Kilimo cha parachichi ni njia rahisi ya kuufikia utajiri mkubwa

Aug 15, 2022
19
46
Uhitaji ya zao la parachichi unazidi kuongezeka siku hadi siku kutokana na kuwepo kwa viwanda vingi vinavyotumia zao hili la parachichi kama moja ya malighafi za kutengenezea bidhaa mbalimbali kama mafuta na bidhaa nyingine nyingi.

Lakini pia zao la parachichi limekuwa hitaji kubwa sana kutokana soko kubwa nje ya nchi kuongezeka kwa mfano India ni nchi ambayo inatumia sana zao la parachichi kutengenezea bidhaa mbalimbali.

Aina za parachichi.
Parachichi zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni kama ifuatavyo:

1. Parachichi za kienyeji,aina hii ya parachichi hutumia mda mrefu kukua na kutoa matunda lakini hutoa mazao machache ,mara nyingi watu hupanda aina hii kwa matumizi ya kawaida tu ya nyumbani na sio kwa ajili ya biashara.

2. Parachichi za kiasasa, hii ni aina ambayo hutumiwa sana ma watu wengi kwa ajili ya biashara zaidi yani unapofanya kilimo cha aina hii ya parachichi basi tegemea mazao mengi sana kwa ajili ya biashara.

Lakini pia katika aina hii ya parachichi ambayo ndio lengo langu kubwa tujifunze kupitia makala hii zipo aina mbalimbali za parachichi za kisasa,zifuatazo ni baadhi tu ya aina hizo.

i) Hass, hii ni aina maarufu sana ambayo huwa na vipele lakini pia limechongoka kwa juu lakini pia ni aina ya parachichi ambayo ni rahisi kuhifadhi.

IMG_2299.jpeg

(picha chanzo:gregrda.com)

ii) Fuerte,parachichi hizi au aina hii ni laini sana ngozi yake huteleza lakini pia lina mafuta mengi hivyo huoza mapema,ni zuri kwa matumizi ya karibu kwa sababu huwahi kuoza.Hutoa mafuta mengi sana yanayoweza kutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali hasa za ngozi.

IMG_2300.jpeg

(picha chanzo:four winds growers)

iii) X-Ikulu,hii pia ni moja ya aina ya kisasa ya parachichi ambayo pia ni maarufu sana.Hutumia muda mrefu sana kustawi lakini pia matunda yake ni gharama sana na hutuoa matunda makubwa.

IMG_2301.jpeg

(picha chanzo;matukio na ngilangwa michael)

Namna ya kupanda parachichi.
Kwanza kabisa unatakiwa kuandaa shamba lako kwa ajili ya kupanda.Upandaji wa parachichi zingatia sana nafasi kati ya shimo moja na jingine lakini pia zingatia mstari mmoja na mwingine.
Nafasi yaweza kuwa hivi,Mita 8 X Mita 8 (Huu ni urefu kutoka shimo moja hadi jingine na upana kutoka mtari mmoja na mwingine)kwa nafasi hii utakuwa na miche kuanzia 60 kwa heka moja,Mita 9 X Mita 9 kwa nafasi hii unaweza kuwa na miche 49 kwa heka moja lakini pia unaweza kutumia vipimo vya Mita 10 kwa mita 10 ambapo hapa utakuwa na miche 40 kwa heka moja.

Shimo linatakiwa liwe na ukubwa huu,Kimo sentimita 75 x Upana sentimita 75 na Urefu sentimita 75( 75 x 75 x 75).

Wakati wa upandaji wa parachichi matumizi ya mbolea ni muhimu sana kwa mazao mazuri. Mbolea inashauriwa sana kutumiwa katika upandaji wa parachichi ni mbolea ya samadi na mboji yan mbolea ile ya asili. Kipimo cha mbolea ya samadi kwa shino moja moja tumia kilogramu 16 hadi 20. Lakini pia kama utapandia mbolea ya viwandani kama DAP,Minjingu au nyinginezo tumia gramu 100 hadi 200 kwa shimo moja.Mbolea ichanganywe vizuri sana na udongo.

Zao la parachichi huweza kuchanganywa na mazao mengine hasa ya muda mfupi kwa mfano mahindi,viazi,kunde,maharage na mengine mengi .

Kukomaa kwa parachichi na mavuno yake.
Kukomaa kwa parachichi hizi za kisasa huanza kuanzia miezi 18 hadi 24 huanza kwa kutoa matunda machache na madogo kwa miezi hii ya mwanzo.Unaweza kupata matunda 50 hadi 100 kwa mti mmoja.Matunda huongezeka kwa kadri umri unavyoongezeka.
Kufikia miaka 5 hadi 6 mti mmjo unaweza kutoa matunda 1000 kwa mwaka.

Faida
Ukiachilia mbali faida tunazopata kiafya tunapokula au kutumia parachichi kama chakula zipo faida nyingine nyingi za kiuchumi.

Faida kubwa sana hupatikana kwenye kilimo hichi cha parachichi.Endapo mti mmoja ulio na umri wa miaka mitano hadi saba unaweza kutoa matunda 1000. Kipimo cha mita 10 x mita 10 kwa heka moja utakuwa na miti isiyopungua 35 na kwa mti mmja unaweza kukupa matunda zaidi ya 1000 kwa mwaka,hivyo kwa miti 35 utakuwa na matunda 3500(35x1000),uza kwa bei ya shambani ambayo ni 250 kwa tunda moja utakuwa na 875,000 (250x3500) hayo ni makadirio ya chini.

Kilimo cha parachichi kinafaida kubwa sana ukiwa muangalifu na mvumilivu.

Magonjwa na matunzo ya zao parachichi.
Parachichi hushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama yalivyo mazao mengine,hushambuliwa na magonjwa kama ukungu na wadudu.
Kutibu wadudu kama Karate na matchi tumia dawa ya (Actellic 50 EC).
Kutibu ukungu au fangasi tumia dawa kama( Ridomil Gold na Ebony 72 WP)

Zingatia kutembelea shamba lako mara kwa mata ili kugundua magonjwa kwa wakatu na kutibu kwa wakati ili upate mavuno mazuri

Parachichi huitaji lishe ili likupe mavuno mazuri na mengi sana,lishe ya parachichi ni mbolea na maji.Mwagilia maji kipindi ambacho si cha mvua kwa wastani wa lita 10 kwa mti mmoja mara mja moja kwa kili juma.

Nihitimishe kwa kusema kilimo cha parachichi kinaweza kukutoa katika umasikini endapo itawekeza juhudi nguvu na uvumilivu wako.Parachichi linaweza kukutoa katika umasikini anza leo
 
Wakati nanunua pori kule Tukuyu, enzi hizo nikiwa mwajiriwa kinda kabisa PPF Head Quarters watu walinicheka sana.

Nilipowaambia ndoto yangu ni kulima parachichi walinikebehi kwa maneno mengi ya shombo. Wengine wakaniambia bora niwe dalali soko la Mabibo kuliko niwe mkulima.

Maneno yao ya kunikatisha tamaa, yakanichoma, nikasema kwenye kupigwa vita ndio kuna ushindi. Nikaacha kuwaeleza mambo yangu.

Basi kila ijumaa jioni naondokea kazì, nawahi hakuna kulala na wakati mwingine gari za IT na za magazeti, asubuhi niko shambani Tukuyu.

Leo kila mtu anatamani awe kama mimi. Sijawa mchoyo, nimekuwa mwonyesha njia kwa yeyote anayenifuata.

Kilimo cha alizeti Mbeya na Njombe, kilimo cha mahindi, kilimo cha mpunga Kamsamba, ufugaji ng'ombe wa maziwa nk vinanifanya nitambe.

Sasa rasmi nimeingia kwenye kilimo cha soya beans kwa ajili ya exportation. Hii nchi kuna fursa sana lakini vijana wanaziona miyeyusho.
 
Wakati nanunua pori kule Tukuyu, enzi hizo nikiwa mwajiriwa kinda kabisa PPF Head Quarters watu walinicheka sana.
Hizi mambo hizi zinataka determined mind na passion. Kwenye nyuzi kama hizi madogo hutowaona, wamelundikana MMU wanajilizaliza kwa mijishangazi, huku wakipiga kelele kataa ndoa.

Time flies very fast. Wakija kushtuka wana 45yrs na bado wanaishi kwa mama
 
Asante sana mkuu TREE OF LIFE FOUNDATION kwa kushirikisha mawaza haya...nimenunua ardhi Kilindi Tanga na nimesafisha kwa sehemu...ili kuifikia ndoto ya kuwa mkulima wa kati na hatimaye mkubwa...bado naendelea na kautafiti mdogo.... hizi Parachichi za Hass kweli nasikia zina soko ila temperature ya pale kilindi naihofia ina-range between 17-31 degree-Centigrade
Mkuu TAJIRI MKUU WA MATAJIRI uzoefu wako wa Newala ukoje bro..
 
Uhitaji ya zao la parachichi unazidi kuongezeka siku hadi siku kutokana na kuwepo kwa viwanda vingi vinavyotumia zao hili la parachichi kama moja ya malighafi za kutengenezea bidhaa mbalimbali kama mafuta na bidhaa nyingine nyingi.

Lakini pia zao la parachichi limekuwa hitaji kubwa sana kutokana soko kubwa nje ya nchi kuongezeka kwa mfano India ni nchi ambayo inatumia sana zao la parachichi kutengenezea bidhaa mbalimbali.

Aina za parachichi.
Parachichi zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni kama ifuatavyo:

1. Parachichi za kienyeji,aina hii ya parachichi hutumia mda mrefu kukua na kutoa matunda lakini hutoa mazao machache ,mara nyingi watu hupanda aina hii kwa matumizi ya kawaida tu ya nyumbani na sio kwa ajili ya biashara.

2. Parachichi za kiasasa, hii ni aina ambayo hutumiwa sana ma watu wengi kwa ajili ya biashara zaidi yani unapofanya kilimo cha aina hii ya parachichi basi tegemea mazao mengi sana kwa ajili ya biashara.

Lakini pia katika aina hii ya parachichi ambayo ndio lengo langu kubwa tujifunze kupitia makala hii zipo aina mbalimbali za parachichi za kisasa,zifuatazo ni baadhi tu ya aina hizo.

i) Hass, hii ni aina maarufu sana ambayo huwa na vipele lakini pia limechongoka kwa juu lakini pia ni aina ya parachichi ambayo ni rahisi kuhifadhi.

IMG_2299.jpeg

(picha chanzo:gregrda.com)

ii) Fuerte,parachichi hizi au aina hii ni laini sana ngozi yake huteleza lakini pia lina mafuta mengi hivyo huoza mapema,ni zuri kwa matumizi ya karibu kwa sababu huwahi kuoza.Hutoa mafuta mengi sana yanayoweza kutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali hasa za ngozi.

IMG_2300.jpeg

(picha chanzo:four winds growers)

iii) X-Ikulu,hii pia ni moja ya aina ya kisasa ya parachichi ambayo pia ni maarufu sana.Hutumia muda mrefu sana kustawi lakini pia matunda yake ni gharama sana na hutuoa matunda makubwa.

IMG_2301.jpeg

(picha chanzo;matukio na ngilangwa michael)

Namna ya kupanda parachichi.
Kwanza kabisa unatakiwa kuandaa shamba lako kwa ajili ya kupanda.Upandaji wa parachichi zingatia sana nafasi kati ya shimo moja na jingine lakini pia zingatia mstari mmoja na mwingine.
Nafasi yaweza kuwa hivi,Mita 8 X Mita 8 (Huu ni urefu kutoka shimo moja hadi jingine na upana kutoka mtari mmoja na mwingine)kwa nafasi hii utakuwa na miche kuanzia 60 kwa heka moja,Mita 9 X Mita 9 kwa nafasi hii unaweza kuwa na miche 49 kwa heka moja lakini pia unaweza kutumia vipimo vya Mita 10 kwa mita 10 ambapo hapa utakuwa na miche 40 kwa heka moja.

Shimo linatakiwa liwe na ukubwa huu,Kimo sentimita 75 x Upana sentimita 75 na Urefu sentimita 75( 75 x 75 x 75).

Wakati wa upandaji wa parachichi matumizi ya mbolea ni muhimu sana kwa mazao mazuri. Mbolea inashauriwa sana kutumiwa katika upandaji wa parachichi ni mbolea ya samadi na mboji yan mbolea ile ya asili. Kipimo cha mbolea ya samadi kwa shino moja moja tumia kilogramu 16 hadi 20. Lakini pia kama utapandia mbolea ya viwandani kama DAP,Minjingu au nyinginezo tumia gramu 100 hadi 200 kwa shimo moja.Mbolea ichanganywe vizuri sana na udongo.

Zao la parachichi huweza kuchanganywa na mazao mengine hasa ya muda mfupi kwa mfano mahindi,viazi,kunde,maharage na mengine mengi .

Kukomaa kwa parachichi na mavuno yake.
Kukomaa kwa parachichi hizi za kisasa huanza kuanzia miezi 18 hadi 24 huanza kwa kutoa matunda machache na madogo kwa miezi hii ya mwanzo.Unaweza kupata matunda 50 hadi 100 kwa mti mmoja.Matunda huongezeka kwa kadri umri unavyoongezeka.
Kufikia miaka 5 hadi 6 mti mmjo unaweza kutoa matunda 1000 kwa mwaka.

Faida
Ukiachilia mbali faida tunazopata kiafya tunapokula au kutumia parachichi kama chakula zipo faida nyingine nyingi za kiuchumi.

Faida kubwa sana hupatikana kwenye kilimo hichi cha parachichi.Endapo mti mmoja ulio na umri wa miaka mitano hadi saba unaweza kutoa matunda 1000. Kipimo cha mita 10 x mita 10 kwa heka moja utakuwa na miti isiyopungua 35 na kwa mti mmja unaweza kukupa matunda zaidi ya 1000 kwa mwaka,hivyo kwa miti 35 utakuwa na matunda 3500(35x1000),uza kwa bei ya shambani ambayo ni 250 kwa tunda moja utakuwa na 875,000 (250x3500) hayo ni makadirio ya chini.

Kilimo cha parachichi kinafaida kubwa sana ukiwa muangalifu na mvumilivu.

Magonjwa na matunzo ya zao parachichi.
Parachichi hushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama yalivyo mazao mengine,hushambuliwa na magonjwa kama ukungu na wadudu.
Kutibu wadudu kama Karate na matchi tumia dawa ya (Actellic 50 EC).
Kutibu ukungu au fangasi tumia dawa kama( Ridomil Gold na Ebony 72 WP)

Zingatia kutembelea shamba lako mara kwa mata ili kugundua magonjwa kwa wakatu na kutibu kwa wakati ili upate mavuno mazuri

Parachichi huitaji lishe ili likupe mavuno mazuri na mengi sana,lishe ya parachichi ni mbolea na maji.Mwagilia maji kipindi ambacho si cha mvua kwa wastani wa lita 10 kwa mti mmoja mara mja moja kwa kili juma.

Nihitimishe kwa kusema kilimo cha parachichi kinaweza kukutoa katika umasikini endapo itawekeza juhudi nguvu na uvumilivu wako.Parachichi linaweza kukutoa katika umasikini anza leo
Vipi kuhusu soko
 
Write your reply...Nimezunguka sana kutafuta utajiri nikaona kilimo kinaweza nifanya kuwa tajiri, huwa natamani sana kupanda hata zaidi ya hekari 10 lakini changamoto kubwa inakuwa ni jinsi gani ya kupata miche ya kisasa. Huku kwetu mkoa wa Rukwa ni kama upatikanaji wa miche ni changamoto sana, Kama ingekuwa inapatikana ningefanya juhudi nitenge hata hekar 5
 
Cheki na huyu mwamba yuko njombe, anaweza kukutumia miche kwa mabasi

0764575728
 
Hizi mambo hizi zinataka determined mind na passion. Kwenye nyuzi kama hizi madogo hutowaona, wamelundikana MMU wanajilizaliza kwa mijishangazi, huku wakipiga kelele kataa ndoa.

Time flies very fast. Wakija kushtuka wana 45yrs na bado wanaishi kwa mama
Tatizo vijana siku hizi wanafikiria kubet tu. Wanadhani shughuli za kilimo na ufugaji ni kwa ajili ya watu wa vijijini na hazilipi. Siku moja nitakuja na ushuhuda wa Kilimo cha Viazi Uporoto, Makete na Ndagha, nitawasimulia namna tunavyobet kwenye kilimo hadi unanunua Scania Mende. Sasa hivi kimepamba moto kilimo cha ngano ya Ukraine huko Makete. Azam kila mwaka anaenda huko kununua ngano ya kutengenezea maaandazi na mikate.
 
Back
Top Bottom