MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 34
- 30
Umaskini hususani wa kipato ni moja kati ya maadui wa maendeleo ambao Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali zetu pamoja na wadau wa maendeleo wameendelea kupambana nao kwa nguvu zote.
Binafsi nimekuwa nashirikiana na madiwani wenzangu 22 wa Jimbo letu la Vunjo pamoja na viongozi wa serikali ngazi zote ikiwemo wizara yetu ya Kilimo kutekeleza mipango mbalimbali yenye lengo la kuinua ubora wa maisha, ustawi wa jamii na kupunguza umaskini ikiwemo uwezeshaji wa mafunzo ya kilimo cha parachichi pamoja na ugawaji wa miche ya parachichi aina ya Hass bure kwa wananchi wenye utayari.
Ukiwa sasa ni msimu wa pili, Wananchi wameonesha mwamko mkubwa wa kuhitaji miche hii ya parachichi hii inatokana na wao kutambua fursa za kiuchumi zitokanazo na zao hili.
Kwa kutambua ardhi yetu na hali yetu ya hewa inakubali kilimo cha zao la parachichi ambalo pia lina soko kubwa kimataifa tumejiwekea lengo la kugawa miche 20,000 ifikapo 2025. Mkakati huu utawapa Wananchi wetu kipato kizuri, utaongeza ajira na itaiongezea mapato halmashauri yetu.
Tunaendelea kushirikiana na TAHA kuzalisha miche bora ya parachichi ambayo tutaigawa mwishoni mwa Januari mwaka 2024. Nitoe rai kwa wananchi wetu kufuata utaratibu ule ule wa kujisajili au kuandikisha majina kwenye ofisi za watendaji wa kata na madiwani wetu watatufikishia majina hayo.
Wananchi waliopata miche hiyo mapema mwaka huu ambapo tuligawa miche 5,000 wanaendelea vizuri na utunzaji. Upande wa zao la kahawa kwa kushirikiana na bodi ya kahawa Tanzania tumegawa miche 10,000 toka TACRI kwa wakulima wetu wa kahawa kupitia vyama vya msingi na kushirikiana na mashika ya kimataifa kusaidia mitaji na huduma za ugavi ili kuongeza uzalishaji wa kahawa, uhifadhi pamoja na masoko.
Naomba tuendelee kushirikiana kuijenga Vunjo yetu.
PAMOJA TUNAWEZA, KAZI IENDELEE!
Dkt Charles Stephen Kimei
Mbunge Jimbo la Vunjo