EWURA: Bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kuanzia Jumatano, tarehe 3 Agosti 2022

Mama Debora

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
1,482
2,581
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 3 Agosti 2022.

Bei za Mafuta katika soko la dunia zimeendelea kuongezeka na kusababisha bei za mafuta katika soko la ndani kuongezeka pia. Ili kupunguza madhara ya ongezeko hilo katika soko la ndani, Serikali imetoa ruzuku ya bilioni 100 kwa ajili ya bei za mafuta hapa nchini kwa Agosti 2022. Serikali kwa kutoa ruzuku hiyo, imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa Agosti 2022 kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 1.

1.JPG


Katika kutekeleza bei hizi, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta watatakiwa kuzingatia yafuatayo: -

EWURA inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.​
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.​
Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (Price cap) au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa kupitia Magazeti ya Serikali Na. 2A na 57 ya tarehe 3 Januari 2022 na 28 Januari 2022, sawia.
Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.
Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia, risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya mafuta ya petroli.​
Wauzaji wa Mafuta ya petroli wa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei yenye ruzuku kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 3. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili

Wauzaji wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei yenye ruzuku kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 4. Isipokuwa kwa wateja ambao wana msamaha wa kodi Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.
 

Attachments

  • Cap Prices Publication wef 3 Agosti 2022 - Kiswahili .pdf
    146.3 KB · Views: 11
Watanzania ni mahodari wa kulalama kwenye key boards, crude oil 🛢 imeshuka bei kwa zaidi ya 8usd per barrel (106usd),bei ya mafuta ilitakiwa ISHUKE ,nini kimepandisha bei juu?,simple ni thamani ya shs yetu kuwa chini(refer mjadala wa juzi kati kati ya ZWK vs TSHS)na kodi nyingi !
 
Watanzania ni mahodari wa kulalama kwenye key boards, crude oil 🛢 imeshuka bei kwa zaidi ya 8usd per barrel (106usd),bei ya mafuta ilitakiwa ISHUKE ,nini kimepandisha bei juu?,simple ni thamani ya shs yetu kuwa chini(refer mjadala wa juzi kati kati ya ZWK vs TSHS)na kodi nyingi !
USD imekuwa stronger against any currencies ndani ya kipindi cha wiki mbili hizi, sio shilingi tu ambayo imezingua.
 
Back
Top Bottom