Fahamu utajiri wa kudumu uliojificha kwenye zao la Parachichi Mkoani Njombe

Umetoa mada nzuri ushauli tuu hiyo space mlioweka ni ndogo mno miti itashonana na kushindwa kuzaa vzr parachichi ni mti mkubwa 10m*10m au iwe 10m*8m angalau kidogo.
 
Umetoa mada nzuri ushauli tuu hiyo space mlioweka ni ndogo mno miti itashonana na kushindwa kuzaa vzr parachichi ni mti mkubwa 10m*10m au iwe 10m*8m angalau kidogo.
Kuna sehemu tumepanda Parachichi mita 8 kwa nane. Hilo eneo Lina udongo wa mfinyanzi kuanzia Tabaka la pili hivyo mategemeo ni Miti haitakuwa na uwezo wa kutanuka SANA.
 
UNAWEZA KUYATAJA HAYO MASHIRIKA? NINACHOFAHAMU MIMI, PARACHICHI INAPANDWA KWA MBOJI/MBOLEA YA MIFUGO, DAP, NPK, TSP AU MINJINGU-MOHP. HAKUNA MBOLEA YA AJABU. HATA DAWA WAKULIMA WANASHAURIWA WATUMIE DAWA YA ASILI MFANO PILIPILI.
(Je hujui kuwa Marekani wanalima Parachichi?)

Kuna uchafu unaitwa vibinjo kazi yao kuwatafutia wanunuzi (how???) kwa nini watafutiwe wanunuzi? Halafu bei anapanga mnunuzi (utaona kabisa hii dhuluma) halafu mnunuzi ananunua matunda anayotaka yeye mengine anayaacha yaozee shambani
SIJUI KWA NJOMBE, ILA KWA TUKUYU WANANUNUA KILA KITU KWA MKATABA, KUNA USHINDANI.

Ninyi ndio mlipashwa kuwatetea wakulima hawa sio kuwauzia watu maeneo na kuwapa sijui elekezi la zao la parachichi....[/QUOTE]

(Ni vizuri kama wakulima wakiwa kwenye umoja wa Ushirika wanaweza kujadiliana Bei na kutafuta elimu zaidi).

Waziri husika anapashwa kufuatilia Kilimo mikoa mikuu inayozalisha mazao ya chakula na biashara.....[/QUOTE]
[/QUOTE]
Sijakuelewa ujue
 
Habari ya majukumu wakuu. Niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.

Maparachichi ni matunda bustanini na mashambani. Maparachichi yana matumizi mengi yenye faida kubwa kwa wakulima na wadau wengine.

Maparachichi ni chakula chenye viini lishe bora kama vitamini {A, B2, C, D, E, K} na madini {P, K,Mn, S} ambavyolinda mwili , mafuta kwa wingi asilimia 5 mpaka 30ambayo huleta joto mwilini, protin asilimia 1 mpaka 5ambayo hujenga mwili na kiasi cha colories 250 ambayo huleta nguvu mwilini.

Tofauti na matunda mengine, maparachichi ni malighafi ya viwandani kutengenezea madawa ya ngozi pamoja na vipodozi mfano mafuta ya nywele, shampoo na sabuni. Vilevile majani yake na mbegu hutumika kama dawa.

Aina bora za parachichi ambazo zimefanyiwa utafditi na kukubalika kwa wakulima na walaji ni pamoja na HASS, FUERTE, WEISAL IKULU, MWAIKOKESYA, EX TENGERU NA NABALI. Aina hizi zinazaa matunda mengi na bora pia huchukua muda mfupi kukomaa . kiasi chs matunda kwa mti ni klati ya 300 hadi 800 kutegemeana na matunda

Njia bora ya kuzalisha miche ya maparachichini kwa njia ya vikonyo. Faida zinazotokaana na njia hii ni

Miti kuchukua muda mfupi kukomaa na kuzaa matunda {miaka 3}
Miti huwa na umbo na urefu wa wastani
Kuepusha magonjwa hasa virus
Miche mingi kuzalishwa kwa wakati mmoja

HATUA ZA KUFUATA KABLA YA KUZALISHA MICHE KWA NJIA YA VIKONYO
1. Kuzalisha miche ya kubebeshea vikonyo kutokana na mbegu
2. Kubebesha vikonyo kwenye miche. Vifaa vinavyohitajika ni mifuko ya plastiki yenye kipenyo cha 5 -6 na urefu wa 5-6, udongo safi usio na magonjwa hasa wa msituni, samadi, mchanga/pumba za mchele kwa uwiano wa 3;1;1, mbolea ya TSP
3. Andaa kitalu sehemu wazi na tengeneza kichanja ili kuzuia jua na mvua
4. Changanya udongo na jaza kwenye viliba
5. Panda mbegu kwenye viliba
6. Uwagilia maji
7. Baada ya wiki 2-3 mbegu zitaanza kuota
8. Tunza miche hadi kufikia umri wa kubebeshwa miezi 3-4 au unene wa penseli. ZINGATIA ukuaji wa miche hutegemea hali ya hewa

JINSI YA KUBEBESHA VIKONYO
Ni muhimu kuchagua tawi zuri kwenye mti uliokomaa na kuzaa matunda ili kuharakisha kukomaana kuzaa matunda kwa mti uliobebeshwa, usichsgue kikonyo chenye maua, kikonyo kikianza kuchipua hakifai kwa kubebesha kwa sababu ni kichanga.
miche inayobebeshwa itoke kwenye jamii moja
  • Urefu wa kikonyo uwe sm 15-20 na chonga kikonyo bapa sm 2-3
  • Mche wa kubebeshea kikonyo ukatwe juu kwenye shina sm 20-25kutoka usawa wa udongo na kata kipenyo cha sm 2-3
  • Urefu wa kikonyo ulingane na urefu wa bapa la kikonyo
  • Sehemu ya mmea yenye mirija ya kupitisha chakula na maji zihakikishwe zinaungana
  • Fungia vizuri kikonyo kwenye shina na mkanda [strip] wa nailoni nyeupe. Tendo hili lifanyike kwenye mazingirea safina haraka ili utomvu kwenye bapa na kipenyo usikauke
  • Funika mche na mfuko wa nailoni nyeupe inayopitisha mwanga mradi isiwe nyeusi
Baada ya wiki 2-3 vikonyo vilivyopona vitaanza kuchipua. Tunza miche ya kitaluni kwa kumwagilia maji na kuondoa machipukizi'

UCHIMBAJI WA MASHIMO
Pima nafasi za kupanda ambazo ni 6m kwa 5m, 6m kwa 6m au 6m kwa 8m. Tenganisha udongo wa wa chini na wa juu. Changanya udongo wa juu na samadi. Rudisha udongon wa juu kwenye shimo. Weka kijiti katikati ya shimo. Rudisha udongo wa chini. Panda miche wakati wa masika. Chagua miche yenye afya nzuri. Fungua mikanda ya nailoni iliyounganisha shimo nsa kikonyo wiki 2-3 baada ya kupanda mche

SHUGHULI NYINGINE MUHIMU NI:
Palizi, kumwagilia maji, kuondoa machipukizi na kuzuia magonjwa na wadudu

MAVUNO YA PARACHICHI NA FAIDA YAKE
Mche mmoja wa parachichi aina ya HASS huanza kwa kutoa kg 40 mpaka kg 60 kwa mavuno yake kwa msimu wa kwanza. Bei ya soko kwa sasa KAMPUNI YA AGRIWORTH TANZANIA tununua kutoka kwa mkulima shambani tsh 1500 KWA KG 1. Hivyo 1500 zidisha kwa kg 40 =60000 kwa mche mmoja kwa kadirio la chini

Ekari moja hupandwa miche 70. MICHE 70 zidisha kwa 60000= 4200000.
Soko la parachini ni kubwa sana duniani kwa sasa.

Miche hii hudumu zaidi ya miaka 50 ya mavuno yake shambani

KWA MAHITAJI YA SHAMBA ZA KILIMO CHA PARACHICHI MKOA WA NJOMBE
Bei ya shamba ni tsh 150,000= kwa ekari moja mkoano Njombe. Ofisi zetu zipo mkoani Njombe. Pia tunatoa huduma ya usimamizi wa shamba mpaka kipindi cha mavuno kwa walio tayari kusimamiwa shughuli zao na kampuni.
Mkuu nisaidie mawasiliano please
 
ASALI KUTOKA TABORA.

Nauza Asali Ya Jumla Na Rejareja
Ipo Ya Nyuki Wadogo Na Nyuki Wakubwa.

Tunafunga Kwa Vipimo Tofauti Tofautii

Bei Ya Rejareja
Lita1 - 10,000 (Nyuki Wa Kubwa)
Lita1 - 25,000 (Nyuko Wa Dogo)

Bei Ya Jumla
Tuwasiliane Maana Kuna Ofa Zaidi

#0658357537
Call/ WhatsApp/Sms
Tabora

Tunafanya Delivery Nchi Nzima
honey-nutritional-values.jpg
 
Tupeni mrejesho wazee wa parachichi, hali ikoje? Kwa kila ekari moja mmepata kilo ngapi za parachichi?
 
Mwishoni mwa Mwezi february maeneo ya mbwewe kuna semi ya kenya ilichochora huezi amini ile container 40FT ilikuwa imemanda parachichi zimepakiwa kwenye makasha hivi inaenda kenya.

Hakika ilinifikirisha sana.
 
Hii sio kweli, gharama za kutunza shamba mbona hujaweka? Nijuavyo parachichi linahitaji mbolea at least Mara mbili kwa mwaka, madawa ya ukungu wadudu etc. Pia zao linaitaji kumwagilia hawa kipindi cha kiangazi, kupalilia kama utataka.matokeo chanya.
Mkoani Njombe mvua ni nyingi hivyo huhitaji kumwagilia miche ya parachichi. Labda suala la mdawa ingawa mleta mada amelitolea ufafanuzi.
 
Mkoani Njombe mvua ni nyingi hivyo huhitaji kumwagilia miche ya parachichi. Labda suala la mdawa ingawa mleta mada amelitolea ufafanuzi.
Acha kudanganya mkuu, mvua njombe za vipindi, zikiisha kumwagilia ni muhimu lasivyo kila rangi utaiona. Tembelea mashamba ya parachichi njombe then utajua mengi siyo kusikia stori mtaani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom