Fahamu kuhusu Uchawi wa Mapenzi (Limbwata)

Fahamu kuhusu Uchawi wa Mapenzi (Limbwata)

Akaendelea. "Labda tu nikuambie ukweli kuwa jikoni ni maabara ya kutengeneza kemikali zenye uwezo wa kumjenga binadamu, kumbomoa, kumuua, kumbadili tabia na kadha wa kadha. Watu wote wenye akili timamu huajiri mpishi mwenye akili na taaluma ya upishi kwa sababu hii. Mpishi asiyejua kabichi ina magnesium kwa wingi basi atamfanya anayempikia akala awe mpole sana na kama hajui kuwa nyama inaua kuliko kumjenga mtu basi atakuwa hajui anampunguzia maisha mlaji wake kwa kuwa takwimu zinaonyesha wala nyama wote walikufa kwenye miaka ya 60 na waliobaki wapo hoi kwa maradhi ya moyo, figo, ini, na saratani za aina tofauti."

Limbwata haina tofauti na mungu, shetani, Bigfoot, Loch Ness Monster, leprechauns, na viumbe wengine kama hao!
 
Msomaji wangu, Dr. Kalongoti alikuwa ameniacha hoi. Amenifunulia mengi, lakini bado sijajua limbwata ni kitu gani hasa. Nilirudia tena swali langu. "Ina maana sasa limbwata lina sura gani katika haya uliyonieleza?" Akameza mate, na kunigeukia tena. "Limbwata Dr. Haule ni mapishi. Ni mapishi ambayo humfanya mlaji apate utulivu wa ubongo kutokana na vitamin, madini, virutubisho pamoja na Amino acids zinazopatikana katika mlo unaomwandalia tu basi… Utamwona tu mlaji wako kama alikuwa na tabia ya ukali inapotea taratibu na kama alikuwa na wasiwasi utaona unamtoka, kama alikuwa mwoga basi utaona anapata ujasiri lakini utafaidi sana kumwona mtu aliyekuwa hajui kuongea taratibu akiwa mkimya sana!" hili ndo jibu la Dr. Kalongoti kuhusu limbwata jamani.
 
Sie wanaume tunalishwa vitu vya ajabu sana.....si ajabu matumbo yanajaa utadhani kitambi cha menu kumbe matakataka tu...
 
Dr. Kalongoti akamalizia kwa kusema hivi "Limbwata ni Domestic Science" tu na kila mpishi anatakiwa aijue tena hasa wanawake wa Tanzania ambao wamebeba jukumu la upishi kwa kiasi kikubwa sana. Hapa sigawi dawa, ila huwa natoa mafunzo ya kumpikia mtu mkorofi asiyetulia na hata familia nzima isiwe na mapepe ukala hasara. "Wanakuja hapa tunaongelea shida zao, tunakubaliana, wanalipa kuja kujifunza na kupata mafunzo haya adimu nchini."
 
s.jpg
 
Back
Top Bottom