Fahamu kuhusu talaka na taratibu zake katika Uislam

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
FAHAMU kuhusu TALAKA na taratibu zake katika UISLAMU.

Sehemu Ya 1

‏اَلسَلامُ عَلَيْكُم وَرَحْمَةُ اَللهِ وَبَرَكاتُهُ‎)

As-salāmu alaikum wa-rahmatullahi wabarakātuh.

Peace be upon you as well as God's mercy and blessings.

Amani iwe juu yako pamoja na rehema na baraka za Mwenyezi Mungu.

Ndugu yangu mpendwa,
Kwa majina naitwa Mr George Francis, kwa taaluma ni mwanasheria.

Ahsante kwa kuendelea kufuatilia mada mbalimbali Mwenyezi Mungu alizonifunulia kuziandaa na kukuletea.

Leo naomba tuwe pamoja, tukienda kuaangazia kuhusu TALAKA na taratibu zake kwa mujibu wa sheria za dini ya kiislamu.

Ndoa iliyofungwa kwa mujibu wa dini ya kiislamu inaweza kuvunjwa kwa kufuata taratibu za kisheria ka mujibu wa dini ya kiislamu.

Ndoa ya kiislamu ni miongoni mwa ndoa zinazotambulika kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa.

Ndoa ya kiislamu ni ile inayofungwa kwa kufuata taratibu zinazokubalika katika dini ya kiislamu.
⚖️Kifungu cha 25(3)(b) cha Sheria ya Ndoa.

Ndoa inatokana na makubaliano ya hiyari kati ya mwanamume na mwanamke bila kushinikizwa na mtu yeyote.

Katika uislamu, Mwanamume anaruhusiwa kuoa wake zaidi ya mmoja hadi wanne.

Muhimu ni kuwa na uwezo wa kuwapa matunzo na huduma zote kwa kuzingatia haki na usawa bila ya upendeleo.

Kama ilivyo katika ndoa nyingine, uislamu pia unaruhusu mume na mke kuachana kwa TALAKA kwa kuzingatia utaratibu.

TALAKA kutoka neno la kiarabu طلاق) au talaaq ni utaratibu wa kuvunja ndoa baina ya mume na mke kabla mume au mke kufariki.

Sheria ya ndoa imeweka utaratibu au masharti ya kuvunja ndoa iliyofungwa kwa mujibu wa sheria za dini ya kiislamu.

Mahakama ni lazima ijirizishe kuwa,
(i).Ndoa ilifungwa kwa mujibu wa dini ya kiislamu.
⚖️ Kifungu cha 107(3)(a) cha Sheria ya Ndoa.

(ii). Bodi ya usuluhishi ya ndoa imethibitisha kuwa imeshindwa kusuluhisha na imetoa hati kwamba imeshindwa kusuluhisha wanandoa hao.
⚖️ Kifungu cha 107(3)(b) cha Sheria ya Ndoa.

(iii). Mmoja kati ya wanandoa amefanya kitendo kinachoonesha kuvunjika kwa ndoa hiyo kwa mujibu wa sheria za dini ya kiislamu.
⚖️ Kifungu cha 107(3)(c) cha Sheria ya Ndoa.

Mfano: Mwanaume amempa mkewe talaka kwa mujibu wa dini kama vile talaka ya kwanza, talaka ya pili na ya tatu kabla ya amri ya TALAKA ya Mahakama kutolewa.

Inaendelea....

#No_learnig_No_earning
So we have to Learn.

Prepared By
George G Francis
IMG_20231107_165958_349.jpg

Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
 
FAHAMU kuhusu TALAKA na taratibu zake katika UISLAMU.

Sehemu Ya 2

Tukisoma kesi ya
MWINYIHAMISI KASIMU vs ZAINABU BAKARI, (1985) TLR 217,
Mahakama iliamua kwamba, ili kutoa amri ya TALAKA kama ilivyo kwa mujibu wa kifungu cha 107(3) cha Sheria ya Ndoa,
Ni lazima kwanza ijirizishe mambo yafuatayo,

(i). Wanandoa walioana chini ya sheria ya kiislamu.

(ii). Bodi ya usuluhishi ya ndoa imethibitisha kuwa imeshindwa kuwasuluhishwa wanandoa husika.

(iii). Pamoja na Bodi ya usuluhishi kushindwa kusuluhisha, lakini mmoja ya wanandoa amefanya kitendo ambacho kwa mujibu wa sheria za kiislamu kinatosha kuvunjika kwa ndoa husika.

Katika kesi hii, Mahakama haikuizinisha TALAKA kwasababu hakukuwa na kitendo kinachoonesha kuvunjika kwa ndoa chini ya sheria ya kiislamu.

Katika kesi hii, Mahakama ya mwanzo ilikataa ombi la TALAKA la mwanamke na hata alipokata rufaa Mahakama ya wilaya, ombi la TALAKA lilikataliwa pia.

Lakini hakimu alishauri kwamba, kwasababu ndoa yao ilikuwa ni ya kiislamu Bi Zainabu anaweza kupata TALAKA kama ataamua kujikului kwa kurudisha mahari ambayo mwanaume alitoa.

Hiki ni miongoni mwa vitendo ambavyo mwanamke anaweza kufanya kama anataka TALAKA kwa mujibu wa kifungu cha 107(3)(c) cha Sheria ya Ndoa.

TALAKA inaruhusiwa kwa mujibu wa sheria za dini ya kiislamu na kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa.

Binadamu huwa tunabadilika, hivyo kuliko kuvumilia maudhi na karaha zisizokwisha na mwisho kuuana, ni afadhali kuachana kwa amani.

Lakini wagombanao ndio wanaopatana.

Kabla ya kufikia maamuzi ya kuachana mume na mke kwanza wanahimizwa kupatana.

TALAKA inakuja baada kushindikana kwa mapatano.

Mume na mke wakishindwa kupatanawatawaita watu wawili, mmoja wa upande wa mke namwingine wa upande wa mume.

Kusudi baada ya kuchunguza ugomviwao, wajaribu kila njia kuwapatanisha na endapo
hawakupatana basi wenyewe sasa wataamua kama
kuachana na waachane kwa wema.

Katika uislamu kuna utaratibu wa TALAKA tatu.

Mume akitoa Talaka ya kwanza na ya pili anaweza kumrejea mkewe kama wakikubaliana kurejeana na kuishi pamoja.

Lakini mume akimwacha mke kwa Talaka tatu hawezi kumrejea mkewe hadi mke huyo aolewe tena na mtu mwingine na washiriki tendo la ndoa, kisha waachane kwa Talaka ndipo mwanaume uweze kumwoa tena kwa kufuata upya utaratibu wa kufunga ndoa.

Inaendelea..

#No_learnig_No_earning
So we have to Learn.

Prepared By
Mr George Francis
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com

IMG_20231107_201152_169.jpg
 
FAHAMU kuhusu TALAKA na taratibu zake katika UISLAMU.

Sehemu Ya 3

Kwa mujibu wa Qur'an Tukufu,
wanawake waliopewa talaka wangoje mpaka
hedhi tatu zipite.

Na waume wao wana haki zaidi ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka isilahi au kuwaacha kwa wema.

Qur'an inasema,
"Talaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri."
⚖️Soma (Sura 2 aya 229).

Mwanamke aishapo kupewatalaka, basi mpaka siku ya hedhi yake zifikapo na kuisha,huhesabiwa talaka moja.

Hata hedhi ya pili kuwa ni talaka yapili. Mpaka hedhi ya tatu kama mume akimrudia kabla yakwisha muda wake huwa ni mkewe.

Lakini hedhi ya tatu ikiisha
na mume hakumrudia mkewe huwa si mkewe tena, na hapondiyo huhesabiwa amekwisha mwacha.

Na kama mke ana
mimba pia anatakiwa kuweka wazi.

Katika kipindi cha utolewaji wa TALAKA hizo, mwanaume anapaswa kuwa anahesabu siku za eda.

Lakini pia mwanaume hawapaswi kumtoa mwanawake katika nyumba yake wala mwanawake hapaswi kutoka mwenyewe mpaka muda wa siku za eda upite na hatimae kuachana kwa wema.

Katika Suratul Baqarah sura ya 2:232, Qur’ani inasema:

وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَنْ يَنْكِحْنَ أَزْوَاجَهُنَّ إِذَا تَرَاضَوْا بَيْنَهُمْ بِالْمَعْرُوفِ

“Mnapokuwa mmewataliki wake zenu, na wamemaliza eda zao, ama kaeni (warejeeni) nao kwa wema au waacheni kwa wema.

Msiwashikilie kwa nguvu ili muwatese, hamuwarejei wala hamuwaachi."

Mume kama umeamua kumrea mkeo baada ya TALAKA ya kwanza au ya pili basi mrejee na kuishi nae kwa wema.

Lakini kama umeamua kumwacha mojakwamoja pia mwache kwa wema.

Katika uislamu, mwanamke anawezakujikomboa kwa kudai talaka na kurudisha mahari aliyopewa na mumewe.

Lakini mwanamume mcha Mungu, anatakiwa kusamehe kurejeshewa mahari kutokana na hali ya kimaisha ya mke japokuwa kupokea ni haki yake.

Qur’ani Tukufu inasema;

وَكَيْفَ تَأْخُذُونَهُ وَقَدْ أَفْضَىٰ بَعْضُكُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ وَأَخَذْنَ مِنْكُمْ مِيثَاقًا غَلِيظًا

“Vipi mnaweza kunyang’anya mahari (mliyowapa) na hali mmeshaingiliana nao, na wamechukua kwenu ahadi thabiti (ya kuwalipa mahari kamili)
⚖️Suratul Nisaa, 4:21.

Mume mwenyewe akimwacha mkewe, mahari hairudishwi.

Qur‘aninasema,
“Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlichowapa wake zenu, ila ikiwa wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Allah.
⚖️Sura 2 aya 230.

Kama mume mwenyewe ndiye anayetaka kumwacha mkewe, hapaswi kudai mahari.

Kuachana Sio Uadui. Mlipendana kwa wema, achaneni kwa wema.

Inaendelea....

Prepared By
George G Francis
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com

IMG_20231107_224632_923.jpg
 
FAHAMU kuhusu TALAKA na taratibu zake katika UISLAMU.

Sehemu Ya 4

Katika uislamu Kuna aina mbalimbali za TALKA, Kwa mujibu wa sheria ama shari'a.

Nazo ni kama zifuatazo,
(i). Talaka ya kutamka
💔Hiki ni kitendo cha mojakwamoja cha mwanamume kutamka kumwacha mkewe.

Mfano: kwenye kesi ya
⚖️BIBIE MAURIDI vs MOHAMED IBRAHIM (1989) TLR 162,
Katika kesi hii wanandoa walifunga ndoa chini ya sheria (shari'a) ya kiislamu.

Mgogoro wao ulipelekwa katika Bodi ya usuluhishi ya Ndoa ambayo ili ilikili kushindwa kupata suluhu ya mgogoro wao.

Mwisho wa kesi hii katika Mahakama Kuu, iliamliwa kwamba,
"Kitendo cha mwanamume kumtamkia mkewe "talaka" kililenga kuvunjika kwa ndoa husika."

Hapa mume anatamka au kutoa talaka kwa mkewe, ambapo kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya kiislamu ni talaka ya kwanza, ya pili na ya tatu katika kipindi cha miezi minne.

(ii). Talaka ya kujikhului (Khul'u) au Kulha Divorce.
💔Hii inafanywa na mwanamke.
Hapa mke anafanya kitendo cha kujikhului au kujitoa kwenye ndoa husika kwa kurejesha kiwango cha mahari kwa mume wake.

Mume baada ya kupokea mahari aliyorejeshewa atatoa talaka.

Lakini, kwa mujibu wa shari'a mume anaweza kupokea au la! anaweza kusamehe japo kupokea ni haki yake.
⚖️ Soma Qur'an (2:229).

Mwisho wa siku, lengo ni kuachana kwa wema kama mwanzo walivyooana na kuishi Kwa wema.

Shari'a inafundisha katika kutendeana mema katika nyakati zote, iwe nyakati za mapatano au za kuachana.
⚖️Soma kesi ya MWINYIHAMISI KASIMU vs ZAINABU BAKARI (1985) TLR 217

(iii). Talaka ya Mubaarat.
💔 Ni aina ya talaka ambapo mume na mke hukubaliana kuachana kwa wema baada ya kutofikia lengo la ndoa.

Hapa mume na mke wanakubaliana kwa pamoja na kwa hiyari kuvunja ndoa baina yao kwa wema na amani baada ya kuona hawataweza kuendelea kuishi tena pamoja.

(iv). Talaka ya ‘Ilaa
💔 Ni aina ya talaka ambapo mume humtenga mkewe kwa zaidi ya miezi mine.

Katika aina hii ya Talaka, mume anahapa kutoshiriki tendo la ndoa na mkewe tena.

Ikipita miezi minne bado mume ameendelea kumtenga mkewe, hapo mke atadai talaka kwa kukosa haki ya kushiriki tendo la ndoa na mume wake.
⚖️ Soma, Qur’an (2:226)

Inaendelea...

Soma Sehemu inayofuata....

Prepared By
Mr George Francis
Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
IMG_20231109_112208_540.jpg
 
FAHAMU kuhusu TALAKA na taratibu zake katika UISLAMU.

Sehemu Ya 5

Sehemu iliyopita tulianza kuangalia aina mbalimbali za TALAKA katika sheria za dini ya kiislamu.

Ufuatao ni mwendelezo wa aina hizo,

(v). Talaka kabla ya Jimai.
💔Ni kuvunja mkataba wa ndoa kabla ya kufanya tendo la jimai (ndoa).

Mume anamwacha mke aliyefunga nae ndoa wakiwa bado hawajashiriki tendo la ndoa.

Talaka hii ina taratibu zifuatazo;

•Hakuna kukaa eda kwa mwanamke aliyeachwa kabla ya tendoa la jimai (ndoa)

•Kama mume ndiye anayemwacha mke na ameshatoa mahari, haruhusiwi kudai chochote.

•Mume atalazimika kumpa mkewe kitoka nyumba kama ndiye aliyeamua kumuacha.

=Mumehana budi kumpa mke fedha kidogo au chochote kile chakumzawadia kadri ya uwezo wake.

=Lengo ni kumsaidia mke naye aweze kuendesha maisha yake vizuri baada ya kuachana.

NB:
Kanuni ni ileile,
"Mlioana kwa wema, mmeishi kwa wema basi na mwachane kwa wema."

•Ikiwa mume alikuwa hajatoa mahari, atalazimika kutoa nusu ya mahari.
⚖️Soma (Qur'an 2:37)

•Kama mke ndiye aliyedai talaka atamrudishia mumewe mahari aliyompa.
⚖️ Soma Qur’an (2:236-237)

NB:
Mume kupokea mahari inayorejeshwa na mkewe aliyedai talaka ni hiyari.

Japo ni haki yake lakini anaweza kusamehe akiona kuwa ni vyema kufanya hivyo.

(vi). Talaka ya Li’aan.
💔Ni talaka inayopatikana baada ya mume au mke kumshika ugoni mwenzake bila ya kuwa na mashahidi wanne.

Katika aina hii ya talaka, kila mmoja ataishuhudilia nafsi yake kwa kula kiapo mara tano mbele ya kadhi na baada ya hapo ndoa itavunjika na kutorejeana tena.
⚖️Soma Qur’an (24:6-9)

(vii). Talaka moja
💔Ni aina ya talaka ambapo mume humtamkia au kumuandikia mkewe “NIMEKUACHA” kwa talaka moja akiwa twahara.

(viii). Talaka mbili
💔Ni aina ya talaka ambapo mume humuacha mara ya pili baada ya kumuacha kwa talaka moja kisha akamrejea katika twahara mbili tofauti.
⚖️Soma Qur’an (2:229)

(ix). Talaka tatu (Tahliil)
💔Ni talaka ambayo mume humuacha mkewe baada ya kumrejea kutoka talaka mbili alizomuacha na kumrejea hapo awali.
⚖️Soma Qur’an (2:230), (65:1)

NB:
TALAKA hutolewa kwa matamshi au maandishi kuwa "NIMEKUACHA" au maneno yenye maana hiyo mbele ya mashahidi wawili waadilifu.

Inaendelea....

Prepared By
Mr George Francis
Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
 
FAHAMU kuhusu TALAKA na taratibu zake katika UISLAMU
IMG_20231109_134753_101.jpg
.

Sehemu Ya 5

Sehemu iliyopita tulianza kuangalia aina mbalimbali za TALAKA katika sheria za dini ya kiislamu.

Ufuatao ni mwendelezo wa aina hizo,

(v). Talaka kabla ya Jimai.
💔Ni kuvunja mkataba wa ndoa kabla ya kufanya tendo la jimai (ndoa).

Mume anamwacha mke aliyefunga nae ndoa wakiwa bado hawajashiriki tendo la ndoa.

Talaka hii ina taratibu zifuatazo;

•Hakuna kukaa eda kwa mwanamke aliyeachwa kabla ya tendoa la jimai (ndoa)

•Kama mume ndiye anayemwacha mke na ameshatoa mahari, haruhusiwi kudai chochote.

•Mume atalazimika kumpa mkewe kitoka nyumba kama ndiye aliyeamua kumuacha.

=Mumehana budi kumpa mke fedha kidogo au chochote kile chakumzawadia kadri ya uwezo wake.

=Lengo ni kumsaidia mke naye aweze kuendesha maisha yake vizuri baada ya kuachana.

NB:
Kanuni ni ileile,
"Mlioana kwa wema, mmeishi kwa wema basi na mwachane kwa wema."

•Ikiwa mume alikuwa hajatoa mahari, atalazimika kutoa nusu ya mahari.
⚖️Soma (Qur'an 2:37)

•Kama mke ndiye aliyedai talaka atamrudishia mumewe mahari aliyompa.
⚖️ Soma Qur’an (2:236-237)

NB:
Mume kupokea mahari inayorejeshwa na mkewe aliyedai talaka ni hiyari.

Japo ni haki yake lakini anaweza kusamehe akiona kuwa ni vyema kufanya hivyo.

(vi). Talaka ya Li’aan.
💔Ni talaka inayopatikana baada ya mume au mke kumshika ugoni mwenzake bila ya kuwa na mashahidi wanne.

Katika aina hii ya talaka, kila mmoja ataishuhudilia nafsi yake kwa kula kiapo mara tano mbele ya kadhi na baada ya hapo ndoa itavunjika na kutorejeana tena.
⚖️Soma Qur’an (24:6-9)

(vii). Talaka moja
💔Ni aina ya talaka ambapo mume humtamkia au kumuandikia mkewe “NIMEKUACHA” kwa talaka moja akiwa twahara.

(viii). Talaka mbili
💔Ni aina ya talaka ambapo mume humuacha mara ya pili baada ya kumuacha kwa talaka moja kisha akamrejea katika twahara mbili tofauti.
⚖️Soma Qur’an (2:229)

(ix). Talaka tatu (Tahliil)
💔Ni talaka ambayo mume humuacha mkewe baada ya kumrejea kutoka talaka mbili alizomuacha na kumrejea hapo awali.
⚖️Soma Qur’an (2:230), (65:1)

NB:
TALAKA hutolewa kwa matamshi au maandishi kuwa "NIMEKUACHA" au maneno yenye maana hiyo mbele ya mashahidi wawili waadilifu.

Inaendelea....

Prepared By
Mr George Francis
Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
 
FAHAMU kuhusu TALAKA na taratibu zake katika UISLAMU.

Sehemu Ya 6

Utaratibu wa TALAKA katika uislamu, umeleta debate mbalimbali baina ya majaji na Mahakimu.

Baadhi wametofautiana katika kutafsiri kifungu cha 107(3) cha Sheria ya Ndoa.

Baadhi yao wanasema, =baada ya mume kutamka TALAKA wanandoa wanaenda Mahakamani kupata uthibitisho tu kwamba ndoa imeshavunjika.

Wengine wanasema si hivyo tu bali lazima taratibu nyingine zifuatwe.

Mfano:
Kweye kesi ya
HALIMA ATHUMAN vs MAULIDI (1991) TLR 179
Mahakama iliamua kwamba,
Kama Bodi ya usuluhishi imeshindwa kuwasuluhisha, Mke anaweza kufanya yafuatayo.

(i). Kuomba khului mbele ya sheikh.
Hapa mke anaomba kujivua kwenye ndoa kwa kurejesha mahari.

(ii). Kuomba Talaka ya mubaarat.
Hapa mume na mke wanakaa pamoja na kukubaliana kuvunja ndoa yao wenyewe.

LAKINI, mume anaweza kufanya yafuatayo,
(i) Kutoa talaka tatu kwa utaratibu unaokubalika.
Yaani talaka ya kwanza, ya pili hadi ya tatu.

(ii). Baada ya kukamilika kwa talaka tatu, mume utakiwa kwenda Mahakamani ili talaka yake itamburike kisheria.

LAKINI utaratibu sahihi ni kwamba, kazi ya Mahakama sio tu kuifanya talaka aliyotoa mume kutamburika bali kusikiliza na kutoa maamuzi yake.

Mahakama itasikiliza shauri na kuamua kama ikubali kutoa amri ya TALAKA au kukataa kutoa amri ya TALAKA kutokana na sababu zitakazoletwa mbele ya Mahakama.

LAKINI pamoja na mambo yote tukumbuke kuwa, chombo pekee chenye mamlaka ya kutoa amri ya TALAKA nchini Tanzania ni Mahakama.

Hivyo, Mahakama itasikiliza shauri husika na kuangalia kama ndoa imevunjika kiasi cha kutoweza kurekebishika ili itoe amri ya TALAKA au sababu zao za kuvunja ndoa hazina mashiko.

Kama sababu zilizoelezwa hazina mashiko Mahakama itakataa kutoa amri ya TALAKA.

NB:
Baada ya Mahakama kutoa amri ya TALAKA, mwanamke anatakiwa kukaa eda kabla ya kufunga ndoa nyingine.
⚖️ Kifungu cha 38(1)(i) cha Sheria ya Ndoa.

Mwisho, nakuhusia na kuihusia nafsi yangu,

Kuoana ni kwa wema, kuachana ni kwa wema wala si kwa ubaya.

Haifai kutoleana siri zenu au kudharirishana kwa namna yoyote baada ya kuachana.

Mungu abariki sote tudumu katika ndoa zetu.

#inshaAllah

#No_Learning_No_Earning
So we have to Learn.

Prepared By
Mr George Francis
Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
IMG_20231109_172205_182.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom