Epuka gharama kwa kuacha kununua vitu visivyo vya lazima, tumia mbinu hizi

Powell Gonzalez

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
622
1,276
Bila shaka kila Mtu ameshawahi kununua kitu alafu baadae akajihisi kama anajutia kukinunua Aidha Kwa sababu hakina umuhimu au kimemuingiza gharama zisizo za msingi.Hapa mara nyingi vitu kama simu,vifaa vya usafiri,nguo na vitu vingine ambavyo ni luxurious huwa vinahusishwa.

Mimi Kwa utafiti wangu hasa Kwa kupitia literature review nimeona kuna Hizi mbinu ambazo unaweza kuzitumia kuepuka kununua vitu ambavyo havina ulazima na kuokoa gharama zako,nimeamua kuandika mbinu hizi baada ya kuziona ziko practicable na zikitumika zinaweza kufaa,ingawa si nyingi ni mbili tu.
Kabla sijazitaja hizi mbinu mbili ningependa niseme kuwa mpaka Mtu anaamua kununua kitu kuna kuwa na sababu mbili,ambazo ni;
  • Uhitaji( kuwa na uhitaji hasa na kitu hicho
  • Tamaa ( kutamani kununua kitu Aidha Kwa ajili ya kujionyesha au mihemko ya kimwili/kiakili)
Kwa kuwa hizi ndio sababu zinazomfanya Mtu aamue kununua kitu,na sababu ya msingi ni Ile ya uhitaji basi mbinu hizi mbili zifuatazo zinaweza kuwa na msaada wa kumuepusha MTU kununua vitu Kwa tamaa;
1.Ukiwa na wazo la kununua kitu chochote kile basi usikinunue mpaka baada ya siku mbili toka ulipopata wazo la kukinunua.Hii ni Kwa sababu unaweza ukawa umepata wazo la kununua kitu Kwa tamaa Tu,na Tamaa huwa inatengezwa na ubongo na huwa haidumu Kwa Muda mrefu tamaa huwa ni ya muda mfupi, hivyo basi unapoacha kununua ndani ya muda wa siku mbili hapo utaruhusu Tamaa yako ya kununua kitu hicho kupotea na hivyo ukatumia pesa hiyo kwenye mambo mengine.Lakini ikatokea umekaa siku mbili na bado wazo la kununua hicho kitu bado lipo kichwani basi jua kweli unahitaji kuwa na kitu hicho na si Tamaa iliyokuongoza kukitaka.

2. Unapotaka kununua kitu hasa luxurious jiulize je unaweza kununua hicho kitu mara mbili,kama jibu ni ndio basi hicho kitu kipo katika uwezo wako nunua,na kama la si hivyo basi kipo nje na uwezo wako hivyo si vyema ukakinunua.

Kwa mfano umepata wazo kununua Aina fulani ya simu, jiulize hivi Kwa uwezo Wangu wa kifedha naweza kununua simu za Aina mbili Kwa wakati huu? kama unaweza basi hiyo simu Ni affordable to you,Ila kama huwezi basi hiyo haiendani na kipato chako.

Kimsingi mbinu hii itasaidia kuacha kununua vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wako,Kwa mfano unaweza kukuta MTU anamshahara WA laki SITA kwa mwezi na baada ya kupokea hiyo laki SITA akaenda kununua simu ya laki ya tano,Hii si hadhi yake,ilimpasa anunue simu ambayo IPO chini ya laki Tatu ambapo atakuwa ametumia 50% ya kipato chake(hata hii principle ya kujiuliza ikiwa anaweza kukinunua mara mbili inakuwa applied),na sio simu Tu kila kitu luxurious ikiwemo magari na branded outfits.

Wazungu wao husema "IF YOU CAN'T BUY IT TWICE THEN YOU CAN'T AFFORD IT"
ni ushauri Tu,ahsanteni.
Instagram;, raphaelkalolo23
email; raphaelmathewkalolo@gmail.com
 
Hapo unataka nijiunge na vicoba sasa na mikopo kausha damu nianze kupata tabu mjini hapa😃😃... Nyie nunueni tu hayo macho yenu...mimi galaxy tu unanitosha na nafurahia maisha yangu bila stress 😂😂😂
Kumbe ni Galaxy S23 ultra mpwa?🤣🤣🤣
 
Sehemu nyingine ambapo waweza nunua kitu bila kutarajia ni kwenye maduka makubwa ya bidhaa yaani super market. Tahadhari Sana uendapo katika maduka kama hayo. Ni vyema ukiwa umeandika orodha ya vitu unavyovihitaji ambavyo utavinunua na kuachana kabisa na vile ambayo hukuviorodhesha.
 
Back
Top Bottom