Fahamu haya kuhusu ajira za nje ya nchi

Emmanuel Zao

Member
Mar 8, 2015
6
16
Hii ni kwa yeyote mwenye ndoto ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi:

Ili mwajili wa nje ya nchi akupe stahiki zako kama mfanyakazi na wewe ufurahie fursa hiyo basi ni lazima uwe na:

1. Elimu ya uhakika sababu ndio kigezo cha mtu anaejitambua kwa Dunia ya leo.

2. Uzoefu na taaluma yenye ushindani kwenye soko la ajira. (Hapa unatakiwa kuwa muwazi ni kazi gani hasa unataka na sio kusema yoyote tu).

3. Diplomasia nzuri ya nchi yako na nchi unayokwenda.

4. Kumbukumbu nzuri za uhalifu na afya yako.

5.Japo sio lazima ila ni vizuri ukajua lugha zingine za kimataifa hasa ya hiyo nchi unakwenda.

6. Bima ya afya na mwana sheria/Mshauri atakae simamia mkataba wako, ubalozi na taariza zingine muhimu hasa za kisheria kwa mujibu wa kanuni.

Kama una hivyo vigezo hakikisha una

1. Electronic Passport ambayo ni Valid kuanzia miaka minne nakuendelea.

2. Anza kutafuta ajira kwa jia mbali ikiwemo mitandao ya kijamii kama LinkedIn n.k.

3. Kadi ya homa ya manjano.

4. Gharama za kumlipa mshauri wako(Consultant) endapo utapata ajira.

5. Kutokana na janga la Covid-19, uwe na pesa ya ziada kwaajili ya PCR test &certificate ama chanjo kabisa.

6. Kuhus ticket, Check up test,Visa, work permit au resident permit hizo atagharamia mwajili lakini uwe na pesa ya ziada endapo atataka ulipie kimoja wapo.

ANGALIZO:
Ukitumia njia ya mkato kupitia mawakala amabao hawatambuliki kisheria unaweza kubahatika na kila kitu kikaenda shwari lakini hiyo ni ku-bet kwa kuhatarisha sana. Zaidi ya yote tegemea haya:

1. Kuibiwa pesa zako na kazi usipate.

2. Kutumikishwa kingono, mwili n.k.

3. Mshahara mdogo

4. Kukosa haki yakueleza shida na changamoto zako kazini.

5. Manyanyaso mengineyo au kifo kabisa, sababu mara nyingi nchi yako haijui kinachoendelea zaidi ya ww kuwa kwenye hiyo nchi.

Kama huna Elimu wala ujuzi au taaluma rasmi zipo kazi kwaajili yako lakini kumbuka zinaweza kufanywa na wengi tu hasa wazawa sasa kwanini wakuchukue wewe?

Ili kuzipata tafuta mpenzi au marafiki kwenye nchi husika ambao baadae watakusaida kupata nafasi hizo kama rafiki kisha utaratibu wa ajira ufuate kanuni na sheria kupitia ubalozi.

Kabla sijaweka kalamu chini, Janga la virusi vya Corona limeathiri nyanja nyingi za maisha ikiwemo ajira hivyo basi ukikosa fursa nchini haimanishi kwingine zinapatikana kirahisi lakini ukibahatika mshukuru sana Mungu na ukumbuke ulikotoka.

Ahsanteni sana😎
 
Hii ni kwa yeyote mwenye ndoto ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi sijamlenga:

Ili mwajili wa nje ya nchi akupe stahiki zako kama mfanyakazi na wewe ufurahie fursa hiyo basi ni lazima uwe na:

1. Elimu ya uhakika sababu ndio kigezo cha mtu anaejitambua kwa Dunia ya leo.

2. Uzoefu na taaluma yenye ushindani kwenye soko la ajira. (Hapa unatakiwa kuwa muwazi ni kazi gani hasa unataka na sio kusema yoyote tu).

3. Diplomasia nzuri ya nchi yako na nchi unayokwenda.

4. Kumbukumbu nzuri za uhalifu na afya yako.

5.Japo sio lazima ila ni vizuri ukajua lugha zingine za kimataifa hasa ya hiyo nchi unakwenda.

6. Bima ya afya na mwana sheria/Mshauri atakae simamia mkataba wako, ubalozi na taariza zingine muhimu hasa za kisheria kwa mujibu wa kanuni.

Kama una hivyo vigezo hakikisha una

1. Electronic Passport ambayo ni Valid kuanzia miaka minne nakuendelea.

2. Anza kutafuta ajira kwa jia mbali ikiwemo mitandao ya kijamii kama LinkedIn n.k.

3. Kadi ya homa ya manjano.

4. Gharama za kumlipa mshauri wako(Consultant) endapo utapata ajira.

5. Kutokana na janga la Covid-19, uwe na pesa ya ziada kwaajili ya PCR test &certificate ama chanjo kabisa.

6. Kuhus ticket, Check up test,Visa, work permit au resident permit hizo atagharamia mwajili lakini uwe na pesa ya ziada endapo atataka ulipie kimoja wapo.

ANGALIZO:
Ukitumia njia ya mkato kupitia mawakala amabao hawatambuliki kisheria unaweza kubahatika na kila kitu kikaenda shwari lakini hiyo ni ku-bet kwa kuhatarisha sana, sana sana tegemea haya:

1. Kuibiwa pesa zako na kazi usipate.

2. Kutumikishwa kingono, mwili n.k.

3. Mshahara mdogo

4. Kukosa haki yakueleza shida na changamoto zako kazini.

5. Manyanyaso mengineyo au kifo kabisa, sababu mara nyingi nchi yako haijui kinachoendelea zaidi ya ww kuwa kwenye hiyo nchi.

Kama huna Elimu wala ujuzi au taaluma rasmi zipo kazi kwaajili yako lakini kumbuka zinaweza kufanywa na wengi tu hasa wazawa sasa kwanini wakuchukue wewe?

Ili kuzipata tafuta mpenzi au marafiki kwenye nchi husika ambao baadae watakusaida kupata nafasi hizo kama rafiki kisha utaratibu wa ajira ufuate kanuni na sheria kupitia ubalozi.

Kabla sijaweka kalamu chini, Janga la virusi vya Corona limeathiri nyanja nyingi za maisha ikiwemo ajira hivyo basi ukikosa fursa nchini haimanishi kwingine zinapatikana kirahisi lakini ukibahatika mshukuru sana Mungu na ukumbuke ulikotoka.

Ahsanteni sana✌️😎
Ushauri mzuri sana, uamuzi ubaki juu ya mhusika
 
Hapo number 4 kwa consultants una maanisha Nini?
Dadavua please
Consultant(Mshauri) anaweza kuwa mwanasheria ama taasisi au kampuni ya uwakala iliyosajiliwa na inatambulika kisheria, kazi yao hasa kwenye maswala ya ajira za nje ni kuusaidia ubalozi kuwasilisha na kufuatilia mchakato wa nyaraka zako mpaka unapata mkataba wa kazi.

Hawa ni watu wanaokushauri ni nyaraka gani zinatakiwa ili kufanikisha swala lako, lakini pia watakusaidia kutatua changamoto zako uwapo kazini, hasa hasa kuijulisha serikali kupitia balozi zote mbili.

Moja ya Consultation agency ninayoijua nii👉🏻Vision Consultancy:Best Immigration Consultants of Canada, USA and Germany in Abu Dhabi
Ahsante.
 
Back
Top Bottom