Tumia mbinu hii ya KIJESHI kuua ushindani kwenye biashara yako

Seif Mselem

JF-Expert Member
Oct 16, 2023
257
441
…kama Umewahi kwenda Jeshini basi…
.
Utakuwa umeshawahi Kukutana au Kusikia Mbinu nyingi za Kivita Zikifundishwa…
.
Hata kama Hujawahi kusikia basi Ondoa shaka...
.
Kwasababu…
.
Hapa chini Naenda kukuonesha Mbinu moja Hatari ambayo Unaweza kwenda kuitumia kwenye Biashara yako pia
.
…Mbinu hii Imewahi Kutumiwa na Billionea “Bill Gates” Kuuwa Ushindani Sokoni…
.
ILA…
.
Kabla Sijakwambia Hiyo Mbinu Ngoja kwanza Nikupe Hii STORY Kati ya…
.
Microsoft Vs Apple!
.
Okay… Tuanze Hapa
.
…kama Utakumbuka mwaka 1981 Kipindi…
.
Microsoft anatoa Operating System (OS) yake ya kwanza walikuwa wapo kwenye Usindani mkali na kampuni ya…Apple!
.
Kwahiyo…
.
Wakati Microsoft wanatoa OS yao ya kwanza Iliyokuwa Inaitwa… “Disk Operating System”
.
Ambayo ilikuwa inatumika kwenye Personal Computer za Kampuni ya…IBM!
.
Apple… Hawakukubali!
.
…Wao walikuja na OS yao kali ambayo Ingetawala soko la Personal Computer
.
Walikuja na hii Inaitwa… “GUI Based Operating System” ambayo Ilikuwa kali zaidi ya ile ya Microsoft
.
Na…
.
Apple chini ya CEO wake makini…Steve Jobs walijua wamemaliza Ushindani Sokoni
.
Kwasababu…
.
Apple na Microsoft walikuwa ni washindani kwenye Soko la Computer hasa kwenye utengenezaji wa Operating System
.
Na…
.
Tunaposema OS kwenye Computer ni sawa na Kusema… Android na IOS kwenye Simu
.
Kwahiyo…
.
Baada ya Apple kutoa hiyo GUI walijua tayari wamemaliza Ushindani Sokoni kwasababu OS waliyotoa Ilikuwa kali zaidi ya ile ya Microsoft ambaye alikuwa ni Mshindani wao mkubwa
.
Na…
.
Kama Utakumbuka…
.
Apple alikuwa anatengeneza OS ambazo zilikuwa zinatumika kwenye Personal Computer zake za…Mac!
.
Wakati huku Microsoft hawakuwa na Computer na walikuwa wakitoa OS zao zinatumika kwenye Computer za…IBM!
.
Kwahiyo…
.
Hapa moja kwa moja Apple walijua wameshinda Vita ya Ushindani Sokoni
.
Kwa Siri sana Bila Apple Kujua…
.
Kumbe huku Microsoft chini ya Mtu makini…Bill Gates
.
Walikuwa wanaandaa BOMU…Walikuja na OS Bora na Makini zaidi kuwahi kutokea kwenye Soko la Computer
.
Walikuja na Hiki Kinaitwa…
.
“Microsoft Window”
.
…Operating System Ilikuja kuwa Bora mara kumi zaidi ya Ile ya Apple
.
Na…
.
Baada ya hapo kilichobaki ni Historia tu…
.
Microsoft Window imekuja kuwa Ndio OS Bora zaidi kuwahi kutengenezwa na Ilimfanya Bill Gates kuwa Tajiri #1 Duniani baada ya kuwashinda Apple kwenye Mauzo ya OS zao
.
Ndio sababu hadi leo Computer za Apple hazina Soko kubwa kama Ilivyo kwa Computer zinazotumia Window kama Operating System yake
.
Na…
.
Mbinu ya Kijeshi iliyotumiwa na Microsoft chini ya Bill Gates Inaitwa…
.
“Surprise Tactic”
.
Inasema Hivi…
.
“If You Can Surprise Your Opponent, You Take Away His Ability to Plan and He Must React in a Befuddled State of Mind”
.
Usihangaike Nimekuwekea Maelezo yake hapa Chini…
.
Angalia Ilivokuwa…
.
…kipindi Microsoft wametoa OS yao ya kwanza (DOS) Ilikuwa ni Mtego kwa Mshindani wake Apple
.
DOS Ilikuwa ni Os ya kawaida ambayo Iliwafanya Apple watoe kile Kilicho bora kwenye makabati yao wakiwa wanajua kuwa Microsoft hawana tena cha Kutoa Sokoni
.
Bila wao Kujua (Apple)…
.
Kuwa Microsoft wamehifadhi Bomu kubwa ndani ambayo ndio Ilikuwa OS yao Bora zaidi kuliko Ile walioitoa mwanzo kama Mtego
.
Kwa Ufupi Tu…
.
Walitoa DOS Ili kuwachanganya na kujua Apple ana nini kwenye Makabati yake kwahiyo baada ya Apple kutoa GUI wao wakawa na Muda wa kuiboresha Window na kuwa OS Bora zaidi ya ile ya Apple
.
Then…BINGOO!
.
Kwahiyo…
.
Hata kama wewe pia uko kwenye Biashara ya Ushindani mkali kabla Hujatoa bidhaa/huduma yako kali na ya Moto zaidi kuliko zote
.
Unaanza kwa kutoa bidhaa/huduma Ingine yoyote ya kawaida ili Kumfanya Mpinzani wako atoe kile anachokiamini kwa Lengo la kuwa amekushinda kwa Ubora kisha…
.
Wewe unapata muda wa Kujua na Kuona kile alichonacho Mshindani wako na Unapata muda zaidi wa Kuirekebisha ile bidhaa yako Unayoiamini kabla ya Kuitoa Sokoni
.
Na…
.
Hicho Ndicho alichofanya Bill Gates kwa Mshindani wake wa OS Steve Jobs!
.
Vile vile…
.
Hii Mbinu inaweza Ikawa ndio Kaitumia Diamond Platnumz na timu yake, Yaani… Kaachia Ep ya FOA kama Mtego wa kujua washindani zake wana nini
.
Kisha yeye akija kutoa Album yake anakuwa na Uhakika ni kali zaidi ya Zile zilizotangulia
.
Kwahiyo…
.
Hii ni Mbinu unaweza Kuitumia kama uko kwenye Biashara yenye Ushindani mkali na Washindani wako wanapenda kuiga iga
.
Hii Ndio Dawa ya Kuwaliza
.
I Hope Umejifunza Kitu…
.
Uwe na Siku Njema!
.
Gracias
.
Seif Mselem
 
Hovyoo, diamond huo mfano hovyo, na mbinu ya kivita mfano hovyo, yaani hujalink kabisa maelezo na mbinu ya kivita, una kitu ila umeshindwa kukuwakilisha.

Alafu yaani kibiashara sijui nikwambiaje ila hiyo mbinu zero.

Kkoo unaweza agiza mzigo mkubwa, mpaka ufike bongo ukakuta wenzako tayari wanao.

Kkoo hiyo hiyo, unaweza fikisha mzigo watu wakaununua wote na ww hukuwa na mzigo mwingine.
Sikuhizi watu ni ma mafia.
 
Mada ilikuwa nzuri ila umeiboronga baada ya kumtaja Diamond Platinum,Diamond mziki anaoimba una ubora gani ukilinganisha na wasanii wengine zaidi ya kuimba matusi tu na kukopi nyimbo za nchi za watu kisha anageuza lugha tu?Jina tu linamuokoa ila kuna wasanii wadogo wengi tu wana nyimbo zenye ubora kumzidi Diamond
 
Kwanini Usiandike na Wewe Tuone?..
Wewe ni mpishi.

Mimi ni mlaji, yaweza kua una mpango wa kutengeneza pesa online kwa kupitia freelancing ya uandishi.

Mimi mlaji nakuonyesha unapokosea. Mpishi unanitishia kwamba kwanini nisiandike ili muone.

Mi nilishaandika wakati nipo kama freelancer kama unajifurahisha acha hivyo hivyo kama una mpango wa kutengeneza pesa angalia kama unaweza kurekebisha hiyo style.
 
Mbinu ni nzuri but Ina some weekness, mfano unaweza kuingiza kitu sokon kibovu ili kumpima mpizan wko ana nn, mwisho wa siku wateja wakakereka na hio huduma yko huoni utakuwa umeshaaribu brand hata ukija kutoa kinzur means inatakiwa kutumia nguvu kuwaamisha wateja wko kuwa ulichotoa Kwa Sasa ni Bora kuliko ulichotoa mwanzon.
 
Back
Top Bottom