TIARAEI ndiyo wapi? Au ina maana ya Ti Ar Ei? hihiiii Mie nilishachekwa kuwa sisi Watanzania tunaitamka vibaya R. Tunasema ARA badala ya AR... Sijui upi ni ukweli. Wakali wa lugha nijulisheni ili siku nyingine nijitete.
Huu ukabila mama naomba unisaidie. Mie najua tatizo lipo na inabidi liongelewe ila kuna wengine wanadai kuwa hiyo imesababishwa na HISTORIA ya nchi katika devide and rule..... Au mie nina KIHINDIHINDI nini? Maana Kizunguzungu Tanzania hakipo tena na sasa kwa mbali nahisi Kichagakichaga. Just asking.
Ukabila
Kwa mara nyingine zile chuki dhidi ya wachagga zinaendelea kujitokeza kila jina la Kichagga linapotajwa. Tumefikia mahali wachagga wasiwe viongozi wa idara yoyote ile Tanzania na serikali itoe Memo kuelezea kuwa Wachagga hawastahili kushika nafasi yoyote ya juu, na kama wanashika wahakikishe kuwa akija mchagga "mwenzao" kuomba kazi asipewe nafasi hayo ili kusije kuonekana ukabila.
Na wachagga wote wenye kushika nafasi za juu serikalini wajiuzulu ili kupisha wananchi wa makabila mengine.
Mwanakijiji, something whiff aroud, naogopa sana kuproject this issue. Tunakoendea sijui as watu wameshakuwa sensitive na sijui kama kuna uwezekano wa hao watu kuondoka na kuwaachia makabila mengine. Kuna Wahaya na wanyakyusa wamedominate positions pia.
My take, ianzishwe directorate ya serikali na agency zake zote. Nafasi zote za kazi ziwe zinapelekwa kwenye hiyo directorate ambayo itazitangaza na kufanya usaili kwa kuhusisha experts from the appropriate unit inayotaka mfanyakazi.
Mama hata ikianzishwa hiyo directorate n.k itakuwaje kama Wachagga, Wanyakyusa na Wahaya wakizidi kujazana, they have had had an unfair advantage toka zamani. Kwanini tusiwazuie kuajiriwa angalau kwa miaka mitano?
Bonus Sh 122,000,000/= ?????? lol! imekua vodacom sasa hii.....halafu mtu kama huyu utakuta bado haridhiki na hapo..anafanya na ufisadi juu.!! Hii ndio TZ
Watanzania bwana!
Tunalilia hatulipwi mishahara mizuri, halafu tunakimbilia kuingiza vimisheni tauni, kujiongezea.
Tumelewa UJAMAA uliosema kuwa kuwa Tajiri au kuwa na Kipato kikubwa ni dhambi, aliyekuwa na mshahara mkubwa tulimuita MNYONYAJI, BEPARI, BWANA na sisi kulea UNYONGE na UTWANA!
Nashangaa sana kuwa mpaka leo hakuna mipango mizuri iliyofanywa kuhakikisha kuwa mchakato wa Mishahara Tanzania unabadilishwa kwenda sambamba na mfumo wa Kiuchumi tulionao.
Kila siku Wafanyakazi wa Tanzania wanapunjwa mishahara kutokana na Serikali kujenga tabaka la watu tegemezi. Kila siku unasoma Serikali yetu iliyodai tumeindia UCHUMI HURIA inafanya mambo ya welfare, kusaidia jamii na wafanyakazi hasa Waalimu, Wauguzi, Askari, Polisi wajengewe nyumba na Serikali, lakini mishahara yao inabakia kuwa duni.
Kwa nini badala ya kuwajengea nyumba, wawalipe Watumishi wa Serikali na Mashirika mishahara mizuri na wawape mikopo ya kujengea hizo nyumba?
Hili la Mrema la watu kudai analipwa pesa nyingi sana na ni tatizo, halina nguvu. Kama mshahara uliotangazwa ulionyesha kuwa hicho ndicho kiwango, na Mrema alipoanza majadiliano ya kuingia mkataba wa kufanya kazi akaweza kushawishi kwa kutumia vigezo vya Utaalamu wake, na mshahara aliopewa Mghana, hakuna kesi kuwa eti yeye ni Fisadi.
La kujifunza kutoka hapa ni kutaka reform ya mishahara Tanzania! Tunataka Serikali iunde uchumi mzuri ambao utaruhusu kuongfezeka kwa mishahara na kupunguza makali ya Maisha.