Eti Watanzania ni wadokozi? Au Waajiri ndo wanyonyaji wanawalipa Watanzania kidogo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Watanzania ni wadokozi? Au Waajiri ndo wanyonyaji wanawalipa Watanzania kidogo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Dec 21, 2009.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Juzi Snow Crest Imefunguliwa Arusha, na wafanyakazi wageni wameajiriwa kwa wingi. Na Watanzania wameitwa wadokozi

  Sababu ni nini??

  Watanzania ni Wadokozi? Au Waajiri ndo wanyonyaji wanawalipa watanzania mshahara kidogo ukilinganisha na wageni.

  Mfano Mshahara wa Graduate wa Kitanzania ni laki 3 while graduate wa Kenya Au Ulaya ni Millioni moja??

  Huyo Mtanzania ataweza kupanga nyumba ya hadhi yake? Ataweza kupanda gari ya hadhi yake? Mtanzania ataweza kujiwekea akiba ili baadae ajenge nyumba au anunue gari au asomeshe watoto?

  Kwa hiyo Wadau hapa JF jadilini kama Watanzania ni wadokozi kweli au Watanzania wanaonewa??
   
 2. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  NI kweli sisi ni wadokozi wa kijinga!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hivi hao Wakenya wametuzidi nini wabongo hadi wawe wanalipwa mishahara inayotuzidi? Mimi kila siku huku nakutana na Wakenya ambao sioni chochote walichonizidi. Sana sana ni wachovu na washamba na wanaotamani wangekuwa Watanzania. Sielewi kabisa hii ya kuwalipa mishahara iliyotuzidi
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mpadmire,

  Lazima tujiulize kwanza sisi wenyewe, hao Wakenya wanatuzidi nini mpaka walipwe zaidi ya mara tatu ya Watanzania?

  Sidhani kama kuna mwajiri ambaye angependa akachukue wakenya na kuwaacha Watanzania wakati skills zao zinafanana.

  Kwenye dunia hii ya ushindani ni bora tujiandae na kukuza skills zetu ili tushindane na hao wengine.
  Inasikitisha kuona ajira zinazotengenezwa zinaenda kwa wageni huku Watanzania tunaachwa kwenye mataa.
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Amini usiamini kuna kitu waKenya wametuzidi... kimojawapo hiki hapa.

  Mkenya akifanya kitu ana-communicate kwamba amefanya, kina faida gani kwenye taasisi husika na kuweka open kwa organization husika,

  Mtanzania anaweza kufanya mambo mazuri na makubwa sana... alafu anakaa hayo aliyofanya moyoni kwake au kwenye kitengo chake...

  Matokeo yake anakuwa -invisible kwenye organisation na mwishowe kuonekana hafanyi kazi!
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Dec 21, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Aaah wapi! mimi nakataa katakata. Wakenya hawajatuzidi lolote. Basi tu sisi tuna matatizo yetu ya kutukuza vya nje. Ujinga mtupu.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Heeeee...!
  We Kasheshe we!..Unataka ban eeh? Invisible hafanyi kazi wakati jeiefu iko hewani 24/7!
   
 8. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wana JF mumepotosha mada. Mada sio wakenya. Mada ni sisi wa Tz wadokozi. Nasikitikitika mumeshindwa kuona kwamba rais ametuangusha hapa kwa kushabikia wageni kuchukua kazi zetu eti sisi wadokozi. Hoja ya kitoto....
   
 9. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nadhani tofauti iliyopo ni uwezo wa kung'ang'ania tunachotaka (kujitetea kimaslahi). Wakenya wana uwezo wa kusema wanachokitaka na kukitetea.

  Si kweli kuwa waKenya wanafanya kazi zaidi yetu. Wala si kweli kuwa waTanzania ni wadokozi kuliko waKenya. Inawezekana kinyume chake ikawa kweli na hiyo ni imani yangu. Mimi nimeishi Kenya nimeona uwezo wa wengi wao.

  Kuna imani potofu kuwa ukijua kiingereza sana, unakuwa na ujuzi mkubwa. Labda kuna wanaoweza kutetea hoja hiyo. Ila lugha ni kitu kimoja na uwezo wa kufanya kazi ni kitu kingine. Hao wenye Crest Hotel watakuwa wanataka watu wenye uzoefu mkubwa (command) ya English. Wasitukane watu kuwa ni wezi.
   
 10. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Udokozi ni tabia ya mtu: hauna rangi, kabila au taifa. Kusema kwamba watanzania ni wadokozi si sahihi, japo kwa kweli wapo baadhi yao ambao ni wadokozi kama ilivyo kwa wakenya, nk ambao baadhi yao ni wadokozi. Ila mi nadhani sababu ya watanzania kutopendelewa na wenye ajira ni tabia ya watanzania ya kutojua kujipendekeza, kulamba miguu ya waajiri. Kwa kifupi ni watu "jeuri" japo maskini. Wanajifanya wajuaji na wenye kujua haki zao. Waajiri wengi hawapendi watu wa aina hii. Wanawakimbia na kukimbilia wale wenye kusema "ndiyo mkuu" na kutetemekea mwajiri.

  Pili, ni kasumba tu! kwamba msomi kutoka Kenya ni bora kuliko msomi wa Tanzania. Huu ni ugonjwa! Hasa ukizingatia na ung'eng'e wa kubahatisha wa wasomi wengi wa kitanzania. Kumbe kwa kuwa lugha hiyo "tukufu" hawaimung'nyi vilivyo inaonekana kwa waajiri kwamba hawakusoma sawasawa. Jambo ambalo si kweli. Wanashindwa kutofautisha kati ya maarifa na lugha.
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nimepigwa BUTWAA na hii assumption ya rais wetu kukubaliana na hoja ya KIJINGA kutoka kwa wamiliki wa hoteli.
  Kama ni udokozi, kwani vyombo ya dola vipo kwa ajili ya nini? Huyu rais kweli ananichosha. unamchekea mtu anayemtoboa mwanao macho?

  Nadhani wawekezaji wa kigeni wameshamjulia muungwana wetu kwamba tell him anything that makes him to SMILE.

  Am soooo down very low ktk hili suala
   
 12. A

  August JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni viongozi wetu waliowafanya weatanzania kuwa wadokozi, bila kuwabadili viongozi hao, basi mwendo wetu utakuwa hivyo, kitu kimoja cha msingi kinacho wafanya watanzanias kuwa wadokozi ni
  kukosa mikopo ya kujenga nyumba, hivyo kumlazimisha mtu atafute mashali pakuanzia kwa wizi.
  pili ni viongozi wenyewe kuwa wadokozi hivyo hawaoni shida za watanzania wengi. na kufikiria kwamba watu wanaweza kuishi bila mikopo.
  nk nk
   
 13. _ BABA _

  _ BABA _ JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  mkuu nakuunga mkono 100% kabisa wakenya hawatuzidi lolote bali ni uwoga wetu watz na zaidi ni hatuna confidence hususani pale tunapomwona mgeni...hapo ndo tatizo kubwa huanzia, tunauwezo zaidi yao kabisa...mie naishi,nasoma,nafanya kazi nao hapa Europe mbona sioni walilonizidi.....wabongo tuache woga mazee....we can do the best of best.
   
 14. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Suala hapa si woga! Suala ni kwamba waajiri wanatunyanyapaa watanzania. hawatutaki. sababu yao ni kwamba tuko wadokozi.
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kunjygroup,
  Nakubaliana na wewe kuwa rais ametuangusha. Amewapa aid and comfort wawekezaji ambao wanavunja sheria kwa kuleta "so called wafanyikazi" kutoka nchi zao hata kwa nafasi za kazi ambazo zingefanywa vizuri tu na Watanzania. Amewapa justification ya kuendelea kuleta makarani, madreva, wapishi kutoka nchi zao simply kwa kuwa hata rais anaafiki kuwa Watanzania ni wadokozi.
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..wananchi na sisi turuhusiwe kuchagua expatriates ktk nafasi ya Raisi kwasababu hawa wazazi [mwinyi,mkapa,kikwete] wameishia kuwa wezi wakubwa.
   
 17. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Juli:

  Ukienda Kenya matajiri wa matatu wanapenda vijana wa Tanzania kwa sababu mashapu. Hivyo kuna vitu tuna-excel kuliko waKenya.

  Tukirudi kwenye kazi za professional. Kuna kitu watanzania wa-lag behind. Kwanza english kwa watanzania wengi ni second language. Lakini wengi hatutaki ku-improve.

  Hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwa watanzania wawili wenye qualification sawa lakini mmoja akawa na command nzuri ya English, mwenye command nzuri ata-excel. Hata hapa viwanja naona tofauti.

  Pili watanzania wanapokuwa shule wanakuwa tight sana. Hawajiandai kuwa profession. Wengi wakiwa mashuleni wanasoma kama vile wanataka kuwa academicians.
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  My bro, we have to face it. Hata mimi kama nikiwa na kampuni naweza kuajiri wakenya nitaacha watanzania. Hakuna kikubwa walichotuzidi wakenya, lakini kidogo walichotuzidi ni kikubwa sana kwa employers.

  Kuna wabongo wavivu sana(wapo wachache wanafanya kazi vizuri sana), they are good at being puctual and attending to work, but they hardly work. Ajabu ni kuwa wanataka mishahara mikubwa. Udokozi ni moja ya sababu ambayo inatuponza sana wabongo, tuna mfano mzuri sana Shoprite, na kwenye mashirika mengi ya Tanzania, na hata serikalini. Tunajiibia hata wenyewe, so that makes it easy kuwaibia wageni.

  Lakini tumejitakia sisi wenyewe, nani aliwapa vibali hao wakenya? ni sisi wenyewe? nani amewafanya hao employers wachague wakenya? ni sisi wenyewe.
   
 19. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wametuzidi kwa kingereza! Asilimia kubwa ya watanzania hawajui kingereza fasaha, na wanababaishababaisha sana wakati wa kuongea na kuandika.
  Ukiona mtanzania anaongea na mdhungu basi ni yees kwa sana na kuchekacheka hatakama jambo halichekeshi.
  Kutokujua kingereza kwa wabongo nadhani kinachangiwa na kuwa na waalimu feki,wanaochaguliwa kujiunga na ualimu ni wale waliofeli form four au six! Kwahiyo tunafundishwa na ma-failures! unategemea nini hapo?
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Dec 22, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Zakumi, kwani Kiingereza kwa Wakenya sio lugha ya pili au ya tatu? Kama ni hivyo basi hakuna tofauti sana na Watanzania. Hivi umewahi kumsikia raisi wao akiongea Kiingereza? Hata Kikwete ana afadhali!

  Still, mimi bado sijashawishika kuwa eti Wakenya wanatuzidi. Mimi kila siku nawaona na sioni lolote spesheli walichonacho. Wanazimia Kiswahili changu na Kiingereza changu cha kubabaisha. Haki ya nani tena Wakenya hawatuzidi kabisa! Tatizo tulilonalo (Watanzania kwa ujumla) labda ni perceptions tu. Perceptions tulizonazo ni kwamba wanatuzidi (supposedly wanaongea kiingereza kizuri-kitu ambacho nakataa) wakati actual reality ni kwamba hawatuzidi lolote.
   
Loading...