Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Mark Francis

Verified Member
Nov 19, 2010
605
195
Restaurant.jpg

Nimefungua biashara ya Mgahawa sehemu flani hapa jijini Dar es Salaam, nimeweka wafanya kazi 3; mmoja kwa ajili ya chips na wa2 kwa ajili ya chakula kwa sababu biashara yenyewe bado changa. Eneo ambalo nafanyia biashara lina population kubwa na halina competition kubwa sana. Mimi napitia mida ya jioni kucheki jinsi biashara inavyoendela na kuhakikisha hesabu zinaenda vizuri.

Tatizo mpaka sa hizi ni zaidi ya mwezi na sioni faida yoyote zaidi ya kuwalipa wafanyakazi wangu kwa kipato changu kidogo ambacho ninakipata kwenye kaajira kangu kwa mhindi. Naombeni mnisaidie yafuatayo;
  1. Nifanyaje ili niweke kuvutia wateja zaidi bila kutumia kiasi kikubwa cha fedha?
  2. Nifanyaje ili niweze kupata faida kubwa, yaani kuwa na matumizi kidogo na mauzo mengi?
  3. Nifanyeje ili kuwabana wafanyakzi wangu waisimamie biashara vizuri na kupata faida?
NAOMBENI USHAURI WENU

WADAU WANAOHITAJI MUONGOZO KATIKA BIASHARA HII
Habari wadau,

Napenda kuuliza hivi: Kuuza au biashara ya chakula inalipa au?

Naombeni mawazo yenu.
Habarini,
Kwa wanaofahamu na wenye uelewa na hii kitu naombeni mchanganuo wa hii biashara ya chakula kwa mgahawa wa kawaida, inatakiwa uwe na shilingi ngapi?
Habari zenu ndgugu zangu,

Mimi ni mgeni katika ukurasa huu naomba kufahamishwa ni njia gani na taratibu gani na gharama za kuanzisha au kufungua cafe nzuri ya wastani.

Msaada wenu tafadhali.
Habarini za leo wadau!

Nimepata wazo la biashara, nataka nikodi frem nifungue mgahawa, nafikiria kumtafuta mama yeyote ili aniendeshee, yani namuanzishia kila kitu halafu yeye anaendelea.

Nataka nikubaliane naye awe ananipa kiasi fulani cha faida tu aidha kwa siku au kwa wiki. Basi wadau naomba wenye uzoefu na hii biashara au changamoto zozote tushirikishane!

Mtaji wangu ni laki saba. 700,000/=MICHANGO YA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
Vitu vya kuzingatia na vifaa muhimu kwa biashara hii

Kabla ya kuwa na hivyo vitu fanya survey ya sehemu unayotaka kuwekeza hakikisha kuna mzunguko wa fedha au eneo lenye mkusanyiko wa watu kama stand ya daladala, vyuo, soko, makanisa makubwa (RC, Luth, etc), mikusanyiko ya taasisi na maeneo yote yenye makutano ya barabara zinazofanya hata bodaboda wajazane (boda boda ni indicator kubwa ya kuonyesha sehemu potential ya biashara hiyo), ukijiridhisha andaa vifuatavyo:

1. Viti vya plastic 20
2. Meza 5 za kulia chakula za plastic ni nzuri japo sio lazima hata mabenchi yaeza faa
3. Jiko la gesi zuri la kilo 30
4. Jiko ya mkaa 4 (jiko moja chapati, la maharage, la supu, la maji ya kunawa wateja) chai tumia jiko la gesi
5. Frying pan na vyombo vya kukaangia (ya maandazi, ya chapati, ya kukaangia mayai, etc)
6. Sufuria kubwa tatu(ugali, wali na maharage) na visufuria vidogo hata 7
7. Stand ya kunawia wateja na ndoo yake
8. Blenda ya kutengezea juice na kuponda nyanya
9. Sahani na vijiko vya kulia chakula 50
10 Stirer ya kuchanganyia changanyia bagia, mikate,etc
11. Freezer kubwa (ndogo inafaa kishida shida), ukiwa na oven sio shida
12. Case ya kubebea vyombo (usafi zaidi)
13. Tengeneza sehemu nzuri ya kupikia(mazingira yanayohamasisha usafi)
14. Tumia muda wako kujifunza hii shughuli tafuta wafanyakazi wenye ujuzi wa kupika aina tofauti za chakula na wasafi
15. Ulizia mahali wanapika vyakula vitam hasa vya kipemba watu wengi wanapenda sana
16. Kuwa mbunifu usiwe bahili wekeza fedha na walipe vizuri na kwa wakati wafanyakazi wako

KUMBUKA NI HATARI KUPIMA KINA CHA MAJI KWA KUTUMBUKIZA MIGUU YOTE - anza taratibu kwa kuweka vitu vidogo vidogo huku ukiusoma mchezo the more the response the more u invest boresha huduma na waelekeze wafanyakazi wawe na majibu mazuri na kuvutia wateja slowly utakuta demand inakuwa kubwa kulko suply na hapo ndiyo unaongeza uwekezaji.
Biashara ya mgahawa inaendana na vitu vifuatavyo

Mkuu biashara ya mgahawa inaendana na vitu vifuatavyo.
- Location
- Usafi
- Chakula
- Wahudumu
- Bei
- unicness/ je kwenye mgahawa wako kuna kitu cha ziada

1. Lazima kuwe na chakula chaenye ubora na si bora chakula
2. Location yake lazima iwenzuri na ya kuingilika na wateja.
3. Wahudumu lazima wawe na kauri nzuri na lazima wawe wasafi mda wote
4. Hotel lazima iwe safi time zote na muda ambao wateja unakuta wamepungua au kukata wanapitisha dekio ili kuweka mazingira ya usafi

kuhusu kutopata faida labda nikujibu ifuatavyo.
1. Inategemeana na bei ya msosi wako. Je umeweka bei ya kuvutia tu wateja bila kuajali kama kuna profiti?

2 Au umeweka bei ya juu kiasi kwamba wateja wanashindwa kuingia?
angalia bei yako kama ina meet cost na kutengeneza profit kidogo

3. Hao wahudumu wako je niwaminifu kiasi gani? Je ni ndugu zako wa karibu sana? But kwenye pesa hakuna cha undugu hata mke wako anaweza kuchakachua tu.

- jaribu kuspend siku nzima pale na ucheki wateja wanao ingia ni kiasi gani na pesa inayo patikana ni kiasi gani.

- then hapo utaweza fanya analysisi ya kujua kama huwa wanakuibia au

NB: Biashara ya hotel ni moja ya biashara ambazo kwa kweli huwa hazina hasara kubwa na ni moja ya business ambazo huwa zinatengeneza profit kwa haraka sana ukilinganisha na biashara za duka
Vitu vya kuzingatia

Siku zote katika biashara kuna vitu vya kuzingatia hasa 1.Quality 2. Location 3. Price ya chakula. Naomba niongelee issue ya quality. Hapa zingatiaa quality ya chakula pia usafi wa wafanya kazi.chakula kinawezaa kuwa kizuri but wafanya kazi wachafu, Nguo hazina ubora walizo vaa.

Pia kuna kitu kinaitwa customer relationship management. Ni namna gani wafanya kazi wako wanazungumzaa na wateja.mfano mtu anagiza chakula then mfanyakazi anajibu kwa kinunaa, hapo wateja hawarud na marejesho hupunguaa.

Nakusihi angalia ubora wa chakula, angalia bei ulioweka inaendana na watu wa eneo hilo, angalia uzungumzaji wa wafanya kazi na wateja, angalia usafi wa wafanya kazi.
Mambo ya kuzingatia unapoanzisha biashara ya chakula:-

1. Usafi wa watu/mtu na mahala pa kufanyia kazi (hili ni muhimu mnooo)

2. Kujua bei za bidhaa, kujihimu kudamka sokoni (masoko makuu) Nazi ya kawaida unaweza kuinunua kwa shilingi 1,500 mda wa kawaida, lakini ukidamka sokoni unaipata kwa mia saba ama elfu moja.

3. Kujua aina ya wateja waliokuzunguka na wanataka nini. Huwezi kupiga mchele kwenye eneo la Wasukuma wengi.

4. Kujali maslahi ya wafanyakazi wako na kuwa na ukaribu nao

5. Kuwa na tabia ya kudamkia Feri siku za weekend, kusanya stock ya wiki nzima badala ya kununua rejareja (feri utajifunza meng)

6. Ubunifu na ucheshi kwa wateja
Biashara nzuri fanya mwenyewe ujionee changamoto zake

Aisee, biashara nzuri ukiifanya mwenyewe ujionee changamoto zake na namna ya kuzitatua, kwa ninavyoona umejipanga kurudi jioni na kukusanya mapato huku ukiwapangia cha kufanya jiandae kupoteza hiyo milioni yako.

Nakupa mfano miaka mi 4 iliyopita nilifanya hiki unachokifanya tena kwa ukubwa haswa nikitafuta wamama wapishi wazuri (akiwemo shangazi yangu), nikafungua cafeteria chuo kimoja kipo hapo mbezi jogoo, nilitengeneza mfumo mzuri wa uendeshaji huku nikiwuweka shangazi yangu kama manager, mimi mara moja moja mwisho wa wiki ndio ninaenda, kukagua na kuchukua mapato kutenga budget ya wiki inayofuatia n.k

Walichonifanya baada ya kuona kuwa ninakuj kuchukua hela tuu na kuwapangia cha kufanya wakataka nyongeza ya mshahara, nikawapa. Hawakuridhika nilikuwa nimepanga wafanyakazi kila mtu kitengo chake kuna mtu wa kuosha vyombo, wa juice, chips, chai na vitafunwa na wa bites, kila mmoja kwa kitengo chake wakaanza kunipiga taratibu mfano mtu wa bites (karanga, ubuyu n.k)anatengeneza wa kwake anauza ukiisha ndio anauza vyangu.

Mapato yakaanza kuporomoka, nikachukua likizo, na kwenda kusimamia mwenyewe waliacha kazi watatu wenyewe na wengine nilifukuza taratibu akiwemo shangazi yangu ambaye nilimtimua mpaka leo hatuongei.

Kuwa makini, usije ukawa umempa mtu mtaji afanye yake.
Ili uipatie hii biashara ziangatia ushauri ufuatao

Hongera kwa kufikiria kuanzidha biashara ya chakula ambayo ndio biashara inayolipa kwa wakatu huu kwani lazima ule kwa njia yoyote. ili uipatie hii biashara ziangatia ushauri ufuatao.

1. Mpishi. Lazima uwe na mpishi ambaye atapika vyakula vikuu kutoka na na sehemu husika na vyenye ladha ambayo hata mtu akiwa tegeta asijisikie vibaya kuja bunju kula plate ya ubwabwa kwa dada naniliu.

2. Viungo. Matumizi sahihi ya viungo na kwa mapishi gani? nilishaona sehemu wametia binzari ya mchuzi kwenye chai wakidhani tea masala. usipike chai ya rangi ukatia maji na majani hamna hata karafuu, maganda ya iliki, mdalasini wala mchaichai.

3. Usafi. Usafi wa mpishi, sehemu unayofanyia biashara, vyombo vya kupikia na vyombo vya kulia vyakula chakula. sio vyombo vichafu vinasuuzwa baada ya kuoshwa na kufanya rangi ya sahani imebadilika na unaweza ukajiongeza kwa kuvizuuza na maji ya uvuguvugu kuuwa bakteria.

4. Bei. Kwa kuwa unaanza hakikisha bei zako ni rafiki pamoja na kuwa ladha ya chakula chako ni tofauti na banda la mama lishe.

5. Vitendea kazi. Lazima uwe na vitende akazi tofauti kama blenda, microwave, jiko la gesi dogo na mtungi wake, sio mteja anataka chakula anapata chakula cha baridi japo kuwa amekujamida ambayo sio ya kibiashara kivile.

6. Mahitaji. Hakikisha unakwenda kwenye masoko makuu kwa mahitaji na epukakununua mahitaji mengi sana kwa wakati mmoja kama samaki na kuku unawaweka kwnye friza mwezi mzima kwani huwa wana tabia ya kuwa na kaharufu ambacho hakikati hata umuunge vp. usinunue mchicha jumapili uje kupika ijumaa hapana, Jitahidi japo mara mbili kwa week sio mbaya uwe unakwenda mwenyewe marikiti.

6. Jiongeze. Usiuze chakula kikuu tu kama wali pilau, la ongeza najuice za viwandani na za kutengeneza mwenyewe matunda mengi ni kupata ujuzi tu, tengeneza salad baada ya kachumbari kwa kulia chakula, tengeneza pilipili za kupikana sio mteja atake pilipili umpe nzima akate mwenyewe, kwani kuna vitu vidogo vinavutia wateja sana na kama sio mjuzo sana ingia hata you tube utaona mapishi ya tofauti.

Kama kuna la ziada njoo pm nitakupa maujuzi zaidi.

ZAIDI, SOMA:

Jinsi ya kufanikiwa kibiashara kwa kufungua mgahawa

Mgahawa ni wazo zuri kwa kuanza mradi wa biashara, Mara baada ya kujenga na kupata imani, mgahawa utawavutia wateja bila matatizo yoyote. Lakini, kabla ya kuamua kufungua mgahawa unatakiwa kuzingatia mambo kadhaa kama vile kujenga, masuala ya leseni na kisheria pamoja na mahitaji mbalimbali yaliyowekwa na mamlaka za afya mfano TFDA kwa Tanzania. Baada ya kujaza mahitaji yote, unaweza kuanza mradi wako wa biashara katika utulivu wa muda mrefu na kwa umakini kuhakikisha unapata mafanikio.

1 -. Kama miradi mingine yoyote, eneo la biashara ni kipengele muhimu kwa ajili ya mgahawa. Chagua sehemu ambayo ni katika eneo la msongamano ambapo kuna mzunguko wa mara kwa mara na idadi kubwa ya watu.. lazima pia kuwa na maegesho mazuri, ambayo itaruhusu watu kuhifadhia vinywaji vichache na vitafunwa

2 -. Huduma za Mgahawa zitolewe katika njia ya kisasa, ili kuvutia watu kutembelea na kuchunguza yaliyomo ndani yake sababu mgahawa utakuwa ukijitangaza wenyewe kwa uzuri wa huduma zake (wahudumu wakarimu, waelewa na wasio wepesi wa kuonesha kuudhika). Aina ya vyakula na vinywaji ni lazima izingatie uhitaji wa wateja na mchanganyiko wake uwe wa kisasa. Ni lazima pia kuwa na nafasi ya kutosha katika mgahawa wako ili kutoa nafasi inayoweza kuenea wageni zaidi wakati wa masaa ya biashara. Unaweza kuweka/kuongeza eneo la bar sehemu ya wazi kwa ajili ya vinywaji ili kutoa nafasi ya kutosha kwa wateja wanaohitaji vinywaji pekee.

3 -. Kama utahitaji kuuza vileo katika bar, lazima kupata vibali muhimu kwa ajili ya matumizi ya pombe kabla ya kufungua . Pamoja na taratibu za kisheria, unatakiwa kuwa makini na mambo mengine kuhusiana na taratibu za afya. Ni muhimu kujijengea uaminifu na kulinda afya ya wateja wako pia kwa kuzingatia maelekezo yote yanayoamriwa na idara ya afya kamavile kuhakikisha jiko na eneo la kuhifadhi chakula viko katika mahali maalum na katika hali ya usafi. Pia vyombo vinavyotumika na kila kitu kinachohusika katika mgahawa wako view katika hali ya usafi ikiwa ni pamoja na usafi binafsi wa wahudumu.

4 - Daima angalia mshindani wako analenga kufanya nini au amefanya nini ili wewe ufanye ubunifu wa tofauti kuwavuta wateja wengi kwako. Kabla ya ufunguzi wa mgahawa pia ni muhimu kufahamu washindani wa karibu ambao utapambana nao kibiashara kwa ajili ya kuanzisha mgahawa wako katika namna mpya. Tathmini kabisa faida na hasara katika kusimamia kazi,maamuzi na utekelezaji wa mikakati ya biashara.

5 -. Ni vyema kuchukua uongozi na ushauri kutoka kwa mtu ambaye tayari ana uzoefu katika kuendesha mgahawa wenye mafanikio au café. Mara nyingi mshindani wako hawezi kukupa ushauri utakaokufaa. Watu ambao wana uzoefu wa kufanya kazi na migahawa watakwambia baadhi ya vidokezo muhimu na vitendo kwa ajili ya kuanzisha biashara ambayo itakuwa na mchakato rahisi sana. Kama wewe utaendelea sana zaidi na kupata maarifa ya kutosha unaweza kuwa hata mshauri biashara kwa watu wengine.

Chanzo: inamotoselfemployment
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
7,060
2,000
Mkuu biashara ya mgahawa inaendana na vitu vifuatavyo.

- Location
- Usafi
- Chakula
- Wahudumu
- Bei
- Uniqueness/ Je, kwenye mgahawa wako kuna kitu cha ziada


1. Lazima kuwe na chakula chaenye ubora na si bora chakula
2. Location yake lazima iwenzuri na ya kuingilika na wateja.
3. Wahudumu lazima wawe na kauri nzuri na lazima wawe wasafi mda wote
4. Hotel lazima iwe safi time zote na muda ambao wateja unakuta wamepungua au kukata wanapitisha dekio ili kuweka mazingira ya usafi

Kuhusu kuto pata faida labda nikujibu ifuatavyo.
1.
Inategemeana na bei ya msosi wako. Je umeweka bei ya kuvutia tu wateja bila kuajali kama kuna profiti?
2 au umeweka bei ya juu kiasi kwamba wateja wanashindwa kuingia?
angalia bei yako kama ina meet cost na kutengeneza profit kidogo
3.
hao wahudumu wako je niwaminifu kiasi gani? Je ni ndugu zako wa karibu sana? But kwenye pesa hakuna cha undugu hata mke wako anaweza kuchakachua tu.

- jaribu kuspend siku nzima pale na ucheki wateja wanao ingia ni kiasi gani na pesa inayo patikana ni kiasi gani.
- then hapo utaweza fanya analysisi ya kujua kama huwa wanakuibia au
nb: Biashara ya hotel ni moja ya biashara ambazo kwa kweli huwa hazina hasara kubwa na ni moja ya business ambazo huwa zinatengeneza profit kwa haraka sana ukilinganisha na biashara za duka
 

ureni

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,263
1,250
Hongera mkuu biashara ya hoteli na chakula inalipa sana manake mtu yeyote lazima ale na ashibe kwa hiyo sio biashara ya kukuingiza hasara.

Sasa ushauri fanya hivii chukua likizo huko kazini kwako siku 30, nenda kasimamie mwenyewe kwenye hizo siku hakikisha unaweka hesabu vizuri kama chips agalia guia la viazi umenunua kwa kiasi gani umeliuza kwa mda gani umepata faida ya kiasi gani na unapata faida ya kiasi gani hapo utaweza kuielewa vizuri biashara yako kuna viti vingi vya kujua, kama usafi, ugha wanayotumia watu wako huo,pia unasikiliza mawazo ya wateja kwa kweli wateja huaga wana bonge ya mawazo ambayo ni ya manufaa sana.
 

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,773
2,000
Pamoja na yote waliyoongea wachangiaji waliotangulia, hakikisha chakula kinachopikwa ni kizuri kwa maana ya taste.
Jaribu kuangalia aina ya wateja ulionao na upange bei kuzingatia vipato vyao.

Unaweza kutenga sehemu mbili, moja ikawa na special foods ukaset price yake na sehemu nyingine ikawa na vyakula vya kawaida na bei yake.

Pata muda ukusanye maoni ya wateja na wape trainning ya customer care hao wahudumu wako.
NB: biashara nyingi mwanzo huwa ni ngumu na huna budi kukubali hasara.
 

Dr wa ukweli

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
898
250
1. Usisahau kulipa kodi TRA, na nyinginezo
2. BIASHARA KAULI hao wahudumu kama hawajui kuuza maneno walah mtume huuzi!
3. Kwenye biashara kuna ushirikina sana (i) utafute kimzizi pemba, bagamoyo, sumbawanga, nk kikusaidie kuvuta wateja

AU (ii)MAOMBI OMBEA BIASHARA YAKO ITAFANIKIWA.

NB: HAPA MJINI CHUMA ULETE NI NYINGI SANA ZINGATIA NO 3 (ii)
 

Kingdom_man

JF-Expert Member
May 19, 2010
405
500
Mkuu biashara ya mgahawa inaendana na vitu vifuatavyo:
- Location
- Usafi
- Chakula
- Wahudumu
- Bei
- Uniqueness/ je, kwenye mgahawa wako kuna kitu cha ziada


1. Lazima kuwe na chakula chaenye ubora na si bora chakula
2. Location yake lazima iwenzuri na ya kuingilika na wateja.
3. Wahudumu lazima wawe na kauri nzuri na lazima wawe wasafi mda wote
4. Hotel lazima iwe safi time zote na muda ambao wateja unakuta wamepungua au kukata wanapitisha dekio ili kuweka mazingira ya usafi

Kuhusu kuto pata faida labda nikujibu ifuatavyo:


1. Inategemeana na bei ya msosi wako. Je umeweka bei ya kuvutia tu wateja bila kuajali kama kuna profiti?
2 Au umeweka bei ya juu kiasi kwamba wateja wanashindwa kuingia?
angalia bei yako kama ina meet cost na kutengeneza profit kidogo
3. Hao wahudumu wako je niwaminifu kiasi gani? Je, ni ndugu zako wa karibu sana? But kwenye pesa hakuna cha undugu hata mke wako anaweza kuchakachua tu.

- Jaribu kuspend siku nzima pale na ucheki wateja wanao ingia ni kiasi gani na pesa inayo patikana ni kiasi gani.
- Then hapo utaweza fanya analysisi ya kujua kama huwa wanakuibia au
NB: Biashara ya hotel ni moja ya biashara ambazo kwa kweli huwa hazina hasara kubwa na ni moja ya business ambazo huwa zinatengeneza profit kwa haraka sana ukilinganisha na biashara za duka

Useful contribution. Excellent!!!
 

kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
1,500
Mimi si mfanyabiashara,lakini najua kitu kimoja kuwa biashara ni kununua na sio kuuza. Mchango wangu ni huu, je bidhaa za mgahawani kwako unanunua wapi na nani ananunua? Je bei za bidha hizo umejaribu kulinganisha na masoko mengine? Jaribu kufanya zoezi hili uone.
Malila hebu eleza zaidi hapo kwenye RED
 

rakeyescarl

JF-Expert Member
Dec 9, 2007
469
250
Mkuu nimependa hapo kwenye blue-I salute you-JF ,KUNA VICHWA VYA MAANA KWELI HUMU!,sikulijua hili![QUOTE=Malila;2249518]Mimi si mfanyabiashara,lakini najua kitu kimoja kuwa biashara ni kununua na sio kuuza. Mchango wangu ni huu, je bidhaa za mgahawani kwako unanunua wapi na nani ananunua? Je bei za bidha hizo umejaribu kulinganisha na masoko mengine? Jaribu kufanya zoezi hili uone.[/QUOTE]
 

jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
7,486
2,000
Nimefungua biashara ya Mgahawa sehemu flani hapa mjini DSM, nimeweka wafanya kazi 3; mmoja kwa ajili ya chips na wa2 kwa ajili ya chakula kwa sababu biashara yenyewe bado changa. Eneo ambalo nafanyia biashara lina population kubwa na halina competition kubwa sana. Mimi napitia mida ya jioni kucheki jinsi biashara inavyoendela na kuhakikisha hesabu zinaenda vizuri.

Tatizo mpaka sa hizi ni zaidi ya mwezi na sioni faida yoyote zaid ya kuwalipa wafanyakazi wangu kwa kipato changu kidogo ambacho ninakipata kwenye kaajira kangu kwa mhindi. Naombeni mnisaidie yafuatayo;
  1. Nifanyaje ili niweke kuvutia wateja zaidi bila kutumia kiasi kikubwa cha fedha?
  2. Nifanyaje ili niweze kupata faida kubwa, yani kuwa na matumizi kidogo na mauzo mengi?
  3. Nifanyeje ili kuwabana wafanyakzi wngu waisimamie biashara vizuri na kupata faida?
NAOMBENI USHAURI WENU.

Kama alivyoshauri jamaa mmoja hapo chiini au juu. Inabidi uchukue likizo kama yamiezi 2, hatakama sio ya malipo.
Simamia mwenyewe kuanzia unaponunua sukari, chumvi mpaka vyakula na vyombo vya hapo mgahawani.

Hapo utajua kuwa hio boashara inalipa au hailipi, na kama inalipa basi kwa siku ni kiasi gani, na ni chai ya namna gani wateja wanaipenda au chakula gani cha mchana au siku wateja ndio wanunua sana.

Kuanzisha biashara ni bomba ila unatakiwa ujue hio business inaingiza roughly kiasi gani kwa siku, hapo itakua rahisi kuwabana wasimamizi kama kuna short.
 

Mbogela

JF-Expert Member
Jan 28, 2008
1,379
1,250
Mkuu nimependa hapo kwenye blue-I salute you-JF ,KUNA VICHWA VYA MAANA KWELI HUMU!,sikulijua hili![QUOTE=Malila;2249518]Mimi si mfanyabiashara,lakini najua kitu kimoja kuwa biashara ni kununua na sio kuuza. Mchango wangu ni huu, je bidhaa za mgahawani kwako unanunua wapi na nani ananunua? Je bei za bidha hizo umejaribu kulinganisha na masoko mengine? Jaribu kufanya zoezi hili uone.
[/QUOTE]hiyo cocept kailezea vizuri robert kiyosaki ktk poo dad, rich dad 2, the cashflow quadrant. Napendekeza ukisome
 
Mar 4, 2011
13
0
Ndugu unatakiwa ugeuze baadhi ya vyakula na vinywaji au uongozee baadhi yake ili upate wateja zaidi na pia ni uzuri kutizama migahawa ilioko kabli yako wanatumia mbinu gani ili kupasi kuchukuwa ujuzi wao ila pia pengine sehemu wenyewe inawezekana kuwa si ya kuvutia kabisa kwa hivyo ndugu nakushauri ufanye mabadilisho ili uweze kuendelea na biashara yako
 

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,770
1,195
Sema maeneo tuweze kukusaidia vizuri. Kuna maeneo mengine yanaitaji vyakula vizuri, maeneo mengine yanaitaji matangazo, maeneo mengine kuna aina ya vyakula wanavyopenda.
 

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,618
2,000
Tunaposema biashara ni kununua sio kuuza,tuna maana kuwa bei ya soko inajulikana kwa hiyo ni lazima upate faida kabla hujauza bidhaa zako kwa kununua kwa bei nzuri/chini kiasi toka ktk chanzo(supplier mzuri).

Mfano, Kilo moja ya mchele ni Tsh 1600/ soko la Kariakoo na mchele huo huo ni Tsh 1350/ pale Tandika na wewe mgahawa wako uko Buguruni, yaani nauli ya daladala ni sawa. Tayari huyu wa Tandika ameshaokoa Tsh 250/ kwa kila kilo atakayo nunua. Kwa hiyo mkija Buguruni ktk migahawa yenu,mnaanza kutafuta faida kwa kuuza wali ktk soko kwa bei moja,mwenzio ana Tsh 250/ aliyoiokoa ktk manunuzi na wewe una Tsh 0/.

Kwa hiyo utaona huyu wa Kariakoo lazima apunguze kipimo cha sahani moja au aongeze ufundi ktk mapishi, sasa huyu wa pili anachofanya ni kuongeza ukubwa wa kipimo cha sahani kidogo na anaimarisha mapishi, ni lazima apate wateja wengi kila siku bila kulaza chakula, mwisho anapata muda wa kutosha kufanya maandalizi ya kesho na kupumzika, kufanya usafi wa eneo lake la biashara nk.

Siku moja nenda Kitunda/Kivule/Majohe asubuhi sana uone vijana wa mjini wanachofanya?
 

sajosojo

JF-Expert Member
Apr 14, 2010
928
500
Helo wadau naomba ushauri wenu niko hapa dar nina kama mil 1 nataka kufungua biashara ya mama lishe, nimwajili mtu wa kupika. Je, itanilipa?
 

Mgombezi

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
610
0
Nimekuwa nikiwashauri wajasiriamali wengi kwamba furaha yako katika biashara isiwe katika fedha/faida unazopata; lazima kuwe ni jambo la zaidi linalokusukuma kuanzisha biashara. Fursa yeyote ya biashara hutokana na uhitaji wa huduma/bidhaa katika eneo husika, hivyo basi biashara yako inapaswa kulenga au kufikia zaidi jamii inayokuzunguka kulinga na uhitaji wao.

Kila biashara inalipa, bali hutegemeana na uhitaji uliopo katika eneo husika, ikiwa umeona uhitaji wa kuwepo kwa huduma hiyo katika eneo husika basi utapata faida tu; bali kama huduma hiyo inapatikana katika eneo husika na unahitaji kuongeza ushindani tu, inabidi ujipange vizuri.
 

ESAM

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,141
2,000
Songa mbele na kazi maana biashara ya chakula lazima watu wale tu. Ila kama alivyoshauri Mgombezi angalia uhitaji wa huduma katika eneo husika au soko la bidhaa yako. Lakini pia kumbuka suala la chakula lazima liambatane na usafi wa hali ya juu, yaani mazingira pamoja na vifaa utakavyotumia.

Pia usisahau kumwomba Mungu akusaidie na kuibariki biashara yako, ila fungu la KUMI umtolee usimwibie. Baada ya hapo mafanikio ni lazima tu.
 

Autorun

JF-Expert Member
Mar 21, 2008
557
250
Biashara hyo nzuri mtaji ulionao usikupe hofu ili uweze kucompete vizur biashara hyo inahitaji mambo kadha yawe sawasawa.

1. Usafi unahitajika wa hali ya juu (mazingira ya mgahawa,wahudumu, vyombo na upishi)
2. Kauli nzuri
3. Ubunifu katika upishi
4. Weka huduma za ziada
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom