Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,454
- 872,085
Kuumbuka kwingine kusikie hivihivi
Tuko hotel fulani nzuri na ya hadhi nje kidogo ya mji panafaa kwa kupumzika nk
Tumeamshwa na zogo la walinzi na mteja mmoja ambaye kumbe kachepuka
Jana using huyu jamaa alikuja na binti aliyekuwa na mashauzi na nyodo za kufa mtu wakapatiwa chumba wakalala, alfajiri hii wakatoka kufika getini wakazuiwa kutoka mpaka wafanyiwe ukaguzi
Binti akawa mbogo, akasema wanawahi ndege ila walinzi wakakomaa kuwa hatoki mtu bila kukaguliwa. Jamaa naye akawaka kweli kuwa 'wanawamistreat' wateja lakini walinzi wakashikilia msimamo wao
Maskini binti kuja kusachiwa kakutwa na mataulo 2 ya hotel, makubadhi, glass uma kijiko na kisu, remote ash tray sabuni foronya 2 na air refresher vyote kavisunda kwa ustadi mkubwa kwenye mkoba wake mkubwa mkubwa hivi
Jamaa kabaki mdomo wazi, walinzi wanataka wawapeleke polisi, jamaa anareconsile yaishe kwakuwa hakujua hata kama yule ni mwizi kajiokotea tu, naye ni baba wa familia na ni mtumishi wa serikali
Hali ya hewa imechafuka kweli binti yuko chini ya ulinzi na 'mume' wake na safari ya ea poti imeishia getini