Siamini kabisa kama Mbowe anaweza kuhamia CCM. Akifanya hivyo nitajiuliza sana kama hajapata matatizo makubwa ya kisaikolojia au ya hata afya ya akili.
Kazi aliyoifanya kuijenga CHADEMA hadi kikawa chama tishio kisiasa nchini kiwango kile katika mazingira yale, sio kwa akili ya kawaida. He was a genius for sure.
CCM na serikali yake hawakuweza kugundua tishio analotengeneza Mbowe. Wangeshtuka, wangeua juhudi zake mwanzoni kabisa. Leo chama ni self sustaining; hakihitaji mtu (individual) ku-survive. Hata Mbowe mwenyewe kimempumzisha na kuongeza kasi ya mapambano. Hata Lissu asipokuwepo chama kinachanja mbuga tu. In fact, Tanzania Leo hii, kiuhalisia, hakuna chama kingine cha siasa zaidi ya CHADEMA!
Mbowe, hata kama kaharibu, anaachaje legacy hiyo na kutaka kuhamia CCM anakodharauliwa sana? Vyovyote vile, CHADEMA hawawezi kumkana Mbowe kama muasisi wa chama. Hana budi kuvaa ngozi ngumu na kujiweka sawa na uongozi wa sasa na wanachama ili nafasi yake na hadhi yake ndani ya chama isifutike na kutoweka kabisa.