Ngoja niwahabarishe mambo kadhaa usiyo yajua katika ujenzi

greater than

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
783
1,215
Ngoja niwahabarishe mambo kadhaa usiyo yajua katika ujenzi.

1.Jengo/Nyumba siyo lazima liwe na msingi.
Unabisha....?
Nenda Msasani makangira(Namanga),
Kuna nyumba kadhaa hazina msingi.

2.Unyevu ndiyo sababu kubwa ya kuharibika kwa Majengo .
unabisha....?
Chumvi,ukungu na kutu vyote hutokana na unyevu.

3.Madirisha ya wavu ni bora kuliko ya Vioo.(Kwa mikoa ya Pwani)
Unabisha...?
Vizio umeme ukikatika kwenye nyumba za madirisha ya Aluminium, utaona watu wanavyokimbilia nje.

4.Goba,Mbezi,Kimara na Kinyerezi ni maeneo ambayo ujenzi wa Msingi ni gharama zaidi kuliko maeneo yoyote....
Unabisha....?
Waulize wenye nyumba Goba.

5.Pavements ni moja chanzo kikubwa cha joto ndani nyumba
Unabisha....?

Nenda kwenye nyumba ambapo eneo lote la nje ji paved,,kaa nje mda mchana, utaona fukuto lake.
 
Tupe gharama simple za gorofa ya kawaida mkoani kama Morogoro
Ghorofa ya kawaida ndiyo ikoje...?
-Ina floor ngapi...?
-Ina vyumba vingapi
-Ukubwa wa vyumba ukoje
-Ya makazi au Ofisi
-Itakuwa na paa la aina gani?
 
Ghorofa ya kawaida ndiyo ikoje...?
-Ina floor ngapi...?
-Ina vyumba vingapi
-Ukubwa wa vyumba ukoje
-Ya makazi au Ofisi
-Itakuwa na paa la aina gani?
Floor mbili juu vyumba viwili master na sehemu ndogo ya kupumzika.

Chni vyumba 2 ,sebule ,jiko ,public toilets(viwili) ..Mazaga Mengine kama store
 
Nyumba ya tofali za udongo/tope ni imara kuliko ya tofali za mchanga.
Uimara na Ubora wa matilio za ujenzi hutokana na.
1.Uandaaji wa matilio husika.
Mfano :Mbao ikivunwa na kuandaliwa kwa umakini ,huweza kudumu zaidi ya miaka Mia,
-Pia kioo,kikiandaliwa vizuri kinakuwa na ugumu sawa na zege.

2.Umbo litalowekwa matilio.
Mfano : Mianzi ikikunjwa vizuri, inakuwa na nguvu sawa na nondo
-Hata Yai,matilio yake ni nyepesi ila umbo lake linafanya ushindwe pasua kwa mkono.

3.Kani ya Gravity
-Kadri unavyoenda juu,ndiyo kuna matilio zinazidi kuathiriwa na Gravity.
Ndiyo maana ni Ngumu kukuta ghorofa ndefu za Udongo au mbao.

Kwahiyo matilio zote za ujenzi zina uwezo sawa,ila ni namna utakavyo zitumia.
 
Floor mbili juu vyumba viwili master na sehemu ndogo ya kupumzika.

Chni vyumba 2 ,sebule ,jiko ,public toilets(viwili) ..Mazaga Mengine kama store
Ningekufanyia mahesabu,ila kusema kweli hiyo ni inachukua mda...
Mana lazima nitafute data za bei za matilio za Morogoro, Aina ya magari zinazobeba matilio kama Kokoto,Mchanga na Gharama za kuwalipa mafundi kwa Morogoro zikoje...
Hiyo siwezi kufanya kwa bure.
 
Mwezi wa 4 naingia likizo
Kwa mwenye kuhitaji kutembelewa katika eneo lake, kukagua na kutoa ushauri juu ya tatizo lolote, kuwa huru kunijuza.

Gharama : Huduma hii ni bure
Usafiri : ndiyo pekee utagharamia.
 
Naombeni msaada wa ushauri mimi nataka niweke tiles sebuleni na vyumbani nini faida na hasara yake
 
Mwezi wa 4 naingia likizo
Kwa mwenye kuhitaji kutembelewa katika eneo lake, kukagua na kutoa ushauri juu ya tatizo lolote, kuwa huru kunijuza.

Gharama : Huduma hii ni bure
Usafiri : ndiyo pekee utagharamia.
Uko mkoa gani??
 
Naombeni msaada wa ushauri mimi nataka niweke tiles sebuleni na vyumbani nini faida na hasara yake
Faida za Tiles ,zina saidia
- Kutawanya mwanga ndani ya chumba,maana zina akisi mwanga.
-Rahisi kusafishika.
-Hazi athiriwi na kemikali kiurahisi
-Zina urembo wa michoro mbalimbali.

Hasara za Tiles
-kuteleza zikiwa zimelowa
-kuvunjika (hapa ina tegemeana na ugumu wake)

Zingatio
Umakini wahitajika kwenye uwekaji wake.
 
Faida za Tiles ,zina saidia
- Kutawanya mwanga ndani ya chumba,maana zina akisi mwanga.
-Rahisi kusafishika.
-Hazi athiriwi na kemikali kiurahisi
-Zina urembo wa michoro mbalimbali.

Hasara za Tiles
-kuteleza zikiwa zimelowa
-kuvunjika (hapa ina tegemeana na ugumu wake)

Zingatio
Umakini wahitajika kwenye uwekaji wake.

Ok asante
 
Mwezi wa 4 naingia likizo
Kwa mwenye kuhitaji kutembelewa katika eneo lake, kukagua na kutoa ushauri juu ya tatizo lolote, kuwa huru kunijuza.

Gharama : Huduma hii ni bure
Usafiri : ndiyo pekee utagharamia.
Unapatikana maeneo gani Dar es Salaam, nahitaji kufanya marekebisho ndani ya nyumba yangu, Jikoni, na Choo cha master bedroom.
Nahitaji kujua eneo unalopatikana ili nijue urahisi au ugumu kukufikisha eneo langu, na mawasiliano yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom