Imeandaliwa na John Haule wa Rumours Africa
Kama ilivyo kawaida ya Rumours Africa, kila siku ipo kazini kukuletea minong'ono ya mambo yaliyo jificha katika jamii yetu bila kujali aina ya minong'ono hiyo kwa kuwa lengo la Rumours Africa ni kutafuta tu suluhisho la masuala mbalimbali ya kijamii kwa ujumla wake.
Wiki hii nilitembelea kituo cha tiba asili maeneo ya Temeke. Kituo hiki kimejikita zaidi katika masuala ya LisheTiba na kinaitwa "MiracleFoods" kama shughuli za kituo hicho kilivyo. Watanzania siku hizi ni wastaarabu na kama kawaida nilimpigia simu mmiliki wa kituo hicho cha tiba aitwaye Dr. Febronia Kalongoti ambaye wengi wenu mnamjua huyu mama maarufu kwa vipindi katika runinga na magazeti mbalimbali nchini.
Yeye alifurahi sana kusikia azma yangu ya kumtembelea kwa kuwa kwanza mimi ni mwandishi mwenza wake katika gazeti maarufu sana la waganga na madakitari nchini liitwalo TABIBU, lakini pia mimi ni mtaalamu mwenza katika suala zima la tiba asili na uchawi baridi.
Jana ndio tulikutana. Maongezi yetu ya awali yalizama sana katika matatizo ya kiafya yanayowakabili watanzania na namna anavyo kabiliana nayo. Alionyesha umahiri mkubwa sana katika kuonyesha kuwa anazo LisheTiba bora zenye uhakika wa kumaliza matatizo ya kiafya kwa watanzania.
"Watanzania hawajui kula!" alianza kwa kusema. "Wakiwa na pesa basi wanashindana kurosti bila kujua kuwa nyama hupandisha hasira na uhayawani, baada ya siku chache unasikia mke aliyekuwa bingwa wa kurosti mtaani kaachika kwa mume wake… Hii ni hatari, lakini wenye akili huja hapa kuchukua Limbwata na kwa kweli linawasaidia" alimalizia Dr. Kalongoti.
Swali langu la kwanza lilikuwa nataka kujua limbwata hasa ni nini? Akajibu, "Swali zuri sana Haule. Limbwata ni jina tu ambalo kwa sasa lina tafsiri ya kutishia waume wajeuri lakini kwa undani wake limbwata ni chakula cha kila mtu, na Tanzania ingependeza sana iwapo kila mtu angekula chakula hiki kiitwacho limbwata."
Akaendelea. "Labda tu nikuambie ukweli kuwa jikoni ni maabara ya kutengeneza kemikali zenye uwezo wa kumjenga binadamu, kumbomoa, kumuua, kumbadili tabia na kadha wa kadha. Watu wote wenye akili timamu huajiri mpishi mwenye akili na taaluma ya upishi kwa sababu hii. Mpishi asiyejua kabichi ina magnesium kwa wingi basi atamfanya anayempikia akala awe mpole sana na kama hajui kuwa nyama inaua kuliko kumjenga mtu basi atakuwa hajui anampunguzia maisha mlaji wake kwa kuwa takwimu zinaonyesha wala nyama wote walikufa kwenye miaka ya 60 na waliobaki wapo hoi kwa maradhi ya moyo, figo, ini, na saratani za aina tofauti."
Msomaji wangu, Dr. Kalongoti alikuwa ameniacha hoi. Amenifunulia mengi, lakini bado sijajua limbwata ni kitu gani hasa. Nilirudia tena swali langu. "Ina maana sasa limbwata lina sura gani katika haya uliyonieleza?" Akameza mate, na kunigeukia tena. "Limbwata Dr. Haule ni mapishi. Ni mapishi ambayo humfanya mlaji apate utulivu wa ubongo kutokana na vitamin, madini, virutubisho pamoja na Amino acids zinazopatikana katika mlo unaomwandalia tu basi…
Utamwona tu mlaji wako kama alikuwa na tabia ya ukali inapotea taratibu na kama alikuwa na wasiwasi utaona unamtoka, kama alikuwa mwoga basi utaona anapata ujasiri lakini utafaidi sana kumwona mtu aliyekuwa hajui kuongea taratibu akiwa mkimya sana!" hili ndo jibu la Dr. Kalongoti kuhusu limbwata jamani.
Maswali lukuki sasa yalianza kujijenga akilini mwangu. Haraka haraka tu nilitaka kujua usalama wa walaji limbwata ukoje? Akajibu "Limbwata sio sumu wala uchawi, narudia tena Dr. Haule. Limbwata ni chakula tu ambacho kipo sokoni kinauzwa na kila mtu ananunua na anakula lakini bila kujua kama ni limbwata.
Hivyo limbwata kwa kuwa ni chakula na lishetiba kwa ajili ya wasiwasi, ukali, hofu nk basi kila mtu anapaswa kujua na kwa kweli mama ntilie wote wanapaswa kupata elimu hii maana kwa kutojua wanaandaa kemikali gani pale katika maabara iitwayo jiko, na inawabadilisha walaji vipi na kwa kiasi gani wanakuwa hawajui kuwa wanaandaa vifo baridi vya walaji bila kukusudia."
Dr. Kalongoti akamalizia kwa kusema hivi "Limbwata ni Domestic Science" tu na kila mpishi anatakiwa aijue tena hasa wanawake wa Tanzania ambao wamebeba jukumu la upishi kwa kiasi kikubwa sana. Hapa sigawi dawa, ila huwa natoa mafunzo ya kumpikia mtu mkorofi asiyetulia na hata familia nzima isiwe na mapepe ukala hasara. "Wanakuja hapa tunaongelea shida zao, tunakubaliana, wanalipa kuja kujifunza na kupata mafunzo haya adimu nchini."
Rumours Africa dukani kwetu tunazo limbwata za kizungu. Miaka mingi tu watu wanakuja na tuna wasaidia sana kuwatuliza akili wenza wao. Wengine walifuata hata kwa ajili yao wenyewe kwa kuwa hakuna kinachofanyika ukimeza dawa hizi zaidi ya kukutuliza ubongo na kukurejeshea uwezo wako wa asili kukumbuka na kutunza kumbukumbu zako kwa usahihi zaidi. Dawa zetu ni kutoka kampuni ya kutengeneza dawa lishe ya Nativa South Africa ambao nao wameleta hizi "stress killer" zikahakikiwa na TFDA na sasa ninazo hapa dukani muda wowote ukihitaji njoo.
Hii ni njia ya kupata limbwata haraka kwa waliozidiwa sana. Lakini kama utapenda kujua namna ya kutengeneza jiko lako liwe kiwanda cha kupika Limbwata basi usikonde. Njoo tuongee, tukubaliane, ulipie na uanze kujifunza namna ya kutengeneza limbwata.
Limbwata si SUMU. Nilichogundua ni kuwa Limbwata ni "STRESS KILLER" ambayo kila mtu anaihitaji kwa ajili ya uhakika na umakini wa masuala ya maisha iwe kazi, elimu n.k.
Asanteni kwa kunisoma.
Chanzo; JukwaaHuru