru mkuu insta page yenu ni ipo nahitaji ramani nataka jione sample za nyumba kwanza, nahitaji vyumba vitatu kimoja kiwe sc. jiko p.t na dinning sebule iwe kubwa kidogo.
 
hujahitimish vuzuri,kwa hiyo ilitujenge kwa gharama nafuu inatubidi tujengengeje?
Nunua kiwanja tambalale, ikiwa Sehemu ya kichanga itapendeza zaidi. Wakati unajenga msingi chimba mashimo ya vyoo ili kupunguza gharama za kifusi.

Kuwa na mahusiano mazuri na fundi ili asikununulishe vitu vya gharama bila Sababu. Usimbane fundi Kuhusu malipo yake, atakupa Ushauri mzuri wa kupunguza gharama bila kupunguza ubora
 
Kwa ramani hiyo. Mimi msingi nimetumia milioni tano na point mkuu.

Hakika fundi anaenijengea yuko vizuri. Ingawa jirani yangu hapa naona boma lake lina expansion joint za kutosha kwa ndani
 
Kwa ramani hiyo. Mimi msingi nimetumia milioni tano na point mkuu.

Hakika fundi anaenijengea yuko vizuri. Ingawa jirani yangu hapa naona boma lake lina expansion joint za kutosha kwa ndani
Yaah ni kweli inarange kati ya 5 - 7m kulingana na kiwanja kilivyo
 
Back
Top Bottom